TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, September 21, 2013

HAPPINESS WATIMANYWA AIBUKA KIDEDEA REDD'S MISS TANZANIA 2013.

Redd's Miss Tanzania 2013,Happiness Watimanywa akipungia mkono mara baada ya kutangazwa mshindi wa Taji hilo kwa mwaka huu.Kushoto ni mshindi wa pili,Latifa Mohamed na kushoto ni mshindi wa tatu,Clara Bayo.
 Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakiwa jukwaani usiku huu wakati wa Onyesho la Taifa la Urembo linalofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakifungua shindano la mwaka huu kwa kuonyesha ufundi wao wa kucheza muziki. Shindano la mwaka huu ambalo limedhaminiwa na kampuni ya vinywaji Tanzania.Tanzania Breweries Limited kupitia kinywaji cha Redds limefanyikia katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar-es-salaam. Jumla ya warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali,vyuo nk wameshiriki.

 Warembo walioingia hatua ya kumi na tano bora. 
 Jaji Mkuu wa Shindano la Redd's Miss Tanzania,Dkt. Ramesh Shah akitangaza Warembo walioingia hatua ya tano bora.
Warembo walioingia hatua ya tano bora,toka shoto ni Happiness Watimanya,Elizabert Peter,Clara Bayo,Lucy Tomeka pamoja na Latifa Mohamed.
 Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakipita jukwaani na mavazi ya aina mbali mbali wakati wa Onyesho la Taifa Redd's Miss Tanzania 2013 linalofanyika usiku huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam usiku huu. 
Mwanamuziki Mkongwe wa Muziki wa Kizazi kipya hapa nchini,Lady Jay Dee akitoa burudani kwenye Onyesho la Redd's Miss Tanzania 2013,linalofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam. 
(Picha Kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania). 

Cincinnati fans revolt against use of Katy Perry song to introduce Bengals, so team dumps it

ew gallery
.
When you think about the tough men who made the NFL what it is, and getting fired up for a huge game against a rival, only one name comes to mind: Katy Perry.

Or, not. But someone in the Bengals' office decided that Perry's hit "Roar" would work perfectly for their games, including as the song to introduce the team. Bengals? Roar? Get it? Yeah.
This was not thought out that well. There has to be some context. Metallica is fine. "Until It Sleeps" by Metallica just before NFL game is not. To the surprise of nobody, Bengals fans were quite unhappy with the pop star's anthem, which played before, during and after its home opener against Pittsburgh on Monday night.
It's a nice enough song if you're a 12-year-old girl, but I would have paid good money to see James Harrison's reaction when he heard it playing over the stadium speakers.

VITA NI VITA MULA: HUKO ENGLAND NI MPAMBANO KATI YA YAYA TOURE WA CITY NA MAROUANE WA UNITED

Viungo Yaya Toure wa City ataonyeshana ufundi na Marouane Fellaini wa United kesho kwenye uwanja wa Etihad.
Manchester, England. Mashabiki wa Manchester United wamefanikiwa kumpata Marouane Fellaini na kiungo huyo wa Ubelgiji ameonyesha kiwango cha juu kwa kutoa pasi nzuri na kunyang’anya mpira wakielekea katika mchezo wa kesho dhidi ya mahasimu wao City. Mabingwa wa msimu uliopita na washindi wa pili wanakutana kwenye Uwanja wa Etihad, wakiwa na rekodi ya ushindi waliopata katikati ya wiki katika Ligi ya Mabingwa.
Mshambuliaji wa Wayne Rooney amerudi kwenye kiwango chake na Jumanne alifunga mabao mawili wakishinda 4-2 dhidi ya Bayer Leverkusen, lakini uwepo wa Fellaini katika nafasi ya kiungo aliyeonyesha uwezo mzuri wa kumiliki mpira umeongeza ladha ya mchezo wa kesho. Wapinzani wao City baada ya kupoteza dira katika ligi katikati ya wiki walishinda 3-0 dhidi ya Viktoria Plzen katika Ligi ya Mabingwa, ushindi unaomfanya kocha Manuel Pellegrini kuamini kwamba umerudisha kujiamini kwa wachezaji wake.
“Tuna mechi ngumu Jumapili na ushindi wa ugenini katika Ligi ya Mabingwa tena wa mabao matatu, nafikiri umerudisha kujiamini kwa wachezaji.” Kiungo wa City,Yaya Toure, ambaye ni kama Fellaini ameonyesha kiwango cha juu, cha kutengeneza magoli na uwezo mkubwa wa kusoma mchezo, pia alifunga bao moja dhidi ya Plzen na kesho inategemewa itakuwa ni vita kubwa kati ya viungo hao wawili.
Hii ni mechi ya kwanza ya miamba ya Manchester kukutana wakati timu zote zikiwa na makocha wapya ambao wanajua kuwa City imekusanya pointi 10 kutoka kwa United katika michezo saba ya ligi waliokutana katika misimu mitatu iliyopita.
KUJIULIZA UPYA
Liverpool walioanza kwa kishindo msimu huu wakiongoza kwa pointi 10, leo watakuwa wenyeji wa Southampton, lakini watamkosa kiungo wao Philippe Coutinho aliyeumia bega na atakuwa nje ya uwanja hadi mwezi ujao. Tegemeo lao litabaki kwa Daniel Sturridge ambaye amefunga bao kila mechi aliyocheza msimu huu, kabla ya kurejea kwa mshambuliaji wa Uruguay, Luis Suarez anayemaliza kifungo chake cha mechi 10, baada ya mchezo wa leo.
Baadaye leo, Chelsea watawakaribisha Fulham huku wakiwa na kumbukumbu ya vipigo viwili mfululizo kutoka kwa Everton wiki iliyopita pia walichapwa nyumbani na Basel katika Ligi ya Mabingwa.

MISS TANZANIA KUPATA MWAKILISHI WA DUNIA LEO

Mashindano ya 20 ya kumsaka mrembo bora wa Tanzania maarufu kwa jina la Miss Tanzania inafanyika leo jijini Dar es Salaam ikishirikisha warembo 30. Miss Tanzania, mashindano yaliyoanza mwaka 1994 ndiyo mashindano makubwa zaidi nchini ya urembo yanayoanzia ngazi za chini hadi yanafikia ngazi ya taifa ambayo yanafanyika leo.
Pamoja na miaka mingi ya kufanyika kwa mashindano hayo bado Tanzania imekuwa haifanyi vizuri katika mashindano ya kumtafuta mrembo bora wa dunia, Miss World. Ni mwaka 2005 tu ndiyo bendera ya Tanzania ilipeperushwa vyema katika mashindano ya Miss World kwa Nancy Sumari kufanya vyema na kuwa mrembo bora wa Bara la Afrika.
Kwa hiyo, wakati mashindano hayo yakifikia kilele leo tunaamini kwamba ni wajibu wa majaji wa mashindano hayo kufanya kazi yao kwa weledi ili kuipatia Tanzania mrembp bora. Ni vyema mrembo atakeyachaguliwa kuvaa taji la Miss Tanzania awe ana sifa za kutosha na vigezo vikubwa zaidi kuliko washiriki wengine kiasi kwamba akichaguliwa hakuna mtu
atakayethubutu kulalamika. Tungependa apatikane mshindi ambaye atakuwa na uwezo wa kuiwakilisha vyema Tanzania katika mashindano ya urembo ya dunia na kuing’arisha nchi katika mashindano hayo. Kufanya vizuri kwa mrembo wetu katika mashindano hayo ya dunia kutasaidia kuitangaza nchi yetu duniani jambo ambalo linaweza kusaidia katika kukuza utalii na kuimarisha uchumi wetu. 
Kwa utaratibu wa sasa mrembo atakayetwaa taji la Miss Tanzania leo atakuwa na kipindi cha mwaka mmoja kabla ya kushiriki mashindano ya Dunia ya Miss World. Kipindi hicho ni kikubwa ikiwa waandaji wa mashindano ya Miss Tanzania kama watataka kukitumia vyema kwa kumwuandaa mrembo huyo kabla ya kwenda kwenye mashindano ya Miss World.
Ikiwa waandaaji na wadhamini wa mashindano hayo watakuwa makini wana muda wa kutosha wa kumwuongezea ujuzi na uwezo Miss Tanzania kabla ya kupanda jukwaani katika mashindano ya dunia. Tunashauri ili kumjengea uzoefu Miss Tanzania apelekwe kwenye mashindano ya mwaka huu ya Miss World ambayo Tanzania itawakilishwa na Brigitte Alfred aliyetwaa taji la Miss Tanzania mwaka jana.
Mbali na kupenda kuona Miss Tanzania akifanya vizuri katika anga ya kimataifa tunashauri washiriki wote wa mashindano hayo wawe mfano mzuri katika jamii kwa kuishi maisha yenye weledi. Wasichana waliopata nafasi ya kushiriki Miss Tanzania walkionyesha nidhamu ya hali ya juu katika maisha ya kila siku kutatoa fursa kwa wazazi kutokuwa na wasiwasi kwa watoto wapo kushiriki katika mashindano hayo.
Ni wajibu kwa waandaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Lino International Agency kuhakikisha kwamba inawajenga wasichana wanaoshiriki katika mashindano yao kwa kuwapa mbinu za kupambana na maisha ya kila siku. Kwa kufanya hivyo mashindano hayo yatakuwa na faida ya ziada na itakuwa inatoa mfano kwa waliopata nafasi ya kushiriki kwa kuwa raia wema.

. KAYA 10 NGORONGORO KUPATA OFA YA WAZIRI MKUU KATIKA CHAKULA

Ngorongoro. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ametangaza neema kwa wakazi wa Tarafa ya Ngorongoro ya kutoa maguni kumi kwa kila kaya kwa mwaka ili kusaidia wakazi wa eneo hilo kukabiliana na njaa.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Enduleni jana, Waziri Mkuu huyo alisema Serikali imefikia uamuzi huo wa maombi ya wananchi wa tarafa hiyo ya kuomba kuruhusiwa kulima kama njia ya kujikimu kimaisha yakifanyiwa kazi.
Waziri Mkuu alisema Serikali,itakuwa ikitoa gunia tano kwa kila kaya kila baada ya miezi sita na hivyo kaya 20,000 za tarafa hiyo zenye watu 87,000 zitakuwa zikipatiwa magunia 200,000. Eneo hili mnaloishi ni la kipekee dunia kwani limetangazwa ni urithi wa dunia na moja ya maajabu saba ya asili ya Afrika hivyo tunapaswa kulilinda na tukiruhusu kilimo bila kuwa na utaratibu tutaliharibu,”alisema Pinda.
Hata hivyo wakizungumza baada ya ahadi hiyo ya chakula cha bure, wananchi wa tarafa hiyo,walionyesha wasiwasi wao kama ahadi hiyo itatekelezwa kwa kuwa tayari Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamisi Kagasheki aliagiza wapewe chakula bure wakati wa njaa lakini baadaye walitakiwa kununua.
Eliamani Laltaika, William ole Sekei na Nasyera Nangai walisema hawana tatizo na ahadi ya chakula cha bure, lakini uzoefu unaonyesha ni vigumu kutekelezwa kwa kuwa haitawezekana kulishwa kwa maisha yao yote. Ole Sekei alisema kilimo kiliporuhusiwa mwaka 1992 ilitokana na hali ya njaa kama ilivyo sasa na Serikali ilitoa ahadi nyingi lakini hazikutekelezwa .
Waziri mkuu,Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema ahadi hiyo itatekelezwa mara moja sambamba na kuliongezea fedha Baraza la Wafugaji pia kuongezwa fedha za miradi ya maendeleo kutoka Sh5 bilioni hadi kufikia Sh8 bilioni kwa mwaka.

