WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda ameendesha harambee ya papo hapo na kufanikiwa
kuchangisha sh. milioni nane kwa ajili ya ukarabati wa pampu za visima
tisa vya maji kwa wakazi wa kijiji cha Magamba, kata ya Magamba wilaya
ya Mlele mkoani Katavi.
Waziri Mkuu
alilazimika kuendesha harambee hiyo jana mchana (Jumapili, Januari 6,
2013) wakati akijibu hoja za wakazi wa kata hiyo kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Magamba wilayani Mlele.
Kaimu Mhandisi wa Maji wa Wilaya
hiyo, Bw. Enock Msengi alisema wanakijiji hao kupitia kamati ya maji
walikuwa na sh. 150, 000/- kwenye akaunti yao. “Kama wangekuwa na fedha
walau sh. milioni tatu, tungemudu baadhi ya gharama, lakini kwa hizi
fedha alizochangisha Waziri Mkuu, tunaweza kukarabati visima vyote na
vikafanya kazi… vinavyohitajika zaidi ni vipuri vya pampu,” alisema mara
baada ya mkutano huo.
Akizungumza na wakazi hao,
Waziri Mkuu aliwasisitiza watumie kilimo cha sesa ili kiwe mkombozi wao.
Alipowaita mbele ya hadhara mabalozi wa mashina 18 na kuhoji kila mmoja
wao analima ekari ngapi na anatumia kilimo gani, alibaini kuwa ni
balozi mmoja tu ambaye anatumia kilimo cha sesa na amepanda kwa mistari
na kutumia mbolea.
“Hawa wana ekari moja hadi ekari
tano lakini wengi wao mmesikia ni matuta, matuta, matuta hata kwenye
karanga wametumia matuta. Nawasihi sana mwakani kila mmoja atumie kilimo
cha sesa kwa sababu kina tija zaidi kuliko hayo matuta… yanapoteza
sehemu kubwa ya ardhi ya kilimo,” alisisitiza.
Waziri Mkuu ambaye alikuwa
anamalizia ziara yake ya jimbo kwenye kata mbili kati ya 14 zilizobakia
wakati wa ziara yake Desemba mwaka jana, aliwasihi mabalozi hao watumie
umoja wa kikundi chao cha kilimo kuelimishana na akaahidi kuwatafutia
majembe ya kukokotwa na ng’ombe ikiwa ni pamoja na kuwanunulia maksai
ili waboreshe kilimo na wawe viongozi wa mfano.
WALIOFAULU DARASA LA SABA 2012 KWENDA KAWE UKWAMANI WARIPOTI SHULENI LEO
Mwalimu
wa Shule ya Sekondari Kawe Ukwamani, jijini Dar es Salaa, Peter John
(wa nne kushoto mwenye suruali) akiwaelekeza baadhi ya wanafunzi
walioripoti shuleni hapo leo asubuhi kwa ajili ya kuanza muhula wa
masomo ya Sekondari baada ya kufalu mtihani wa darasa la saba wa 2012 na
kuchaguliwa kujiunga na shule hiyo. Wanafunzi wote waliochanguliwa
kujiunga na masomo ya Sekondari Kidacho cha kwanza, na wale wa sekondari
waliokuwa mapumzikoni, wametakiwa kuripoti shuleni hii leo kote nchini.
Picha na www.sufianimafoto.blogspot.com
RAIS MSTAAFU KARUME AFUNGUA SKULI YA DONGE ZANZIBAR
Rais
Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akisalimiana na Mkuu wa Mkoa
wa Kaskazini Unguja Pembe Juma Khamis mara alipowasili katika Ufunguzi
wa Skuli ya Secondary huko Donge Muanda Kaskazini Unguja.
Rais
Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akikata Utepe kuashiria
Ufunguzi wa Skuli ya Secondary huko Donge Muanda Kaskazini Unguja.
Rais
Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akikunjuwa Kitambaa kuashiria
Ufunguzi wa Skuli ya Secondary huko Donge Muanda Kaskazini Unguja.
Mke
wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mama Shadya Karume akitia saini Kitabu cha
Wageni mara baada ya kuhudhuria Ufunguzi wa Skuli ya Secondary huko
Donge Muanda Kaskazini Unguja.
Rais
Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akipanda Mti katika Uwanja wa
Skuli mara baada ya kufungua skuli hio ya Secondary huko Donge Muanda
Kaskazini Unguja.
Rais
Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akikagua baadhi ya madarasa
ya skuli ya Secondary ya Donge Muanda ilioko huko Kaskazini Unguja.
Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akitoa hotuba yake ya kufungua skuli ya Donge Muanda ilioko huko Kaskazini Unguja ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi.
Rais
Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume katika picha ya pamoja na
Maofisa mbali mbali katika hafla ya ufunguzi wa skuli ya Donge Muanda
ilioko huko Kaskazini Unguja ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya
Mapinduzi.
PICHA NA YUSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
YUSUF OMAR CHUNDA AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUWA NA VITAMBULISHO (PRESSCARD)
Na Radhia Abdalla PEMBA
Mkurugenzi Idara ya
Habari,Maelezo Zanzibar Yusuf Omar Chunda amewataka waandishi wa Habari
Nchini kuhakikisha kwamba wanafanya kazi zao wakiwa na leseni za
uwandishi wa habari (PRESSCARD) ilikuhakikisha kwamba wanafanya kazi zao
hizo kwa mujibu wa sheriaNo5 ya mwaka 1988 ya magazeti .
Hayo ameyaeleza leo wakati
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali huko
katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Chake chake Pemba.juu ya
utendaji wa kazi za Idara hiyo kwa mwaka 2012na kuomba mawazo yao kwa
utendaji wa kazi kwa mwaka 2013.
Amesema kuwa na kitambulisho
kitamrahishia mwandishi huyo kufanya kazi kwa mujibu wa sheri na kupata
habari anazozihitaji kwa wahusika bila ya matatizo ambazo
zitachapishwa na kutangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari.
Mkurugenzi huyo amewataka
waandishi hao kutopuuza agizo hilo la kuwa na kitambulisho kwani ni kwa
faida yao wenyewe kutokana na kazi zao wanazo zifanya kila siku.
Chunda amesema kuwa viongozi
wasionekane wagumu pale wanapotaka kutoa habari kwanza kwa kuuliza
waandishi vitambulisho vyao kwani wao wanahitaji kupata uhakika wa
mwandishi huyo kama amepata kibali cha kuandika habari nchini kama
sheria inavyotaka .
Amesema kuwa ni vyema kwa
waandishi kuelewa kazi zote zinakwenda kwa mujibu wa sheria kwa hivyo
waandishi kama kioo cha jamii na wao wanastahiki kufanya kazi zao kwa
mujibu wa sheria na wawe mfano.
Mkurugenzi huyo amewashukuru
waandishi wa habari wote kisiwani Pemba kwa mashirikiano mazuri walioipa
idara yake katika utendaji wa kazi kwa mwaka 2012 na amewataka
mashirikiano hayo yawe endelevu ili kufanikisha shughuli za idara hiyo
na Taifa kwa Ujumla .
Aidha amewashukuru pia waandishi
wa habari, viongozi wa dini pamoja na NGOs za habari kwa mashirikiano
walioyatoa wakati wakutoa mawazo yao juu ya mabadiliko ya sheria No5 ya
mwaka 1988 ya magazeti na Majarida Zanzibar
Wasanii watakiwa kushiriki Tamasha la Sanaa la Afrika Mashariki
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imewataka wasanii nchini
kujitokeza kushiriki tamasha la sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika
Mashariki ambalo litafanyika nchini Rwanda mwezi ujao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam
jana, kwa Niaba ya Katibu Mkuu, afisa Utamaduni Mwandamizi wa Wizara
hiyo Makao makuu, Habibu Mohamed amesema tamasha hilo lijulikanalo kama
JAMAFEST litafanyika kwa siku nane kuanzia Februari 9 hadi 16 mwaka huu.
“ Kwanza napenda kuwajulisha
kuwa tumepata mwaliko wa kushiriki Tamasha la Sanaa na Utamaduni la
Jumuiya ya Afrika Mashariki, ‘JAMAFEST – 2013’ ambalo ni tamasha muhimu
sana kwa wasanii wetu kushiriki katika hatua ya kutangaza na kuuza kazi
zao katika soko la sanaa la Afrika Mashairiki,” amesema Habibu.
Amesema kutokana na mwaliko huo
wa Jumuiya, Wizara inatoa mwaliko kwa wasanii, asasi, vikundi, wabunifu
wa mavazi na kampuni kwa hapa nchini, ambao zitaweza kufanya maonesho
na kuuza bidhaa na huduma za Sanaa na Utamaduni, katika mabanda ya
Tanzania kutuma maombi yao wizarani ambapo mwisho wa kutuma maombi ni
Januari 25.
Amesema washiriki watajigharamia nauli ya kwenda na kurudi, chakula na malazi katika kushiriki tamasha hilo.
SHUKRANI ZA DHATI KUTOKA WATANZANIA WAISHIO NJE YA NCHI KWA RAIS DK.JAKAYA KIKWETE NA SERIKALI YAKE YA AWAMU YA NNE.
Naomba
kuchukua fursa hii kutoa shukrani za dhati na wazi kwa Rais wa Jamhuri
ya Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Kikwete na Serikali yake ya awamu ya nne,
kwa niaba yangu binafsi na kwa niaba yaTawi la CCM UK na nina imani
kwa niaba ya wana jamii ya Wa-Tanzania Walioko Nje ya Nchi (Dispora)
kwa Ujumla, katika juhudi anazofanya kujumuisha Dispora Tanzania kwenye
kuchangia maendeleao ya Nchi yetu.
Wana-Dispora tulio wengi tumeshuhudia kwa vitendo
tangu Rais Jakaya
Kikwete na Serikali yake imeingia Madarakani , jitihada na mikakati
tofauti na iliyo wazi ya Serikali Kuu kutafuta mbinu za kudumu ili
kushirikiana na kuwahusisha wana Diaspora, katika kuchangiamaendeleo ya Kiuchumi na Kijamii ya Nyumbani, Tanzania.
Nakumbuka Mheshimiwa Rais Kikwete
katika kikao chake cha kwanza na Watanzania waishio Uingereza Mnamo
mwaka wa fedha 2006/2007 pale Churchill Hotel, UK , katika Hotuba yake
ambayo mbali na kutuelezea mafanikio na mikakati mbalimbali iliyopangwa
na serikali yake kwenye utekelezaji wa Sera zake za ya awamu ya nne, kwa
nia ya kutimiza maazimio ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2005 na baadae
2010, vile vile alituahidi wana-Dispora kuwa atahakikisha yeye Binafsi
atafanya jitihada zake zote kwa kadri ya uwezo wake aliyopewa na
Mwenyezi Mungu na Serikali yake haitusahau na katuacha nyuma Wana
Dispora . Kilichoendelea baada ya Mkutano ule wana Dispora UK tulishudia
thamani yetu kwa Serikali na Taifa letu ,kwani tumekuwa tukipewa
kipaumbele kwa kila Kiongozi Mkuu wakiwemo Mawaziri na Wabunge wetu
tofauti, anapotembelea Uingereza (na nina imani Nchi mbalimbali )
mbali na kuwa na ratiba zao ndefu za kikazi, wanapata muda wa
kubadilishana mawazo nasi na tunaona matunda ya mchango wetu huu
yameanza kuonekana ,licha ya kuwepo changamoto za kawaida
zinazokabilika. Hili tunamshukuru sana Rais wetu kwa kulipa uzito
unaostahili na kuonyesha mfano wa Uongozi wake bora na uliotukuka.
Kwa mara ya kwanza Tanzania
Dispora tumepata sauti na kuthaminiwa kwa wazi kwa Mchango wetu wa hali
na mali tunaorudisha nyumbani ili kuchangia Maendeleo . Wana-Dispora
sasa tunajivunia kupewa na Rais wetu jina la Mkoa . Baada ya kuanza
na dawati la Dispora pale Wizara ya Mambo ya Nje, ili kuweka mfumo wa
kudumu na kutimiza ahadi yake Mheshimiwa Rais mwaka ulipita 2012 aliteua
Mkurugenzi wa Idara ya Dispora. Sasa tuna Idara/Kitengo kizima na si
dawati tena. Kitengo/Idara yenye jukumu la kushughulikia mambo muhimu na
tofauti ya Dispora. Hii ni hatua kubwa sana na ya muhimu na hatutaacha
kumshukuru Rais wetu kwa kuliona na kulitambua hili na kutuletea matunda
yake.
MIRAJI MRISHO KIKWETE ATEULIWA KUWA “MAKAMU WA RAIS” WA IBF/AFRIKA MAENDELEO YA VIJANA
Shirikisho
la Ngumi la Kimataifa Africa (IBF/Africa) limemteua bwana Miraji Mrisho
Kikwete kuwa Makamu wa Rais anayeshughulikia maendeleo ya vijana katika
bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati. Uteuzi wa Miraji
unaanza January mwaka mpya 2013.
Katika
kumteua Miraji, Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na
Mashariki ya Kati bwana Onesmo Ngowi alisema kuwa Miraji ana uwezo wa
kuwahamasisha na kuwaunganisha vijana katika shughuli za maendeleo.
Aliendelea
kusema kuwa Miraji atakuwa anawahamashisha vijana, kuwaunganisha,
kuwajengea uwezo wa kimaendeleo yatakayoratibiwa na IBF.
