WAMILIKI wa vyombo vya habari nchini, (MOAT),wameaswa
kuzingatia muda na wakati wa kurusha matangazo katika vyombo vyao, kwa
sababu baadhi yake yameonekana kupoteza maadili kwa jamii hususani
watoto ambao ni Taifa la baadaye.
Akizungumza na FULLSHANGWEBLOG jijini Dar es Salaam
jana, Katibu wa Taasisi ya kupambana na Udanganyifu wa matumizi ya
rasilimali za Taifa (CFRI), Andendekisye Mwakabalula, alieleza kuwa
kutokana na mfumo mbaya wa matangazo hususankatika televisheni utasababisha madhara kwa kizazi hiki na cha baadaye.
Katika hilo, aliwataka wamiliki
hao kuangalia njia mbadala ambayo haitaleta madhara kwa jamii pindi wa
matangazo hayo yatakaporushwa au kuonyeshwa kwenye vyombo hivyo.
Mwakabalula aliyataja baadhi ya
matangazo ambayo yanachochea uvunjifu wa maadili ni mfano wa matangazo
ya mpira wa kiume ‘kondomu’,filamu za ngono pamoja na mengine ambayo
hayafundishi maadili bali yanapotosha.
“Ikiwa wamiliki wa vyombo vya
habari wamebaini wazi kuwa maadili ya nchi yameporomoka, walitakiwa kuwa
mifano mizuri ya kuigwa ndani ya jamii, hususani kwa kutumia fursa ya
matangazo yanayoibadili katika suala zima la maadili” alisema
Mwakabalula
Aidha, alisema ikiwa wamiliki
hao watatumia vyombo vyao kuhamasisha juu ya maambukizi ya virusi vya
ukimwi (HIV), kupitia matangazo mbalimbali basi waangalia muda na wakati
wa kuyaonyesha kwa lengo la kutowaumiza watoto ambao hawajafikia umri
wa kuyasikiliza au kuyatizama.
Pamoja na hilo, aliitaka Katiba
mpya kupitia mchakato wa mapendekezo ya maoni ya wananchi, kuangalia
namna ya kuiweka kipengele cha mkakati huo wa matumizi ya matangazo ili
kuleta uwiano na manufaa ndani ya jamii.
No comments:
Post a Comment