Na Mwandishi wetu,
Benkiya Maendeleo ya Kilimo
(TADB) imefanikiwa kupata faida ya zaidi Shilingi 1.72 bilioni kwa miezi sita (6)
ya mwaka wa fedha 2016 tangu kuanza kutoa mikopo kwa wakulima wadogo nchini.
Akizungumza katika Maonesho hayo,
Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi alisema kwamba Benki yake imetimiza mwaka mmoja kwa kutengeneza faida kwa kupata jumla ya kiasi
cha Shilingi 450 milioni kwa mwaka jana na Shilingi 1.72 bilioni kwa miezi sita (6)
ya mwaka 2016.
“Benki imeanza kazi kwa kishindo kwa kutengeneza faida jambo linaloonyesha uimara wa Benki katika kuwahudumia wakulima wa nchi nzima,”
alisemaBw. Samkyi.
Bw. Samkyi aliongeza
kuwa mpaka sasa TADB imefanikiwa kukopesha jumla ya wakulima 1720 kutoka mikoa mitatu
(3) ya wilaya saba (7) za mikoa ya mwanzo ya majaribio ambayo ni Dar es Salaam, Pwani,
Morogoro, Tanga, Iringa na Njombe.
Aliongeza kuwa TADB
imejipanga kuwa benki ya mfano na ya kisasa katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania
kutoka kilimo cha kujikimu kwenda katika kilimo cha
kibiashara na uzalishaji wenye tija katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
“Tumedhamiria na kujizatiti na kuhakikisha tunachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia wakulima wadogo na wakulima wakubwa wanaosaidia wakulima wadogo kwa kuwapatia mikopo yenye gharama nafuu,”
aliongeza.
Mkurugenzi Mwendeshaji huyo alisema Benki imejidhatiti katika kufanya tathmini ya
kina
katika mnyororo mzima wa thamani ilikutambua mapengo na mapungufu yanayohitaji utatuzi kwa minajili ya kuongeza thamani naushindani kwenye masoko nchi nzima.
“Sera ya TADB
ni kutathmini mnyororo mzima wa thamani ilikutambua mapengo na mapungufu ya nayohitaji utatuzi,
na ambayo utatuzi wake utaongeza tija na uwezo wa ushindani kwenye masoko,
na hivyo kukuza uchumi wa walio wengi na kupunguza umaskini nchini kote,” aliongeza.
Wakati huo huo, katika kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB)
imepanga kuanza kutoa mikopo kwa wakulima wadogo na wakulima wakubwa wanaosaidia wakulima wadogo nchi nzima ili kuharakisha mapinduzi ya kilimo nchini.
Mikakati hiyo iliwekwa bayana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo,
Bibi Rosebud Kurwijila wakati wa Maonesho ya Nane
Nane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mjini Lindi.
Bibi Kurwijila alisema
kuwa TADB
inalenga kutekeleza kwa vitendo Maelekezo ya Serikali ya kupunguza changamoto zinazowakabili wakulima nchikote,
hivyo TADB imejipanga kuwafikia wakulima wadogo nchi nzima ili kuharakisha mapinduzi ya kilimo nchini.
“Benki imejipanga kutoa mikopo yenye riba nafuu katika muda mfupi,
wakati na mrefu kwa Wakulima wadogo wadogo,
wakati na wakubwa, hususan kuziba pengo la
upatikanaji wa fedha za kwenye mnyororo wa ongezeko la thamani ili kuharakisha mapinduzi ya kilimo katika tasnia za kilimo,
mifugo, uvuvi na mazao ya misitu (ufugaji nyuki),” alisema Bibi Kurwijila.
Aliongeza kuwa
kwa sasa Benki imeanza kupokea maombi kutoka kwa wakulima wanaohitaji mikopo nchi nzima ili kuwakwamua na changamoto ya ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini.
Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania ilizinduliwa Rasmi na Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wakulima nchini,
mnamo tarehe 8 Agosti 2015 mjini Lindi.
Uanzishwaji wa Benki hii ni utekelezaji wa malengo ya muda mrefu ya Serikali,
katika kuitikia wito wa wananchi na wadau wengine wa maendeleo ili Tanzania
iweze kupiga hatua endelevu za kimaendeleo.
Mkurugenzi
Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi (Kulia) akizungumza na wanahabari wakati
wa Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mjini
Lindi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bibi Rosebud
Kurwijila
Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kushoto) akizungumza na wanahabari
wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo
mjini Lindi. Kulia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki hiyo Bw. Thomas Samkyi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB,
Bibi Rosebud Kurwijila (Wapili Kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ndg.
Godfrey Weston Zambi (Wapili Kulia) wakati wa Maonesho ya Nane Nane
yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mjini Lindi. Wengine pichani ni
viongozi waandamizi wa TADB wakiongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki hiyo
Bw. Thomas Samkyi (Kushoto).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi, Dkt. Florens Turuka (Wapili Kulia), akizungumza na Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Wapili Kushoto). Wengine
pichani ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki hiyo Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) na
Bw. Adam Kamanda (Kulia).
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii
na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (Kushoto)
akipata maelezo kuhusu Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kutoka kwa Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Benki hiyo Bw. Thomas Samkyi (Kulia).
Afisa wa TADB, Bw. Victor Mziray (Kulia)
akiwahudumia wateja waliojitokeza kutembelea Banda la Benki ya Kilimo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB,
Bibi Rosebud Kurwijila (Kulia) akimsikiliza Bibi Constancia Mahanga (Kushoto) wa
Kikundi Umoja kutoka Tandahimba wanaodhaminiwa na TADB.
Afisa Masoko wa Wakala wa Mbegu, Bi.
Jacqueline Itatiro (Kushoto) akimuelezea namna ya Wakala huo unavyofanya kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB,
Bibi Rosebud Kurwijila (Kulia). Wengine pichani ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki
hiyo Bw. Thomas Samkyi (Wapili Kulia) na viongozi wengine wa Benki hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kulia) akiangalia unga wa muhogo
unaozalishwa na Kikundi cha Vijana cha Agripreneur. Kushoto wanakikundi wa
kikundi hicho, Bw. Fortunata Mwananjela na Bi. Veronica Kichanta.
Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Katikati) na Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Benki hiyo Bw. Thomas Samkyi (Wapili kulia) wakimsikiliza Katibu
wa Chama cha Wakulima cha Nzihi, Bw. Emmanuel Fungo anayewakilisha vikundi nane(8) vya mkoa wa Iringa waliopatiwa mkopo na TADB.
(Picha Zote Kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).