TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, January 13, 2016
UCHUMI WA TANZANIA WAZIDI KUSHIKA KASI
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi za Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa takwimu za pato la Taifa kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2015 (Julai – Septemba), kulia ni Mhadhiri Mwandamizi wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Haji Semboja na kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Utafiti toka Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) Bw. Hussein Kamote.
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA YATOA MSAADA WA VITU MBALIMBALI KWA MAHABUSU YA WATOTO JIJINI DAR ES SALAAM.
Na. Aron Msigwa-MAELEZO.
13/1/2016. Dar es salaam.
Jamii imeaswa kujenga utamaduni wa kuwasaidia watu na makundi yenye mahitaji maalumu hususan wafungwa walio magerezani na wasiojiweza ili kudumisha upendo na kuyafanya makundi hayo kujiona yanathaminiwa katika jamii.
Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mahakama Kuu ya Tanzania Bw. Nurdin Ndimbe wakati akikabidhi msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kwa Mahabusu ya Watoto ya jijini Dar es salaam vilivyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania kama zawadi yao ya mpya 2016.
Bw. Ndimbe amesema Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo Mchele, Sabuni, Vinywaji, Chumvi, Unga wa Ngano, Unga wa Sembe, Mchele ,Sukari na Mafuta ya kupikia kwa Mahabusu hao kuonyesha Upendo na namna Mahakama hiyo inavyowathamini watoto hao.
Ameongeza kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa msaada huo kwa lengo la kujenga mahusiano mema baina yake na watoto hao ili waendelee kuipenda na kuwa na mtazamo chanya juu ya utendaji wake.
‘ Nimekuja kukabidhi msaada huu kwa niaba ya Mahakama Kuu ya Tanzania kwa Mahabusu hii ya Watoto ikiwa ni zawadi yao ya mwaka mpya, lengo letu ni kujenga mahusiano mema kati yetu Mahakama na watoto hawa wajue kuwa tunasaidia jamii katika masuala mbalimbali’’ Amesema Bw. Ndimbe.
Kwa upande wake Afisa Mfawidhi wa Mahabusu hiyo Bw. Ramadhan Yahaya akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo ameishukuru Mahakama Kuu ya Tanzania kwa uamuzi wake wa kuwakumbuka Mahabusu hao.
Amesema kitendo cha Mahakama Kuu ya Tanzania kuwapatia msaada huo kimewapa faraja watoto hao na kuwafanya wajione wanathaminiwa na kupendwa na Mahakama hiyo.
Ametoa wito kwa Taasisi na Mashirika mengine kuiga mfano huo ulioonyeshwa na Mahakama Kuu ya Tanzania ili kudumisha upendo miongoni mwa makundi ya watu wenye mahitaji maalum.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mahakama Kuu ya Tanzania Bw. Nurdin Ndimbe (kushoto) akimkabidhi Afisa Mfawidhi wa Mahabusu ya Watoto jijini Dar es salaam Bw. Ramadhan Yahaya (kulia) msaada wa vyakula na vitu mbalimbali vilivyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania leo.
Tuesday, January 12, 2016
VIONGOZI WA WILAYA YA MISUNGWI WAKUTANA NA WAZIRI KITWANGA KATIKA KUCHANGIA MIRADI YA MAENDELEO.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza mara baada ya kupokelewa wilayani hapo. Waziri Kitwanga aliwataka viongozi hao kuongeza nguvu kubwa ya kukusanya kodi kwa wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa na si kuwasumbua wafanyabiashara wadogowadogo. Pia aliwataka viongozi hao wahakikishe hakuna mwanafunzi atakayekaa chini darasani ifikapo mwakani.
Sunday, January 10, 2016
Special East African Resident Accommodation Rates
Special East African Resident Accommodation Rates. Serengeti Serena Lodge | Lake Manyara Lodge | Ngorongoro Serena Lodge | Mbuzi Mawe Serena Camp | Kirawira Serena Camp | Zanzibar Serena Hotel | Can't see images?Click here... |
|
Subscribe to:
Posts (Atom)