*Awashukia wanaotakiwa kujivua gamba *Adai wanatumika kumuhusisha na ufisadi *Asema ndani ya CCM wote si Richmond
Katibu Mkuu wa CCM Bw.Wilson Mukama.
Agnes Mwaijega na David John
KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Wilson Mukama, amedai kukerwa na
baadhi ya watu wanaomuhusisha na ufisadi uliofanyika kwenye miradi ya
machinjio, maji na kusisitiza yeye ni msafi.
Bw. Mukama aliyasema
hayo Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu
ya tuhuma dhidi yake ambazo zimetolewa katika vyombo vya habari
vikimuhusisha na ubadhirifu wa fedha za miradi hiyo.
Alisema si
kweli kwamba viongozi wote ndani ya CCM wanahusika na ubadhirifu katika
miradi mbalimbali bali inawezekana tuhuma hizo zimeelekezwa kwake kwa
sababu anahusika katika mapambano ya kuwavua magamba watu wanaokiuka
maadili ndani ya CCM.
“Ndani ya CCM, si watendaji wote ni
Richmond, inaonekana wengine wanatumia fursa hiyo kutaka kunichafua ili
nionekane nashiriki ufisadi, mimi ni msafi nafanya kazi kwa kuzingatia
maadili na nina wito ndiyo maana pamoja na kuwa mstaafu, bado
nilionekana nafaa kuwa na wadhifa ndani chama,” alisema.
Aliongeza
kuwa, taratibu za kisheria zipo hivyo kama kuna mtu ambaye mwenye hatia
kwa tuhuma kama hizo kuna vyombo ambavyo vinaweza kushughulikia.
“Nashangazwa
na baadhi ya watu kusema vitu ambavyo hawavijui undani wake, ni vema
akaonesha uhalisia wa kitu anachokisema, miradi mingi ya maendeleo
nchini inakufa kutokana na mabadiliko ya uongozi si ulaji wa fedha kama
wengi wanavyodhani.
“Ieleweke wazi kuwa, miradi inakufa
inapotokea yule aliyepewa nafasi ya kusimamia anapoondolewa na kuwekwa
mwingine ambaye anashindwa kuuendeleza,” alisema Bw. Mukama.
Alisema
kuna watu ambao hujitahidi kuonesha juhudi zao ili kuiwezesha nchi
kupiga hatua lakini wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuandamwa,
kusakamwa na kusemwa vibaya bila wahusika kufanya uchunguzi yakinifu.
“Katika
nchi hii wanaofikiri kwa kina na kuumiza vichwa kwa ajili ya mafanikio
wanaandamwa kila kukicha lakini waliokaa tu, wanaachwa na kuonekana wa
maana.
“Tatizo kubwa la nchi hii wajinga ni wengi kuliko waelevu
lakini haiwezekani nchi ikawa chini ya uongozi wa wajinga na wahuni
ambao hawawezi kuliletea taifa manufaa.
“Watu wanaleta siasa
magazetini badala ya kujikita katika kazi za msingi lakini mimi najua
ninachokifanya, siwezi kuendelea kuona nchi haina mabadiliko,”
alisistiza Bw. Mukama.
Aliongeza kuwa, suala la kujivua gamba
katika chama litaendelea kwa wananchama wote ambao wataonekana kwenda
kinyume na maadili na taratibu za chama.
Akizungumzia utendaji wa
kamati za bunge, Bw. Mukama alisema kwa mujibu wa sheria, taratibu na
kanuni masuala yanayojadiliwa katika kamati hizo hayakupaswa kuwafikia
wananchi kabla ya kumfikia spika na kujadiliwa bungeni.
Alisema
kazi ya kamati mbalimbali si kutoa taarifa zilizojadiliwa na wabunge
kwenye kamati husika bali zipo kwa kurahisisha utendaji wa wabunge.
“Mimi
sioni kama ni sahihi masuala ya kamati mbalimbali za bunge kujulikana
kabla ya kufika bungeni ambako ndiko yanapaswa kutolewa maamuzi,”
alisema.
|
*Polisi kuimarisha ulinzi maeneo mengi Na Waandishi Wetu, Arusha MACHO
na masikio ya wafuasi na wakereketwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo yanaelekezwa jijini
Arusha ambapo Mahakama Kanda ya Arusha, itatoa hukumu ya kesi ya kupinga
matokeo ya ubunge Jimbo la Arusha Mjini.