MBUNGE SAME KUNG'OLEWA NA CHADEMA

Same. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza operesheni maalumu ya kumng’oa ubunge, Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi, Dk David Mathayo David katika Uchanguzi Mkuu wa 2015.
Operesheni hiyo iliyopewa jina la “Operesheni Mathayo Out” kwa kifupi OMO ilianza wiki iliyopita kwa kufanya mikutano ya hadhara jimboni humo na itaendelea tena wiki ijayo.
Mmoja wa makamanda wa operesheni hiyo, Gervas Mgonja alisema jimbo hilo limekuwa chini ya himaya ya CCM tangu Uhuru lakini wananchi wake wapo kama wamefunga ndoa na tatizo la maji.
Dk Mathayo ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi alipoulizwa kuhusu operesheni hiyo ya kumng’oa alisema, Chadema ni chama kidogo na hakimnyi usingizi kwa madai uwezo wa kampeni unaishia Himo.

MRAMBA NA SHAHIDI WAKE WALETA MTAFARUKU KISHERIA

Dar es Salaam. Shahidi wa Waziri wa Fedha wa zamani, Basil Mramba, Kamishna wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Felician Busigara, jana alizua mvutano mkali kati ya mawakili wa mashtaka na wale wa utetezi.
Busigara ambaye ni shahidi wa pili wa Mramba, alipanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ili kumtetea Mramba katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka katika ofisi za umma na kuisababishia Serikali hasara.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni, Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona na Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja. Wanakabiliwa na mashtaka ya kuisamehe kodi isivyo halali, Kampuni ya Ukaguzi wa Madini ya Alex Stewart (Assayers) ya Uingereza na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.7 bilioni.
Mvutano huo ulizuka baada ya upande wa mashtaka, kumpinga shahidi huyo, kutoa ushahidi wake kama mtaalamu wa masuala ya kodi, ukidai kuwa upande wa utetezi haukufuata taratibu za utoaji wa maoni kama mtaalamu. Wakati akitoa ushahidi wake huku akiongozwa na Wakili Herbert Nyange, anayemtetea Mramba, Wakili wa Serikali Mkuu, Oswald Tibabyekomya, alikuwa akinyanyuka mara kwa mara na kuweka pingamizi shahidi huyo kutoa ushahidi kama mtaalamu.Mbali na Wakili Tibabyekomya kupinga, mahakama pia ilikuwa ikihoji sababu za shahidi huyo kutoa ushahidi kama mtaalamu.
Akiongozwa na Wakili Nyange, Busigara alidai kuwa sheria ya kodi ya mapato inamtaja mwenye mamlaka ya kusamehe kodi kuwa ni Waziri wa Fedha. “Nyange kuna haja gani ya kumleta shahidi anayezungumzia sheria, sheria zipo katika vitabu, hata wakili unaweza kuzungumzia hizo sheria katika majumuisho yako, mashahidi wako wasituambie kuhusu sheria,” alihoji Jaji Rumanyika.
Shahidi aliendelea kutoa ushahidi kwa kusoma kipengele kimoja cha mkataba kati ya Alex Stewart na BoT, akidai kuwa mkataba huo ulionyesha kwamba atakayelipa kodi ni benki na kampuni itapata fedha yake baada ya kodi.  Jambo lililosababisha Jaji Rumanyika kuingilia tena kati.