Aidha,
Rais huyo alisema kuwa Miraji atakuwa anabuni njia mbalimbali za
kuwaunganisha vijana wa Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati ili
waweze kufaidika na miradi ya IBF ambayo inalenga kwenye elimu, kujenga
vipaji pamoja na kuwaunganisha kwenye biashara ya utalii wa michezo.
Katika
mkutano wake wa mwaka uliofanyika katika jiji la Honolulu, jimbo la
Hawaii, nchini Marekani hivi karibuni IBF iliupokea mradi wa “Utalii wa
Michezo” uliobuniwa na kuwakilisshwa na Rais wa IBF katika bara la
Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtazania Onesmo Ngowi.
Lengo
kuu la mradi huu ni kulifanya bara la Afrika hususan Tanzania kuwa
kitovu kikuu cha “Utalii Michezo” hivyo kujenga uchumi imara. Nchi za
Tanzania na Ghana ziliteuliwa kuwa nchi za mfano kwenye mradi huu.
Katika
mradi huu, IBF itatumia mtandao walionao katika nchi zaidi ya 203
duniani kuhamasisha wanachama wake na famlia zao, wapenzi pamoja na
marafiki zao kuja Afrika/Tanzania kutalii pamoja na kuwekeza katika
miradi mbalimbali.
Uteuzi
wa Miraji utasaidia kuwaunganisha vijana ili waweze kuchangia na
kufaidika na biashara ya utalii kwenye mradi huu umefanywa wakati
muafaka.
Miraji
ambaye ni Mjasiliamali amejipambanua katika maendeleo ya jamii na ana
mchango mkubwa sana katima kuendeleza vijana nchini Tanzania.
Rais
Ngowi alimwelezea Miraji kama tegemeo ambalo vijana wanalihitaji kwani
wanahitaji uhamasishaji wa hali ya juu na Miraji ana uwezo wa kufanya
kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa kwani alishawahi kuifanya kwa kipindi
kitefu.
Miraji
Mrisho Kikwete ni msomi wa chuo kikuu cha nchini Oman ambako amesomea
elimu ya utawala wa biashara ambayo ndiyo lengo kuu la uteuzi wake. Ana
haiba ya kupendwa na vijana pamoja na uwezo wa kujichanganya nao.
RAIS JAKAYA KIKWETE AANZA ZIARA YA SIKU NNE KATIKA MKOA WA TABORA
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipkea ripoti ya mkoa wa Tabora toka kwa Mkuu wa
Mkoa Mhe Fatma Mwassa huo aliyosomewa mara baada ya kuwasili mkoani
humo jana kuanza ziara ya kikazi ya siku nne.
(PICHA NA IKULU)
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe Fatma
Mwassa wakati alipokuwa akisoma ripoti hiyo mbele ya Rais mara baada ya
kuwasili kuanza ziara ya kikazi ya siku nne.
RAIS AHUDHURIA SHEREHE ZA KUSIMIKWA WAKFU ASKOFU DKT ALEX SEIF MKUMBO WA KKKT DAYOSISI YA KATI
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt
Alex Seif Mkumbo (mwenye fimbo) pamoja na viongozi wa kanisa hilo
wakiongozwa na Askofu Mkuu Dkt Alex Gehaz Malasusa (kulia kwa Rais),
Msaidizi mpya wa Dayosisi hiyo Mchungaji Syprian Yohana Hilinti (wa tatu
kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Kone na viongozi wengine katika
sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la
Singida jana Januari 6, 2013.
PICHA NA IKULU
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na kiongozi wa kanisa la KKKT
nchini Dkt Alex Gehaz Malasusa na Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya
kati Dkt Alex Seif Mkumbo baada ya sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu
Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida jana Januari 6, 2013
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na kiongozi wa kanisa la KKKT
nchini Dkt Alex Gehaz Malasusa baada ya kupokea kamba kama ishara ya
kupokea zawadi ya ngombe toka kwa Dayosisi hiyo huku Askofu mpya wa
KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo akishuhudia katika sherehe
ya Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida jana
Januari 6, 2013
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wasaidizi wa
Maaskofu wa Kanisa la KKKT baada ya sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu
Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida leo Januari 6, 2013
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa
Kanisa la KKKT baada ya sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo
katika kanisa la KKKT la Singida jana Januari 6, 2013
BARAZA LA MADIWANI ARUSHA LARIDHIA KUACHIA ENEO LA LAKILAKI
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu(TAMISEMI) Hawa Ghasia
Mahmoud Ahmad Arumeru
……………………………………..
