Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mpango wa Taifa wa
Kudhibiti Ukimwai, chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt.
Angela Ramadhan, wakati alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonyesho
katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, yaliyofanyika kwenye
Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Kaimu Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantum Mahiza, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume
ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dkt. Fatma Mrisho. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahi
na mtoto Samir Isagetee (miezi 7) akiwa na Mama yake, Lilian Amani,
wakati alipotembelea katika Banda la Watu wanaoishi na Virusi vya
Ukimwi NACOPHA, katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani,
zilizofanyika leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Mtoto huyo ni mmoja kati ya watoto waliozaliwa na wazazi wenye
maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na yeye kuzaliwa salama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea mabanda katika maadhimisho hayo.
Baadhi ya wanafunzi wakipita na mabango yenye ujumbe mbalimbali mbele ya Jukwaa
Kuu, wakati Makamu alipokuwa akipokea maandamano hayo kwenye
maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,
jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia
wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, kwenye
Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Mpango Mkakati wa 3 wa
Kitaifa wa Kudhibiti Ukimwi (NMSF3), wakati wa sherehe za Maadhimisho ya
Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii, Dkt. Seif Rashid, (wa pili kulia) ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Mwantum Mahiza, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi
Tanzania, Dkt. Fatma Mrisho.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi. Picha Zote na OMR
No comments:
Post a Comment