Kesi hiyo ambayo
ilifunguliwa na wapiga kura watatu ni ya kupinga matokeo yaliyompa
ushindi mbunge wa jimbo hilo Bw. Godbless Lema (CHADEMA), dhidi ya
mpinzania wake, Dkt. Batlida Burian (CCM).
Wachambuzi wa masuala
ya kisiasa waliozungumza na Majira, walisema hukumu hiyo itatikisa jiji
hilo ambapo taarifa za kuaminika kutoka vyanzo mbalimbali, zinadai
ulinzi katika maeneo mbalimbali utaimarishwa ili kuhakikisha hakuna
uvunjifu wa amani.
Hukumu hiyo inatolewa katika kipindi ambacho
wafuasi na wapenzi wa CHADEMA wakisherehekea matokeo ya kura yaliyompa
ushindi mbunge mteule wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari, huku CCM
ikiwa inatafakari ni wapi ilijikwaa hadi mgombea wake, Bw. Sioi Sumari
akabwagwa chini.
Siku ya jana katika baadhi ya maeneo, gumzo
kubwa lilikuwa hukumu hiyo ambapo baadhi ya watu walisikika wakisema
hukumu itakayotolewa iwe ushindi wa Bw. Lema au kutenguliwa, utatikisa
jiji hilo.
Jaji ambaye atatengua kitandawili hicho ni Gabriel
Rwakibarila wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga baada ya upande wa
walalamikiwa kumkataa Jaji Joyce Mujulizi ambaye awali alipangiwa
kusikiliza kesi hiyo kwa madai ya kutokuwa na imani naye.
Wakati
wa kusikilizwa kesi hiyo, upande wa Bw. Lema uliwasilisha mashahidi
wanne. Katika uchaguzi huo uliofanyika 2010, Bw. Lema aliibuka mshindi
kwa kura 56,169, wakati mpinzani wake Dkt. Burian akipata 37,460.
|
Askari
wa kikosi cha zimamoto na Uokoaji cha Halimashauri ya Jiji la Dar es
salaam wakipambana kuzima moto uliolipuka na kuteketeza majiko ya soko
la Samaki la kimataifa la feli jana chanzo cha moto huo ni mlipuko wa
mafuta katika moja ya majiko ya kukaangia samaki.
|
Na Bahati Mohamed
WANACHAMA
wa Chama cha Tanzanian Labour Party (TLP), wamempa Mwenyekiti wa chama
hicho Taifa Bw. Augustino Mrema muda wa siku 40 awe amejiuzulu wadhifa
wake kwa madai ya kuchangia chama hicho kishindwe katika uchaguzi wa
mdogo wa ubunge Jimbo Arumeru Mashariki, mkoani Arusha. Aliyekuwa
Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Hamad Tao, aliyasema hayo Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema tamko la
kumtaka Bw. Mrema kujiuzulu analitoa kwa niaba ya wanachama wa chama
hicho kutokana na matokeo mabaya ya kura 18 walizopata katika kata zote
za jimbo hilo na kusisitiza kama atashindwa kujiuzulu ndani ya muda huo,
wataitisha maandamano nchi nzima ili kushinikiza aondoke.
“Bw.
Mrema alipewa fedha za kutosha kwa ajili ya kampeni lakini hatukuona
alichofanya zaidi ya kuzitumia kwa matumizi binafsi,” alisema Bw. Tao.
Aliongeza
kuwa, wanachama wa TLP hawakuridhishwa na uchaguzi uliofanyika katika
chama chao juu kumpata mtu ambaye atawania nafasi ya ubunge wa Afrika
Mashariki.
Alisema aliyechaguliwa kugombea nafasi hiyo kwa tiketi
ya TLP si mwanachama wa muda mrefu bali alipewa kadi ya uanachama
akitokea CCM ili aweze kuwania nafasi hiyo.
