TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, May 28, 2012

UONGOZI WIZARA YA MIUNDOMBINU MAWASILIANO WAKUTANA NA DK. SHEIN

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa  Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano, katika utekelezaji wa mpango wa kazi za Ofisi za Wizara
hiyo huko Ikulu Mjini Zanzibar juzi,  [ Picha  na Ramadhan
Othman,IKULU.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa  Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano, katika utekelezaji wa mpango wa kazi za Ofisi za Wizara
hiyo huko Ikulu Mjini Zanzibar juzi,  [ Picha  na Ramadhan
Othman,IKULU.]

MAONYESHO YA WANAFUNZI UDOM YAFANA JANA KATIKA UKUMBI WA CHIMWAGA ULIOPO CHUO KIKUU CHA DODOMA(UDOM)

 Muandaaji wa Maonyesho haya Ester Zangi ambaye pia ni Mwanafunzi wa Mwaka wa 3 anayesomea shahada ya kwanza ya sayansi ya siasa na utawala wa umma(Wa Kwanza Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma ambao Wameonyesha vipaji vyao Vya Kuchora Michoro inayoonekana hapo katika maonyesho yaliyofanyika jana Chuo Kikuu Cha Dodoma katika Ukumbi wa Chimwaga
PICHA NA JOSEPHAT LUKAZA WA http://josephatlukaza.blogspot.com
 Mwanafunzi wa Mwaka wa 3 anayesoma shahada ya kwanza ya filamu na sanaa anayejulikana kwa jina la wacko jacko akiwa amesimama pembeni mwa moja ya michoro aliyochora kwa Mikono yake na hapo alikua katika maonyesho yaliyofanyika chuo kikuu cha Dodoma jana
Mmiliki wa Mtandao wa Lukaza Blog Mh Josephat Lukaza (Wa kwanza Kulia) akiwa katika Picha ya Pamoja na Wadau wa Lukaza Blog mara baada ya Kumalizika kwa Maonyesho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) katikati ni Mh Mzagamba Thobias Kutoka Uswis na Wa Kwanza Kulia ni Atu Mwanafunzi wa Mwaka wa 3 UDOM.
Wanafunzi wa UDOM wanaosoma shahada ya kwanza ya Filamu na Sanaa, Kiswahili wakionyesha uwezo wao wa kucheza boringo katika maonyesho yaliyofanyika jana Katika Ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu Cah Dodoma (UDOM)
Mmoja wa wanakamati wa maandilizi ya maonyesho haya ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa 3 Bi Atu anayesoma shahada ya kwanza ya Mazingira ya Chuo Kikuu Cha Dodoma alipokua akitoa neno wakati wa maonyesho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Chimwaga uliopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) jana
Mmiliki na Mwendeshaji wa Mtandao wa Lukaza Blog Mh Josephat Lukaza alipokua akitoa maelekezo jinsi ya Lukaza Blog inavyofanya kazi na vilevile Mtandao wa Lukaza Blog unavyopatikana na ulivyoweza kupokelewa Vizuri ndani ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) na vyuo vikuu tanzania wakati wa Maonyesho yaliyofanyika Chuoni hapo jana
Mmoja wa Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sanaa na Filamu Babra Kalugira akiwa kwenye Kirekodi Video (VIDEO CAMERA) akichukua video ya matukio yaliyokuwa yakiendelea katika Maonyesho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuoni Hapo

Big Brother StarGame: Eviction (Sunday May 27, 2012)

The 91 day reality super-series Big Brother StarGame, produced for M-Net’s AfricaMagic, is being screened live 24/7 on DStv 197 & 198. Last night (Sunday 27 May) Mampi was evicted while Ghana’s Mildred & Keitta and Botswana’s Edith & Eve were randomly nominated to face eviction this week.
For more information log on to www.africamagic.tv/bigbrother
Pictured here: Mampi and IK
The 91 day reality super-series Big Brother StarGame, produced for M-Net’s AfricaMagic, is being screened live 24/7 on DStv 197 & 198. Last night (Sunday 27 May) Mampi was evicted while Ghana’s Mildred & Keitta and Botswana’s Edith & Eve were randomly nominated to face eviction this week.
For more information log on to www.africamagic.tv/bigbrother
Pictured here: Tanzanian artist Diamond Platinumz

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA BALOZI WA IRAN KWA MAZUNGUMZO IKULU DAR ES SALAAM LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mohsen Movahhed Ghomi, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Mei 28, 2012 kwa mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Iran Nchini Tanzania,  Mohsen Movahhed Ghomi, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo Mei 28, 2012 kwa mazungumzo.

