TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, January 10, 2013

KANISA LA VISITATION CATHOLIC PARISH-PAROKIA YA MAWELLA, KITOVU CHA MASOMO YA BIBLIA MJINI MOSHI


 Mwalimu wa Masomo ya Biblia wa kanisa la Visitation Catholic- Parokia ya Mawella- Jimbo la Moshi Mjini ,akifundisha katika Kanisa hilo mapema Asubuhi leo.

Wednesday, January 9, 2013

RAIS DK. SHEIN AZINDUA SHULI YA MADUNGU PEMBA

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipowasili
kufungua Skuli ya Sekondari ya Madungu Wilaya Chake chake Pemba
jana,katika kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar,{Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.}
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akifunua pazia kuashiria kufunguliwa kwa  Skuli ya Sekondari ya Madungu Wilaya
Chake chake Pemba jana,katika kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali
Juma Shamuhuna,{Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.}
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,Akifungua Skuli ya Sekondari ya Madungu Wilaya Chake chake Pemba
jana,katika kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar,{Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.}

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akitembelea katika maabara ya Skuli ya Sekondari ya Madungu
Wilaya Chake chake Pemba jana,baada ya kuifungua rasmi katika
kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,{Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.}
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akitembelea katika chumba cha maktaba  ya Skuli ya Sekondari ya
Madungu Wilaya Chake chake Pemba jana,baada ya kuifungua rasmi katika
kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,{Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.}

Mwisho wa kubadilisha Leseni mpya za madereva ni Machi 31 Mwaka huu

 
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Mohamed Mpinga.
…………………………………………………………………
Na Mobini Sarya, Tanpress
JESHI la Polisi nchini kwa kushirikiana na Mamlaka mapato nchini (TRA) limeboresha mfumo wa utoaji leseni za udereva ambazo zimeanza kutolewa kwa njia aya Smart Card ili kuendana na ukuaji wa Teknolojia duniani.
Wakizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mnadhimu  wa kikosi cha usalama barabarani ACP Johandani Kahatano na Naibu Kamishna wa TRA Yusuph Salum wamesema kuwa mwisho wa kubadilisha leseni kwa maedeleva wote ni Machi 31 Mwaka huu.
Wameeleza kuwa baada ya muda huo zoezi la ubadilishaji Leseni za aina zote halitafanyika na mfumo wa utoaji Leseni utabadilishwa ili kubakia na uwezo wa kutoa Lesseni kwa madereva wanaoomba Lesseni kwa mara ya kwanza.
Hivyo madereva wote wametakiwa kuhakikisha wanatumia muda huo wa miezi mitatu iliyotolewa kubadilisha Leseni zao ili kujiepusha na usumbufu unaoweza kuwapata.
Aidha Kamanda Kahatano amesema kuwa Dereva atakayekutwa anaendesha gari wakati leseni yake imekwisha atafikishwa mahakamani pamoja na mmiliki wa gari hilo.
     Zoezi la kutoa leseni mpya za udereva lilianza Oktoba Mosi  Mwaka 2010 kwa awamu ya kwanza iliyohusisha mikoa (9) na machi 2011 mikoa mingine 13 ilianza kutoa leseni hivyo zoezi hilo kukamilika.
Kamanda huyo amesema kuwa madhumini ya zoezi hilo ni kubadili mfumo huo na kuondoa tatizo la kughushi pamoja na kudhibiti mienendo ya madreva kwa kutunza kumbukumbuku za makosa yao.
Hadi kufikia Disemba 31 Mwaka jana leseni 616,349 zilizokuwa zimetolewa kwa nchi nzima ambapo kati ya hizo leseni 135721 ni za kundi lenye madaraja C zingine 480,628 ni za makundi mengine.
Hata hivyo takwimu hizo zikilinganishwa na idadi ya vyombo vya moto vilivyosajiliwa na Mamlaka ya TRA nchini hadi kufikia Disemba 2012 vinafikia 1,164,574 hiyo inaoonyesha kuwa kuna madereva wanaoendesha vyombo vya moto bila ya kuwa na leseni halali.

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AFUNGUA SKULI YA MBUYU TENDE ZANZIBAR

 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamhuna mara alipowasili katika Kijiji cha Mbuyu Tende Wilaya ya Kaskazini “A”kwa ajili ya kufungua Skuli ya Primary yenye madarasa Manne,ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikata Utepe kuashiria kufungua Skuli yenye madarasa manne katika Kijiji cha Mbuyu Tende Wilaya ya Kaskazini “A”,ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akipanda Mche wa Mnazi baada ya kuupanda katika eneo la Skuli ya Mbuyu Tende Wilaya ya Kaskazini “A”,Baada ya Kuifungua Skuli hiyo ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Wanafunzi wa Skuli ya Mbuyu Tende Wilaya ya Kaskazini “A”,wakifurahia Baada ya 
kufunguliwa kwa Skuli yao ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
……………………………………………………….

                     Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar                      
 Makamo wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad amewataka Wazazi na Walezi wa Wanafunzi wa Skuli ya Mbuyu Tende kujenga Mashirikiano na Walimu ili  kuweza kuwapatia  haki na fursa sawa wanafunzi wa kike na wakiume Skulini hapo.      
Hayo ameyasema leo huko Skuli ya Msingi Mbuyu Tende Wilaya Kaskazini “A” Unguja wakati wa ufunguzi wa skuli hiyo ikiwa ni mwendelezo wa shamra shamra za kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Maalim Seif  amewataka Wazazi wasikubali kuwaozesha watoto wa kike waume mapema kwani hali hiyo ndiyo inayochangia ukosefu wa Walimu wa kike wazawa katika Vijiji  vingi.
 Aidha alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaendelea kuwapatia wananchi wake haki ya elimu bila ya malipo ili kuondosha adui ujinga na kuwaletea maendeleo.
  “Elimu ni msingi wa maisha kwa vijana na ndio inayoleta maendeleo na mwangaza hasa wakati wa sasa na ujinga ni kiza katika maisha ya leo,”alisisitiza Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Nyota wa Seattle Sounders FC kuendesha semina ya soka nchini

 
Mchezaji Kasey Keller wa klabu ya Seattle Sounders ya Marekani.
 
Aliyekuwa Kipa Marc Burchklabu ya Seattle Sounders ya Marekani
………………………………………………………………………
WAWAKILISHI wawili wa klabu ya Seattle Sounders ya Marekani  wataendesha semina kwa wadau wa michezo  hapa nchini katika ziara yao ya siku tisa kuanzia leo.
Wawakilishi hao ni beki wa timu hiyo, Marc Burch na kipa aliyestaafu  ambaye kwa sasa ni mtangazaji , Kasey Keller .
Wakiwa nchini, wachezaji hao wataendesha semina kwa vilabu vya Ligi Kuu ya Tanzania Bara na shule za msingi katika siku na muda ambao  utangazwa hapo baadaye. Z
iara hiyo ni moja ya kukuza ushirikiano baina ya Seattle Sounders na  wadau wa michezo nchini na ikumbukwe kuwa timu hiyo iliwahi kumchukua mchezaji nyota wa Tanzania, Mrisho Ngassa kucheza mechi ya kihistoria dhidi ya timu ya Manchester United.
Kwa kushirikiana na Washington Global Health Alliance (WGHA),  wawakilsihi wa timu hiyo pia watatembelea miradi mitatu ya upande wa afya iliyopo mkoani Arusha  ikiwa pamoja na World Vision, taasisu ya PATH  na Chuo kijulikanacho kwa jina la Washington State University’s Paul G. Allen School for Global Animal.
 ”Ziara hii itadumisha na kuhimarisha uhusiano wetu na serikali ya Tanzania, “ alisema Mmiliki wa timu hiyo, Joe Roth ambaye pia alisema Kesey na March watakuwa mabalozi wakubwa wa timu yao katika ziara hiyo.
Alisema kuwa wajumbe hao pia watatembelea vivutio vya utalii kama Ngorongoro Crater na jiji kubwa la Tanzania, Dar es Salaam. Timu hiyo ya Marekani iliingia katika ushirikiano na WGHA mwaka 2009. Mpango huo una lengo la kushughulika na masuala ya afya kwa binadamu nchini na Kimataifa.

Wamiliki wa vyombo vya habari nchini, (MOAT)waaswa kuzingatia maadili

WAMILIKI wa vyombo vya habari nchini, (MOAT),wameaswa kuzingatia muda na wakati wa kurusha matangazo katika vyombo vyao, kwa sababu baadhi yake yameonekana  kupoteza maadili kwa jamii hususani watoto ambao ni Taifa la baadaye.
Akizungumza na FULLSHANGWEBLOG jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Taasisi ya kupambana na Udanganyifu wa matumizi ya rasilimali za Taifa (CFRI), Andendekisye Mwakabalula, alieleza kuwa kutokana na mfumo mbaya wa matangazo hususankatika televisheni  utasababisha madhara kwa kizazi hiki na cha baadaye.
Katika hilo, aliwataka wamiliki hao kuangalia njia mbadala ambayo haitaleta madhara kwa jamii pindi wa matangazo hayo yatakaporushwa au kuonyeshwa kwenye vyombo hivyo.
Mwakabalula aliyataja baadhi ya matangazo ambayo yanachochea uvunjifu wa maadili ni mfano wa matangazo ya mpira wa kiume ‘kondomu’,filamu za ngono pamoja na mengine ambayo hayafundishi maadili bali yanapotosha.
 “Ikiwa wamiliki wa vyombo vya habari wamebaini wazi kuwa maadili ya nchi yameporomoka, walitakiwa kuwa mifano mizuri ya kuigwa ndani ya jamii, hususani kwa kutumia fursa ya matangazo yanayoibadili katika suala zima la maadili” alisema Mwakabalula
Aidha, alisema ikiwa wamiliki hao watatumia vyombo vyao kuhamasisha juu ya maambukizi ya virusi vya ukimwi (HIV), kupitia matangazo mbalimbali basi waangalia muda na wakati wa kuyaonyesha kwa lengo la kutowaumiza watoto ambao hawajafikia umri wa kuyasikiliza au kuyatizama.
Pamoja na hilo, aliitaka Katiba mpya kupitia mchakato wa mapendekezo ya maoni ya wananchi, kuangalia namna ya kuiweka kipengele cha mkakati huo wa matumizi ya  matangazo ili kuleta uwiano na manufaa ndani ya jamii.

WAZIRI MKUU PINDA AZINDUA KITABU CHA WAPIMBWE

    
*Ataka makabila mengine yatunze historia zao.
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amezindua kitabu cha historia ya kabila la Wapimbwe lililoko mkoani Katavi na kutayataka makabila mengine kuandika historia zao ili waweze kutunza kumbukumbu kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Akizindua kitabu hicho hivi karibuni mjini Mpanda, Waziri Mkuu aliwataka watu wa makabila mengine ya mkoa wa Katavi ambayo ni Waruira, Wabende, Wakonongo na Warungwa wafanye tafiti kuhusu mila na tamaduni zao na kisha waandike vitabu vyao.
Kabla ya uzinduzi huo, mtunzi wa kitabu hicho, Bw. Peter Mgawe alisema kitabu hicho kimetokana na utafiti uliofanywa tangu mwaka 2007 ambao ulilenga kukusanya  taarifa na masimulizi mbalimbali kutoka kwa wazee wa Kipimbwe ambao wameishi miaka mingi huku wakiwa na hazina ya mila na tamaduni za kabila hilo ambalo pia ni kabila lake Waziri Mkuu Pinda. 
“Hili ni kabila dogo lisilofahamika na wengi, nimekuwa nikitafuta taarifa na machapisho (literature) mbalimbali kuhusu kabila hili lakini sikuwahi kupata chochote… ndipo nikamshirikisha Mheshimiwa Waziri Mkuu juuya kufanya utafiti na kuandika historia yetu naye akalikubali wazo langu,” alisema Bw. Mgawe ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Dar es Salaam.
Akizungumza na wakazi waliohudhuria uzinduzi huo, Waziri Mkuu alisema utafiti huo usiishie hapo tu, bali wafanye tafiti nyingine kuhusu mavazi, vyakula, ndege, wanyama waliokuwa wakipendelewa na mababu zao ili kuongeza hazina ya taarifa ya kabila hilo.
“Lengo la kitabu hiki lilikuwa ni kuhifadhi katika maandishi historia ambayo ilikuwa imefichika ndani ya vichwa vya wazee wetu kutoka vijiji mbalimbali vya Mpimbwe… nafurahi kwamba tunao wazee watatu waliokuwa katika warsha ya kwanza kabisa iliyofanyika mwaka 2008. Leo hii wako hapa na wanashuhudia matunda ya kazi yao,” alisema Waziri Mkuu.
Wazee hao ni Mzee Simba Pangani Kalulu (76) kutoka kijiji cha Mamba, Mzee Valeri Kipande (76)  kutoka kijiji cha Lyangalile na Mzee Moses Kasalani (67) kutoka kijiji cha Mirumba. Vijiji vyote hivyo viko wilaya ya Mlele, mkoani Katavi.
Waziri Mkuu amerejea jijini Dar es Salaam leo mchana (Jumanne, Januari 9, 2013) akitokea kijijini kwake Kibaoni, wilayani Mlele, Katavi ambako alifanya ziara ya siku 10 kwenye jimbo lake la Katavi na kisha kuwa na mapumziko ya Krismasi na mwisho wa mwaka.

