TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, December 5, 2013

VIJANA WA NJOMBE WANAOJISHUGHULISHA NA KILIMO WAKABIDHIWA TREKTA NA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi funguo za Trekta kwa Mwenyekiti kwa vijana Tumsume Shemgogo lililotolewa na chama cha Mapunduzi CCM  kwa vijana wa mkoa wa Njombe katika makabidhiano yaloyofanyika kwenye Kambi ya vijana iliyopo kwenye kijiji cha Mlengu Kata ya Kiangala Tarafa ya Ikuo mkoani Njombe ambapo kambi hiyo ina eneo lenye ukubwa wa  hekta 300 za mashamba, Kinana aliahidi kutoa  trekta hilo wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani Njombe mwezi Agosti mwaka huu  baada ya kuelezwa jinsi vijana hao walivyojiunga pamoja katika kikundi na kuamua kushughulika na kilimo ili kujkwamua kiuchumi, Leo Abdulrahman Kinana alishiriki kulima kwa trekta kabla ya kukabidhi trekta hilo kama anavyoonekana katika baadhi ya picha akilima shambani  kwa trekta.  Kushoto anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Nape Nnauye Katibu wa NEC  Siasa, Itikadi na Uenezi, Katika Ziara hiyo Kinana  pia ameongozana  na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kamataifa na Mbunge wa kuteuliwa. 2a 
Wananchi wa kijiji cha Mlengu wakimsikiliza Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati alipokuwa akizungmza nao. 16 
Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapten Aseri Msangi akiuliza swali kwa mwanafunzi Tito Fungo uimara wa matofari hayo huku Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Dr. Asha Rose Migiro  wakisikiliza kwa makini. 22 
Nape Nnauye akijenga njia zinazopita chuni hapo kwa matofari madogo huku Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  na viongozi wengine wakiangalia. 23 
25

TANZANIA KUOMBOLEZA SIKU TATU KIFO CHA MZEE NELSON MADIBA MANDELA.

Marehemu Nelson Rolihlahla Mandela enzi za uhai wake.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amefariki dunia muda mfupi uliopita akiwa na umri wa miaka 95 jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma amethibitisha taarifa hizo!
Rais Zuma amesema "taifa limepoteza mtu muhimu" na kuongeza "kwa sasa amepumzika. Yupo mahala pema"
Mzee Mandela aliyekuwa akisumbuliwa na homa ya mapafu amefariki akiwa amezungukwa na familia yake nyumbani kwake Johannesburg.
Mandela atazikwa kitaifa na bendera zitapepea nusu mlingoti alisema Rais Zuma.
Alikuwa akipatiwa matibabu kwa takribani miaka mitatu iliyopita na hali yake ilibadilika zaidi katika miezi sita ya mwisho kabla ya kifo chake.
Mpiganaji huyo wa ubaguzi wa rangi, aliingia Ikulu ya Afrika Kusini akiwa mtu mweusi wa kwanza kuiongoza nchi hiyo mwaka 1994 mpaka 1999 baada ya kutumikia kifungo cha miaka 27 gerezani.
 Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na kupitia kwake, kwa mkewe Bi. Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu". Ameongeza Rais Kikwete.
Kufuatia kifo hicho Rais ametangaza siku 3 za maombolezo kuanzia leo tarehe 6 hadi 8 Disemba, 2013. Aidha, Mheshimiwa Rais ameagiza kuwa katika siku hizo 3 bendera zote zipepee nusu mlingoti.
Wengine waliotuma salam za rambi rambi ni pamoja na rais Barack Obama wa marekani na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema: "taa kubwa imezimika duniani
"Nelson Mandela alikuwa shujaa"

Rais Dkt. Kikwete ahudhuria Mkutano wa Ushirikiano kati ya Afrika na Ufaransa


D92A0160 D92A0163 
Rais Francois Hollande wa Ufaransa akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jijini Paris kwenye mkutano unaohimiza kukuza ushirikiano wa kiuchumi kati ya Ufaransa na Afrika.Akizungumza katika mkutano huo Rais Kikwete alisema kuwa mbali na kuwa bado bara la Afrika linahitaji misaada ya uchumi nchi zilizoendelea lazima ziwekeze mitaji katika nchi za kiafrika.
D92A0259 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Francois Hollande wa Ufaransa,Rais Allasane Ouatarra wa Ivory Coast na Rais Mac Sall wav Senegal wakiwa katika mkutano wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Afrika na nchi za kiafrika(picha na Freddy Maro)

KERO YA UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA YAPATIWA UFUMBUZI, NAFASI KUTANGAZWA MTANDAONI

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe,Makongoro Mahanga akitoa hotuba yake.


SERIKALI imezindua mfumo maalumu wa kielektroniki wa taarifa za soko la ajira, ambao utamuwezesha mtafuta kazi kufahamu nafasi mbalimbali za kazi zinazotangazwa ndani na nje ya nchi.
Mtandao huo ambao umeelezwa kuwa utakuwa msaada mkubwa hususani kwa vijana, utamuwezesha muomba kazi kuomba nafasi hizo moja kwa moja katika makampuni husika kulingana na vigezo vitakavyokuwa vikihitajika.
Akizundua mtandao pamoja na maonyesho ya shughuli za huduma za ajira jana jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Makongoro Mahanga alisema, mbali na kutangaza nafasi za ajira pia mfumo huo utawawezesha watu wenye nia ya kuwekeza hapa nchini kutambua aina ya ujuzi unaopatikana nchini na kuwarahisishia katika kuajiri.
“Hii itapunguza waajiri kuajiri wageni zaidi katika zile nafasi ambazo zina wataalumu nchini kutokana na kufahamu mapema. Pia kwa wanafunzi wqa vyuo vikuu watafahamu mapema ujuzi na taalumu wanazopaswa kusoma kwa kuwa utatoa taarifa zitakazowezesha mtu kujua mahitaji ya sasa na ya siku za usoni katika soko la ajira,” aliongeza.
Kwa upande wa waajiri mfumo huo utawawezesha kutangaza nafasi za kazi walizonazo ikiwa ni pamoja na sifa za mtafuta kazi wanayemhitaji.
“Wataweza kupata wafanyakazi wenye viwango wanavyovitaka kwa urahisi kwa kujiunga na mtandao huu,” alisema.
Alisema hatua ya mtandao huo utasaidia kupunguza ukosefu vwa ajira kwa vijana kwani kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2006 tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana lilikuwa kwa asilimia 13.4 hivyo ni matarajio kiwango hicho kitapungua baada ya waajiri wengi kutangaza ajira kupitia mtandao huo.
Mahanga ametoa wito kwa waajiri wote nchini kutumia mfumo huo kutangaza ajira na watafuta kazi na kuutumia kupata taarifa sahihi ili kuweza kuomba nafasi hizo.
Mtandao huo ambao umezinduliwa ni www.ajiralmis.go.tz, vijana wametakiwa kuutumia kwa usahihi zaidi ili kunufaika na ajira zinazotangazwa
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe Makongoro Mahanga, akimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaEsA), Boniface Chandaruba wakati akielezea kazi wanazofanya kuhusiana na ajira kwa vija mara baada ya kutembelea banda hilo, 007Wafanyakazi wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaEsA), wakiwa kwenye picha ya pamoja katika kongamano la  siku mbili jinsi ya kuandika barua ya maombi ya kazi  katika  ukumbi wa Mw. Julius Kambarage Nyerere jijin dar es Salaam.

Dkt Bilal Azindua Kampeni ya Kuzuia Malaria Maarufu kama Zinduka.

