Kiwanda ambacho mbao za Vyama Vya Ushirika wa Uswaa/Mamba, Shari na Kyeeri Zimehifadhiwa, baada ya kukamatwa katika Mashamba ya Silverdale na mbono, Kisha Mahakama kuhamuru zihifadhiwe mahali hapa.
Mbao ambazo zimehifadhiwa katika ghara ya Imara Daima, za wanaushirika wa vyama vya Uswaa/Mamba, Sheri na Kyeeri, zilizotolewa katika Mashamba ya Silverdale na Mbono
Mbao ambazo zimehifadhiwa katika ghara ya Imara Daima, za wanaushirika
wa vyama vya Uswaa/Mamba, Sheri na Kyeeri, zilizotolewa katika Mashamba
ya Silverdale na Mbono
Kutokana na Mashamba ya Silverdale na mbono kutokuwa na shughuli baada ya mahakama kusitisha, wakazi wa maeneo ya Jirani wamejitokeza kukata kuni kwa ajili ya Matumizi yao Binafsi
Mbao ambazo zimehifadhiwa katika Stoo zilizoko katika Mashamba ya Silverdale na Mbono, ambazo zimeanza kuharibika baa ya kukaa muda mrefu
Kutokana na Mashamba ya Silverdale na mbono kutokuwa na shughuli baada ya mahakama kusitisha, wakazi wa maeneo ya Jirani wamejitokeza kukata kuni kwa ajili ya Matumizi yao Binafs
Mkazi wa Jirani na Mashamba ya Silverdale akitoka kupata kuni katika Mashamba hayo
Mbao ambazo zimehifadhiwa katika Stoo zilizoko katika Mashamba ya
Silverdale na Mbono, ambazo zimeanza kuharibika baa ya kukaa muda mrefu
Mkazi wa Uswaa/Mamba, akikata majani katika Mashamba ya Silverdale na Mbono
Wenye viti wa Ushirika wa Uswaa/Mamba, Shari na Kyeeri wakijadili jambo baada ya kutembelea Mashamba ya Silverdale na mbono wakati wa Ukaguzi
Wenye viti wa Ushirika wa Uswaa/Mamba, Shari na Kyeeri wakijadili jambo
baada ya kutembelea Mashamba ya Silverdale na mbono wakati wa Ukaguzi, katika jengo la Ofisi lililo katika Mashamba hayo
Sehemu ya Mashamba ya Silverdale na mbono
Sehemu ya Mashamba ya Silverdale na mbono
Wenyeviti wa Ushirika wa Vyama vya Uswaa/Mamba, Shari na Kyeeri wakiwa katika kutathmini uharibifu wa Mbao zinazoendelea kuharibika katika Stoo za majengo yaliyoko katika Mashamba ya Silverdale na Mbono
Wenyeviti wa Ushirika wa Vyama vya Uswaa/Mamba, Shari na Kyeeri wakiwa
katika kutathmini uharibifu wa Mbao zinazoendelea kuharibika katika Stoo
za majengo yaliyoko katika Mashamba ya Silverdale na Mbono
Wenyeviti wa Ushirika wa Vyama vya Uswaa/Mamba, Shari na Kyeeri wakiwa
katika kutathmini uharibifu wa Mbao zinazoendelea kuharibika katika Stoo
za majengo yaliyoko katika Mashamba ya Silverdale na Mbono
Wenyeviti wa Ushirika wa Vyama vya Uswaa/Mamba, Shari na Kyeeri wakiwa
katika kutathmini uharibifu wa Mbao zinazoendelea kuharibika katika Stoo
za majengo yaliyoko katika Mashamba ya Silverdale na Mbono
Wenyeviti wa Ushirika wa Vyama vya Uswaa/Mamba, Shari na Kyeeri wakiwa
katika kutathmini uharibifu wa Mashine zinazoendelea kuharibika katika Stoo
za majengo yaliyoko katika Mashamba ya Silverdale na Mbono
Hapa wanafungua Milango ambayo ilikuwa aijafunguliwa kwa muda mrefu
Walinzi wa Mashamba ya Silverdale na Mbono, wakifungua Maghara ambayo yamehifadhi Mbao.
aidha mashamba hayo ambayo yalimilikishwa Vyama
vya Ushirika vitatu; yaani Uswaa/Mamba, Shari na Kyeeeri wakati serikali ya
Muungano ya Tanzania ilipotaifisha mashamba yaliyokuwa yanamilikiwa na wakulima
Wageni Mkoani Kilimanjaro mwaka 1973 na 1974.
Shabaha ya Serikali kumilisha vyama vya ushirika mashamba haya ilikuwa mapato yake yawezeshe wanavijiji husika kusukuma mbele maendeleo yao.
Shabaha ya Serikali kumilisha vyama vya ushirika mashamba haya ilikuwa mapato yake yawezeshe wanavijiji husika kusukuma mbele maendeleo yao.