WANA NCHI WA KATA YA ITENKA .A. WAPANDA JUU YA MITI KUMUONA WAZIRI MKUU ALIPOKUWA ANAWAHUTUBIA

 
Wana nchi wa kata ya Itenka A jimbo la katavi wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Mh waziri mkuu Mizengo Pinda alipo kuwa ana hutubia kuhimiza watu kulima kwa kutumia kilimo cha kisasa mwishoni mwa wiki wana nchi wengine walilazimika kupanda juu ya miti (Picha na Chris Mfinanga)
 
Mke wa Waziri mkuu Mh Tunu Pinda akiwa ana sugua chungu ambacho hutumika katika ngoma marufu itwayo Nsimba  ya kabila la wapimbwe ambayo ilikuwa ikichezwa katika kata ya Itenka A na kikundi hicho  kinaitwa Pinda (Picha na Chris Mfinanga)

KAMPUN YA SIMU ZA MKONONI TIGO YAZINDUA OFA MPYA YA “TIGO TIME”

 
Mtaalamu wa kubuni Ofa kutoka kampuni ya simu za mkononi ya TIGO Jacqueline Nnunduma akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena Dar es salaam leo jijini Dar es salaam kuielezea ofa hiyo.
……………………………………………..
Tigo imetambulisha huduma mpya kwa wateja ujulikanayo kama Tigo Time, ambayo inatoa punguzo kubwa sana la gharama ya kupiga simu masaa ishirini na nne kwa wiki (24/7 ikitegemeana na muda na wakati wa siku na eneo mteja atakalokuwa.
Kusajili  huduma kwa mteja piga *149*90# au tuma neno “TIGO TIME” kwenda namba “15372” na baada ya hapo utapokea ujumbe ambao utaonyesha kwamba umefanikiwa kusajili na unaweza kuanza kutumia huduma hii na ufurahie punguzo kubwa sana la gharama. Baada ya kusajili, Tigo Time itakujulisha punguzo lako la gharama la kupiga simu kutokana na  muda wa siku  na eneo ulipo. Gharama ya huduma hii  ya kusajili itakuwa ni Tshs 149 kwa kiwango cha chini.
“Tigo inatambua kwamba wateja wetu wanahitaji huduma bora na kwa gharama nafuu na hii ni njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma zenye ubora wa juu na vifurushi ambavyo vitawapatia unafuu wa bei kwa muda wowote.” Alisema Bi. Jacqueline Nnunduma, Mbunifu wa ofa za Tigo. “Kwa punguzo hili kubwa la bei lililopita kifani, hakuna shaka kuwa Tigo Time itakuwa huduma maarufu kama ilivyokuwa huduma ya ya Kwa Sekunde tuliyoianzisha miaka kadhaa iliyopita.” Alimalizia Bi. Nnunduma. 

ALIOFUZU KUINGIA KWENYE SHINDANO LA GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE WAKABIDHIWA HATI ZAO ZA KUSAFIRIA NA MAELEKEZO YA SAFARI YA AFRIKA KUSINI



Meneja wa kinywaji cha Guinness kutoka kampuni ya bia ya Serengeti akikabidhi hati ya kusafiria kwa Lukwesa Kanakamfumu, mmoja wa washiriki wa Guinness Football Challenge washiriki wa shindano hilo wanatarajiwa kuondoka mwishoni mwa wiki hii kuelekea Afrika Kusini
 
Wakiwa katika picha ya pamoja meneja wa kinywaji cha Guinness Davis Kambi(katikati) na washiriki wa Guinness Football Challenge baada ya kupokea hati zao za kusafiria
 
Mratibu wa safari Bi. Caroline akitoa maelekezo na taratibu za safari kwa washiriki waliofuzu kuingia katika mashindano ya Guinness Football Challenge wanaotarajiwa kusafiri karibuni.

RAIS WA ZANZIBAR DK ALI MOHD SHEIN AFUNGUA BARABARA YA MFENESINI-BUMBWINI KASKAZINI UNGUJA


 
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein akikunjuwa kitambaa kuashiria Ufunguzi wa Barabara ya  Mfenesini Bumbwini iliojengwa na Kampuni ya Mecco,ikiwa ni katika shamra shamra za  kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein wamwanzo kulia akikata utepe pamoja na Mwakilishi Mkaazi wa Benki ya Maendeleo ya Africa (AFDP)Tonia Kandiero katika ufunguzi wa Barabara ya  Mfenesini Bumbwini iliojengwa na Kampuni ya Mecco,ikiwa ni katika shamra shamra za  kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein katikati akitembea kwa Miguu katika Barabara ya Mfenesini Bumbwini baada ya kuifungua rasmi,ikiwa ni katika shamra shamra za  kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika sherehe za Ufunguzi wa Barabara ya Mfenesini Bumbwini iliojengwa na Kampuni ya Mecco,ikiwa ni katika shamra shamra za  kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein akifafanua jambo wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa Barabara ya Mfenesini Bumbwini iliojengwa na Kampuni ya Mecco,ikiwa ni katika shamra shamra za  kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein akiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi pamoja na Watendaji wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano katika Ufunguzi waBarabara ya Mfenesini Bumbwini iliojengwa na Kampuni ya Mecco,ikiwa ni katika shamra shamra za  kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 PICHA NA YUSSUF SIMAI -MAELEZO ZANZIBAR.

MHE. WAZIRI AGREY MWANRI AFANYA ZIARA MKOANI RUKWA


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Aggrey Mwanri akikagua mradi wa maabara katika kituo cha afya cha Matai katika Wilaya mpya ya Kalambo leo. Naibu Waziri huyo amepiga marufuku miradi yote ya serikali hususani inayohusisha mbao kupigwa rangi na badala yake ipakwe vanish, hiyo ni kutokana na baadhi ya wakandarasi kutumia staili hiyo kuiibia Serikali kwa kuweka mbao za bei nafuu na kuzipiga rangi. Mhe. Mwanri yupo Mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi ya siku saba ambapo ataembelea halmashauri zote za Mkoa wa Rukwa na kukagua miradi mbalimbali iliyopo chini ya Halmashauri hizo.
Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri (kulia) akikagua ujenzi wa banio la mradi wa umwagiliji katika kijiji cha Katuka katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Mhe Mwanri aligoma kuweka jiwe la msingi katika mradi huu kutokana na mkandarasi kujenga mradi huo chini ya kiwango kinyume na mchoro halisi wa mradi huo. Aliagiza mapungufu yarekebishwe ndipo Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang’a aweke jiwe hilo kwa niaba yake.
 
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Mussa Chang’a akimkaribisha Mhe. Mwanri azungumze na wananchi wa Wilaya ya Kalambo katika ziara yake ambayo amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kutumia fursa ya miundombinu inayoendelea kujengwa Mkoani Rukwa pamoja na ujio wa Halmashauri yao mpya katika kuwekeza na kujiendeleza kiuchumi.
Kutoka kushoto ni Mama Mwanri mke wa Naibu Waziri, Mhe. Agrey Mwanri Naibu Waziri TAMISEMI, Mhe. Moshi Chang’a Mkuu wa Wilaya ya Kalmabo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Godfrey Schona wakiwa katika picha ya pamoja pembezoni mwa fukwe za Ziwa Tanganyika katika Hoteli ya Liemba Beach Resort walipotembelea ikiwa ni sehemu ya ziara yake Mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akiweka jiwe la msingi katika nyumba ya mganga wa kituo cha afya Matai mapema hii leo. Katika miradi miwili aliyotembelea Mhe. Mwanri aligoma kuweka mawe ya msingi hadi hapo marekebisho aliyoagiza yatakapofanyiwa kazi ndipo mawe hayo yawekwe kwa niaba yake. 
Mama Mwanri akiwasalimu wananchi wa Matai katika Wilaya ya Kalmbo.
 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Kipeta kabla ya Mhe. Mwanri kuzungumza nao kwenye ziara yake ya kuhamasisha shughuli za maendeleo Mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Ndugu Agrey Mwanri akipanda kwa tahadhari kubwa katika daraja la Mto Momba linalounganisha wananchi wa Kilyamatundu Mkoani Rukwa na wale wa Kamsamba Mkaoni Mbeya. Daraja hili lililojengwa kwa kamba limekuwa halikidhi haja ya wananchi hao jambo wanaloomba Serikali kuwajengea daraja litakalowawezesha kuvuka na kuvusha mazao yao kirahisi. 
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa – rukwareview.blogspot.com)