IMG_5749Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye hafla ya Maadhimisho ya miaka 50 ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. IMG_5801Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye  uzinduzi wa Kampeni ya Kuzuia Malaria inayojulikana kama ‘M-Zinduka’ inayoendeshwa kwa pamoja kati ya Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom,  Tanzania House of Talents na Malaria  no more   
(Picha na OMR)

Chadema yaijia juu Polisi tukio la moto Arusha,

lema+px
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema.PICHA|MAKTABA 
……………………………………………………………………………………
Arusha.Polisi mkoani Arusha imekamilisha uchunguzi wake kuhusiana na kuungua kwa Ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kusema wanachama wa chama hicho ndio waliohusika.
Hata hivyo, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amepinga kauli hiyo na kulipa jeshi hilo siku nne kuwakamata na kuwahoji watuhumiwa watano baada ya kulipatia majina hayo akidai kuwa ndio wanaohusika na uchomaji moto ofisi za chama hicho.
“Tumewapatia polisi majina… tunaamini walihusika moja kwa moja la sivyo, chama kitatumia vijana wetu wa Red Brigade kuwakamata na kuwafikisha polisi,” Lema aliwaambia waandishi wa habari jana.
Ofisi cha Chadema zilizoko katika eneo la Ngarenaro, zilinusurika kuteketea kwa moto juzi baada ya watu wasiojulikana kuwasha moto katika moja ya vyumba vyake.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Japhet Lusinga alisema:
“Katika uchunguzi wetu, tumebaini kuwa hakuna mahali palipovunjwa kutoka nje ya uzio na kuruhusu watu kuingia ndani… tumegundua kuna tundu dogo darini eneo la kuelekea bafuni la upana wa futi moja na nusu kiasi haliwezi kuruhusu mtu kupita.
“Tumejiridhisha kuwa hakuna mtu anayeweza kupita hapo na ndani tulikuta majivu na baadhi ya vitu vilivyoungua na vifaa vingine.”
Lema akiwa na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro alisema: “Tumebaini polisi wanataka kulifanya jambo hili kama la siasa ndiyo sababu juzi badala ya kuanza kuchunguza waliohusika, waliwakamata Mtunza Ofisi na mlinzi wetu na kuwalaza rumande hadi leo (jana) asubuhi kwa madai eti wanawahoji.
“Hatukubaliani na taarifa yao, hii ni siasa. Kulitokea mauaji ya bomu, wakasema Chadema wamejilipua, leo ofisi imechomwa wanasema Chadema wenyewe, hili hatukubali, “ alisema.
Msajili alaani
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amelaani tukio la kuchomwa moto ofisi hizo za Chadema na kusisitiza kuwa wananchi hususan wanasiasa wasiwe wepesi kuingiza hisia kwenye makosa ya kijinai.
Alisema kuwa tukio hilo linapaswa kukemewa kwa hali yoyote ile kwa kuwa linavuruga na kuhatarisha amani ya nchi.
Dk Slaa aanza ziara
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa amesema hakuna mtu yeyote mkubwa kuliko katiba ya chama hicho.
Dk Slaa aliyasema hayo jana kwenye Uwanja wa CDT, Kahama mkoani Shinyanga, alipokuwa akihutubia mamia ya wanachama na mashabiki wa chama hicho akiwa katika ziara yake kuimarisha chama katika mikoa ya Shinyanga na Kigoma.
“Chadema ni chama makini, kina kila kitu kwenye katiba yake kuliko hata CCM, kina itifaki, kina maadili hata mimi na Mwenyekiti Mbowe (Freeman) imetuwekea mipaka ya utendaji… “Chama hakiwezi kumwonea mtu, kinatenda haki na yanayotokea sasa ni msukumo wa baadhi ya vyombo vya usalama na hayakuanza leo.”
Kauli yake ilionekana kutoa ufafanuzi wa hatua ya Kamati Kuu ambayo ilimvua nyadhifa zake zote aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na wenzake wawili kwa madai ya kuandaa waraka kuhamasisha mabadiliko hatua iliyosababisha mvutano mkubwa ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

yatima hatarini kufanyiwa ukatili wa kijinsia-UNICEF:


Jennifa Chiwute
Mwakilishi wa Mitandao ya Kijamii nchini (CCT), Jennifa Chiwute
Watoto yatima nchini  wako hatarini  kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ilikinganishwa na kundi la wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.
Akizungumza jana katika  mdahalo  ulioandaliwa na mtandao wa kupinga ukatili wa kijinsia (MKUKI) ulioratibiwa na  Shirika la Kupinga Ukatili wa Kijinsia Tanzania (AFNET)Kanda ya Kati uliofanyika mjini hapa, Mwakilishi wa Mitandao ya Kijamii nchini (CCT), Jennifa Chiwute, alisema  taarifa ya  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa mwaka 2009 kuhusiana na vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini,  imeonyesha kundi hilo la watoto yatima liko kwenye hatari zaidi ya kufanyiwa vitendo hivyo kwa kuwa wengi wao hawana ulinzi kutoka kwa mtu yeyote.
Akiwasilisha mada kuhusiana na mpango wa kukomesha vitendo hivyo, Chiwute,  alisema taarifa hiyo ilionyesha kuwa asilimia 30 ya wasichana na asilimia 14.3 ya wavulana,  waliwahi kutendewa kitendo kimoja cha ukatili wa kijinsia kabla ya kufikisha umri wa miaka 18 huku asilimia 60 ya wasichana walilazimishwa kujamiina.
Alibainisha  pia inaonyesha kuwa wasichana hao walilazimishwa kujamiiana na ndugu,  jirani, marafiki na watu wasiowafahamu wenye umri mkubwa.
“Waathirika wenyewe wanafanyiwa kwenye maeneo ya nyumbani kwa mtu, shuleni au njiani wakati wa kwenda au wa kurudi shuleni,” alisema Chiwute.
Alisema vitendo hivyo ni pamoja  na ukatili wa kipigo, ukeketaji, kingono na kiakili.
Alionya kuwa iwapo vyombo vya dola havitachukua hatua za kisheria kwa wanaotenda vitendo hivyo, hali itazidi kuwa mbaya zaidi kwa siku zijazo.
“Vyombo vya serikali vimeshindwa kusimamia kwa dhati utekelezaji wa sheria zinazolinda haki za wanawake, watoto na watu wenye ulemavu kwa sababu ya rushwa,”alisema Chiwute.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa  AFNET Tanzania,  Sarah Mwaga, alisema ni wajibu wa wadau wote na watetezi wa haki za binadamu kuungana kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vina madhara makubwa kwa watendewa.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Dawati la Jinsia Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, Hamida Hiki, alisema kuwa jeshi hilo linakabiliwa na changamoto ya jamii kuwa na mfumo dume ambao ndiyo chanzo cha vitendo vya ukatili ambavyo vinasababisha wimbi la watoto wa mazingira hatarishi mitaani.

MTANI JEMBE DESEMBA 21 UWANJA WA TAIFA.

2037137_orig 
Dar es Salaam: Mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Simba na Yanga zinazodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itachezwa Jumamosi, Desemba 21, 2013 saa kumi kamili jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe amesema “Tayari Simba na Yanga zimesaini makubaliano ya kucheza MECHI YA NANI MTANI JEMBE (NANI MTANI JEMBE MATCH). Pambano hili  ni zawadi ya kufungia mwaka kwa mashabiki na kila timu imetia sahihi makubaliano kwamba itachezesha kikosi cha kwanza ili kuwapa mashabiki burudani ya uhakika.”
Kavishe aliongeza kuwa mechi hii ni maalum kwa ajili ya kuhitimisha kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo imeendeshwa kwa zaidi ya miezi miwili ikiwapa fursa mashabiki wa timu hizi kuchangia timu zao kila wanapoburudika na bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Kilimanjaro Premium Lager   ilitenga kiasi cha shilingi milioni 100 zinazoshindaniwa na Simba na Yanga kupitia mashabiki wake na tarehe 21 Desemba ndio utakuwa mwisho wa kampeni ya Nani Mtani Jembe ambapo baada ya mechi  fedha hizo zitagawanywa kwa kila timu kulingana na matokeo ya kura za mashabiki na klabu zitajiamulia namna ya kutumia fedha hizo.
Kampeni hii imeleta msisimko mkubwa sana kati ya mashabiki na hadi sasa matokeo ya kampeni hii yanaonyesha kwamba Yanga wanaongoza wakiwa na kiasi cha shilingi milioni 76 huku Simba wakiwa na kiasi cha shilingi milioni 24
Mashabiki wa Simba na Yanga wanaoshiriki katika kampeni ya Nani Mtani Jembe wanaendelea kunufaika zaidi na zawadi kabambe zilizoandaliwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager ili kuongeza msisimko na ushiriki katika kampeni hiyo ambapo mashabiki watatu wa Simba na mashabiki watatu wa Yanga wanajishindia kiasi cha shilingi 300,000/= kila mmoja katika droo zinazofanyika mara moja kila wiki. Droo kubwa itafanyika tarehe 21 Desemba.  Ambapo katika droo hiyo kubwa shilingi milioni 6 zitatolewa kama zawadi kwa washindi wawili –  mmoja shabiki wa Yanga na mwingine shabiki wa Simba ambapo kila mmoja atajishindia shilingi milioni tatu.