Bw. Tao aliipongeza CHADEMA kwa kupata ushindi katika uchaguzi uliofanyika Arumeru Mashariki.
|
TATIZO la rushwa nchini lipo katika sekta mbalimbali lakini hali hiyo haina maana kuwa inakubalika katika jamii. Ukweli
ni kwamba, rushwa haikubaliki kutokana na madhara yake ndio maana
Serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha vitendo hivyo
vinatokomezwa.
Rushwa inaathiri maendeleo ya mtu binafsi,
familia, Taifa na kushusha hadhi ya mtoaji na mpokeaji. Rushwa
inachangia kupindisha kanuni za maadili wakati wa kutekeleza majukumu
kwa maslahi ya umma, mtu au kikundi fulani.
Vitendo hivyo
vinajumuisha matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha baadhi ya
viongozi wa umma na sekta binafsi, kutumia madaraka waliyonayo kinyume
cha sheria ili kujinufaisha.
Rushwa 'imebatizwa' majina mengi, wengine huiita mlungula, kitu kidogo, shati la mikono mirefu au zawadi.
Watu
wanaojihusisha na vitendo hivyo, wanawanyima wananchi mategemeo ya kuwa
na maisha bora, kuwakosesha elimu, huduma bora za afya, chakula, maji
na mahitaji mengine ya kibinadamu.
Sisi tunasema kuwa, rushwa ni
wizi dhidi ya Taifa na wananchi ambao wanategemea maisha bora,
inachochea makosa ya jinai yanayovuka mipaka, kuvunja amani na utulivu.
Rushwa
ina madhara makubwa kiuchumi kwa lugha nyepesi ni uovu unaowavunja moyo
Watanzania na wafanyabiashara ambao wangependa kuwekeza nchini.
Inaongeza ugumu wa maisha kwa wananchi wakati mwingine husababisha kupungua ubora wa bidhaa ambazo huzalishwa viwandani.
Imani
yetu ni kwamba, rushwa husababisha mapato ya Serikali Kuu na Serikali
za Mitaa kupungua hivyo kupuguza uwezo wa kutoa huduma kwa wananchi
kutekeleza malengo ya kuboresha maisha yao na miundombinu ya nchi.
Uovu
wa rushwa unachangia kuongeza umaskini katika jamii, kuathiri ubora wa
elimu na sekta nyingine nchini. Rushwa inaweza kusababisha mgonjwa
asipone haraka au kupoteza maisha kama atakataa au kukosa kile
alichodaiwa kukitoa.
Tukifikia kiwango cha kuibubali rushwa kama
sehemu ya utamaduni wetu katika vyombo vya sheria, waathiriwa wataamua
kujilinda wenyewe kwa kuchukua sheria mkononi hivyo kuharibu sifa ya
amani na utulivu tulionao.
|
Na Godwin Msalichuma, Kilwa WAKULIMA wa korosho wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi, wamekitaka chama kikuu cha ushirika mkoani humo, Ilulu kutenga korosho kwa ajili ya kubangulia ili kuziongezea thamani ya zao hilo na zingine kuzitafutia soko nje ya nchi. Hali
hiyo itasaidia kuacha kutegemea wanunuzi wa kati ambao wengi wao ni
wababaishaji na wanachangia soko la zao hilo na hivyo kusababisha
mkulima kukosa malipo kwa wakati na kuendelea kulima kilimo kisicho na
tija.
Mwito huo ulitolewa hivi karibuni na wakulima hao waliokutana katika mkutano wa wadau wa kilimo ulioitishwa na shirika lisilo la kiserikali la kimataifa la Action Aid Internainal Tanzania (AAIT) ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kuimarisha na kukuza kilimo cha zao hilo wilayani humo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha maendeleo ya wananchi mjini Kilwa masoko.
