Na Woinde Shizza alivyotembelea ,Mwanza .
Uvuvi
haramu wa kutumia sumu kali,pamoja na neti umekua ukitishia uhifadhi
katika hifadhi ya Taifa ya Saa Nane na Lubondo ambazo zimepewa jukumu la
kulinda mazalia ya samaki ili samaki hao wasipotee kwenye uso wa dunia.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Ofisini kwake waliofanya ziara ya kutembelea
hifadhi hiyo ya Saa Nane iliyoko jijini Mwanza ,ziara iliyoratibiwa na
Tanapa Mhifadhi Mkuu Donatus Bayona amesema kuwa changamoto
inayowakabili ni uvuvi haramu na uvamizi wa maeneo ya hifadhi unaofanywa
na wavuvi wanaojipatia kipato bila kujali kuwa wanaharibu mazalia ya
samaki .
Askari
Wanyamapori katika hifadhi hiyo Aloyce Mong`ee amesema kuwa wamekua
wakiimarisha doria katika mipaka ya hifadhi ili kuzuia shughuli hizo za
uvuvi ambazo ni tishio kwa uhifadhi.“Kuna mipaka ambayo tumeweka hakuna
mtu anayeruhusiwa kufanya uvuvi ndani ya eneo la hifadhi ili kuhifadhi
mazalia ya samaki” Alisema Askari huyo.
Mhifadhi
huyo amesema kuwa Hifadhi hiyo ambayo iko katikati ya jiji la Mwanza
inaongoza kwa kuwa na watalii wengi wa ndani ambao ni asilimia 90% ya
wageni wanaotembelea hifadhi hiyo.Alisema
Hifadhi ya Saa Nane ni moja kati ya hifadhi zilizopo kati kati ya miji
hivyo kuvutia watanzania wengi kutembelea eneo hilo ambali lina wanyama
pori pundamilia,swala na sokwe weusi pamoja na madhari nzuri na
maridhawa ambazo hutumika kama sehemu ya kujifunzia na kupumzikia.
No comments:
Post a Comment