TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, July 19, 2014

HAKI NA MISINGI YA DEMOKRASIA IZINGATIWE KWA WOTE.: WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI ILALA.

 
 
HII NDIYO SHULE YETU YA WIKI HII TAREHE 20/7/2014.
kama unavyofahamu tena sisi wajibu wetu ni kujaribu kufuatilia kwa makini maendeleo ya wanafunzi, juu ya haki zao za msingi kisheria na Demokrasia ya Kweli. Shule hii ipo eneo la Vingunguti / Kipawa ni kwa mwendo kama wa dakika 10 kwa miguu toka barabara kubwa liendalo gongolamboto buguruni, ambapo jicho na darubini yetu ilipiga kambi kwa siri. Kati ya Mambo mazuri katika Shule hii ni pamoja na Wanafunzi Kupenda Utulivu wakati wote, wanafunzi hawa wanakuwa kila mmoja bize na masomo pamoja na kwamba wapo wengine ambao muda mwingine pia wanapata fulsa ya kupenya penya hapa na pale kwa kuchengana na walimu wao kwa tofauti ambazo ni za kimasomo.
Aidha Darubini yetu ilifanikiwa pia kufanya mazungumzo na baadhi ya Wanafunzi na Walimu kuhusu Shule hiyo," Eh wewe kwani ni nani? Mpiga Picha au? aliuliza mwanafunzi mmoja aliyekuwa ameketi kwenye kundi la Wenziwe huku wakiendelea kupiga Stori, Wakati ilikuwa yapata majira ya saa sita, wakati huo njaa pia zilikuwa zinaonekana kuwakwaza maana vijembe navyo vilisikika vya uchokozi wao kwa wao, "wewe naye unataka kuwa mwandishi wa habari, au unatafuta habari? njaa tu inakuwasha tumboni muda huu, unamuuliza huyo mtu wa watu yeye nani kwani wewe unataka awe nani? je kama ni mwandishi wa habari anatafuta habari, unataka kumpa hizo habari? yaani watoto wale kiboko, mie " mi nataka nimpe habari akauze vizuri kama kweli yeye anatafuta habari, wewe mkaka uje unipige picha, kwani ni bure au na hela? na hela nikamjibu ili nisije nikaharibu kabisa dili lenyewe, " je ni shilingi ngapi? " ni mia tano ila nikikuletea utanipa sawa," oh kumbe Simple tu, aisee niphotoe haraka kabla Walimu hawajaleta zao, maana kuna mmoja huyo mnokon kweli utadhani nini, hataki hata sisi Wanafunzi tupige picha za kumbukumbu tunapokuwa kwenye pozi zetu, sijui yeye alipokuwa anasoma wakati wake hapakuwa na kamera? eti wewe mpiga picha ni Sahihi kupiga picha sisi tukitaka za kumbukumbu au ni makosa?
Swali lake ilikuwa mtego sana kwangu, lakini baada ya kutafakari nikampa " kwani Shule ni ya Nani? Shule ipo kwa ajili ya Walimu au Shule kwa ajili ya Wanafunzi? nikampa na hiyo" Lakini wakati zoezi linaendelea mara yule asiyependa wanafunzi wapige picha akatokea wakaanza kutoka mbio, nikajaribu kuwasihii wamsikilize mwalimu wao maana alikuwa sasa anawaita kwa asira, kama unavyofahamu tabia za wanafunzi, wakimuona mwalimu wanageuza mgongo ili wasionekane sura, kwa hiyo mimi nikawambia hapa msikimbie nyie msikilizeni tu na mimi hapa nitajaribu kuwatetea maana sidhani kama kuna kosa kwenu kupiga picha za ukumbusho baina yenu, isipokuwa kosa ni kujaribu/kupiga picha chafu.
basi baada ya kuitikia wito wa mwalimu wao, msamaha wa mwalimu huyo kwanza kabisa ilikuwa ni wote kupiga magoti kwenye eneo la jua kali,(Wakati wanapigishwa magoti tayari ailitwa asikari kuja kutazama kama wanatimiza adhabu, baada ya hapo huyo mwalimu akaniita na mimi na kutoa oda picha zote zilizoko ndani ya kamera zifutwe, " Askari ulikuwa wapi wakati hawa Vitoto wanapiga piga picha, ili lingine litazame hata akili hamnazo kabisa lakini kwa Picha, Hakikisha Picha zote zilizomo kwenye hiyo kamera zimefutwa. Inaendelea katika ukurasa wetu wa mtandao wa Blogs: www.missdemokrasia.blogspot.com/ www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com