Walisema ili kuondokana na ubabaishaji unaofanywa na wanunuzi wa kati ni vyema Ilulu ikatafuta soko la zao hilo nje ya nchi na kuuza ,moja kwa moja kwa wanunuzi wakubwa mara baada ya kukusanya korosho kutoka kwa wakulima na kuachana na utaratibu wa sasa ambapo chama hicho kinawauzia wanunuzi wa kati ambao nao wanaenda kuuza kwa wanunuzi wakubwa wanauza nje ya nchi. “Mfumo wa ununuzi unaotumika ni mzuri lakini linapokuja suala la soko ndio tatizo linapoanzia hapo…tunadhani ili kuondokana na tatizo hili ni vyema chama chetu kikuu kikatafuta soko nje ya nchi…lakini pia kiwe na mipango madhubuti ya kubangua angalau kiasi kidogo ili kuongeza thamani korosho zetu”, alisema Bw.Yusufu Mcheni Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha TAPWA.
Naye Bw. Athumani Kingolopi wa Chama cha Msingi Ujirani Mwema , alisema kuwa ununuzi ulikwenda vizuri mwaka jana chini ya mfumo wa stakabadhi ghalani na kuwa mfamo mzuri wa kuigwa, lakini mwaka huu wanunuzi waligoma kununua kwa bei nzuri mnadani na hivyo kuyumbisha wakulima ambao wengi wao hadi leo hawajalipwa malipo yao ya pili.
“Kwa maoni yangu naona ni bora tutenge kiasi fulani kwaajili ya kubangua na zinazobaki zikuzanywe na kuuzwa moja kwa moja nje ya nchi ili kuondokana na tatizo hili na kumuongezea mkulima kipato…hawa wanunuzi wa kati wanatuyumbisha”, alisema Bw. Kingolopi.
Awali Mkuu wa Idara ya Kilimo na Usalama wa Chakula kutoka Action aid Makao Makuu, Bw. Elias Mtinda, alisema kuwa shirika hilo lipo tayari kuwadhamini wakulima hao ili kupata mkopo kutoka vyombo vya fedha kwa ajili ya kununulia mashine za kubangulia korosho zao.
|
Na Said Hauni, Lindi
WATU
wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamevamia makazi ya viongozi wa dini ya
Kikristo Parokia ya Nyangao Wilaya na Mkoa wa Lindi huku wakipora fedha
taslimu sh. milioni tano.
Pia
inadaiwa licha ya kupora fedha hizo viongozi hao, ilidaiwa walijeruhiwa
watu wanne wakiwemo viongozi wawili na walinzi wao wawili kwa
kuwacharanga mapanga sehemu mbalimbali ya miili yao.
Habari
kutoka Kata ya Nyangao ambazo zilithibitishwa na Jeshi la Polisi mkoani
hapa zilieleza kuwa tukio hilo lilifanyika Machi 30, mwaka huu majira ya
saa 6:45 za usiku.
Kaimu Kamanda wa Polisi, Bw. George
Mwakajinga alisema katika tukio hilo watu watatu kati ya hao
walishambuliwa kwa kupigwa mapanga sehemu mbalimbali za miili yao wakati
mmoja alifungwa kamba na kutupiwa kwenye shimo la taka.
Bw.
Mwakajinga aliwataja walioshambuliwa kuwa ni ni, Paroko Housiager Hugo
(74) na Padri Michael Mrope (75), Bw. Victor Hanga (58) na Joseph
Mathias (45) ambao ni walinzi wa nyumba za viongozi hao.
Alisema,
Bw.Hugo ambaye kwa sasa amelazwa Hospitali ya Mision ya Ndanda iliyopo
Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara alipigwa mapanga kichwani na mbavuni
ambapo, Bw. Hanga ambaye ni mlinzi pia alijeruhiwa na panga kichwani na
kulazwa Hospitali Teule ya Nyangao.
Pia aliongeza kuwa Padri
Mrope alishambuliwa kwa kupigwa huku mlinzi wake, Bw. Michael akifungwa
kamba na kutupiwa kwenye shimo la taka hadi majambazi hayo yalipoondoka
na kuokolewa na askari polisi waliofika kwenye eneo hilo.
Alisema,
majambazi hayo ambayo yanasadikiwa kufikia zaidi ya 10 walikuwa na
silaa mbalimbali yakiwemo mapanga, marungu na bunduki na walivamia
makazi ya viongozi hao na kufanikiwa kupora fedha taslimu kiasi cha
shilingi milioni tano na kutokomea nazo kusikojulikana.
