Ni simulizi ya kweli ambayo
imewatokea watu mbali mbali.
Mtunzi : Shaaban Mpalule
kufanya maamuzi siku zote ni jambo
gumu linalomuweka mtu kwenye wakati
mgumu sana, nampenda sana mke wangu, nipotayari kufa kwa ajili yake kwa kuwa
nafahamu thamani yake kwangu, lakini nitaonekanaje kwa wananchi ninapotakiwa
kumteka Mhe Rais ili nimuokoe mke wangu asiuwawe, japo ni jambo gumu ila mimi
nitaweza tu?
Niliumiza sana kichwa changu kuwaza huyu
mwanamke, ninavyompenda, ilikuwa ni mara tu baada ya kukutana naye kwa mara ya
kwanza, wakati huo tukiwa bado vijana, macho yangu yalipogongana na macho ya mrembo
huyo ghafla mwili na mapigo ya moyo yalinienda mbio sana, sikuwa na njia ingine
zaidi ya kutaka kumfahamu, lakini sikuweza kupata fulsa ya kuzungumza naye pamoja
na kwamba macho yetu tulipotazamana kila mmoja alihisi kitu Fulani.
Usiku wa siku hiyo nilikuwa nimezoea chakula mapema sana lakini siku hiyo
sikuwa na furaha hata chembe, nilihisi nimeshiba pamoja na kwamba sikuwa
nimepata kula kwa masaa hayo ya usiku,na muda mwingi nilibaki kuwaza kwa nini
imenitokea hali hiyo na aijawahi kutokea wakati wote pamoja kwamba
nimewahi kukutana na wasichana wengi warembo, na wakati mwingine nilipewa jina
mitaani kwamba mtu wa warembokutokana na sifa niliyokuwa nayo ya kuwa karibu
sana na wasichana wengi warembo ambao ni wazuri sana.
“Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia
msaidizi wa kufanana naye.”
Sasa kama mungu alisema si vema huyo mtu kuwa peke yake, nikajiuliza, je huyu
ni nani basi ambaye mungu amemweka ili afanane naye?
Tena Bwana Mungu akasisitiza katika kumwagiza huyo mtu, akisema, Matunda
ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na
mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Kumbe wakati najaribu kutafakari tayari usingizi mzito ukanipitia nikalala;
nilipostuka ilikuwa ni usiku mkubwa sana , sikupata tena usingizi maana
nakumbuka nilikurupuka kutoka usingizi ule mzito nikiwa nimelowa jasho mwili
wote kutokana na joto la chumba kuwa kali, hivyo nilichukua kitabu change Agano
jipya –kitabu cha neno la mungu na kuanza kusoma hadi ilipofika asubuhi.
Hakuna kitu kibaya kama moyo kupenda, moyo ukipenda unaweza kuwa kichaa
tena unaweza kuitwa chizi wa mapenzi, au utasikia kachizika huyu, ndiyo ile mtu
anaonekana kuwa na mapenzi ya fujo, wakati mapenzi ni matamu na yanatakiwa kuwa
mapenzi ya kweli (Mapenzi ni maisha).
Niliendelea na shuguli zangu mapema
asubihi ya siku hiyo, nakumbuka niliamka 11:30 alfajili, nikavaa vifaa vyangu
vya michezo hadi uwanjani ambako ilinibidi nifanye mazoezi mengi ili kupoteza
hisia za mawazo iliyokuwa inatawala ndani ya nafsi yangu, na bahati nzuri hali
ya hewa ya siku hiyo ilikuwa ya mvua mvua ivyo nilifanya mazoezi kwa muda mrefu tofauti na siku nilizofanya
mazoezi najua.
“Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi
usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,
wana
wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake
wo wote waliowachagua” nilijaribu kuitafakari sana hiyo mistari ilikuwa ni
baada ya kusoma neno la mungu usiku wa jana kwa hiyo ilikuwa imekaa kichwani,
nikaanza kujiuliza Wana wa MUNGU ni kina nani na waliwaona Binti za Wanadamu ya
kuwa ni wazuri wakajitwalia wowote, je
kumbe kuna wana wa mungu na binti za wanadamu, ndipo nilipogundua kwamba kumbe
inawezekana wewe ukawa ni bint wa wanadamu, ama wewe ni mwana wa mungu? Lakini mbona
mungu mwenyewe ameweka utaratibu huo kuwa “wana wa Mungu walipoingia kwa binti za
binadamu,wakazaa nao wana; hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye
sifa.
Je ni sahihi kuwaza mambo ya kale na ambayo ni mabaya katika kutengeneza
jambo jema? “Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na
kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote.
Bwana
akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.
Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa
nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana
naghairi ya kwamba nimewafanya.
Wakati wa nuhu kila mnyama wa mwitu
kwa jinsi yake, na kila mnyama wa kufugwa kwa jinsi yake, na kila kitambaacho,
chenye kutambaa juu ya nchi, kwa jinsi yake, na kirukacho kwa jinsi yake, kila
ndege wa namna yo yote.
Waliingia katika safina alimo Nuhu, wawili wawili, wa kila chenye
mwili kilicho na pumzi ya uhai ndani yake. Na walioingia, waliingia mume na
mke, wa kila kitu chenye mwili, kama vile alivyomwamuru Mungu;
Usikose kufuatilia Adithi hii kila
siku 0713869133/0767869133