RAIS KIKWETE AFUNGUA DARAJA LA RUHEKEI LINALOUNGANISHA WILAYA YA MBINGA NA WILAYA YA NYASA MKOANI RUVUMA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katikati akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli wa kwanza kulia wakifanya ishara ya kuweka jiwe la msingi na kufungua Daraja la Ruhekei linalounganisha kati ya Mbinga na Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria kufungua Daraja la Ruhekei lililopo katika Barabara ya Mbinga-Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katikati akifurahia kikundi cha Ngoma cha mkoa wa Ruvuma katika sherehe ya uzinduzi wa Daraja la Ruhekei lililopo katika barabara Mbinga –Mbamba bay mkoani Ruvuma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli, Mama Salma Kikwete pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakipita juu ya Daraja la Mto Ruhekei baada ya kulifungua mkoani Ruvuma. Daraja hilo ni kiungo muhimu kati ya Wilaya mpya ya Nyasa pamoja na Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) kushoto akizungumza na Mwenyekiti wa kamati ya Miundombinu Profesa Juma Athumani Kapuya (Mb) kabla ya uzinduzi wa Daraja la Ruhekei lililopo katika Barabara ya Mbinga-Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) katikati akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe wakati wakisubiri kuwasili kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Dkt.Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya ufunguzi wa Daraja la Mto Ruhekei mkoani Ruvuma.

AJALI MBAYA IMETOKEA MOROGORO, WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA JEZI WAANGUKIWA NA LORI,MTU MMOJA AMEFARIKI PAPO HAPO NA WENGINE KUJERUHIWA.

Wananchi wakiwa wamejazana huku wakiliangalia lori aina ya fuso lililowagonga wafanyakazi sita wa kiwanda cha Mazava na mmoja kufariki dunia papo hapo kwa kuangukiwa na lori hilo baada ya kupinduka wakati dereva wake akijaribu kumkwepa mwendesha pikipiki katika barabara kuu ya Iringa-Morogoro eneo la Bene Msamvu mkoani Morogoro.
Mkono ukiwa unanekana huku mwili ukiwa umekandamizwa na kichwa cha lori hilo kabla ya mwili kutolewa katika eneo la tukio.
 Hapa mwili ukiwa bado haujatolewa.
Baada ya magari yenye kunyanyua vitu vizito kunyanyua na wananchi kupata nafasi ya kuutoa mwili uliokuwa umekandamizwa na lori hilo.

 Kamanda wa polisi Morogoro akizungumza jambo na waandishi.
 Hapa Kamanda Leonard Paul akizungumza na maafisa wake eneo la tukio.
Wapiga picha za facebook wakichukua picha.
Hamida Shariff, Morogoro.
Mfanyakazi kiwanda cha kushona jezi cha Mazava amefariki dunia na wengine sita wamejeruhiwa baada ya lori lililokuwa limebena kokoto kuacha njia na kupinduka kisha kuwafukia na kokoto hizo.
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 10:30 kwenye eneo la Bene Msamvu barabara ya Morogoro- Iringa na kwamba aliyefariki katika ajali hiyo ni Hanifa Bakari (20-30) ambaye ni mfanyakazi wa kiwanda hicho.
Ajali hiyo ilihusisha lori hilo aina ya Tiper lenye namba za usajili T 824 CVS lililokuwa likitokea Chamwino kwenda Msamvu na pikipiki aiana ya Honda yenye namba za usajili T823 CAE.
Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Happines Santus (22), Anita Leonard (22), Shiza Ramadhani (23), Eliyas Banka, Adamu Mapande (18) na Fatuma Selemani (22) na mwanaume mmoja ambaye bado hajafahamika jina lake.
Akizungumza mara baada ya kuokolewa mmoja wa majeruhi hao Shiza Ramadhani alisema wakiwa wanatembea kandokando ya barabara ghafla walilioona lori hilo likiacha njia na kuwafuata upande waliokuwepo na kuwagonga kisha kufunikwa na kokoto.
Alisema kuwa kabla ya gari hilo kuwagonga alishuhudia pikipiki iliyokatiza ghafla mbele na dereva wa gari alipotaka kumkwepa ndipo aliacha njia na kwenda kuwagonga ambapo walitumbukia kwenye mtaro na kufukiwa na kokoto.
“Kama ingepita nusu saa bila ya kuokolewa kwa kweli ningekufa palepale kwa sababu tayari nilishaanza kuishiwa nguvu na kukosa hewa na sehemu kubwa ya mwili ilikuwa imefukiwa na kokoto,” alisema Shiza.
Hata hivyo baadhi ya watu waliofika kuwaokoa majeruhi hao walisema kuwa zana duni za uokoaji imekuwa ni tatizo kubwa mkoani hapa hivyo yanapotokea majanga ya aina hiyo vifo vimekuwa vikitokea kutokana na kuchelewa kwa zoezi la uokoaji.
Mmoja wa waokoaji hao Moris Masala alisema kuwa mara baada ya ajali hiyo kutokea kila mtu alikuwa hajui namna ya kuokoa majeruhi hivyo kwa gharama zake alilazimika kwenda kutafuta gari maalumu ya kunyanyau vitu vizito lakini ilishindwa kunyanyua gari hilo.
Moris alisema kuwa watu walianza kufukua kokoto hizo kwa kutumia zana duni za makoleo na hivyo kufanikiwa kuwatoa wafanyakazi hao sita na mmoja alitolewa akiwa tayari ameshafariki dunia.
Naye mbunge wa jimbo la Morogoro mjini AbdulAziz Abood alioneshwa kukerwa na tabia ya mmiliki wa kiwanda hicho ya kuwalazimisha wafanyakazi kutoka na kuingia kwa kutumia lango ambalo liko jirani na barabara kuu ya Morogoro- Iringa na hivyo kuhatarisha usalama wa wafanyakazi hasa wakati wa kuvuka barabara hiyo.
Hivyo alimtaka mmiliki huyo kufuata sheria na taratibu alizopewa kwani madhara ajali iliyotokea imesababisha kifo na majehara kwa wafanyakazi ambao ni watanzania.
Pia Abood alilitaka jeshi la polisi kuweka askari wa kudumu katika eneo hilo ambalo mara kadhaa ajali zimekuwa zikitokea na pia aliiomba wakara wa barabara nchini Tanroads kuweka matuta katika eneo hilo ili kudhibiti mwendokasi wa maredeva.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoani hapa Leonard Paulo alikiri eneo hilo kuwa hatarishi na hivyo kuahidi kuweka askari wa usalama barabarani ambao watakaa muda wote kudhibiti mwendo kasi ili kupunguza ajali zinazotokea mara kwa mara katika eneo hilo.
Alisema kuwa tayari dereva wa gari lillilosababisha ajali Ayubu Swai (27) na dereva wa Pikipiki Samwel Noel (32) wameshakamatwa kwa mahojiano zaidi na watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi wa polisi kukamilika.
Hata hivyo alisema majeruhi waliolazwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro wanaendelea vizuri.(.PICHA/MTANDA BLOG).