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri
ya wilaya ya Arusha, hatimaye jana januari 5.2013 limeidhinisha
kuliachia eneo la Lakilaki lililopangwa kujengwa mji wa mfano wa
Arusha(Arusha Safari Town) na kukabidhi hati miliki ya ardhi hiyo, kwa
Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa ajili ya ujenzi
wa majengo ya Taasisi za Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Afrika ya
Mashariki.
Maamuzi hayo, yalifikiwa jana
katika kikao cha dharura ambacho, kilihudhuriwa na waziri wa Nchi ofisi
ya Waziri Mkuu(TAMISEMI) Hawa Ghasia, baada ya serikali kukubali
kulipa mkopo uliokopwa na halmashauri hiyo kutoka Benki ya biashara
ya Afrika(CBA) kiasi cha sh 8.6 bilioni pamoja na riba sambamba na
kurejesha gharama za mradi huo kiasi cha sh 788.2 bilioni na faida
ambayo halmashauri hiyo, ingepata kiasi cha sh5.6 bilioni.
Akizungumza mara baada ya
madiwani hao, kwa kauli moja kukubali kulitoa eneo hilo, Waziri Ghasia
alisema Serikali imekubali kulipa gharama hizo, ili kuhakikisha
inapatikana ardhi hiyo kwa manufaa ya Taifa zima.
Waziri huyo, pia alisema Rais
Jakaya Kikwete alikuwa akifuatilia kupatikana kwa ardhi hiyo na
ameiondoa hofu halmashauri hiyo, kupoteza fedha ambazo tayari wametumia
na ambazo wangepata kama wangetekeleza mradi huo.
Hata hivyo, kabla ya madiwani hao,
kukubali kutoa ardhi hiyo, walitaka uthibitsho wa maandishi wa Serikali
kukubali kulipa deni la benki na gharama zote, hoja ambayo ilikubaliwa
na waziri huyo, ambaye alisema tayari aliandika barua kwa halmashauri
hiyo kueleza jinsi watakavyorejeshewa fedha zao.
Awali mkurugenzi wa halmashauri
ya Arusha, Halfani Hida alisema mradi wa awali kama ungetekelezwa
tayari walikuwa wamepima jumla ya viwanja 348 ambavyo vingegawanywa kwa
wananchi na kuipatia halmashauri hiyo mapato ya sh 13.3 bilioni, pia
viwanja vya biashara vingeingiza mapato ya sh 1.7 bilioni huku maeneo
ya huduma yalitarajiwa kuingiza sh 332.6 milioni.
Eneo hilo la laki laki lina
ukubwa wa ekari, 430 lilinunuliwa na halmashauri hiyo toka kwa Valahala
Estate limited kwa sh 8.6 bilioni lakini wakati mradi ulipotaka kuanza
ndipo mgogoro uliibuka baina ya halmashauri na watendaji wa serikali nje
ya halmashauri na ndipo baadaye eneo hilo lilitwaliwa na Wizara ya
Ardhi na Maendeleo ya makazi ambapo lilichukuliwa na wizara ya mambo ya
nje
Rais Dk. Shein azindua Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi
wa Jengo la Bohari Kuu ya Dawa,Maruhubi Nje ya Mji wa Zanzibar jana
ikiwa ni shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu
ya zanzibar,(kulia) Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Alfonso
Lenhardt.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi
wa Jengo la Bohari Kuu ya Dawa,Maruhubi Nje ya Mji wa Zanzibar jana
ikiwa ni shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu
ya zanzibar,(kulia) Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Alfonso
Lenhardt.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikata utepe kama ishara ya uzinduzi
wa Jengo la Bohari Kuu ya Dawa,huko Maruhubi Nje ya Mji wa Zanzibar
jana ikiwa ni shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi
Matukufu ya zanzibar,(kulia) ni Naibu waziri wa Afya Sira Ubwa Mamboya
na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Alfonso Lenhardt.[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikata utepe kama ishara ya uzinduzi
wa Jengo la Bohari Kuu ya Dawa,huko Maruhubi Nje ya Mji wa Zanzibar
jana ikiwa ni shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi
Matukufu ya zanzibar,(kulia) ni Naibu waziri wa Afya Sira Ubwa Mamboya
na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Alfonso Lenhardt.[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa
Bohari Kuu,Said Mohamed,(kulia) alipotembela sehemu ya kuhifadhia
Dawa,baada ua uzinduzi wa Jengo la Bohari Kuu ya Dawa huko Maruhubi
Nje ya Mji wa Zanzibar,ikiwa ni shamra shamra za kilele cha miaka 49
ya Mapinduzi Matukufu ya zanzibar,(wa tatu kushoto) Balozi wa
Marekani Nchini Tanzania Alfonso Lenhardt.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa
Bohari Kuu,Said Mohamed,(kulia) alipotembela sehemu ya kuhifadhia
Dawa,baada ua uzinduzi wa Jengo la Bohari Kuu ya Dawa huko Maruhubi
Nje ya Mji wa Zanzibar,ikiwa ni shamra shamra za kilele cha miaka 49
ya Mapinduzi Matukufu ya zanzibar,(wa tatu kushoto) Balozi wa
Marekani Nchini Tanzania Alfonso Lenhardt.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu Kulia)pamoja na Viongozi
wengine akiwemo Balozi wa Marekani Nchini Alfonso
Lenhardt.wakiangalia namna ya uchukuwaji dawa kwa kutumia mashine
maalum na kutoa nje ya Bohari kuu ya Dawa,baada ya ufunguzi rasmi jana
huko Maruhubi Nje ya mji wa Zanzibar,ikiwa ni shamra shamra za kilele
cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu Kulia)pamoja na Viongozi
wengine akiwemo Balozi wa Marekani Nchini Alfonso
Lenhardt.wakiangalia namna ya uchukuwaji dawa kwa kutumia mashine
maalum na kutoa nje ya Bohari kuu ya Dawa,baada ya ufunguzi rasmi jana
huko Maruhubi Nje ya mji wa Zanzibar,ikiwa ni shamra shamra za kilele
cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzíbar
………………………………………………
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
amesema uzinduzi wa Bohari kuu ya Dawa utaiwezesha Serikali ya Mapinduzi
Zanzíbar kupanga bajeti yake vyema ya dawa na kusaidia utoaji wa huduma
za afya kwa ubora wa hali ya juu.
Rais
Shein ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Bohari Kuu ya Dawa
iliyopo Maruhubi mjini Zanzibar ikiwa ni mwendelezo wa shamra shamra za
kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi Zanzibar.
Amesema
Bohari hiyo ya kisasa ni matunda ya kujivunia ya Mapinduzi ya Zanzibar
ambayo kwa hakika italeta tija katika upatikanaji wa dawa na uimarisha
wa afya za wananchi.
Dkt.
Shein ameelezea matumaini yake kwa sekta ya afya kupitia Bohari hiyo na
kwamba anaamini baada ya miaka mitatu Zanzibar itakuwa haipeleki tena
Wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu.
Aidha
Dkt. Shein amewataka watumishi wa Serikali kubadilika kiutendaji
kulingana na kasi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa Bohari
hiyo kuitunza vyema ili iendelee kutoa huduma kama inavyotakiwa.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Afya Sira Ubwa amesema Bohari hiyo
itaboresha utoaji wa huduma kwa uhakika kutokana na ubora wa vifaa na
mitambo ya kisasa ambapo wataalamu wataweza kubaini mahitaji ya Dawa
zinazohitajika katika kila Hospitali za Unguja na Pemba.
Kwa
upende wao Mabalozi wa Marekani na Denmark wameelezea kufurahishwa kwao
na juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha afya
ya Wananchi hasa katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Malaria na Ukimwi.
Aidha
wameahidi kuendelea kutoa mashirikiano kwa Serikali hasa katika huduma
za Afya kwa Mama na Watoto, Elimu,Mapambano dhidi ya magonjwa ya
maambukizi pamoja na uzazi wa mpango.
Bohari
hiyo iliyojengwa na Serikali ya Mapinduzi kwa msaada wa Shirika la
USAID na NIDA inaelezewa kuwa ya tatu duniani katika viwango vya ubora
ambapo jumla ya Dolla za Kimarekani Milion 1.2 zimetumika kukamilisha
ujenzi wake.
TPBC KUFANYA UCHAGUZI FEBRUARY 2013
Onesmo Ngowi Rais wa TPBC
………………………………………..
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa
Nchini TPBC) imetangaza kuanza kufanya uchaguzi katika ngazi ya mikoa
kuanzia tarehe 20 February 2013.
Katika chaguzi hizo,
mikoa itafanya chaguzi zake kuwachagua viongozi wake katika nafasi za
Kamishna wa mkoa, Katibu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mweka Hazina
Msaidizi pamoja na wajumbe 10 wa Kamati ya Utendaji ya Mkoa.
Mikoa ambayo itafanya chaguzi ni
pamoja na Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Dar-Es-Salaam, Morogoro, Tanga,
Pwani, Mwanza, Mara na Bukoba.
Baada ya chaguzi za mikoa TPBC
itafanya uchaguzi mkuu katika ngazi ya Taifa mwishoni mwa mwezi wa tatu
(Machi) 2013. Wadau wa ngumi wanahimizwa kujitokeza kwa wingi ili waweze
kushiriki katika chaguzi hizi.
Rais wa TPBC Onesmo Ngowi
ameshatangaza kuwa hatagombea tena uongozi katika Kamisheni na kuwataka
Watanzania wanaopenda mchezo wa ngumi kujitokeza ili waweze kuiongoza
Kamisheni.
MAMLAKA ya Udhibiti
Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imewaagiza wamiliki vyombo vya
usafiri (mabasi ya abiria), kuacha mara moja kuweka matangazo ambayo
yanapoteza uhalisia wa rangi iliyokubalika katika mkataba.
Akizungumza na FULLSHANGWEBLOG
mwishoni wiki jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Udhibiti Usafiri wa
Barabarani, Leo Ngowi, alisema utaratibu huo iliyozuka hivi karibuni
hakubaliki kwa kuwa haiko katika makubaliano kisheria.
Alisema agizo hilo linawataka
wale wote waliofanya hivyo kuhakikisha kuwa wanayaondoa matangazo yote
ili kuondoa usumbufu kwa abiria.
Ngowi alisema wanaupinga
utaratibu huo kutokana na ukweli kwamba hauko kwenye sheria, kwa wale
watakaokaidi agizo hilo gari zao zitakamatwa kwa ajili ya hatua nyingine
za kisheria.
“Kuna gari nyingi zimefanya
hivyo, hususan daladala ambazo zimepoteza kabisa uhalisia wa muonekano
unaotakiwa hali inayoleta usumbufu kwa abiria wa maeneo husika.
“Tulikwisha wambia waache lakini
naona bado wanaendelea kufanya hivyo, hivi karibuni niliwahi kuyakamata
magari matatu kwa makosa kama hayo” alisema Ngowi
Akifafanua, Ngowi alisema
kinacho kubalika ni matangazo madogo ya aina ya stika, na siyo yale
yanayoharibu rangi za gari hizo kwa mfano kuna daladala zimeweka
matangazo ya simtanki ambayo yamefunika bodi lote na kufanya gari hilo
lisijulikane rangi yake halisi.
Ngowi alisema hivi sasa hakuna
makubaliano hayo, hata hivyo, wako kwenye mchakato kwa ajili ya
kuangalia uwezekano wa kupitisha hilo, lakini kwa sasa wasifanye hivyo.
WANANCHI KIJIJI CHA KICHEBA WALALAMIKIA UONGOZI WAO KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA MRADI WA MAJI (TALDO)
(MKUU wa wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Subira Mgalu)
…………………………………………………………….
BAADHI ya wakazi wa Kijiji cha
Kicheba wilayani Muheza, Tanga wameutupia lawama uongozi wa kijiji hicho
kwa kushindwa kusimamia kwa haki upatikanaji wa maji ya mradi wa
‘Taldo’
Akizungumza na FULLSHANGWEBLOG kwa
njia ya simu kwa niaba ya wanakiji wenzake, mkazi huyo, Yusuf Issa,
alisema hali ya upatikanaji wa huduma hiyo umevurugwa kabisa na viongozi
hao kwa tamaa ya kujipatia fedha.
Alisema uongozi huo umevuruga
utaratibu kwa kuruhusu baadhi ya watu kujiunganishia maji hayo
kinyemela, huku wakisababisha vituo maalum vya umma kukosa huduma hiyo,
hivyo kulazimika kwenda kununua maji kwa watu hao tena kwa bei kubwa.
“Lengo la kusaidia wanakijiji
hao la kujipatia huduma hiyo kwa kuchangia kiasi kidogo kwa ajili ya
matengenezo inapotokea kuharibika kwa koki, limetoweka baadala yake
limegeuzwa kitega uchumi cha baadhi ya viongozi kwa kuanzisha vituo vyao
vya kuuza maji kinyemela majumbani mwao, kwa kila ndoo sh 500 ”alisema
Issa.
Issa alisema watu hao wamevuruga
njia zote za bomba kubwa linalopeleka maji katika vituo vya wananchi,
ambapo kwa sasa upatikanaji wamaji umekuwa shida na wa kubahatisha
kutokana na kuzibwa kwa mabomba hayo.
Alipoulizwa Mbunge wa wilaya
hiyo, Hebert Mtangi kuhusu mgogoro huo, alisema ndiyo kwanza anausikia,
hata hivyo, alisema kama wamefanya hivyo hayo ni makosa kuwa hiyo asili
ya mradi huo wa kuweka kuingiza maboma majumbani.
