Sasa mimi najiuliza kweli inakuwaje Moto Mkubwa kama huo unatokea wakati Vyombo husika vipo tena Mwananyamala Siyo Eneo ambalo utasema hakuna vitendea kazi, Vyombo husika vipo na Vimewekeza kwenye ardhi ya Mwananyamala, Watu walikuwapo wengi sana wa kuweza kuleta Amani kwa Kuchukua hatua Mapema, Kila Mtu siku hizi hakosi kuwa na Simu Mkononi, Sasa nikuulize wewe unayesoma muda huu hii habari, hiyo simu yako Mkononi unajua Matumizi yake? au ya kwako kazi yake ni kuwasiliana na huyo Mkeo/Mmeo/Boyfred/mchumba/biashara gani?Wizi tu; au kwa kuwa siku hizi kuna hata simu za Shilingi 1500? ndiyo maana hata wewe unayo, maana Simu ZENU hizo kuwaka zinawaka ila kubonyezeka hazibonyezeki.
Umbea tu unakusumbua, kuwa mwandishi wa habari basi utafute habari na utuletee matukio unayodhani kwamba unapenda yaendelee kutokea, unapata faida gani unaposhuhudia Uharibifu Mkubwa tena wa hatari kubwa ususani kwa Watoto wasiojua jinsi ya kujikwamua, au ndiyo ukomavu sasa wa Watanzania katika Maandalizi ya Uvunjifu wa Amani wa Makusudi unaoutafuta kwa Visingizio Visivyoturidhisha?
Tafakari@Kuhusu Mwananyala.
No comments:
Post a Comment