“Kabla
hawajazichukuwa fedha hizo walipambana na walinzi waliokuwa wakiwalinda,
lakini walizidiwa nguvu na ndipo majambazi hayo yalimfunga kamba mlinzi
mmoja na mwingine kumjeruhi kwa panga kichwani,” alisema Bw.
Mwakajinga.
Kaimu Kamanda huyo alisema katika tukio hilo hakuna
mtu ambaye amekamatwa hadi sasa na kwamba askari wanaendelea na kazi ya
kuyasaka majambazi hayo ili yaweze kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo
kuwafikisha mahakamani.
Baadhi ya wananchi wanaodai waliweza
kushuhudia sakata hilo lakini walishindwa kujitokeza kutoa msaada
kutokana na majambazi hayo kufyatua risasi mbili hewani ambapo
yalielekea kwenye makazi ya viongozi hao wakiwa kwenye gari moja aina ya
Toyota 'Pick Up'.
|
Radhia Ramadhani na Joyce Kambota
WATU
wanne raia wa Nigeria wamekamatwa na madawa ya kulevya aina ya HEROINE
yenye thamani ya shilingi bilioni 1 .4 za kitanzania jijini Dar es
Salaam. Akizungumza na waandishi wa
habari Dar e Salaam, Kamanda wa Polisi kanda maalum mkoa wa Dar
es Salaam Bw. Suleiman Kova alisema watuhumiwa wa kesi hiyo sio
watanzania ni wanaigeria waishio maeneo ya Tabata kinyerezi kibaga.
"
Tukio hilo limekuwa la ajabu sana kwani hatujawahi kukamata dawa za
aina hiyo zilizokuja kwa dizaini ya pakti za chumvi tena zimekaushwa"
alisema Kamanda Kova.
Watuhumiwa hao waliotambulika kama
Bw.Ifeanyi Oko(33),Bw.Uchendu Jerry(35),Bw.Ugwu Valentine(31) na Bi.
Ani Lawretta(27)mbali na kukamatwa na paketi nne pia wamekutwa na kete
12 za madawa zilizokuwa tayari kwa kumezwa.
Kamanda Kova
aliongeza kuwa hadi sasa nchini kumekuwa na mtandao wa madawa ya kulevya
kutoka nchi za nje hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuwafichua watu
ambao wana mashaka nao.
Wakati huohuo Kamanda Kova alisema
walifanikiwa kuwakamata waalifu Sugu (84) kwa tuhuma mbalimbali kufuatia
misako inayoendelea ili kuhakikisha hali ya jiji la Dar es Salaam ni
tulivu.
"Miongoni mwa vitu ambavyo tunaweza kujivunia jeshi la
polisi ni pamoja na juhudi zilizofanywa na kikosi maalum wakishirikiana
na ulinzi shirikishi kwa kufanya dolia na kuwakamata waarifu hao"alisema
Kova.
Baadhi ya watuhumiwa hao ni Bw.Rashid Seif(25),Bi.Habiba
Juma(22),Bw.Ramadhan Suleiman(30),Bw.Shaban Adam(33),Bw.Salehe
Omary(17)na wengine79.
|
MA D I WA N I w a Halmashauri
ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wamesema kupungua kwa ukusanyaji wa
mapato ya halmashauri hiyo ni dalili inayotokana na uvujaji wa fedha
unaofanywa na baadhi ya watumishi.Pia walidai hali hiyo imekuwa ikichangia baadhi ya watumishi kuvujisha na hata kughushi stakabadhi za kukusanyia mapato. Imeelezwa kuwa watumishi hao wamekuwa wakiigeuza halmashauri hiyo kama shamba la bibi kwa kuchota fedha watakavyo na hivyo kusababisha kushuka kwa mapato kutoka sh. milioni 600 zilizokusanywa mwaka jana hadi kufikia sh. milioni 300 mwaka huu. Hayo yalisemwa juzi wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika Ukumbi wa John Mwankenja ambapo walisema kama vitendo vya ufujaji fedha vinavyofanywa na baadhi ya watendaji vitaendelea itabidi Mkurugenzi wa wilaya hiyo Bw. Noel Mahyenga pamoja na Mweka Hazina wa halmashauri Bw. John Shirima wawajibike. Akizungumza katika kikao hicho Diwani wa Kata ya Masukulu, Bw. Rephson Mwaisupule alisema, miezi mitatu iliyopita katika kipindi cha mwaka jana fedha zilizokuwa zimekusanywa katika vyanzo vya ndani vya mapato zilikuwa sh. milioni 600 lakini katika hali ya kushangaza mwaka huu zilizokusanywa ni sh. milioni 300 tu. Naye Diwani wa Kata ya Kawetele Bw. Anyimike Mwasakilali alisema tatizo la ufujaji wa fedha za mapato katika halmasahauri hiyo ni aibu hivyo inatakiwa watendaji wote waliofanya ubadhirifu huo kuchukuliwa hatua za kisheria wakiwemo watendaji wa kata na vijiji wanakusanya fedha katika kata zao na vijiji. Naye Diwani wa Kata ya Lwangwa Bw. Robart Mwaibata alisema baadhi ya watumishi wamekuwa wakiandika ushuru ma l i p o ma k u bwa ka t i k a stakabadhi za malipo lakini fedha zinazofikishwa halmashauri ni kidogo hali ambayo imekuwa ikisababisha halmashauri kujikuta haina mapato ya kutosha. Akizungumzia malalamiko hayo ya madiwani Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bw. Meckison Mwakipunga alisemna kuwa halmashauri tayari imeanza kuchukua hatua dhidi ya watendaji wanaofuja fedha ambapo hadi sasa watumishi 11 wa halmashauri hiyo wamesimamishwa kazi. Alisema kuwa, tayari watumishi hao hawapo kazini baada ya kubainika kufuja fedha hizo na uchunguzi zaidi unaendelea kuhusiana na ufujaji huo ili kujua kama kuna watumishi wengine waliofanya ubadhirifu huo nao waweze kuchukuliwa hatua kama walivyochukuliwa hawa wengine. Tunachoomba ni ushirikiano kwa nyie madiwani kwenye kamati ya fedha ambayo tayari ipo, kazini kushughulikia ubadhirifu huo, tunajua tutawabaini wengine ambao wamejificha kwani fedha hizo zimefunjwa na wengi, alisema Mwenyekiti huyo.
|
Raisi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. JakayaKikwete ajuwa na
mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa kamuni ya UnileverGlobal, Bw. Paul
Polman, Ikulu jijini Dar es Salaam jana. (Picha na Ikulu)
|
Anneth Kagenda na Flora Amon
HALMASHAURI
y a Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara imepewa siku 14 kuwa imepeleka
mchanganuo mpya ambao pamoja na mambo mengine uwe unaainisha vizuri
matumizi ya sh. milioni 77 ambazo inadaiwa kuwalipa wafanyakazi hewa.
Agizo hili lilitolewa Dar es Salaam jana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati
ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Bw. Idd Azzan. Alisema halmashauri hiyo imetumia fedha hizo kuwalipa wafanyakazi hewa na watu waliostaafu, jambo ambalo ni kinyume cha sheria. Alisema watu waliolipwa fedha hizo watatakiwa kuzirudisha na ikiwa watakaidi sheria itachukua mkondo wake. Alisema kuwa halmashauri hiyo inatakiwa kuwabana ili wazirudishe pamoja na kutoa mchanganuo unaoeleweka juu ya fedha sh. milioni 119 ambazo zilikuwa ni za ujenzi wa zahanati. "Tunaomba maagizo yote tuliyotoa yatekelezwe kwa muda muafaka, lakini pia ikumbukwe kwamba kamati imesikitishwa kuona hoja zingine zimeshindwa kupatiwa majibu yanayoeleweka," alisema. Mwenyekiti huyo aliitaka halmashauri hiyo kuwa makini mara tu zinapotakiwa kuwasilisha michanganuo inayoonesha utendaji wao, kutoa ushirikiano kati ya halmashauri ya Babati Mjini na Vijijini. Naye Mwenyekiti wa LAAT Bw. Augustino Mrema, alitoa onyo kali kwa halmashauri hiyo na kusema; "Lazima makosa yao yatafutiwe adhabu ya onyo la mdomo ili kuleta tija" alisema. Wakati huo huo,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetakiwa kupunguza matumizi ya fedha kwenye semina, maonsho. Hayo yalibainisha Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Hesabu za Serikali Bi.Zainabu Vullu,wakati wakupitia hesabu za wizara hiyo. Bi.Vullu alisema, sh. Bilion 1.9 zimetumika kinyume na bajeti ikiwemo sh. milion 729 kutumika kwenye sherehe za nane nane mjini Dodoma. Alisema mbali na fedha hizo pia Wizara ilichangisha kwa Taasis mabalimbali sh. miloni 86.kwa ajili ya sherehe ya nane
|
Watoto
wakicheza kwa kuning'inia katika gari lilokuwa Mtaa wa Braziri eneo la
Kinondoni,Dar es salaam.bila kujua kuwa wanahatarisha usalama
wao.
