Mwenyekiti
Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba akizungumza
na waandishi wa Habri jijini Dar es Salaam jana wakati akitoa tamko la
kulaani kwa kitendo cha Naibu Spika wa Bunge la Muungano wa Tanzania,
Job Ndugai kuwanyanyasa na kuwazalilisha Wabunge wa upinzani akiwepo
Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe. Picha na
Venance Nestory
…………………………………………………………………………………
Dar
es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim
Lipumba ameitaka Serikali kutafuta ufumbuzi wa haraka wa matatizo ya
kiuchumi, kwa kuwa hali ilivyo sasa ni mbaya.
Profesa Lipumba ambaye pia ni
profesa wa uchumi alisema hivi karibuni Dar es Salaam kuwa hali ya
uchumi imezidi kudorora na kusababisha maisha ya wananchi wengi kuwa
magumu.
“Vijana wa siku hizi wengi
hawana simile kushughulika na mambo yanapokwenda sivyo, ajabu ni kwamba
wanaofanya mambo hayo yawe magumu wamekuwa wepesi wa kutetea kwa hoja
zisizo na msingi kwa masilahi yao binafsi,” alisema.
Akizungumzia maazimio
yaliyofikiwa kwenye Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF
kilichofanyika Desemba 21-22 mwaka huu Dar es Salaam, alisema hatua ya
kupandishwa kwa gharama za umeme iliyotangazwa hivi karibuni na Shirika
la Umeme Tanzania (Tanesco) ni miongoni mwa mambo ambayo yanaendelea
kuongeza ugumu wa maisha kwa wananchi, jambo ambalo lingeweza kuzuilika
kwa shirika hilo kudhibiti wizi wa nishati hiyo.
Kuhusu hali ya kisiasa nchini,
Profesa Lipumba alisema Baraza Kuu limetoa wito kwa vyombo vya Dola kuwa
na weledi na uadilifu na kuacha kutekeleza amri za wanasiasa zisizojali
utawala wa sheria na haki za binadamu ili vipunguze uhasama baina yao
na raia.
“Serikali pia isitumie Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kushughulikia masuala ya uvunjifu wa
sheria katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, badala yake kazi hiyo
ifanywe na Jeshi la Polisi kwa mujibu wa taratibu za kisheria. Nao pia
waongezewe uwezo wa kiutendaji,” alisema.
Alisema
CUF inaona si vyema kutumia JWTZ kudhibiti vurugu kwa kuwa wanajeshi
hao hawana mafunzo ya kukamata wananchi wenye tuhuma za uhalifu
isipokuwa wamefundishwa jinsi ya kulinda usalama wa nchi katika mipaka.
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment