Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
HATIMAYE
`Deal Done`!!. Wekundu wa Msimbazi Simba Sc, Taifa Kubwa wamehalalisha
kuondoka kwa kipa wake Mganda, Abel Dhaira baada ya leo hii kumsajili
mlinda mlango wa zamani wa Dar Young Africans, raia wa Ghana, Yaw Berko
kwa mkataba wa miezi 6.
Berko
ametua leo jijini Dar es salaam na pipa akitokea kwao Ghana,
(Magharibi mwa Afrika) na amekuja kufanya kazi na kocha mpya wa klabu ya
Simba, Mserbia Zdravko Lugarusic ambaye pia mchana wa leo amesaini
mkataba wa miaka miwili kurithi mikoba ya kocha, Abdallah Athuman Seif
`King Kibadeni Mputa` aliyabebeshwa virago kwa madai ya kushindwa
kufanya vizuri mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Kusajili
wa kwa Berko kumekalimisha safari ya Dhaira kufanya kazi Msimbazi kwani
tayari uongozi wa klabu hiyo ulishaondoa imani juu ya kipa huyo wakidai
kiwango chake hakiridhishi, kwani amekuwa akifungwa mabao mepesi sana.
Vita
kama kawa: Berko kamwaga wino leo Msimbazi, mpinzani wake wa wakati
ule akiwa Yanga, Juma Kaseja amejiunga na wanajangwani dirisha dogo la
usajili, kutokana na ubora wa makipa hawa wawili, upinzani mkali
unategemewa
Kipa
huyo aliwadakia watani wa jadi wa Simba, Dar Young Africans tangu mwaka
2010 baada ya kujiunga katika dirisha dogo mnamo desemba mwaka 2009
akitokea kufanya kazi na klabu ya Ghana ya Liberty Proffessionals .
Berko
alifanya kazi na Yanga hadi msimu uliopita alipotolewa kwa mkopo
kwenda kufanya kazi yake katika klabu ya FC Lupopo ya DRC Kongo.
Baada
ya kufika mjini Lubumbashi, Berko alizingua kufanya kazi na kuamua
kurejea jijini Dar es salaam kujiunga na Yanga kwa madai ya
kutoridhishwa na hali ya klabu hiyo , lakini uongozi ulimtupilia mbali
kwa kuuvunja mkataba wake na kumlipa `Mtonyo` wake kwani tayari wakati
huo walikuwa wameshapata kipya mpya Ally Mustapha ` Bartez` aliyetokea
Simba na Berko akapaa angani kurejea kwao Ghana.
Tanzania One: Mlinda Mlango mpya wa Yanga, Juma Kaseja ataendelea kupambana na kipa mwenzake bora, Yaw Berko wa Simba.
Wakati
Berko akiidakia Yanga, mpinzani wake langoni alikuwa kipa wa zamani wa
Wekundu wa Msimbazi Simba sc, Juma Kaseja ambaye aliachwa na Simba msimu
uliopita, lakini upinzani unaendelea tena baada ya Kaseja `Tanzania
One` kujiunga na Yanga na leo hii ameanza mazoezi katika uwanja wa Bora
kijitonyama, jijini Dar es salaam.
Kusajiliwa
kwa Kaseja Yanga, kumemkutanisha tena na makipa wenzake wawili aliowahi
kuwakalisha benchi kwa muda wote wakiwa Simba, Ally Mustapha `Bartez`
na Deogratius Munish `Dida`.
Tusubiri maamuzi ya benchi la ufundi la Yanga chini ya kocha Mholanzi, Ernie Brandts kuamua ni kipa gani atakuwa chagua lake.
Leo
hii katika mazoezi ya Yanga, makipa hao Bartez na Kaseja walikuwa
kivutio walipokuwa wakifanya mazoezi pamoja chini ya kocha wa Makipa,
Mkenya Razack Ssiwa
No comments:
Post a Comment