MAANDALIZI
ya kombe la Mapinduzi linalotarajia kuanza kutimua vumbi januari mosi
mwakani yanakwenda vizuri na timu zote zilizothibitisha kushiriki
zinatarajia kuwasili desemba 31 mwaka huu.
Msemaji
wa kamati ya mashindano , Farouk Karim amesema kuwa timu za Tusker fc,
AFC Leopard za Kenya, KCC, URA za Uganda , Simba sc, Yanga, Azam fc na
Mbeya City za Tanzania bara tayari zimeshathibitisha kushiriki na kamati
ya maandalizi imeshakamilisha taratibu za kuzipokea.
SIMBA
imepangwa kufungua pazia la michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kucheza
na AFC Leopards ya Kenya Januari Mosi wakati Yanga wakishuka dimbani
siku inayofuata kuikabili Tusker FC.
kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Italia, Cesare Prandelli.
Karim
amesema mgeni rasmi katika mechi ya ufunguzi itakayopigwa januari mosi
majira ya saa mbili usiku katika uwanja wa Aman kisiwani Unguja baina ya
Simba sc dhidi ya AFC Leopard ya Kenya atakuwa kocha mkuu wa timu ya
Taifa ya Italia, Cesare Prandelli.
Pambano
la Simba na Leopards litatanguliwa na mechi kati ya wenyeji KMKM na KCC
ya Uganda litakalopigwa saa 10 jioni kwenye uwanja huohuo.
“Ninavyozungumza
na wewe muda huu, Prandelli yupo hapa Zanzibar mapumzikoni na tayari
amekubali kufungua michuano hii yenye maana kubwa katika miaka 50 ya
mapinduzi ya Zanzibar”. Alisema Karim.
Kikosi cha Simba sc
Karim alisema katika michuano ya mwaka huu viwanja viwili vitatumika ambavyo ni Gombani kisiwani Pemba na Aman Kisiwani Unguja.
“Uwanja
wa Gombani upo katika hali nzuri na unavyojua una nyasi za bandia.
Uwanja wa Aman umefanyiwa ukarabati mkubwa na hivi sasa wataalamu kutoka
China wapo hatua za mwisho kabisa kukamilisha shughuli yao”. Alisema
Karim.
Mratibu
huyo alitoa wito kwa wadau, wapenzi wa soka visiwani Zanzibar
kujitokeza kwa wingi kwani kamati ya mashindano inategemea mapato ya
milangoni kufanikisha mipango.
“Michuano
hii inagharimu zaidi ya shilingi milioni 600, hatuna fedha hizo,
tunategemea mapato ya milangoni, hivyo mashabiki kufika kwao kwa wingi
ndio mafanikio yetu”. Aliomba Karim.
AFC Leopard
Aidha
ameziomba taasisi na makampuni ya bara na visiwani kujitokeza kufanya
matangazo katika michuano hiyo ili angalau wapate pesa za kuendeshea
michuano hiyo.
Michuano
iliyopita, Azam fc walitwaa ubingwa, lakini mwaka huu kuna changamoto
mpya hasa kutokana na uwepo wa timu za Dar Young Africans na Mbeya City
ambazo hazikushiriki.
Mechi
zote za hatua ya makundi na robo fainali zitafanyika kwenye viwanja wa
Gombani Pemba na Aman Unguja, wakati nusu fainali na fainali zitapigwa
kwenye Uwanja wa Aman.
Katika
michuano iliyopita Simba waliishia nusu fainali baada ya kuondolewa na
Azam FC kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya mechi kumalizika kwa sare ya
2-2 hata baada ya kuongezwa dakika 30.