SERIKALI KUONGEZA MASHAHIDI KESI YA MAMA LEILA, MAHAKAMA YARIDHIA

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeridhia kuongeza mashahidi wawili muhimu wa upande wa mashtaka katika kesi ya kihistoria ya dawa za kulevya zenye thamani ya Sh225 milioni.
Akitoa uamuzi wake jana kuhusu ombi la upande wa mashtaka, Jaji Grace Mwakipesile alisema anashindwa kuelewa kwa nini upande wa mashtaka ulishindwa kuwasilisha ombi hilo la msingi la kisheria, wakati kesi hiyo ikihamishiwa Mahakama Kuu. “Kinachonishangaza ni upande wa mashtaka kwa makusudi na uzembe walishindwa kuwasilisha maombi hayo ya kuongeza mashahidi wawili, wakati kesi ilipokuwa ikihamishwa,” alisema kwa mshangao Jaji Mwakipesile.
Jaji Mwakipesile aliongeza kuwa: “Kutokana na ukweli kwamba vidhibiti viliorodheshwa na mashahidi wawili walitajwa wakati wa kusikiliza kesi, mahakama hii inachukuliwa ushahidi huo siyo wa kutisha. Na kwa kuwa ushahidi huo ni muhimu katika kesi hii, nakubali ombi la kuwaongeza mashahidi hao kutoa ushahidi,” alisema Jaji Mwakipesile wakati akitoa uamuzi wake. Kesi hiyo inawakabili watuhumiwa tisa akiwamo raia wa Kenya, Mwanaidi Ramadhani Mfundo, maarufu kwa jina la Mama Leila au Naima Mohammed Nyakiniwa.
Mama Leila kabla ya kukamatwa Juni 2011 eneo la Mbezi, Dar es Salaam, pia alikuwa akitafutwa na Serikali ya Marekani kwa makosa kama hayo. Watuhumiwa wengine katika kesi hiyo ni Ben Ngare na Anthony Karanja ambao ni raia wa Kenya na Watanzania watano Sara Munuo, Alma Said, Yahya Ibrahim, Aisha Kungwi na Rajabu Juma.
Mashahidi walioongezwa ni Bertha Mamuya kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, ambaye ndiye aliyezifanyia uchunguzi dawa hizo na kisha kuzifunga, pamoja na Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Neema kutoka Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya ambaye pia ndiye mtunza vielelezo hivyo. Awali wakili wa utetezi, Evod Mmanda alitumia Kifungu cha 289 (3) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kupinga hoja ya upande wa mashtaka ya kutaka kuongeza mashahidi wawili.
“Mheshimiwa Jaji, Prosecution (upande wa mashtaka) waliomba jana ahirisho ili waweze ku- file (kuwasilisha) hicho walichokiomba (taarifa ya kumwongeza shahidi), ruhusa umeitoa leo kwenye uamuzi wako, hivyo walitakiwa wa-file notice yao hiyo baada ya uamuzi wako (wa leo),” alisema na kuongeza:
“Hivyo hakuna notisi halali hapa mahakamani. Notisi halali ni ile watakayoiwasilisha baada ya uamuzi wako. Kwa hiyo sisi tunasema kuwa hadi sasa hakuna notisi halali ya kuita mashahidi wa ziada. “Kama Mahakama yako itaikubali hii wanayoita notisi, ingawa sisi tunasema siyo notisi halali, basi tunaomba Mahakama yako ione kuwa haikutolewa ‘in a reasonable time’ (wakati mwafaka).”
“Hawa wanatajwa kuwepo katika mchakato tangu mwanzo. Mamuya anakiri kupokea kifurushi (bahasha yenye vielelezo) Juni 16, 2011, hadi leo ni miaka miwili na miezi mitatu imepita. Hivyo walijua uwepo wa Mamuya mapema.  Huu si wakati mwafaka,’’ alisema Wakili Mmanda. Hata hivyo, alisema hawana maelezo ya maandishi ya Mamuya wala ya ASP Neema huku akidai kuwa maelezo ya ASP Neema yanaonyesha kuwa yameandikwa Juni 11, mwaka huu wakati hatua ya maelezo ya kesi ilishakamilika.
Akijibu hoja hizo, Wakili wa Serikali, Prosper Mwangamila alidai kuwa katika kesi zote za jinai si jukumu la upande wa mashtaka kuwapatia upande wa utetezi nyaraka mbalimbali wanazokusudia kuzitumia katika kesi, bali Mahakama. “Notisi wanayoitaja iko mahakamani tangu jana, hivyo utaratibu uliotumika wao kupata nyaraka nyingine ndio unaotumika kuwapatia notisi hii. Hivyo hoja ya upande wa mashtaka kuchelewa kuwa ‘serve’ (kuwapatia) haina msingi,” alisema Wakili Mwangamila.
Alisema taarifa hiyo iko mahakamani kisheria kwa mujibu wa Kifungu cha 289 (1) na (2) cha CPA na kuiomba mahakama ione kuwa imewasilishwa katika muda mwafaka.

HUKUMU YA MASOGANGE ,MELISA HII HAPA.

Johannesburg. Mtanzania Agnes Gerald, maarufu Masogange, ameachiwa huru na Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, baada ya kulipa faini ya R30,000 (Sh4.8 milioni) kwa kosa la kubeba kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za kulevya.
Wakati Masogange akitozwa faini hiyo mwenzake, Melissa Edward ameachiwa huru na mahakama hiyo, baada ya kukosekana ushahidi wa kumtia hatiani.Msemaji wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai cha Afrika Kusini(Hawk), Kapteni Paul Ramaloko alisema Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kuonekana kuwa hawakubeba dawa za kulevya, bali kemikali aina ya ephedrine.
Hata hivyo, Mahakama ilibaini kuwa, Melissa hana hatia kwa kuwa ilionekana kuwa amemsindikiza Masogange, ambaye alimwomba amsaidie kubeba mzigo huo.“Mahakama iliona kuwa Melissa aliombwa tu kumsaidia kubeba baadhi ya mabegi, lakini hayakuwa yake. Mizigo yote iliandikwa jina la Agness Gerald na si Melissa,” alisema Kapteni Ramaloko.
Kapteni Ramaloko alisema, Melissa alijitetea kuwa hakuwa amesafiri pamoja na Masogange bali walikutana ndani ya ndege na Masogange alimwomba amsaidie kubeba mizigo hiyo, kwani ilikuwa mikubwa.Kwa sheria za Afrika Kusini kubeba kemikali zozote ambazo zimepigwa marufuku ni kosa la jinai kisheria, hivyo mahakama iliamuru Masogange ahukumiwe kwenda jela kwa miezi 30 (miaka miwili na miezi mitano) au alipe faini ya R30, 000 (sawa na Sh4.8 milioni).
Hata hivyo, Kapteni Ramaloko alisema mdhamini wa Masogange alilipa nusu ya fedha na kwamba zinazobaki amalizie baadaye.Alisema kutokana na kutomalizia kulipa fedha hizo ataendelea kubaki nchini humo hadi atakapomaliza kulipa nusu ya faini iliyobaki.Masogange na mwenzake walipokamatwa na SARS ilielezwa walikuwa wamebeba dawa za kulevya aina ya Methamphetamine, lakini Mahakama juzi ilithibitisha walikamatwa na kemikali aina ya Ephedrine, ambayo siyo dawa za kulevya.
Wakati Kamishna Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Geofrey Nzowa alipoulizwa na Mwananchi Jumamosi juzi alisema mzigo walioubeba Masogange na mwenzake haukuwa ni dawa za kulevya bali ni kemikali za dawa za kulevya, lakini Msemaji wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini, (SARS), Marika Muller alieleza kuwa timu ya SARS ina uhakika kuwa mabegi sita yaliyokamatwa Julai 5 ni dawa za kulevya aina ya Methamphetamine.
Jana, Muller alipoambiwa kuwa Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kulipa faini na mmoja kuachiwa huru kwa kuwa Mahakama imeridhika kuwa hazikuwa methamphetamine bali kemikali aina ya Ephedrine, alirudia tena na kueleza kuwa, mamlaka hiyo ina uhakika na kazi yake na iwapo mahakama imewaachia huru basi yeye hana la kusema zaidi.“Kazi yetu kubwa ni kukamata mizigo haramu inayopitishwa uwanja wa ndege, kama Mahakama imeona kuwa si dawa za kulevya, hatuna la kuongeza. Kikubwa tumemaliza kazi yetu,” alisema Muller kwa kujiamini. Hata hivyo, Nzowa jana akizungumzia kuachiwa huru kwa Watanzania hao, alionyesha kushangazwa jinsi Mahakama ilivyotoa adhabu ndogo.
“Hii ni ajabu sana. Kama watu wamebeba mzigo wenye thamani ya Sh6.8 bilioni wanapigwa faini ya milioni nne, hawataogopa kufanya hiyo biashara. Hao watu ni hatari sana,” alisema Nzowa.Alipoulizwa iwapo wakirudi Tanzania wanaweza kushtakiwa, Nzowa alisema kitengo chake hakitaweza kuwashtaki tena kwa sababu wanaweza kujitetea kuwa tayari walishahukumiwa, isipokuwa Mwendesha Mashtaka aliyekuwa akisimamia kesi yao anaweza kukata rufaa.
“Iwapo Mwendesha Mashtaka wa huko akikata rufaa kwa kuona adhabu aliyopewa mhalifu huyo ni ndogo, anaweza kufanya hivyo,” alisema Nzowa.Nzowa alisema, inasikitisha kuwa wakati mapambano ya biashara hiyo yakiwa yanaendelea Tanzania, watuhumiwa hao wanaachiwa.“Adhabu waliyopewa ni ndogo hasa wakati huu ambao Tanzania tunachafuka kwa tuhuma hizi. Lazima kitu kifanyike kubadili hali halisi hapa nchini,” alisema.
Nzowa alieleza kuwa alikwenda Afrika Kusini tangu Septemba Mosi kuwahoji wasichana hao ambao hata hivyo hawakuweza kusema lolote la kuisaidia polisi.Masogange aliandika kwa maandishi kuwa ni kweli mzigo ulikuwa wa kwake, lakini akasema mdogo wake, ambaye ni Melissa, hajui lolote na alikuwa amemsaidia.Julai 5, mwaka huu Masogange na Melissa walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo wakidaiwa wamebeba kilo 150 zilizodaiwa kuwa ni dawa za kulevya aina ya Methamphetamine zenye thamani ya Sh6.8 bilioni.
Dawa hizo zilizokuwa zimepakiwa katika mabegi makubwa sita, zinatajwa kuwa ni kiwango kikubwa kukamatwa katika historia ya SARS ndani ya uwanja huo unaotumiwa na mataifa makubwa duniani.  Taarifa za kukamatwa kwa wasichana hao zilipamba kurasa mbalimbali za magazeti ndani na nje ya Tanzania, jambo lililosababisha Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe kuchukua hatua za kuusafisha Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.
Baada ya uchunguzi wa Dk Mwakyembe ambao ulibaini kuwapo mchezo mzima uliochezwa wakati Masogange na Melissa walipokuwa uwanja wa ndege.Agosti 17 alitoa agizo la kufukuzwa kazi, Koplo Juliana Thadei, Jackson Manyoni, Yusuph Daniel Issa, Koplo Ernest na Mohamed Kalugwan.Mwakyembe alisema katika hali isiyokuwa ya kawaida mfanyabiashara ambaye hakuwa na tiketi ya kusafiri siku hiyo, baadaye alibadili mawazo hapohapo na kuamua kuondoka siku hiyo kwenda Afrika Kusini na kulipia faini ya dola 60 (Sh96, 000) ili kupata tiketi.
Pia Mwakyembe aliliagiza Jeshi la Polisi kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol) kumkamata mfanyabiashara anayedaiwa kumsaidia Masogange kusafirisha dawa za kulevya ambaye alitoweka na mabegi matatu ya dawa hizo huko Afrika Kusini.

VYAMA VYA UPINZANI WAMVAA IGP

Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema (kulia) akiagana na Wenyeviti wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF (kushoto)Freeman Mbowe wa Chadema (wapili kulia) na James Mbatia wa NCCR-Mageuzi, jijini Dar es Salaam jana. Picha Fidelis Felix 
================================================
Dar es Salaam. Vyama vya siasa vya upinzani vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi, leo vitafanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Jangwani kuhamasisha wananchi wapinge kile wanachodai ni hujuma dhidi ya Mchakato wa Katiba Mpya.
Hatua ya kufanya mkutano huo, ilifikiwa jana baada ya wenyeviti wa vyama hivyo kumvamia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema ofisini kwake wakipinga kitendo cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam kupiga marufuku maandamano waliyokuwa wayafanye leo jijini humo.
Katika mkutano wao na IGP Mwema, viongozi hao walikubaliana maandamano hayo yasitishwe kwa sababu za kiusalama, lakini wafanye mkutano huo wa hadhara. Wenyeviti hao wa vyama vya Upinzani, James Mbatia wa NCCR-Mageuzi, Freeman Mbowe (Chadema) na Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), ambao walikutana na Mwema jana mchana.
Hatua ya viongozi hao ilitokana na tamko lililotolewa juzi na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleiman Kova kusitisha maandamano ya vyama hivyo yasifanyike. Kova alitaja sababu za uamuzi huo kuwa ni kuhofia yatasababisha kusitishwa kwa shughuli za kiuchumi pamoja na kuwepo taarifa za kiintelijensia kwamba yatakuwa na vurugu.
Tamko hilo liliwakera viongozi wa vyama hivyo vitatu vilivyotangaza kushirikiana katika kupinga kile wanachodai ni uporaji wa haki ya wananchi kutunga Katiba yao. Mazungumzo wenyeviti hao na IGP yalianza saa 6 mchana na kumalizika saa 11 jioni, ambapo walitoa taarifa ya pamoja kuhusu waliyokubaliana.
Akitangulia kutoa taarifa hiyo, kwa niaba ya wenzake, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba alisema: “Tumekubaliana kesho tutafanya mkutano Viwanja vya Jangwani. Tumekubaliana kusitisha maandamano hadi Oktoba 5, (mwaka huu).” Aliongeza kuwa wamekubaliana pia kwamba watafanya mkutano mwingine wa hadhara Visiwani Zanzibar, Jumatano ijayo.
Hata hivyo, katika taarifa ya pamoja, ulitokea kuhitilafiana kwa kauli, pale IGP Mwema alipokuwa akitoa ya upande wake. Hali hiyo ilitokana na kauli ya Profesa Lipumba kusisitiza kuwa mikutano na maandamano ni haki ya msingi kwa vyama vya siasa na kwamba wanachopaswa ni kutoa taarifa kwa polisi na wala siyo kuomba kibali.
Awali, wakati Mwema akihitimisha taarifa hiyo ya pamoja alisema kuwa wanasiasa hao wanapaswa kuomba kibali cha maandamano hayo ya Oktoba 5. Alisisitiza kuwa kazi ya polisi ni kuhakikisha usalama wa raia na mali zao, hivyo wanasiasa hao wanapaswa kuomba kibali na baada ya polisi kuchunguza watakuwa na mamlaka ya kuridhia au kukataa ombi lao.
Mwema alisema haoni haja ya kuwepo malumbano na wanasiasa hao katika suala hilo kwa sababu lengo lao ni moja nalo ni kudumisha ustawi wa jamii.“Wote tunajenga nyumba moja, sioni sababu ya kugombania fito,” lisema Mwema. Mzozo wa Katiba
Mzozo wa vyama vya siasa vya upinzani ulianzia kwenye Mkutano wa 12 wa Bunge uliomalizika hivi karibuni mjini Dodoma, lakini sasa umehamia nje ya Bunge na vyama hivyo vimetangaza azma ya kuanza kampeni ya kuuhamasisha umma kudai maridhiano kabla ya kuendelea na mchakato wa Katiba Mpya. Viongozi hao wa upinzani wanadai kwamba wabunge wa CCM waliongeza baadhi ya mambo kupitia majedwali ya marekebisho.
Wanadai kuwa hali hiyo inatoa mwanya kwa Serikali inayoongozwa na CCM kupitia kwa rais kuwa na mamlaka zaidi ya uteuzi wa wajumbe husika. Vyama hivyo viliazimia kuanza rasmi leo harakati za kuhamasisha umma kupitia maandamano na mikutano ya hadhara. Ndoa hiyo ya wapinzani waliifunga, Septemba 15, kwa kuandika historia nyingine mpya kwenye tasnia ya siasa za Tanzania wakipinga Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013.
Wanadai mapendekezo mengi yaliyomo katika Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, yalipendekezwa na vyama hivyo, hivyo havitakuwa tayari kuona maoni hayo pamoja na ya Watanzania wengi yakichakachuliwa. Wanasema muungano wao ni mwanzo wa kuunganisha umma wa Watanzania kufanya uamuzi wa kunusuru utekaji madaraka na mamlaka ya nchi kutoka kwa wananchi. 
Vyama hivyo vinadai kuwa vinaungwa mkono na makundi mbalimbali yakiwamo asasi za kiraia, taasisi za dini, vyama vingine vya siasa, wasomi na taasisi za elimu. Makundi mengine ni pamoja na vyama vya wafanyakazi, jumuiya za wakulima, wafugaji, wavuvi, sekta binafsi, watu wenye ulemavu, jumuiya za wanawake, vijana na wastaafu.
Misimamo ya wenyeviti Profesa Lipumba anasema wanachopigania ni kuurejesha mchakato wa Katiba Mpya mikononi mwa umma, anaongeza kuwa suala hilo kwa sasa limehodhiwa na CCM. “Tunamshauri Rais Kikwete asisaini muswada huu, aurejeshe bungeni ufanyiwe marekebisho yenye kujenga kuaminiana na mwafaka wa kitaifa kwenye mchakato wa mabadiliko ya Katiba. Hatutakwenda kumwona, ila aurejeshe bungeni,” anasema Lipumba na kuongeza:
“Mchakato huu unahitaji uvumilivu, staha na hekima na usitawaliwe na nia mbaya, ubabe, mabavu, kejeli na dharau hasa kutoka kwa watawala. Misingi hii ikipuuzwa mchakato mzima unaweza kutumbukiza taifa letu katika mpasuko, migogoro na hata machafuko.” Mbatia anasema historia ya nchi inaonyesha kuwa waasisi wa kutaka sauti, kauli na mawazo ya umma isikike katika kudai Katiba Mpya ni vyama vya upinzani.
“CCM ndio nini… Wanatakiwa kujua kuwa Tanzania kwanza vyama baadaye, vyama vya siasa vilivyokuwa vikitawala nchini Kenya, Zambia vimekufa, lakini nchi hizo bado zipo. CCM inaweza kufa, lakini Tanzania itaendelea kubakia” anasema na kuongeza; “CCM wakisema wapinzani tunafanya vurugu wanakosea, hatuwezi kuangamiza wazo letu la kutaka Katiba Mpya, katika taifa hili Watanzania hawajawahi kuandika Katiba iliyotokana na mawazo yao.”
Mbowe anasema wameamua kuweka pembeni tofauti zao kwa ajili ya kudai Katiba Mpya ya Watanzania wote, kwamba hata wanahabari wanatakiwa kuweka pembeni itikadi za vyombo vyao vya habari vinavyomilikiwa na vyama vya siasa, kuwa wakweli katika kudai Katiba Mpya. “Waandishi wa habari msiwe vipaza sauti vya watawala bila kutafakari kwa kina Tanzania ya miaka 100 ijayo itakuwaje, wanahabari mnaweza kutunyima Katiba Mpya au mkatunyima kama ikitumika vibaya,” anasema.
Anaongeza kuwa amani ya nchi inaweza kuvurugwa kama mchakato wa katiba utahodhiwa na chama kimoja cha siasa (CCM), “Ikiwa hivyo, sisi hatutakubali kuwa kondoo. Wanaohubiri amani watambue kuwa kuna misingi ya kuipata amani hiyo, amani inapatikana kunapokuwepo na haki.”
Huku akinukuu kitabu cha Mwalimu Julius Nyerere cha ‘Freedom and Unity’, anasema, “Ni rahisi mno kuliwasha taifa la watu ambao wamekwazika, taifa hili watu wamekwazika sana. Mchakato wa katiba unaweza kutibu majeraha makubwa ambayo yanalikabili taifa.” Anasema fursa adimu ya kupata Katiba Mpya inapotezwa na bunge na CCM na anasisitiza kwamba wapinzani watatumia kila aina ya mbinu kuwaelewesha Watanzania kinachoendelea ili washiriki katika kuidai katiba iliyotokana na mawazo yao.
“Wapinzani hatutarudi nyuma na hatutakubali nchi kurejeshwa chini ya uongozi wa katiba ya sasa. Hilo wenzangu (wenyeviti wenzangu) naomba mnielewe, Chadema hatukubali na naomba na nyinyi msikubali, maana ndani ya CCM kuna kundi linataka kurudi katika katiba hii tunayoilalamikia,” alisema. Anasema katika kitabu hicho, Mwalimu Nyerere alisema, ‘Kuna siku wananchi watachagua kifo kama viongozi hawatakuwa makini’, kwamba hoja ya kutaka Amani itaharibiwa na wale wenye dola, siyo vyama vya upinzani.