NIDA Textile Mills Ltd, waonywa na Waziri wa Mazingira, kwa kukiuka taratibu za usafi

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Binilith Mahenge (mwenye shati la drafti) akipiga picha maji yanayopita kwenye mto Kibandu kutoka kiwanda cha NIDA Textile Mills Ltd.Kulia ni Diwani wa Kata ya Kigogo Richard Chengula.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk.  Binilith Mahenge (kulia) akipiga picha bomba linalotiririsha maji machafu kutoka kiwanda cha NIDA kilichopo Kigogo Mkuyuni jijini Dar es Salaam, 
 Bomba linalotiririsha maji machafu kutoka kiwanda cha NIDA kilichopo Kigogo Mkuyuni jijini Dar es Salaam, 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Binilith Mahenge (katikati) akiongozwa na Meneja Mkuu wa NIDA Textile Mills Ltd Imran Lohya kupanda kwenye tenki la maji yanayutumika na kiwanda hicho.

TAARIFA ZA KUWAKA MOTO KWA HOTEL YA NAURA SPRINGS SI SAHIHI

SEHEMU YA JENGO LA HOTEL HIYO LIONEKAVYO KWA NJE.
MENEJA WA HOTEL HIYO BI.BEATRICE DALLARIS AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI,JUU YA  TAARIFA ZA UZUSHI ZILIZOSAMBAZWA KWENYE MITANDAO YA KIJAMI KUWA HOTEL HIYO IMEUNGUA MOTO MAPEMA LEO JIJINI ARUSHA.
UTAWALA NA WAFANYAKAZI WA HOTELI YA NAURA SPRINGS IMESIKITISHWA KWA TAARIFA ZILIZOSAMBAA KWENYE MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII KUHUSU KUWA HOTELI YETU INAWAKA MOTO NA KUSABABISHA USUMBUFU MKUBWA KWA WATU WA MKOA WETU, NDUGU NA JAMAA WA WAFANYAKAZI WA HOTEL ,VIONGIOZI MBALIMBALI, VYOMBO VYA USALAMA, IDARA YA ZIMA MOTO, WAANDISHI WA HABARI WA VYOMBO MBALI MBALII VYA HABARI NA PIA KUSABABISHA WASIWASI NA KUTOWESHA UTULIVU NA AMANI WA MJI WETU.
TUMESIKITISHWA SANA NA TUMEOMBA UONGOZI WA MKOA WETU WALISHUGHULIKIE SWALA HILI KIKAMILIFU KWANI HILI SIO LA KUCHUKULIA MZAHA NA TUNGEOMBA HATUA KALI ZICHUKULIWE KWA HARAKA SANA KWA ALIE TOA TAARIFA HIYO YA UONGO.

TUNAWASHUKURU WATU WOTE WALIOFUATILIA SWALA HILI NAPIA TUNATOA TAMKO KUWA HABARI HIZI ZA KUWA HOTELI YETU INAUNGUA NI ZA UONGO.
BEATRICE DIMITRIS DALLARIS
HOTEL MANAGER

Thursday, July 17, 2014

HAPPINESS MAGESE KUKOJOA KWA KUTUMIA MIRIJA MAARUM

                    HIVI NDIVYO ANAVYO KOJOA SASA

JINA lake kamili anajulikana kama Happiness Millen Magese. Ni mshindi wa Shindano la Miss Tanzania Mwaka 2001.Happiness Magese (35), alikuwa akifanya kazi zake za uanamitindo nchini Afrika Kusini chini ya Kampuni ya Ice Model Management na alikaa huko kwa miaka nane kabla hajahamia katika Jiji la New York, nchini Marekani ambapo amesaini mkataba na Kampuni ya Ford Models mpaka sasa hivi. Ana miaka minne na tayari ameshaongezewa miaka miwili zaidi ya fani hiyo ya uanamitindo duniani.
Happiness Magese anasihi wanawake kucheki afya zao mara kwa mara wasije wakakutwa na tatizo kama lake la ugumba ambalo limeharibu na kibofu chake na kupelekea hata kushindwa kukojoa kwa njia ya kawaida na badala yake anatumia mipira, ni vema kuchek afya mara kwa mara.

MATAWI MAALUMU YA UMOJA WA VIJANA WA CCM KUIMARISHWA VYUONI.

Mkuu wa utawala wa UVCCM Taifa Comred OMARI MWANANG'WALU akizungumza na baadi ya vijana kutoka vyuo mbalimbali vya mkoa wa DSM ambao walikuja kujifunza mambo mbalimbali ya UVCCM MAKAO MAKUU,,,KAMA VILE ,KANUNI YA UVCCM NA IDARA ZA UVCCM MAKAO MAKUU,,,,,
AKIAMBATANA NA COM MPOKWA,,kwa pamoja waliwapongeza vijana hao kwa moyo wao wakujenga UVCCM imara...
mkuu wautawala alisema.."..tunatafuta utaratibu mzuri zaidi wa kuona tunaimarishaje matawi ya umoja wa vijana vyuoni nchi nzima,,,baada ya kikao na viongozi wenzangu tutawajulisha nini tumeamua kwa pamoja....."

MOTO WA MWANANYAMALA NA ROHO ZA UKATILI WA MIOYO YA WATANZANIA


Hii Ilikuwa Kama Picha ya Kivietinamu, maana tukio lenyewe ilikuwa kama jambo la kawaida kuona moshi wa Moto, ukianza Mdogo mdogo, Kamera Yetu inayoangaza pande zote yenyewe kazi yake ilikuwa ni kuhakikisha inakusanya vipande vipande (Crips) za Matukio isipikuwa Mkanda huu meneja aliyeandaa Vipande hivi naona hakutarajia kama kutatokea madhara makubwa kama ilivyo sasa, Pengine kwa mtazamo wake baada ya kuangalia Mikanda ya Wenzetu wa huko Majuu, Maana Movie za wenzetu kama unavyojua  tena, Wakiamua kutumia Magari basi Wanayateketeza kwa moto ili mradi tu Sinema hiyo Ikamilike, Tren na hata NDEGE.
Sasa mimi najiuliza kweli inakuwaje Moto Mkubwa kama huo unatokea wakati Vyombo husika vipo tena Mwananyamala Siyo Eneo ambalo utasema hakuna vitendea kazi, Vyombo husika vipo na Vimewekeza kwenye ardhi ya Mwananyamala, Watu walikuwapo wengi sana wa kuweza kuleta Amani kwa Kuchukua hatua Mapema, Kila Mtu siku hizi hakosi kuwa na Simu Mkononi, Sasa nikuulize wewe unayesoma muda huu hii habari, hiyo simu yako Mkononi unajua Matumizi yake? au ya kwako kazi yake ni kuwasiliana na huyo Mkeo/Mmeo/Boyfred/mchumba/biashara gani?Wizi tu; au kwa kuwa siku hizi kuna hata simu za Shilingi 1500? ndiyo maana hata wewe unayo, maana Simu ZENU hizo kuwaka zinawaka ila kubonyezeka hazibonyezeki.
Umbea tu unakusumbua, kuwa mwandishi wa habari basi utafute habari na utuletee matukio unayodhani kwamba unapenda yaendelee kutokea, unapata faida gani unaposhuhudia Uharibifu Mkubwa tena wa hatari kubwa ususani kwa Watoto wasiojua jinsi ya kujikwamua, au ndiyo ukomavu sasa wa Watanzania katika Maandalizi ya Uvunjifu wa Amani wa Makusudi unaoutafuta kwa Visingizio Visivyoturidhisha?
Tafakari@Kuhusu Mwananyala.