mkataba wa ubia wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite wawekwa hadharani

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi (kushoto)  akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jana (leo) mjini Dar es salaam wakati wa halfa fupi ya kusaini hati za mkataba wa ubia  kuhusu uchimbaji  wa pamoja wa madini ya Tanzanite katika kitalu c kwenye eneo la Mererani kati ya Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na TanzaniaOne . wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)Gray Mwakalukwa (katikati) na  Mwenyekiti wa  Kampuni ya Madini ya TanzaniaOne(kulia ) Balozi Ami Mpungwe.

badilishanaMkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)Gray Mwakalukwa (kushoto) na  Mwenyekiti wa  Kampuni ya Madini ya TanzaniaOne(kulia ) Balozi Ami Mpungwe  wakibadilishana hati za mkataba wa ubia  kuhusu uchimbaji  wa pamoja wa madini ya Tanzanite katika kitalu c kwenye eneo la Mererani. Sherehe hizo zilifanyika jana mjini Dar es salaam.
Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO_Dar es salaam

Lukuvi Kuwa Mgeni Tamasha la Krismasi Dar es Salaam.

William Lukuvi 
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Krismasi Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Desemba 25 mwaka huu.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa maandalizi kuhusiana na tamasha hilo yanaenda vizuri.
“Hamasa imekuwa kubwa pengine kuliko matamasha mengine ambayo Kampuni yangu ya Msama Promotions imewahi kuyaandaa. Waimbaji wanatamani siku ifike wafanye mambo, mashabiki nao wanatamani siku ifike waone mambo.
“Pia nafurahi kuwajulisha kuwa Waziri Lukuvi amekubali kuwa mgeni rasmi Desemba 25 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, naamini siku hiyo itakuwa burudani ya aina yake. Namshukuru sana kwa kuungana nasi,” alisema Msama, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Tamasha la Pasaka.
Alisema kiingilio cha chini katika tamasha hilo kwa upande wa Uwanja wa Taifa kitakuwa sh. 5000 na viingilio vingine vitakuwa sh 10,000 na sh.20,000 kwa majukwaa maalum A na B.
“Pia watoto watachangia sh. 2,000, tumeweka viingilio vya kawaida ili wote tuweze kuhudhuria Uwanja wa Taifa,” alisema Msama na kuongeza kuwa kwa mikoani viingilio ni sh 5,000 kwa wakubwa na watoto itakuwa Sh 2,000.
Waandaaji hao wamepanga tamasha hilo lifanyike Desemba 25 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na siku inayofuata Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, kisha Desemba 28 Uwanja wa Mkwakwani Tanga na Desemba 29 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