|
Anneth Kagenda na Frola Amon
ADHA y a k u k a t i k a umeme mara kwa mara imewawakumba wabunge waliokuwa wakihudhuria vikao vya kamati za bunge kwenye Ofisi Ndogo ya Bunge, hatua iliyowalazimu kuahirisha vikao hivyo. Akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) Mwenyekiti wake, Bw. John Cheyo, alisema kutokana na adha hiyo, walilazimika kusitisha vikao vyao baada ya kusubiri umeme urudi bila
mafanikio. "Waheshimiwa wajumbe naahirisha kamati hadi (kesho) kwani leo, hatuwezi kuendelea bila umeme," alisema Bw. Cheyo. Wakati akiahirisha kikao hicho tayari watendaji wa Idara ya Mwasibu Mkuu wa serikali walikuwa wamefika ofisi za bunge kuwasilisha taarifa za matumizi ya fedha. Kwa upande wak e Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Bw. Augustino Mrema, yeye alisitisha kusikiliza mchanganuo wa ripoti ya mkoa wa Singida kutokana na matatizo hayo ya umeme. Wa k i z u n g u m z a n a waandishi wa habari baadhi ya wabunge walisema kukatika kwa umeme kunaathiri shughuli nyingi nchini. Mbunge wa Mufindi Kusini Bw. Mendrad Kigola alisema "Kukatika kwa umeme kumetuadhiri kwani mambo mengi yameshindwa
|
Na Charles Mwakipesile, Mbeya
MKUU
wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro, amesema mafisadi wanaoiba dawa za
Serikali, kuzipeleka kwenye maduka ya watu binafsi na kusababisha uhaba
mkubwa wa dawa katika Bohari Kuu (MSD), hawawezi kuvumiliwa. Bw.
Kandoro aliyasema hayo jana mjini Mbeya wakati akifungua warsha ya siku
moja iliyoshirikisha wadau wa MSD kutoka mikoa ya Singida, Dodoma,
Iringa na Njombe.
Alisema Serikali imekuwa ikishuhudia uhaba
mkubwa wa dawa uliopo MSD wakati maduka binafsi yanauza dawa za Serikali
ambazo haziruhusiwi kuuzwa katika maduka hayo.
“Kimsingi
Serikali inatumia mabilioni ya fedha kuhakikisha MSD inakuwa na dawa za
kutosha ambazo zitasambazwa katika hospitali ili ziweze kuwasaidia
Watanzania,” alisema.
Aliongeza kuwa, Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii inapaswa kufanya uchunguzi katika maduka binafsi kubaini mafisadi
wa dawa ili wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria iwe
fundisho kwa watu wengine wenye tabia hiyo.
Bw. Kandoro alisema
tabia ya wizi wa dawa unafanywa na watu wasio na nia njema na uchumi wa
nchi ambao unategemea watu wenye nguvu na afya bora hivyo kinachotakiwa
kufanya uchunguzi ili kuwabaini watu wanaofanya ufisadi wa kuiba dawa
MSD.
“Nawaonya wauzaji dawa katika maduka binafsi kuacha tabia ya
kuuza dawa zilizopita muda wake, kitendo hiki ni sawa na uuaji kwani
matumizi yake ni sawa na sumu mwilini hivyo kusababisha madhara makubwa
kwa mtumiaji kiafya,” alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
Huduma za Kanda, Bw. Cosmas Mwaifwani, alisema MSD imejipanga
kuhakikisha inawahudumia Watanzania kwa kiwango stahiki na kukidhi
mahitaji yao.