Friday, September 20, 2013

Mwanamuziki Mtanzania anayeishi Italy, Remmy williams, Amaliza kurekodi Nyimbo zake mpya Tanzania, ashirikisha wanamuziki wa Tanzania

  Remmy williams Mtanzania anayefanya mziki nchini Italy katika Pozi  Tofauti, wakati akirekodi nyimbo hapa nchini na  Wasanii mbalimbali kama, King Ruston, Moses Thomas& Mirror Rhymes. Wimbo unaojulikana kama, AFRICA,Kazi hiyo imefanyika katika Studio za Overclassic, wakati Video imefanywa na  Kampuni ya Emedia chini mwongozaji Nick Dizo na Sama katika viunga vya Mwanza
(Picha Kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania).

Thursday, September 19, 2013

MISS REDD'S WATAJA VIINGILIO

Na Mwandishi Wetu
WAKATI zikiwa zimebaki siku tatu ili Redd’s Miss Tanzania ajulikane, viingilio kwa ajili ya shindano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na Watanzania wengi vimetangazwa. Kiingilio cha juu katika shindano hilo linalotarajiwa kufanyika keshokutwa (Jumamosi) katika Ukumbi wa Mlimani City, uliopo Mwenge, Dar es Salaam ni Sh 100,000 kwa viti maalumu, huku viti vya kawaida vikiwa Sh 50,000.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa kinywaji cha Redd’s Original, Victoria Kimaro, ambao ndio wadhamini wakuu wa Redd’s Miss Tanzania alisema, wanaamini viingilio hivyo ni vya kawaida kutokana na ubora wa shindano lenyewe. Victoria alisema, burudani katika shindano hilo inatarajiwa kutolewa na msanii mahiri kutoka Uganda, Mike Ross atakayeshirikiana na Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ pamoja na kundi la Mama Afrika katika kukonga nyoyo za mashabiki watakaojitokeza ukumbini hapo.
 
“Tunaamini kabisa wasanii hawa watakonga nyoyo za mashabiki wa tasnia ya urembo hapa nchini, hivyo napenda kutoa wito kwa mashabiki kujinunulia tiketi mapema ili kuepuka usumbufu,” alisema Victoria.   Naye Lady Jadee alisema, kwa kushirikiana na bendi yake ya Machozi wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatoa burudani ya nguvu kwa mashabiki wote watakaohudhuria.
 
“Nawaomba mashabiki wangu na wale urembo kujitokeza kwa wingi ili kufurahia burudani nzuri toka kwangu na bendi yangu ya Machozi, pia wasanii wenzangu waalikwa naamini watafanya vizuri siku hiyo,” alisema.  Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashimu Lundenga ambao ni waratibu wa Redd’s Miss Tanzania alisema, tiketi za shindano hilo tayari zimeshaanza kuuzwa katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
 
Alitaja maeneo ambayo yameteuliwa kuuza tiketi za Redd’s Miss Tanzania kwa mwaka huu ni duka la Shear Illusion lililopo Mlimani City, City Sports Lounge na Steers zilizopo Mtaa wa Samora, Faberk Fashion, Rose Garden Pub na ofisi za Redd’s Miss Tanzania ambazo zote zipo eneo la Mikocheni.
 
“Kwa mara nyingine tena napenda kuwashukuru wadhamini wetu wakuu  kinywaji cha Redd’s Original na wadhamini wenza ambao kwa kweli wamefanya kazi kubwa sana kuhakikisha shindano la mwaka huu linakuwa zuri na lenye tija kubwa.” Lundenga alifafanua kuwa, ili kuwapa fursa watu wengi zaidi tiketi itakayonunuliwa katika vituo vilivyopangwa kabla ya shindano itakuwa ni Sh 80,000 na kutakuwa na ofa kadhaa.
 
Taji la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linashikiliwa na Brigitte Alfred, aliyefanikiwa kulitwaa mwishoni mwa mwaka jana. Shindano la Redd’s Miss Tanzania linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), huku wadhamini wenza wakiwa kinywaji cha Zanzi, hoteli ya Giragge, Star TV, gazeti la Nipashe, Uchumi Supermarket na Marie Stopes.

MIKE ROSS, JAYDEE KUTUMBUIZA FAINALI REDD’S MISS TANZANIA

 Na Mwandishi Wetu

WASANII Mike Ross wa Uganda na Judith Wambura ‘Jaydee’, wanatarajia kutumbuiza katika fainali za Redd’s Miss Tanzania 2013, zinazotarajia kufanyika kesho kutwa. Wakati wasanii hao wanatarajia kutoa uhondo katika fainali hizo, wadhamini wa mashindano hayo Redd’s Original tayari wametangaza viingilio ambavyo watu watatakiwa kulipia.
 
  Kiingilio cha juu katika mashindano hayo ambayo yatafanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, uliopo Mwenge, Dar es Salaam ni sh. 100,000 kwa viti maalumu, huku viti vya kawaida vikiwa sh 50,000.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Meneja, Victoria Kimaro alisema, wanaamini viingilio hivyo ni vya kawaida kutokana na ubora wa mashindano yenyewe.  
Victoria alisema, ili kuongeza uhondo katika mashindano hayo wameamua kumleta msanii mahiri kutoka Uganda, Mike Ross atakayeshirikiana na Jaydee' pamoja na kundi la Mama Afrika."Tunaamini kabisa wasanii hawa watakonga nyoyo za mashabiki wa tasnia ya urembo hapa nchini, hivyo napenda kutoa wito kwa mashabiki kujinunulia tiketi mapema ili kuepuka usumbufu," alisema Victoria. 

Naye Jaydee alisema, kwa kushirikiana na bendi yake ya Machozi wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatoa burudani ya nguvu kwa mashabiki wote watakaohudhuria."Nawaomba mashabiki wangu na wale wa urembo kujitokeza kwa wingi ili kufurahia burudani nzuri kutoka kwangu na bendi yangu ya Machozi, pia wasanii wenzangu waalikwa naamini watafanya vizuri siku hiyo," alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashimu Lundenga ambao ni waratibu wa Redd's Miss Tanzania alisema, tiketi za mashindano hayo tayari zimeshaanza kuuzwa katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam. "Kwa mara nyingine tena napenda kuwashukuru wadhamini wetu wakuu kinywaji cha Redd's Original na wadhamini wenza ambao kwa kweli wamefanya kazi kubwa kuhakikisha shindano la mwaka huu linakuwa zuri na lenye tija kubwa," alisema.

Lundenga alifafanua kuwa, ili kuwapa fursa watu wengi zaidi tiketi itakayonunuliwa katika vituo vilivyopangwa kabla ya mashindano itakuwa ni sh. 80,000 na kutakuwa na ofa kadhaa.Taji la Redd's Miss Tanzania kwa sasa linashikiliwa na Brigitte Alfred, aliyefanikiwa kulitwaa mwishoni mwa mwaka jana. Redd's Miss Tanzania inadhaminiwa na kinywaji cha Redd's Original kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), huku wadhamini wenza wakiwa kinywaji cha Zanzi, hoteli ya Giraffe, Star TV, Uchumi Supermarket na Marie Stopes.

YANGA WAMSHTAKI KALIA KWA TENGA...

Na Elizabeth Mayemba


VIONGOZI wa Matawi ya Yanga Mkoa wa Dar es Salaam wamemshtaki Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi Kuu, Wales Kalia kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga kwa madai ya kuitishia klabu hiyo ambayo inapanga kuandamana. Katika barua yao iliyowasilishwa jana TFF wanachama hao, wamemtaka Kalia ajiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya TFF kwa kuwa ameshindwa kusimamia mpira.Barua hiyo iliyosainiwa na Katibu wao Supa Nyamu, inadai kusikitishwa na kitendo cha kiongozi huyo wa Kamati ya Ligi kupandikiza chuki katika klabu yao kupitia katika kituo kimoja cha redio nchini kwamba atapambana na wanaotaka kuandamana Yanga.

Barua hiyo inaeleza kuwa maneno aliyoyasema Kalia, yanaonesha wazi kuwa si kiongozi kwani anapandikiza chuki binafsi na kuegemea upande mwingine wakati yeye hapaswi kuegemea upande wowote. “Sisi wanachama na wapenzi wa Yanga wakati timu yetu inahujumiwa yeye anashabikia vitendo viovu vya uvunjifu wa amani inavyofanyiwa klabu yetu ya Yanga.“Kalia kwa matamshi yake aliyotoa katika redio ni kuwadhalilisha wana Yanga wote vitendo vinavyofanywa na waamuzi wanaochezesha Ligi Kuu ni ukiukwaji wa sheria 17 za mpira wa miguu,” ilisomeka sehemu hiyo ya barua.  

 Barua hiyo ilieleza kuwa kwa kauli za kiongozi huyo anaidhalilisha Yanga na kuihujumu, hivyo anapaswa kujiuzulu nafasi zake zote zinazompa mamlaka TFF na kuomba vyombo husika, vimchukulie hatua ya kuondolewa kwenye mchakato wa Uchaguzi Mkuu kwa kuwa naye ni mgombea