“Hayo ni makosa lakini kitu
kikubwa kwanza nitakutana na diwani wangu anithibitishie hilo, kama lipo
na baadaye waje wawaeleze wananchi kwenye mkutano wa hadhara kuwa
kibali cha kuwaruhusu watu hao kuweka mabomba majumbani mwao kimetolewa
na nani”alihoji Mtangi.
Mtangi alisema katika kijiji hicho
kuna wenyeviti wa vitongoji, mwenyekiti wa kijii hata mwenyekiti wa
maendeleo wa kata ambaye iweje yatokee hayo, acha nitakutana nao kwa
ajili ya kupata taarifa kuhusu hilo.
WABUNGE WA MKOA WA ARUSHA WATAKIWA KUHUDHURIAVIKAO VYA ALAT ILI KUCHANGIA MAENDELEO YA MKOA
NA GLADNESS MUSHI -LONGIDO
WABUNGE wa Mkoa wa Arusha wametakiwa kuhakikisha
kuwa wanahudhuria kwenye vikao vya jumuiya za Serikali za mitaa(ALAT)na
kuachana na tabia ya kukwepa vikao hivyo kwa muda mrefu sana kwani
michango ya wabunge inaweza kuimarisha jumuiya hiyo pamoja na mkoa wa Arusha ambao unahitaji majibu badala ya maswali kutoka kwa Viongozi.
Hayo yameelezwa jana wilayani
Longido na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa kwa Tawi la
Arusha(ALAT)Goodson Majola katika kikao cha wadau wa Jumuiya hiyo na Viongozi wake
Majola alisema kuwa wabunge
wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanahudhuria vikao kwa kuwa wanajua na
kutambua shida na changamoto mbalimbali ambazo zimo kwenye jamii lakini
kama watakuwa hawahudhurii vikao bado jamii itaendelea kuwa na
changamoto mbalimbali
Aliongeza kuwa wabunge
wanapokwepa vikao mbalimbali hasa vya jumuiya za Serikali za Mitaa
kunasababisha maendeleo kuwa hafifu sana kwenye jamii huku wannachi nao wakiwa na hisia tofautitofauti juu ya utendaji kazi wa wabunge hao pamoja na Halmashauri zao.
“Sasa hivi wabunge wanatakiwa
kujua na kutambua kuwa jamii ambayo inaongoza haitaji maswali bali
inahitaji majibu na hii pia ni hata ndani ya halmashauri zetu kwa hiyo
mpaka sasa wabunge wanatakiwa kutumia Jumuiya hii na kushirikiana na
kisha kutatua kero za jamii,lakini kama watakuwa wanakimbia vikao ni
wazi kuwa Jumuiya hii haitaweza kufikia malengo yake”aliongeza Majola.
Katika hatua Nyingine Katibu wa
Jumuiya hiyo,Khalifa Idda alisema kuwa endapo kama wadau mbalimbali
pamoja na watalamu wa Halmashauri zaa Mkoa wa Arusha wataweza kutumia
Jumuiya hiyo vema basi wataweza kusaidia hata Halmashauri kuepukana na
Hati chafu ambazo zimekuwa zikisumbua sana baadhi ya halmashauri.
Idda alisema kuwa kupitia Jumuiya
hiyo wataweza kujadili mambo mbalimbali ambayo yanasababisha na kuwa
kikwazo cha hati chafu hivyo suala la hati chafu kutoka kwa mkaguzi mkuu
wa Serikali (CAG)litakuwa ni ndoto hivyo kuongeza hata ufanisi zaidi wa
kimapato.
“Suala la hati chafu limekuwa
kikwazo kikubwa sana kwenye Halmashauri zetu lakini kama watu watakuwa
na umoja na watashiriki kwa undani sana kwenye ALAT basi wataepukana na
hilo kwa kuwa hapa tutaweza kujadili kwa wale waliofanikiwa kuvuka na
hata wale walioshindwa na wenyewe tutaelezana kisa kikubwa ni kipi hivyo
ni vema kila halmashauri na wataalamu wake wakatumia vema jumuiya
hiyo”aliongeza Idda
Rais Kikwete akutana na Viongozi wa Mkoa wa Singida
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akitumia laptop yake kuwaonyesha viongozi mbali
mbali wa Mkoa wa Singida wakati alipokuwa akiwaelezea masuala muhimu ya
maendeleo nchini.Rais Kikwete amewasili Mjini Singida Januari 5 kwa
Ziara ya kikazi ya Siku Mbili.Picha na IKULU
No comments:
Post a Comment