MSHINDI WETU WA BAJAJ KATIKA PROMOSHENI YA "VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO" AKABIDHIWA ZAWADI YAKE

Meneja Masoko wa kampuni ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) Kanda ya Ziwa, Patrick Kisaka, kushoto akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kumkabidhi mshindi wa Bajaj wa shindano la Vumbua hazina chini ya kizibo, kulia ni Meneja Mauzo wa SBL Mwanza, Octavian Migire.
Meneja wa Mauzo wa Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya ziwa  Bw Patrick Kisaka akikabidhi  Bajaj kwa mshindi wa huyo katika promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na SBL, Bw. Godfrey Shao mkazi wa mkoa wa Mwanza ambaye alijishindia pikipiki ya matairi matatu( BAJAJ) kupitia bia ya Tusker Lager
Godfrey Shao amesema hakutegemea hata siku moja kupata zawadi kubwa kama ile na kwamba ameishukuru sana kampuni ya bia ya Serengeti kwa kubadilisha maisha yake kwani  sasa anaweza kujiajiri na kuwasaidia wale wanaomtegemea
Bw Godfery Shao ndani ya Bajaj yake akipongezwa na wafanyakazi, wawakilishi, wapenzi na wadau wa kampuni ya bia ya Serengeti baada ya kukabidhiwa Bajaj yake  mpya kabisa

WAZIRI WA ULINZI DK. EMMANUEL NCHIMBI ATUA VISIWANI ZANZIBAR NA KUKEMEA VITENDO VYA VURUGU

Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Dk. Emmanuel Nchimbi ametua Visiwani Zanzibar leo ambapo amekemea vitendo vya vurugu,akiahidi Serikali kuwachukulia hatua ikibidi hata kuwavizia nje ya misikiti kwa wale watakaohusika na uvunjifu wa amani .
Waziri Nchi aliwasili Mjini Zanzibar akiwa na Mkuu wa Jeshi  la Polisi,Inspekta Jenerali Said Mwema kwa pamoja waliitisha mkutano uliowakutanisha viongozi wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar(JUMAZA),Mabalozi,Kamisheni ya Utalii, Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar(JUMIKI).
“Suala la kufuata sheria halina mjadala,lazima kila mmoja wetu afuate na kutii sheria hatutawavumilia watakaovuruga amani ya nchi…maandamano yoyote lazima yapate kibali” Aliwaambia wadau katika mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar,Ziwani.
Waziri Nchi alisema busara ya Polisi imefikia kikomo na kwamba atashangaa sana akiona busara hiyo ikiendelea wakati kuna watu au kikundi kinavunja amani ya nchi.
“Tutashangaa busara ya Polisi ikiendelea wakati watu wanaumia kwa watu wengine kuvunja amani…hatutakubali, tutaendelea kuviziana hata nje ya misikiti tutawakamata” Alisisitiza Waziri Nchi.
Waziri huyo alisema kila mtu anawajibika kitunza amani iliyopo ambapo pia alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenye mfumo wa Umoja wa Kitaifa imefanyakazi nzuri katika kipindi kifupi na kuwapongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd.

ZIARA YA WAZIRI KIGODA KATIKA KIWANDA CHA URAFIKI

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mh, Abdala kigoda akiongea na wajumbe pamoja na Viongozi wa kiwanda cha Urafiki jijini Dar es Salaam alipotembelea kiwanda hicho leo jijini Dar es Salaam ambapo aliziona changamoto nyingi zinazozikabili kiwanda hicho ikiwemo mishahara miidogo ya wafanyakazi na akaahidi kuzifanyia kazi.
Diwani wa kata ya Ubungo  jijini  Dr es Salaam Mh, Bonifas Jacob  akieleza changamoto zinazo wakabili wafanyakazi wa kiwanda hicho pamoja na usimamiaji mbovu wa Kiwanda hicho mbele ya Waziri.
Baadhi ya wafanyakazi, Viongozi pamoja na wajumbe mbalimbali waliohudhuria kwenye ziara hiyo wakimsikiliza Mh, Waziri kwa umakini.
Naibu Meneja uchapishaji na utiaji rangi kwenye kanga Bw, Solomon Laban(kulia) akimuelekeza waziri namana mtambo huo wa utiaji Rangi unavyofanya kazi  akikagua baadhi ya Mitambo ndani ya kiwanda hicho.
Waziri akikagua uzalishaji wa kanga kiwandani hapo.
Mh. Waziri wa viwanda na Biashara akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kiwanda hicho baada ya kumaliza matembezi.

Uzinduzi rasmi wa tawi la Chadema Washington Dc wafanyika

Uongozi wa juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  katika uzinduzi rasmi watawi la Chadema Washington Dc  kwenye meza ya juu wa kwanza kushoto Libe Mwangombe, akifatiwa na Mhe. Peter Msigwa,  Mwenyekiti wa tawi Mhe. Kalley Pandukizi,  Mhe. Zitto Kabwe, na Mhe. Nassari Joshua, Dogo Janja, mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Mirage Hall uliopo University Of Bld, Hysattsville, Maryland Nchini Marekani.
Mhe. Zitto Kabwe akitoa hutba kuelezea mpango mzima wa mambo yanavyoendelea nchini Tanzania
Wantazania waishio DMV Nchini Marekani wakiwa katika uzinduzi wa tawi la chadema Washington  Dc
Wantazania waishio DMV Nchini Marekani wakiwa katika uzinduzi wa tawi la chadema Washington  Dc
Mwanachama wa chadema kutoka Boston kamanda Doto akiuliza masuali tofauti  katika mpango mzima wa uzinduzi rasmi watawi la Chadema Washington Dc uliofanyika jana Mei 27, kwenye ukumbi wa Mirage Hall uliopo University  Bld, Hysattsville, Maryland Nchini Marekani.
Mhe. Leticia Nyererewenye uzinduzi wa watawi la Chadema Washington Dc
Mhe. Peter Msigwa akiandika masuali yaliokuwa yakiulizwa na baadhi ya wakireketwa
Mhe. Maryam Msabaha kwenye uzinduzi wa tawi la Chadema Washington Dc
Baadhi ya wakereketwa wachukua kadi baada ya uzinduzi wa tawi la chadema Washington
 Mhe. Nassari Joshua (Dogo Janja) Akishanga mamia ya wana DMV waliofurika katika uzinduzi rasmi watawi la Chadema Washington Dc

REDD'S MISS TABORA HUYU HAPA

 Mshindi wa taji la Redds Miss Tabora 2012 Sarah Paul katikakati akiwa na washindi wengine wawili Glory Mongi kulia na Alice Amour kushoto mara baada ya kufanikiwa kutawaza washindi wa taji hilo na kufanikiwa kuingia katika kinyanganyiro cha kanda kuelekea kwenye fainali ya Redds Miss Tanzania 2012 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Toleo la Leo.
BIA YA CASTLE LITE SASA KUPATIKANA KATIKA KOPO
Dar es Salaam, May 28. 2012:
Bia maarufu ya Castle Lite, inayozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) leo imezindua rasmi muonekano wa kopo lililojazwa kinywaji hicho ikiwa ni muendelezo wa kuwarahisishia walaji upatikanaji wa Bia hiyo iliyotokea kupendwa na watumiaji wa vileo na kuifanya iwe bia inayokua kwa kasi hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Castle Lite Bi. Pamela Kikuli alisema; Leo tunazindua ujazo mpya wa bia ya Castle lite, bia yenu muipendayo kwa sasa inapatikana katika kopo lenye ujazo wa mililita 330. Uamuzi huu unatokana na mahitaji makubwa toka kwa watumiaji na wapenzi wa bia hii ambayo imekuwa ikipatikana katika chupa yenye ujazo wa mililita 375. Wateja wetu walihitaji kuipata bia yao popote pale walipo au kuwa nayo popote waendapo, hivyo kupatikana kwa bia hii katika chupa peke yake kulipunguza uhuru wa kuwa na bia yao popote waendapo kwani walihitaji kurudisha chupa kila waitumiapo.
Uzinduzi wa Castle lite ya kopo utasaidia zaidi kuongeza upatikanaji wa kinywaji hiki katika maduka ya reja reja (super markets) n.k kote nchini na kuwapa nafasi wapenzi wa castle lite kununua bia yao waipendayo na kwenda nayo nyumbani. Bei ya reja reja kwa kopo ni shilingi 1700/- na bei ya reja reja kwa chupa itaendelea kubaki ile ile 1700/-.
Kwa upande wake Meneja mawasiliano na mahusiano ya jamii wa Tbl Edith Mushi aliwashukuru wapenzi na watumiaji wa bia ya Castle Lite kwa kuweza kuipa mafanikio makubwa katika soko la bia hapa nchini, “ninawahakikishia kuwa mnafanya uamuzi ulio sahihi kwa kuchagua kutumia Castle Lite” nasi tutaendelea kuwapatia bia iliyo bora siku zote. Alisema Edith.
-MWISHO-



 Meneja wa kinywaji cha Castle Lite Pamela Kikuli akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa castle lite ya Kopo, kulia ni meneja habari na mawasiliano ya Umma wa Tbl Edith Mushi.
 
 

Sunday, May 27, 2012

MBUNGE WA JIMBO LA KILOLO PROF PETER MSOLLA AKIMBIA KUWEKWA KITIMOTO NA WAPIGA KURA WAKE

Mwakilishi wa mkurugenzi wa Kilolo John Kiteve akijibu maswali katika mdahalo huo ambao ulipaswa pia kuhudhuria na mbunge wa jimbo la Kilolo Prof.Peter Msolla
Na Francis Godwin,Blog

MBUNGE wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Profesa Peter Msolla amekwepa kushiriki mdahalo wa kimaendeleo katika Kati yake na wananchi wa jimbo hilo leo .

Katika mdahalo huo uliofanyika katika ukumbi wa Upendo Ruaha mbuyuni mbunge Profesa Msolla ambaye pia amepata kuwa waziri wa mawasiliano sayansi na Teknolojia mbali ya kupewa taarifa na waandaaji wa midahalo hiyo ambao ni azaki za kiraia Tanzania ,mbunge huyo alipaswa kufika katika ukumbi huo kuanzia majira ya saa tatu asubuhi ila hadi saa Saba mchana mbunge huyo wala katibu wake hawakuweza kutokea ukumbini na kupelekea mdahalo huo kuchelewa kuanza .

Mratibu wa midahalo hiyo mkoa wa Iringa Raphael Mtitu alisema kuwa mbunge huyo alipewa taarifa kwa wakati juu ya uwepo wa midahalo hiyo japo alisema kuwa anasikitishwa na hatua ya mbunge kutofika na kuwa ni mbunge wa kwanza toka kuanza kwa midahalo hiyo kushindwa kufika huku akidai kuwa kutofika kwake bado hakujazuia mdahalo huo kuendelea

MAADHIMISHO YA SIKU YA AFRIKA YAFANA, LONDON-UINGEREZA

Mheshimiwa Balozi wa Uganda, Mama Joan Rwabyomere, akifungua Maadhimisho ya siku ya Afrika hapa nchini Uingereza, katika sherehe ambazozilifanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Lagham Palace, London.
Mheshimiwa Balozi wa Botswana, Bwana Roy Blackbeard, akihutubia katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afrika.
Kutoka kulia, Dada Rahma Lupatu, Caroline Chipeta, Bwana David Nginila, Bwana Kiondo (maafisa wa Ubalozi wa Tanzania, London) na Dada Jestina George,
Mabalozi ,Maafisa wa Ubalozi na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali za Afrika na wageni waalikwa katika sherehe hizo.
Dada Jestina George na dada Rahma Lupatu, wakijivunia Utanzania wao katika sherehe hizo za siku ya Afrika
Kikundi cha ngoma kutoka Ghana, wakitoa burudani katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afrika hapa London
 
Siku ya Afrika iliadhimisha rasmi jana hapa nchini Uingereza kwa kujuisha nchi zote za Afrika zenye Balozi au Wawakilishi wao hapa nchini Uingereza. Katika sherehe hiyo rasmi ya kuadhimishwa kwa Siku ya Afrika, kulitolewa hotuba na Balozi wa Botswana na mbaye ni Mkuu wa Mabalozi wa nchi za Afrika hapa Uingereza, Mheshimiwa Roy Warren Blackbeard.

Aidha Mheshimiwa Balozi Roy Blackbeard, alitoa salamu maalum kutoka kwa mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa nchi za Afrika, Mheshimiwa Yayi Boni, ambaye pia ni Raisi wa Benin.

Balozi Roy, alielezea changamoto nyingi zinazo tokea Barani Afrika na kwingineko na juhudi maalum zinazofanywa na Jumuiya ya Umoja wa nchi za Afrika kutatua migogoro na matatizo ya mara kwa mara yanayolikumba Bara letu la Afrika.

kabla ya kutolewa hotuba hiyo, Balozi wa Uganda Mheshimiwa Mama Joan Rwabyomere, alifungua kwa kuwakaribisha Mabalozi, Wawakilishi, Marafiki wa Afrika na Wageni mbalimbali waalikwa na kuwashukuru kwa kufika kwao na kujumuika pamoja na waafrika wote duniani kuadhimisha siku hiyo hapa nchini Uingereza. Amani, Upendo, Ushirikiano na Mshikamano miongoni mwa nchi za Afrika vilihimizwa katika maadhimisho hayo.

Airtel yafanya promosheni ya huduma ya ‘Jiunge na Supa 5’ kwa kishindo Mkoani Dodoma.

Wasanii wa kikundi cha Kinoko kutoka Dar es Salaam wakilishambulia
jukwaa wakati wa promosheni ya Airtel Jiunge na Supa 5 katika viwanja
vya Jamhuri, Mkoani Dodoma jana. Uzinduzi rasmi ulifanyika jijini Dar
es Salaam hivi karibuni.
Baadhi ya wakazi wa Dodoma wakihamia Airtel wakati wa promosheni
ya Airtel Jiunge na Supa 5 mkoani humo jana.
Mkazi wa Dodoma, Queen Jackson akishindana kucheza taarab wakati
wa promosheni ya Airtel Jiunge na Supa 5 mkoani humo jana.
Zawadi mbalimbali zikiwemo simu za mkononi zilitolewa ili kufanya
promosheni hiyo iwe ya aina yake.
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria promosheni ya Airtel Jiunge
na Supa 5 Mkoani Dodoma jana.