Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamhuna mara alipowasili
katika Kijiji cha Mbuyu Tende Wilaya ya Kaskazini “A”kwa ajili ya
kufungua Skuli ya Primary yenye madarasa Manne,ikiwa ni Shamra shamra za
Maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikata Utepe
kuashiria kufungua Skuli yenye madarasa manne katika Kijiji cha Mbuyu
Tende Wilaya ya Kaskazini “A”,ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya
Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akipanda Mche wa
Mnazi baada ya kuupanda katika eneo la Skuli ya Mbuyu Tende Wilaya ya
Kaskazini “A”,Baada ya Kuifungua Skuli hiyo ikiwa ni Shamra shamra za
Maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Wanafunzi
wa Skuli ya Mbuyu Tende Wilaya ya Kaskazini “A”,wakifurahia Baada ya
kufunguliwa kwa Skuli yao ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
kufunguliwa kwa Skuli yao ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
……………………………………………………….
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
Makamo
wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Shariff
Hamad amewataka Wazazi na Walezi wa Wanafunzi wa Skuli ya Mbuyu Tende
kujenga Mashirikiano na Walimu ili kuweza kuwapatia haki na fursa sawa
wanafunzi wa kike na wakiume Skulini hapo.
Hayo
ameyasema leo huko Skuli ya Msingi Mbuyu Tende Wilaya Kaskazini “A”
Unguja wakati wa ufunguzi wa skuli hiyo ikiwa ni mwendelezo wa shamra
shamra za kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Maalim
Seif amewataka Wazazi wasikubali kuwaozesha watoto wa kike waume
mapema kwani hali hiyo ndiyo inayochangia ukosefu wa Walimu wa kike
wazawa katika Vijiji vingi.
Aidha
alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaendelea kuwapatia
wananchi wake haki ya elimu bila ya malipo ili kuondosha adui ujinga na
kuwaletea maendeleo.
“Elimu ni msingi wa maisha kwa vijana na ndio inayoleta maendeleo na
mwangaza hasa wakati wa sasa na ujinga ni kiza katika maisha ya
leo,”alisisitiza Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment