Waziri wanchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene akizungumza na Wakuu wa Mikoa leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza baada ya kukabidhi majina hewa
kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo
jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa
Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadik akikabidhi majina hewa kwa kwa
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini
Dar es Salaam.
Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza Waziri wanchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI,
George Simbachawene baada ya kumkabidhi majina watumishi hewa , jijini
Dar es Salaam.
Mkuu wa
Mkoa wa Tabora , Aggrey Mwanri akikabidhi majina ya watumishi hewa kwa
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini
Dar es Salaam.
Mkuu wa
Mkoa wa Lindi ,Godfrey Zambi akikabidhi majina ya watumishi hewa kwa
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini
Dar es Salaam.
TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, March 30, 2016
UGONJWA WA ENDOMETROSIS WAWATESA WANAWAKE.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee,
Dk. Hamis Kigwangalla akizungumza na wanafunzi wa sekondari (hawapo
pichani) juu ya ugonjwa wa Endometrosis katika semina hiyo kutoa elimu
ya ugonjwa iliyoratibiwa na Miss Tanzania 2001, Millen Magese ambaye ni
Mhanga wa Ugonjwa huo leo jijini Dar es Salaam.
Mkuruenzi Millen Magese Foundation na Miss Tanzania 2001, Millen
Magese akizungumza wakati wa semina ya wanafunzi wa sekondari juu ya
ugonjwa wa Endometrosis ambapo yeye ni mhanga wa ugonjwa huo
iliyofanyika leo katika shule sekondari Tulian Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee,
Dk. Hamis Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na Miss Tanzania
2001, Millen Magese na wageni walikwa katika semina ya utoaji wa elimu
ya ugonjwa wa endometrosis leo jijini Dar es Salaam.
Na:Mwandishi Wetu,
IMEELEZWA kuwa kutibu ugonjwa wa Endometrosis ni gharama kubwa na serikali pekee yake haiwezi kushughulikia tatizo hilo.
Ugonjwa huo huwapata wanawake wakati wa hedhi na kufanya mwanake kukosa furaha na kutibu kwake ni gharama kubwa.
Akizungumza
na leo katika semina kutoa uelewa kwa wasichana 400 iliyoandaliwa na
Taasisi ya Miss Tanzania 2001 Millen Magese, Naibu Waziri wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla
amesema kuwa ugonjwa wa Endometrosis unasababisha ugumba kwa wanawake.
Amesema
kugundua ugonjwa huo unachukua kati ya miaka sita hadi 10 na kati ya
wanawake 100 wenye ugonjwa huo nusu hawawezi kupata watoto.
Dk.Kigwangalla
amesema kutambua ugonjwa huo kwa wataalam inachukua miaka saba hadi 10
hivyo kunahitajika elimu hata maeneo vijijini wanawake wanaweza wanaugua
lakini hawajui.
“Wahenga
wanasema raha ya mwanamke na kuzaa mtoto wake mwenye hivyo kuwa na
ugonjwa unafanya mwanamke akose furaha katika maisha yake”amesema
Kigwangalla.
Mkurugenzi
wa Millen Magese Foundation,Miss Tanzania 20O1, Millen Magese amesema
kuwa amefanyiwa operesheni mara 13 na kuamua kutoa elimu juu ya ugonjwa
huo.
Amesema kuwa wanawake wengi wanasumbuliwa na ugonjwa huo lakini wanasema ni siri wakati ni ugonjwa wenye maumivu makali..
Tanzania yapokea msaada wa shilingi bilioni 116.4 kutoka Japan.
Balozi wa Japan
nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida akiongea na waandishi wa habari (hawapo
pichani) mara baada ya kusaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania
na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata
kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.(Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO).
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
WADAU WA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA WAKUTANA KUJADILI MPANGO KAMAMBE WA USAFIRI WA ANGA ( CIVIL AVITIATION MASTER PLAN) JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt Leonard Chamuriho akifungua warsha ya kujadili rasimu ya Mpango Kamambe wa Sekta ya Usafiri wa Anga( The Civil Aviation master Plan) iliyofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA). Banana - Ukonga jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt Leonard Chamuriho(katikati) Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari(Kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Mhandisi George Sambali (kushoto) wakiwa kwenye warsha ya kujadili rasimu ya Mpango Kamambe Sekta ya Usafiri wa Anga( The Civil Aviation master Plan) warsha hiyo ilifanyika katika ofisi za Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) ), Banana - Ukonga jijini Dar es Salaam leo.
WANAWAKE DODOMA WANUFAIKA NA ELIMU YA UJASILIAMALI INAYOTOLEWA NA MANJANO FOUNDATION
Mwanasaikolojia
Anti Sadaka akitoa Mada kwenye Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa
Mkoa wa Dodoma yanayoendeshwa na Taasisi ya Manjano Foundation
yanaoendelea kwenye ukumbi wa LAPF House.
Mwanasaikolojia
Anti Sadaka amewafunda wanawake wa Dodoma wanaoshiriki mafunzo ya
ujasiriamali ya kujikita katika biashara ya Vipodozi vya LuvTouch
Manjano. Mafunzo hayo yanaendeshwa na wataalamu kutoka taasisi ya
Manjano Foundation na mkufunzi wa maswala ya Biashara mjini Dodoma
yanayoendelea kwa wiki nzima.
Anti
Sadaka amewataka wanawake hao kujitambua kwa lengo la kufikia malengo
yao waliojiwekea. Akieleza zaidi katika semina hiyo amewataka wanawake
hao kujitambua wao ni nani, wajiamini, watambue vyeo vyao katika
familia, wana nafasi gani kwenye jamii inayowazunguka, kufanya kazi kwa
bidii na kudumisha nidhamu yao kwa kila wakifanyacho kwa lengo la
kufikia malengo yao.
Pia amewaasa wanawake walioshiriki mafunzo hayo mjini Dodoma kuchangamkia FURSA zinazowazunguka. Semina
hiyo inawanufaisha wanawake wa Dodoma kwa lengo la kuwaongezea kipato
na pia kuweza kujiajiri ili kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira.
Ziara ya Mafuzo ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa
Leo Jumatano tarehe 30 Machi 2016 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Utawala na Serikali za Mitaa chini ya Makamu Mwenyekiti Mh. Dkt.
Pudenciana Kikwembe walipata fursa ya kutembelea ofisi za MKURABITA kwa
ajili ya kujifunza juu ya madhumuni na shughuli za MKURABITA nchini.
Prof. Mbarawa afanya ziara kushtukiza KOJ Kurasini
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na
baadhi ya wafanyakazi wa TPA eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini
(KOJ) Kurasini leo jijini Dar es salaam. Wa kwanza kulia Mhandisi
anayefanya kazi eneo la KOJ Jabiri Muyones.
Kapteni Abdulla Mwingamno (kulia) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) baadhi ya vifaa vya kituo cha kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongozana na Mhandisi anayefanya kazi eneo la KOJ Jabiri Muyones alipotembelea TPA eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini leo jijini Dar es salaam.
Kapteni Abdulla Mwingamno (kulia) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) baadhi ya vifaa vya kituo cha kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongozana na Mhandisi anayefanya kazi eneo la KOJ Jabiri Muyones alipotembelea TPA eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini leo jijini Dar es salaam.
Subscribe to:
Posts (Atom)