MCHUNGAJI MTIKILA AONGOZA CHAMA CHA DP KUTOA MAONI YA KATIBA MPYA

  on January 8, 2013 

Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila (katikati) akizungumza katika mkutano uliofanyika leo (Jumanne, Januari 8, 2013) katika Ofisi za Tume hiyo Jijini Dar es Salaam na Chama hicho kilipowasilisha maoni yao Kuhusu Katiba Mpya mbele ya Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiongozwa na Jaji Joseph Warioba. Kulia ni Katibu wa Tume Assaa Rashid na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akizungumza na Viongozi wa Chama cha Democratic (DP) wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mchungaji Christopher Mtikila (kushoto) waliofika katika Ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam leo (Jumanne Januari 8, 2013) kuwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya. Katikati ni Katibu wa Tume, Assaa Rashid.
 
Viongozi wa Chama cha Democratic (DP) wakiongozwa na Mchungaji Christopher Mtikila (kushoto) wakifuatilia kwa makini hoja zilizokuwa zikitolewa na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa mkutano baina yao uliofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume hiyo Jijini Dar es Salaam leo (jumanne Januari 8, 2013).
 (PICHA NA TUME YA KATIBA)

RAIS JAKAYA KIKWETE AKIWA NA MMOJA WA WAKANDARASI WA BARABARA MKOANI TABORA

 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mmoja wa wahandisi wa kutoka China waliopata kandarasi ya kujenga barabara baada ya kuzindua rasmi  ujenzi wa barabara hiyo akiwa katika ziara yake ya  siku nne ya mkoa wa huo ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.

RAIS KIKWETE AUNGURUMA NZEGA, AWASILI TABORA KUFUNGA MIRADI ZAIDI

 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa maelekezo kwa Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli, Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa kabla hajahutubia Jumatatu mkutano mkubwa wa hadhara mjini Nzega katika ziara yake ya siku nne ya mkoa wa Tabora ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
(PICHA NA IKULU)
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisikiliza maelezo ya Meneja wa TANESCO wa Nzega akielezea mikakati ya kuwapatia wakazi wa hapo nishati hiyo Jumatatu mkutano mkubwa wa hadhara mjini Nzega katika ziara yake ya siku nne ya mkoa wa Tabora ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
 
Umati wa wananchi ukiwa katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Rais Jakaya Kikwete mkoani Tabora
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ripoti ya maendeleo ya Wilaya ya Uyui toka kwa mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Lucy Mayenga wakati Rais alipowasili Tabora mjini kuendelea na ziara yake ya  siku nne ya mkoa wa huo ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji. 
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ripoti ya maendeleo ya Wilaya ya Tabora Mjini toka kwa mkuu wa Wilaya hiyo Mhe  Suleiman Kumchaya  wakati Rais alipowasili Tabora mjini kuendelea na ziara yake ya  siku nne ya mkoa wa huo ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelzo ya ujenzi wa barabara ya Tabora-Ndono kabla hajazindua rasmi i ujenzi wa  barabara hiyo akiwa katika ziara yake ya  siku nne ya mkoa wa huo ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi  ujenzi wa barabara hiyo akiwa katika ziara yake ya  siku nne ya mkoa wa huo ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Jumatatu mkutano mkubwa wa hadhara mjini Nzega katika ziara yake ya siku nne ya mkoa wa Tabora ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.