Lakini zaidi ya Miaka 25 tangu
mashamba haya yalipokuwa chini ya
uongozi wa bodi za vyama vya ushirika hayakuzaa matunda yaliyotazamiwa, Kwa
sababu hiyo wakati wa awamu ya tatu ya utawala chini ya uongozi wa Rais
Benjamini William Mkapa, Serikali ilishauri vyama vya ushirika kutafuta
wawekezaji.
Mnamo
tarehe 3 Septemba 1998
washiriki wa vyama vya Uswaa/Mamba, Shari na Kyeeri walifanya mkutano
wao wa
pamoja uliokaa katika chama cha ushirika Uswaa/Mamba kuwajadili
wawekezaji waliokuwa wameomba kuwekeza katika mashamba ya Silverdale na
Mbono
Baada ya mazungumzo ya kina wanachama kwa kauli moja waliamua kuwa Fiona
Tanzania Ltd ambao wamiliki wake ni Bw. Benjamini A. Mengi na mke wake Millie B. Mengi wapewe
kukodishwa kuwekeza katika mashamba hayo kwa vipindi vya miaka mitano mitano.
Kwa mapatano kwamba kila baada ya miaka mitano ,wanachama wa vyama hivi
vitatu watakaa na kutathmini maendeleo ya shamba na wakiridhika wanaweza
kumruhusu kuendelea kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Mashamba hayo kwa pamoja yana ekari 993 kama ilivyoorodheshwa,
Plot nambari 1 ya hati 9640 ekari 52.4 weruweru, Plot nambari 2 ya hati
9527 ekari 39.4 Weruweru, Plot nambari 3 ya hati 9570 ekari 25.4 Weruweru, Plot
nambari 5 ya hati 9377 ekari 28.4 Weruni, Shamba namba 2450 ya hati 11540 ekari
50.0 Weruni, Shamba nambari 9640 ekari 30.5 jumla yake inakuwa 993.1.
Mkataba kati ya vyama hivi vitatu na kampuni ya Fiona Tanzania Ltd
uliwekwa sahihi tarehe q januari 1999.Kati ya mambo mengine mkataba uliwataka
wakodishiwa wafanye mambo yafuatayo; kulipa kodi ya kila mwaka shilingi
17,500,000 kila ifikapo tarehe 31 Agosti kwa miaka mitano ya kwanza, Kufufua
Mibuni iliyopo shambani na kuongeza miche mipya kutoka eneo la ekari 131 za
sasa kufikia ekari 300 katika kipindi cha miaka 10 ya kwanza, Kukarabati
majengo yote yaliyokuwapo na kuyaweka katika hali nzuri wakati wote, kukarabati
majengo yote yaliyopo na mitambo yote inayohusiana na uzalishaji wa kahawa,
kutokata miti yoyote iwe kwa matumizi ya mbao,nguzo au kuni bila kibali cha
mwenye shamba.
Mnamo tarehe 21 mei 2004 Kampuni ya Fiona Tanzania Ltd, iliingia mkataba
na David Stewart Middleton, hapo mbeleni
Bw. David S. Middleton alikuwa
ameajiriwa na Bw. Benjamini Mengi kama Consultant Agronomist chini ya Kampuni
ya Alpha Tobacco T. Ltd ambayo ilikuwa chini ya Bw. B.A. Mengi ambayo kusudi
lake ilikuwa kuendesha mashamba ya tumbaku.
Katika mkataba huo mpya kati ya Kampuni ya M/S Fiona T. Ltd na David
Stewart Middleton mashamba ambayo
yalikuwa yamekodishwa na kampuni ya M/S Fiona T. Ltd kutoka kwenye vyama
vitatu
vya Ushirika, yaani; Uswaa/Mamba, Shari na Kyeeri, hawa wawili waliamua
kuyaingiza katika kampuni yao mpya kwa jina la Silverdale T. Ltd; wao
wenyewe
wakiwa ndiyo wakurugenzi. Bw. David S. Stewart Middleton akiwa na hisa
asilimia 70 na Bw. B.A. Mengi asilimia 30. Kamapuni hii Mpya Silverdale
T. Ltd ilikuwa
iendeshe shughuli zote ambazo M/S Fiona T. Ltd ilikuwa ikizifanya kwenye
mashamba ya Silverdale na Mbono. Mkataba huo ulitayarishwa kwa mapatano
kwamba
Bw. David Stewart Middleton angemlipa Bw.B.A. Mengi kiasi cha USA $
112,000
yaani fedha za kitanzania kwa thamani ya leo ya Shs. 1,150 ni sawa na
shilingi
128,800,000/=.
Kwa kuwa wadau wa mashamba hayo yaani washirika wa vyama hivyo vya
Ushirika vitatu-Uswaa/Mamba, Shari na Kyeeri ilipasa wajulishwe nia ya mabadiliko hayo mapya na waweze
kuridhia, jambo ambalo halikufanyika, ila inaonekana kuwa marekebisho ya
mkataba huo yaliwekwa sahihi na wenyeviti wa vyama hivyo vitatu bila mihuri ya
vyama husika.
Hapo ndipo penye utata wa aina mbili ambao ni mkubwa sana; kwanza, kampuni ya Fiona T. Ltd ambayo ilipaswa
kutaarifu vyama husika nia yake ya kutaka kufanya marekebisho ya mkataba wa
kwanza hawakufanya hivyo; pili, wenyeviti walioweka sahihi kuwakilisha vyama
husika hawakuweka mihuri ya vyama vyao kuhalalisha ridhaa yao.Pamoja na tata
mbili zilizotajwa hapo juu, upo utata mwingine ambao ni wa msingi kabisa. Afisa
wa vyama vya Ushirika Wilaya ya Hai
alipopata habari kuhusu kusudio hilo la kutaka kufanya marekebisho ya mkataba
wa kukodisha mashamba hayo aliweza kuandika barua kwa wenye viti wa vyama hivyo
kuwataka kusitisha kuweka sahihi mkataba huo mpya hadi wanachama wa vyama vyote
vitatu watakapojulishwa kwenye mkutano wao wa pamoja . Barua hiyo ya tarhe 11
mei,2004 yenye kumbukumbu Na. LY/C.40/32/2 haikuwekwa maanani na wenyeviti hao.
Hapa inaonekana kwamba ulikuwapo ujanja
na hila ambayo haiwezi kukanushwa kwa urahisi. Mwekezaji Fiona T. Ltd na
pia wenye viti wa vyama vitatu vya Ushirika wanapaswa wajieleze kwa nini
walipuuza barua halali ya Afisa Ushirika wa Wilaya.
3. Mkutano wa wanachama wa vyama
vitatu-uswaa/mamba,shari na kyeri.
Kutokana na fununu zilizosikika na baadhi ya washirika wa
vyama vya ushirika kuwa ulikuwepo ugomvi kati ya Bw.B.A Mengi na mshirika wake
Bw.David Stewart Middleton kuhusu mashamba ya Silverdale/Mbono walitaka uongozi
wa vyama vitatu viite mkutano ili wanachama waelezwe kilichokuwa kinaendelea
katika mashamba hayo.
Hatimaye mkutano uliitwa;wanachama wa vyama vyote vitatu
yaani Uswaa/Mamba,Shari na Kyeeri wakakutana katika uwanja wa soko la Bwani
karibu na chama cha ushirika shari tarehe 17.1.2006
Mahudhurio ya kikao:
1.
Wajumbe wanachama 300
2.
Wajumbe wa Halmashauri ya vyama vitatu
3.
Wajumbe wa Halmashauri ya mashamba Silverdale na
Mbono
4.
Afisa ushirika Hai Bw.R.A Masamu,
5.
Msaidizi wa Afisa Ushirika Hai Bw.Fura Uroki
6.
Bw. Menjamini A Mengi –Mwekezaji (Fiona T Ltd)
Wajumbe wa mkutano walielezwa historian na malengo ya
uwekezaji katika mashamba ya Silverdale na Mbono.Pia wakajulishwa kwamba miaka
mitatu ya kwanza hapakuwepo matatizo kati ya mwekezaji na wamiliki wa
shamba.Kwamba mwekezaji alilipa kodi yake kwa wakati ila bodi ya mashamba
haikuita mkutano wa wanachama wa vyama vyote vitatu kwa pamoja kwa kipindi cha
miaka saba;yaani 1999-2005 kama ilivyotazamiwa kuwaeleza maendeleo ya mashamba
yaliyokodishwa na mwekezaji.Vile vile hawakupewa tafsiri ya Kiswahili ya
mkataba kama walivyokuwa wamedai hapo mbeleni waliposomewe mkataba wa kwanza
kwa kuwa wengi wa wanachama hawakujua kiingereza.
Baada ya mazungumzo ya muda mrefu,maswali na majibu kutoka
kwa wajumbe wa halmashauri ya zamani na
mpya,na pia mwekezaji Bw.Benjamen A.Mengi mkutano mkuu uliazimia yafuatayo:-
a)
Kwamba Halmashauri ya zamani ya mashamba ivunjwe
mara moja.
b)
Kwamba halmashauri ya vyama
vitatu-Uswaa/Mamba,Shari na Kyeeri ichukue wajibu wake mara moja.
c)
Kwamba mkutano mkuu hautabui Bw.David Stewart
Middleton ila unatambua mwekezaji ambaye ndiye aliyeandika mkataba nao,yaani
Fiona Tanzania Limited.
d)
Kwamba Halmashauri za vyama
vitatu-Uswaa/mamba,Shari na Kyeeri siteue kamati ndogo miongoni mwake ambayo
ndiyo itakayochukua wajibu zote badala ya Bodi iliyovunjwa kwa niaba yake.
e)
Kwamba kamati mpya izuru mashamba hayo mara moja
na kuona hali ilivyo.
f)
Kwamba kamati hiyo iangalie mkataba uliopo kama
kuna dosari ichukue hatua za kuurekebisha.
itaendelea kesho.
Have you ever heard of the laws of Defamation?
ReplyDeleteNone of what you have printed here has any l;eag content, what you are showing is the theft of British investment-shame on you!
Sarah Hermitage.