Alisema katika mpango wa muda mfupi, wamejipanga
kuhakikisha wanakuwa na utaratibu wa kufikisha dawa hadi vituo vya afya
kwa ajili ya kumaliza tatizo la upungufu na upatikanaji wa dawa.
Aliongeza kuwa, mawakala wamekuwa wakichelewa kupeleka maombi ya dawa MSD hivyo kusababisha zisipatikane kwa wakati.
|
Na Zahoro Mlanzi
KIKAO
cha Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), kimeshindwa kumalizika juzi kama ilivyotarajiwa kutokana
na wajumbe waliohudhuria kikao hicho, baada ya kutokea mvutano katika
kufikia muafaka wa rufani zilizowasilishwa na Klabu ya Yanga.Kikao
hicho kilianza juzi jioni na kuendelea tena jana chini ya Mwenyekiti
wake Kamanda Mstaafu wa Polisi, Alfred Tibaigana akiwa na baadhi ya
wajumbe wake pamoja na viongozi wa Yanga, wajumbe wa Kamati ya Ligi na
wawakilishi wa TFF.Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana
baada ya kuulizwa kilichofikiwa katika kikao cha kamati hiyo
iliyokutana juzi, Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface Wambura
alisema kikao kilishindwa kumalizika na kwamba kilitarajiwa kumalizika
jana usiku."Kwa kweli hatutaweza kutoa taarifa juu ya
kilichoamuliwa katika kikao hicho kama nilivyoahidi kutokana na kuwa
hakikumalizika, hivyo kinaendelea leo (jana) jioni na kwamba
watakalofikia lolote kesho (leo) au keshokutwa tutatoa taarifa," alisema
Wambura.Kikubwa katika rufani hiyo, Yanga walipinga adhabu
iliyotolewa na Kamati ya Ligi ya kuwafungia wachezaji wao watano, pamoja
na kupinga maamuzi yaliyotolewa na mwamuzi Israel Nkongo, katika mechi
yao hiyo dhidi ya Azam FC.Wachezaji waliofungiwa ni Stephano
Mwasika aliyefungiwa mwaka mmoja na faini ya sh. milioni moja, Jerry
Tegete kifungo cha miezi sita na faini ya sh. 500,000, Nadir Haroub
'Cannavaro' alifungiwa mechi sita na faini ya sh. 500,000, Omega Seme na
Nurdin Bakari wao walifungiwa mechi tatu kila mmoja.Kutokana na
adhabu hiyo, Yanga ilikata rufani kwa Kamati ya Tibaigana ambapo baada
ya kamati hiyo kuomba vielelezo kwa kamati husika na kukosekana iliamua
kuzisimamisha kwa siku 14 kutoa nafasi ili kupata ushahidi wa kutosha
isipokuwa kwa zile zilizotolewa ndani ya dakika 90 ya mchezo.Wakati
hilo, likiwa bado halijapatiwa ufumbuzi kamati ya ligi ikaipoka Yanga
pointi tatu na kuipa Coastal Union ya Tanga, pamoja na mabao mawili
kutokana na kumchezesha Canavaro ikidaiwa hajamaliza adhabu aliyotakiwa
kuitumikia ya kukosa mechi tatu kitu ambacho kimeibua mjadala mwingine
upya.Katika hatua nyingine, alipotafutwa Ofisa habari wa Yanga,
Louis Sendeu kuthibitisha kwamba wamekata rufani juu ya kupokwa pointi,
alisema wanasubiri kwanza maamuzi ya Kamati ya Nidhani, ndipo watajua la
kufanya.Hata hivyo wakati gazeti hili linakwenda mitamboni,
zilipatikana taarifa kwamba katika hicho cha Kamati ya Nidhamu kulikuwa
na mvutano mkubwa huku Kamati ya Ligi ikionekana kuzidiwa hoja na
wajumbe wengine juu ya adhabu walizotoa kwa wachezaji wa Yanga.
|