TANZANIAONE , STAMICO KUSHIRIKIANA

badilishana 
Na Kiza Sungura- MAELEZO_Dar es salaam
Shirika la Madini la Taifa [STAMICO] limeingia mkataba wa ubia na Kampuni ya TanzaniteOne Mining Limited [Tanzanite One] kuhusu uchimbaji wa pamoja wa madini, ya Tanzanite katika kitalu C, Mirerani.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO Gray Mwakalukwa wakati akitoa ufafanuzi kwa  waandishi wa habari mara baada ya hafla fupi ya kusaini mkataba huo.
Mwakalukwa alisema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini kutoa leseni ambayo inawawezesha STAMICO  kumiliki asilimia 50 na TanzaniaOne watabaki na  asilimia 50.
Alisema kuwa umiliki huo unatokana na Serikali kusimamia utekelezaji wa Sera ya Madini ya mwaka 2009 na Sheria ya Madini ya mwaka 2010 ambapo chini ya sharia hiyo, Kampuni za kigeni haziruhusiwi kumiliki hisa zaidi ya asilimia 50 katika uchimbaaji wa vito.
Mwakalukwa aliongeza kuwa mkataba huo umezingatia makubaliano ya awali yaliyotiwa saini mapema mwaka huu ambayo yataka STAMICO na Tanzanite One kuwa  na gawio sawa la asilimia 50 kwa hamsini litakalotokana na faida.  
Alitaja baadhi ya mambo waliokubaliana ni pamoja na mitambo ya uchimbaji na uzalishaji itabaki kuwa ni mali ya Tanzanite One itaendelea  kutumika na wabia wataifanyia matengenezo itakapoharibika.
Mwakalukwa alisema kuwa jambo jingine waliokubaliana ni pamoja na kuanzisha kitengo maalum cha ufuatiliaji na tathmini ya shughuli zote za mgodi kitakachoundwa kutoka kwa wajumbe wa kila pande.
Naye Mwenyekiti wa Tanzanite One, Balozi  Ami Mpungwe alisema kuwa hatua ya Kampuni yake kusaini  mkataba huo ni sehemu ya  kutekeleza sera ya uchimbaji  wa madini nchini na ni  hatua nzuri  ya  kuhakikisha ulinzi na usalama madini ya Tanzanite. 

Siku ya Kitaifa ya Maadhimisho Haki za Binadamu yanatarajiwa kufanyika Desemba 10 mwaka huu.

Pichani wadau wa  Haki za binadamu wakifuatilia kwa makini taarifa ya Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora( hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
PIX4-1 
Mwandishi wa habari wa ITV  Ufoo Saro akiuliza swali wakati wa mkutano  wa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Frank Shija – Maelezo

SHEREHE ZA KUTUNUKIWA UZAMILI CHUO KIKUU CHA SAUT MWANZA

Lt. Col. Ludwino Mgumba, (left) Deputy Commissioner General, Fire and Rescue Force; Gabriel Nderumaki (centre) Acting Managing Editor, State-owned Tanzania Standard Newspapers, publishers of Daily News, Habari Leo and Sport Leo newspapers;  and Imani Lwinga (right), Communications Manager , Serengeti Breweries Limited shares a right moment after being conferred with MA degrees in Mass Communication at St. Augustine University of Tanzania, Mwanza on November 30, 2013.
/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-qformat:yes;
mso-style-parent:”";
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin-top:0in;
mso-para-margin-right:0in;
mso-para-margin-bottom:10.0pt;
mso-para-margin-left:0in;
line-height:115%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,”sans-serif”;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-fareast-font-family:”Times New Roman”;
mso-fareast-theme-font:minor-fareast;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-bidi-font-family:”Times New Roman”;
mso-bidi-theme-font:minor-bidi;}
Serengeti Breweries Limited Communications Manager Imani Lwinga (left) in jovial mood with Shukuru Senkondo (2nd right), Joseph Jackson Gahima (2nd  left) and Paul Gyuna (left) after being conferred with degrees of Master of Arts in Mass Communicatio.
 Imani Lwinga of Serengeti Breweries (left) with Shukuru Senkondo, Christina Njovu, Paul Gyuna and Joseph Jackson after getting their MA in Mass Communications
 St. Augustine Alumni Christina Njovu of National Electoral Commission, Wilson Malosha of Ministry of Indutry and Trade, Lt. Col. Ludwino Mgumba of Fire and Rescue Force, Shukuru Senkondo and media editor/consultant, Joseph Jackson Gahima of Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) and Imani Lwinga of Serengeti Breweries Limited after getting their MA degrees in Mass Communications
 Imani Lwinga (right) of Serengeti Breweries Limited, Wilson Malosha (centre) of Ministry of Industry and Trade and Christina Njovu of National Electoral Commission pose for a photo after receiving their MA degrees in Mass Communications at St. Augustine University of Tanzania in Mwanza on 30th November 2013.
Lulu Musa (left) Information Officer in the Vice President’s office – Environment; Gabriel Nderumaki  (centre), Acting Managing Editor, Tanzania Standard Newspapers and Hoyce Temu, Communication Analyst at United Nations office in Tanzania pose for souvenir photo after receiving their MA degrees in Mass Communicatio.

MOI kutumia zaidi ya bilioni 17 katika ujenzi wa jengo jipya la kisasa


Meneja Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bw. Jumaa Almasi akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) Mipango mbalimbali ya Taasisi hiyo ikiwamo utekelezaji wa awamu ya tatu ya MOI (MOI Phase III) itakayosaidia kuboresha huduma za afya nchini,kulia ni Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Patrick Mvungi na kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bw. Frank Mvungi.

Meneja Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bw. Jumaa Almasi akionesha kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) Picha ya sehemu ya kichwa iliyowekewa kifaa maalum(Mayfield Clamp). kulia ni Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Patrick Mvungi.
Na Frank Mvungi
Taasisi yaTiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) imepanga kutumia zaidi ya Bilioni 17 katika ujenzi wa awamu ya Tatu ya Mradi wa Taasisi yaTiba ya Mifupa   na Mishipa ya Fahamu (MOI phase 111) hadi mradi huo utakapokamilika mapema mwakani.
Hayo yamesemwa leo na Meneja Uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Jumaa Almasi wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Almasi alisema kuwa Ujenzi wa jengo hilo jipya lenye ghorofa 7 ambao unaendelea ukikamilika utaongeza maeneo ya kutolea huduma,Vitanda vitafikia 380 kutoka 159 vilivyopo sasa hali ambayo itapanua wigo wa huduma zinazotolewa kwa sasa.
“Mradi huu utasaidia kuongeza ufanisi na huduma zinazotolewa na taasisi kwani ukikamilika utaongeza maeneo ya kutolea huduma kwa kupunguza msongamano wa wagonjwa mawodini kutokana na kuongezeka kwa vitanda kutoka 159 hadi kufikia 380” Alisema Almasi.
Aliongeza kuwa huduma nyingine zitakazotolewa  ni CT SCAN,MRI,huduma za Cybernife na Digital Antiograph ambazo kwa Sasa hazitolewi katika Taasi  hiyo .
Alibainisha kuwa MOI ni moja ya Taasisi  zenye vifaa bora vya upasuaji pamoja na vyumba vya upasuaji vinavyokikidhi viwango vya kimataifa kusini mwa jangwa la Sahara baada ya Afrika ya kusini.
Alisema kuwa hali hiyo ni matokeo ya juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika kuboresha huduma za afya nchini ambapo wameweza kupatiwa vifaa vya kisasa pamoja na wataalamu waliobobea katika  huduma za tiba ya mishipa ya fahamu na upasuaji wa uti wa mgongo.
Bw. Almasi  alibainisha kuwaTaasisi ya MOI imeendelea kushirikiana na Taasisi za Kimataifa  zinazotoa huduma za afya kama SIGN GROUP  ya  nchini Marekani  ambayo imekuwa ikitoa msaada wa vifaa tiba ikiwa ni alama ya ushirikano mzuri uliopo kati ya Taasisi hiyo na mashirika ya Kimataifa.