Masasi.
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa amemmwagia
sifa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa kuwa ni kiongozi
aliyeliongoza taifa kwa uadilifu na umakini.
Lowassa
aliyasema hayo mwishoni mwa wiki mjini Masasi mkoani Mtwara katika
harambee ya kuchangia shughuli za maendeleo za Ushirika wa Mama wa
Kikristo (UMAKI) katika Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Masasi,
“Nimefika
hapa kwa heshima. Nimefika hapa Masasi kutokana na kwamba wilaya hii
imetoa kiongozi, Rais Benjamin Mkapa aliyeliongoza taifa kwa umakini,
uadilifu na ushupavu mkubwa.
Lowassa
ambaye wakati wa uongozi wa Serikali ya Mkapa alikuwa Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) kabla ya kupelekwa
Wizara ya Maji na Mifugo, alisema lazima Watanzania wampe heshima yake
na kumuenzi kutokana na kile alichokifanya kwa Taifa.
Mbali
na hayo, Lowassa alisema yuko tayari kushirikiana na mtu yeyote mwenye
nia ya dhati ya kupambana kuondoa umaskini katika jamii kwa kuwa yeye ni
mdau wa wanaopambana na kuondoa umaskini katika jamii.
“Mtu
yoyote anayepambana na kuondoa umaskini katika jamii, kwa kweli mtu huyo
niko tayari kushirikiana naye katika harambee za harakati hizo,”
alisema Lowassa na kuongeza kuwa wanawake ni jamii inayochukia umaskini.
“Wanawake
ni wadau wakubwa katika kupambana na umaskini, na ndiyo maana chama
changu cha CCM katika Rasimu ya Katiba Mpya inataka kuwe na asilimia 50
kwa 50 ya uwakilishi bungeni na kwamba chama hicho kinawathamini sana
kinamama wote nchini.
Aidha,
katika harambee hiyo, zaidi ya Sh103 milioni zilipatikana huku marafiki
zake wakichangia Sh10 millioni na kuvuka lengo ambalo lilikuwa Sh100
milioni.
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment