Posted: 06 Feb 2013 01:27 AM PST
Mchuuzi wa Samaki, Bw. Aloyce Sebastian akimfunga samaki na mpira (rubber band) ili maji yasiingie katika mapezi, kama alivyokutwa kwenye Soko la Samaki la Kimataifa Feri, Dar es Salaam hivi karibuni. Wateja wengi huamini samaki mwenye mapezi mekundu kuwa ni salama kwa kitoweo. (Picha na Asia Mbwana) |
Posted: 06 Feb 2013 01:24 AM PST
Na Goodluck Hongo KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa, amesema chama hicho kitatumia ngumu ya umma kupeleka hoja zote za wabunge zilizokataliwa bungeni kwa wananchi. Dkt. Slaa aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa, hakuna mahakama nyingine za kuwashtaki Spika wa Bunge Bi. Anne Makinda na Naibu wake, Bw. Job Ndugai. “Hakuna mahakama yoyote ya wananchi iliyowahi kushindwa, nasi tutapeleka hoja zote zilizozimwa na bungeni na Spika Makina pamoja na Naibu wake Ndugai kwa wananchi,” alisema Alisema chama hicho kilishatangaza mwaka huu ni wa nguvu ya umma hivyo kitendo cha Spika na Naibu wake kushindwa kuliongoza Bunge ambalo ndiyo linaisimamia Serikali kwakuzima hoja muhimu kwa masilahi ya nchi na Watanzania,wananchi watatoa hukumu kwa Serikali na CCM. “Wananchi wanashindwa kupata haki zao mahakamani, polisi na sehemu zingine na hivi sasa vitendo hivi vimehamia bungeni kwa kuzima haki za wananchi.“Ipo siku uvumilivu utakwisha na kujua kwa nini nchi za Rwanda na Burundi waliingia vitani...nchi hizi hazijaingia katika vurugu kwa kupenda bali kutokana na ukandamizaji kama huu,” alisema. Alisema mwaka 2011, aliwahi kusema Tanzania haitatawalika na kuitwa mchochezi lakini leo maamuzi ya Spika ni ya kukandamiza wananchi kwani hoja zilizozimwa ni kwa manufaa ya Watanzania ambapo Spika na Naibu wake, wanaongoza Bunge kwa chuki. Aliongeza kuwa, kutokana na hilo amewaagiza wabunge wote wa CHADEMA kutokwenda kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge hadi Spika atakapoweka wazi rufaa 10 zilizokatwa na wabunge hao. Aliwataka wajumbe wote ambao watakwenda katika mabaraza ya kutoa maoni ya Katiba Mpya, watoe mani ya kutaka Spika na Naibu wake wasitokane na chama chochote cha siasa ili Bunge liweze kufanya kazi kwa niaba ya wananchi si kwa matakwa ya CCM. Dkt. Slaa alisema, hivi sasa viongozi wanaoliongoza Bunge hilo, wameshindwa kutekeleza wajibu wao kwa kupindisha kanuni za Bunge wazi wazi na kama zingefuatwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, angejiuzulu. “Samuel Sitta (Mbunge wa Urambo, mkoani Tbaora na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki), aliongoza Bunge kwa aibu pale alipotaka kupindisha sheria lakini Spika wa sasa na Naibu wake ni balaa zaidi,” alisema Dkt. Slaa. Alisema cham hicho kinawapongeza wabunge wote wa upinzania waliosimama bungeni kupinga maamuzi ya Spika na hiyo ndio njia pekee ya kutafuta haki za Watanzania. |
Posted: 06 Feb 2013 01:23 AM PST
Na Rehema Mohamed MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaaam, Machi 11 mwaka huu, inatarajia kutoa hukumu ya kesi ya wizi wa zaidi ya sh. milioni 100, inayowakabili vigogo wa Shirika la VUKA-Tanzania, linalohusika kuendesha miradi ya UKIMWI.Washtakiwa hao ni Mwenyekiti wa shirika hilo Bw. Adolf Mrema, Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Utawala, Bi. Hilda Urassa pamoja na mshauri Bw. Straton Simon, ambao wanadaiwa kutumia fedha za miradi ya UKIMWI. Jana kesi hiyo ililetwa mahakamani hapo kwa ajili ya utetezi ambapo washtakiwa hao, walijitetea mbele ya Hakimu Sundi Fimbo na kufunga ushahidi wao.Wakitoa utetezi wao, washtakiwa hao walikana kutumia isivyo halali fedha hizo kutoka Shirika la Maendeleo la Denmark (DANIDA) na Shirika la SAT-Tanzania. Kwa nyakati tofauti, washtakiwa hao walidai fedha hizo walizitumia kwa ajili ya matumizi ya ofisi kama dawa kwa ajili ya waathirika wa VVU, kuendesha semina na kulipa mishahara ya wafanyakazi wao. Hata hivyo, washtakiwa hao hawakuwa na nyaraka za kuthibitisha matumizi ya fedha hizo na kudai kuwa, nyaraka hizo zilichomwa moto na mwenye nyumba aliyewapangisha ofisi kwa kuwa waliifunga.Walidai mwenye nyumba baada ya kuona wamefunga osifi, aliamua kumpangisha mtu mwingine hivyo kutoa vitu vyao na kusababisha nyaraka zao kupotea na nyingine kuchomwa moto kama uchafu. Katika kesi hiyo, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 37 likiwemo la kugushi, wizi na matumizi mabaya ya fedha.Inadaiwa kuwa, washtakiwa hao walitenda makosa hayo kati ya Juni11,2006 hadi Desemba 2007, Temeke, Dar es Salaam. NYANYA |
Posted: 06 Feb 2013 01:20 AM PST
|
Posted: 06 Feb 2013 01:14 AM PST
Na Charles Mwakipesile, Mbeya MWENYEKITI wa Kanisa la Moravian nchini, Jimbo la Kusini, Mchungaji Clement Mwaitebele, mewataka wachungaji 14 ambao alitangaza kuwafukuza baada ya kukiuka kiapo chao cha utumishi Misheni ya Dar es salaam, kuondoka katika nyumba za kanisa.Akizungumza na Majira jana, Mchungaji Mwaitebele ambaye alionesha kukerwa na wachungaji hao kuvuruga amani ndani ya kanisa hilo kwa kujitangazia Halmashauri Kuu yao kinyume na Katiba, alisema uongozi wa kanisa umechukua hatua stahiki kwa watumishi hao kwa kuwa wasaliti katika jimbo mama. Alisema inashangaza wachungaji hao kudai hawaitambui mamlaka iliyowafukuza badara yake wanasubiri maelekezo ya uongozi wa Bodi ya Dunia (Unity Bord) ulio na Makao Makuu nchini Ujerumani hali inayoonesha kuwa, pamoja na usomi wao bado wameshindwa kutambua taratibu.“Kwa kuwa wameonesha kiburi cha kutoitambua mamlaka yangu kikatiba, natangaza rasmi kuwa kuanzia leo (jana), nimefuta ujio wa Bodi ya Dunia kuja nchini kuzungumzia tatizo hili kwa sababu tayari limekwisha hawana umuhimu wa kuja,” alisema. Mchungaji Mwaitebele alisema Ofisi la Dunia ni Makao Makuu ya Jumuia ya kanisa hilo kama ilivyo Umoja wa Mataifa ambao hauwezi kuingilia mambo ya ndani nchini Tanzania hadi unapopewa taarifa na uongozi wa nchi. “Sisi kama viongozi wa jimbo mama, hatuoni umuhimu wa hawa viongozi Bodi ya Dunia kuja kusikiliza mazungumzo kwa sababu tayari tumemaliza mgogoro uliokuwepo na taratibu za kisheria zinachukuliwa,” alisema. Aliwataka wachungaji hao kuhama mara moja katika nyumba za kanisa kwani hivi sasa si watumishi tena wa kanisa hilo kwa mujibu wa katiba baada ya kushindwa kulinda kiapo chao kilichowataka kuwa watii uongozi badala yake wanatumika kuleta mipasuko.Aliongeza kuwa, wao walifuata utaratibu wa kanisa wa kukaa mezani ili kusikiliza matatizo ya Misheni hiyo baada ya Sinodi ya eneo hilo kumuondoa madarakani aliyekuwa Mwenyekiti wao. “Wakati mazungumzo yakiendelea, Mwenyekiti huyo alitangza Halmashauri Kuu yake jambo lililoonesha wazi usaliti mkubwa katika kanisa,” alisema Mchungaji Mwaitebele.Aliwaonya Watunza Hazina wa kanisa hilo kuepuka kushirikiana na wachungaji hao kwa kuchukua fedha za matumizi yao binafsi kwani uongozi wake utawaburuta mahakamani kwa kosa la wizi wa fedha za umma jambo ambalo asingependa litokee. Alisema Mamlaka iliyowafukuza wachungaji hao ni halali ambayo ilichaguliwa na Mkutano Mkuu wa Kanisa na hivyo madai kuwa walipaswa kufukuzwa kwa pendekezo la Askofu ni upotoshaji wawanaoufanya ili kuliyumbisha kanisa. |
Posted: 06 Feb 2013 01:13 AM PST
Na John Gagarini, Pwani MABAHARIA sita wanahofiwa kufa maji baada ya jahazi walilokuwa wakisafiria kwenye Habari ya Hindi kuzama.Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei, alisema mabaharia hao walipanda jahazi la mizigo na walikuwa saba lakini mmoja ameokolewa. Alisema jahazi hilo linalofahamika kwa jina la Soweto, lilizama katika Visiwa vya Koma, eneo la Mwamba wa Chokaa, wilayani Mkuranga. “Usajiri wa jahazi hili bado haujafahmika na lilikuwa na shehena ya mbao na mirunda likitokea Kyasi kwenda Zanzibar,” alisema.Aliwataja baadhi ya mabaharia wanaohofiwa kufa maji kuwa ni Ally Hasan, Hassan Mamba, Nasoro Isa, Abdala Said na Husein Huku wakati Hasan Rajab, aliokolewa na wanaendelea kutafutwa.Aliwataka wananchi kutoa taarifa polisi kawa wataziona maiti zinazoelea majini. |
Posted: 06 Feb 2013 12:57 AM PST
Na Godfrey Ismaely, Manyara WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, amesema baada ya Rais Jakaya Kikwete kuona matukio ya ujangili nchini yanaongezeka siku hadi siku, muda wowote ataagiza majeshi yote kushirikiana ili kudhibiti matukio hayo.Hatua hiyo inatokana na Serikali ya Tanzania kusaidi dikezo maalumu na Serikali ya Marekani ambalo kushirikiana katika kudhibiti matukio ya ujangili nchini.Balozi Kagasheki aliyasema hayo jana mkoani Manyara katika hafla maalumu ya uzinduzi wa Kituo cha Mapokezi kwa watalii ambacho kipo chini ya Jumuiya ya Usimamizi wa Hifadhi ya Wanyapori Burunge (WMA), Wilaya ya Babati, mkaoni Manyara, kilichojengwa na Marekani kupitia Shirika lake la USAID. Jana (juzi) mimi na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Marekani Bw. David Hayes, tulisaini dokezo hili kwa lengo la kukomesha matukio ya ujangili nchini,” alisema na kuongeza kuwa, matukio ya ujangili yanaichafua nchi pia ni mateso kwa wanyama.Alisema mapambano dhidi ya majangili yanawezekana ambapo Serikali imeanza kujipanga ambapo Rais Kikwete, wakati wowote atatoa uamuzi kamka Amiri Jeshi Mkuu wa nini kifanyike kudhibiti hali hiyo nchini. Alisema suala la kucheleweshwa fedha zinazotokana na makusanyo ya WMA ambayo ni asilimia 50 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi, litafanyiwa kazi na wakati wowote mambo yatakuwa mazuri.Kwa upande wake, Bw. Hayes ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, alisema lengo la nchi yake kutoa ufadhiri kwa jumuiya za WMA nchini, mbali ya kulenga kukomesha ujangili pia jamii zitanufaika kupitia mapato mbalimbali. “Kufanikiwa kwa WMA ni fursa moja wapo ya kukomesha kabisa matukio ya ujangili yanayotokea Tanzania, vitendo hivi vinachangia kuhatarisha usalama wa binadamu, wanyamapori na hata kutatiza shughuli za utalii,” alisema Bw. Hayes.Balozi wa Marekani nchini, Bw. Alfonso Lenhardt's, alisema utaratibu wa wanajamii kuanzisha WMA nchini umeweza kuwa na mafanikio makubwa, kuboresha miradi ya shule, zahanati na kusomesha watoto kutokana na mapato yanayopatikana kutoka kwa wawekezaji walioingia nao mikataba. “Tangu mwaka 2006, WMA tisa zimeweza kuingia mikataba na wawekezaji binafsi katika sekta ya utalii ambapo zimefanikiwa kupokea zaidi ya dola za Marekani milioni tano kutokana na shughuli za uwindaji na upigaji picha. “Hatua hii imewezesha zaidi ya wanajamii 400,000 kunufaika kwa namna moja ama nyingine pamoja na kupata ajira hivyo Marekani itaendelea kuzijengea uwezo jumuiya hizi mara kwa mara ziweze kufikia malengo ya uhifadhi na maendeleo kwa wananchi,” alisema. MADAFU |
Posted: 06 Feb 2013 12:52 AM PST
|
Posted: 06 Feb 2013 12:48 AM PST
Na Masau Bwire, Bunda OFISA Mtendaji wa Kata ya Iramba, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, Bw. Simon Katikizu, amenusurika kifo baada ya wananchi wenye hasira kumshambulia kwa mawe wakimtuhumu kuiba mahindi ya msaada. Tukio hilo lilitokea juzi saa 4 asubuhi, Kijiji cha Isanju ambacho ni Makao Makuu ya kata hiyo ambapo wananchi walikusanyika ili kugawiwa mahindi ya msaada.Wakati kazi ya kugawa mahindi hayo ikiendelea, wananchi hao walibaini upotevu wa magunia zaidi ya 40 na baada ya kufanya uchunguzi, wakagundua wizi huo ulifanywa na Bw. Katikizu hivyo walianza kumshambulia kwa mawe na marungu. “Tumemkamata na mahindi ya msaada akiwa ameyaficha nyumbani kwake, katika Ofisi ya Elimu, kilimo na mengine aliyaweka katika nyumba za rafiki zake, wakati akijaribu kukimbia lilipigwa yowe,” alisema Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM, katika kata hiyo, Bw. Mohamed Gamba.Alisema Serikali ilipeleka msaada wa magunia 318 ya mahindi kwa ajili ya vijiji vitano vya kata hiyo ambapo kila kijiji kilipaswa kupata magunia 63 kutokana na njaa inayowakabili wananchi. Vijiji vilivyokumbwa na tatizo la njaa ni Isanju, Mugara, Sikiro, Nyarugoma na Mwiruruma, lakini Bw. Katikizu aliiba kiasi kikubwa cha mahindi ambapo kijiji cha Nyarugoma, kiliambulia magunia 26 ndipo wananchi walipokuja juu na kugundua wizi huo. Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw. Joshua Mirumbe, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa, tayari amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri amsimamishe kazi Bw. Katikizu kwa kosa hilo. “Huyo Ofisa Mtendaji habari zake ninazo, aliwahi kuiba na kuuza mitumbwi 20 iliyokamatwa katika uvuvi haramu hivyo kutokana na tukio hili, nimeagiza Mkurugenzi amsimamishe kazi kuanzia leo (jana) na ashitakiwe kwa wizi,” alisema Bw. Mirumbe.Alisema viongozi wa namna hiyo hawafahi kuendelea kuongoza na wanaitia doa Serikali hivyo hawana budi kuondoka wabaki viongozi waaminifu na waadilifu watakaowaletea wananchi maendeleo. “Siko tayari kuona viongozi wezi, wabadhilifu na wababaishaji wakiendelea kuwanyonya wananchi kwa kuwaibia, kama wapo wajiondoe kabla sijawafikia, nitaanza na huyo Ofisa Mtendaji ili iwe mfano kwa wengine,” alisema.Majira lilipomtafuta Bw. Katikuzu na kumuuliza juu ya tuhuma hizo alidai madai hayo ni uzushi uzushi na hakuna wizi wowote aliofanya bali yeye ni miongoni mwa Watendaji waadilifu wilayani humo wanaoaminiwa kiutendaji na Bw. Mirumbe. |
Posted: 06 Feb 2013 12:41 AM PST
Na Miriam Sarakikya
BAADHI ya wananchi wanaoishi mabondeni eneo la Tegeta kwa Ndevu, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, wameiomba Serikali iwasaidia kuwapa viwanja ili waweze kuondoka katika maeneo hatarishi kutokana na kero wanayopata kipindi cha mvua.Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti Dar es Salaam juzi, wananchi hao walidai wanashindwa kuondoka maeneo hayo kutokana na ukata wa fedha za kununulia viwanja. “Baadhi yetu wamejenga nyumba zao katika maeneo haya na wengine wamepanga, tunaiomba Serikali isikilize kilio chetu ili tuweze kuhamia maeneo salama tofauti na sasa kwani tunaishi kwa wasiwasi mkubwa,” alisema mkazi wa eneo hilo Bw. Edgar Msanganzila.Mkazi mwingine ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema hivi sasa eneo lao linafurika maji kutokana na mto uliopo jinani na makazi yao hivyo kuhatarisha maisha yao na familia zao. Hivi karibuni wananchi hao waliitisha mkutano wa hadhara na kukubaliana kuupanua mto huo maarufu 'Mto Tegeta', ili kupata njia ya kupitisha maji kirahisi pindi mvua zinaponyesha lakini hadi sasa mpango huo haujafanikiwa. Jela miaka 2 kwa kuua akidai sh. 4,000 |
Posted: 06 Feb 2013 12:40 AM PST
Na Pendo Mtibuche, Dodoma MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dodoma, juzi ilimuhumuku mkazi wa Dodoma Mjini, Yohana Chipini (23), kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua Alord Ndeshio, bila kukusudia wakati akidai sh. 4,000. Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mary Shangali baada ya mshtakiwa kukiri kosa na kumtia hatiani. Jaji Shangali alidai kuwa, amezingatia maelezo yaliyotolewa na upande wa mashtaka pamoja na utetezi kuhusu chanzo cha mauaji hayo ambacho ni ugomvi uliotokea kati yao wakati mshtakiwa alipokwenda kumdai marehemu fedha zake.Aliongeza kuwa, baada ya ugomvi huo mshtakiwa aliokota kipande cha ubao au kitu kinachoaminika kuwa kipande cha chuma na kumpiga nacho marehemu kichwani. “Adhabu ya kuua bila kukusudia ni kifungo cha maisha lakini kutokana na mazingira yalivyoonyesha na utetezi wa mshtakiwa, Mahakama imempunguzia adhabu na hivyo atatumikia kifungo cha miaka miwili gerezani,” alisema. Kabla ya hukumu hiyo, wakili wa mshtakiwa, Steven Kuwayawaya, aliiomba mahakama impunguzie adhabu mshtakiwa akidai kosa hilo ni la kwanza na amekiri kosa. Awali, ilidaiwa na upande wa mashtaka kuw, mshtakiwa alitenda kosa hilo mwaka 2012 katika barabara ya Bahi, Manispaa ya Dodoma. |
Posted: 06 Feb 2013 12:38 AM PST
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Tarakea, mkoani Arusha, Bw. Martin Kija (kushoto) na Balozi wa Japan nchini, Bw. Masaki Okada wakitia saini makubalino, Dar es Salaam jana, ambapo Serikali ya Japan itajenga mabweni ya wasichana ya shule hiyo. Ujenzi wa mabweni hayo utawaondolea tatizo la kutembea umbali mrefu kutoka maeneo wanayoishi. (Picha na Asia Mbwana) |
Posted: 05 Feb 2013 10:33 PM PST
Na Pendo Mtibuche, Dodoma MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dodoma, juzi ilimuhumuku mkazi wa Dodoma Mjini, Yohana Chipini (23), kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua Alord Ndeshio, bila kukusudia wakati akidai sh. 4,000. Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mary Shangali baada ya mshtakiwa kukiri kosa na kumtia hatiani. Jaji Shangali alidai kuwa, amezingatia maelezo yaliyotolewa na upande wa mashtaka pamoja na utetezi kuhusu chanzo cha mauaji hayo ambacho ni ugomvi uliotokea kati yao wakati mshtakiwa alipokwenda kumdai marehemu fedha zake. Aliongeza kuwa, baada ya ugomvi huo mshtakiwa aliokota kipande cha ubao au kitu kinachoaminika kuwa kipande cha chuma na kumpiga nacho marehemu kichwani.“Adhabu ya kuua bila kukusudia ni kifungo cha maisha lakini kutokana na mazingira yalivyoonyesha na utetezi wa mshtakiwa, Mahakama imempunguzia adhabu na hivyo atatumikia kifungo cha miaka miwili gerezani,” alisema. Kabla ya hukumu hiyo, wakili wa mshtakiwa, Steven Kuwayawaya, aliiomba mahakama impunguzie adhabu mshtakiwa akidai kosa hilo ni la kwanza na amekiri kosa.Awali, ilidaiwa na upande wa mashtaka kuw, mshtakiwa alitenda kosa hilo mwaka 2012 katika barabara ya Bahi, Manispaa ya Dodoma. |
Posted: 05 Feb 2013 10:30 PM PST
Na Mariam Mziwanda MAOFISA Kilimo zaidi ya 20 kutoka Wilaya tano nchini, wapo kwenye mafunzo ya mradi shirikishi wa kupunguza wimbi la viwavi jeshi ambavyo ni kero sugu kwa wakulima na kusababisha njaa katika baadhi ya maeneo nchini.Akizungumza katika mafunzo hayo Dar es Salaam juzi, mwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye pia ni Ofisa Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Kanda ya Kaskazini, Bw. Didas Moshi alisema mafunzo hayo yatawasaidia maofisa hao kuwatambua na kuwaangamiza kabla ya kukua. “Tumeanza mafunzo haya na Wilaya tano ambazo ni Kisarawe, Nachingwea, Masasi, Lindi Vijijini na Kilwa, mafunzo haya yanaendeshwa kwa msaada wa watu wa Marekani ambao wameona viwavi jeshi ni kero kwa wakulima,” alisema.Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Afya ya Mimea kutoka katika Wizara hiyo, Cornelius Mkondo, alisema mazao mengi ya wakulima nchini yamekuwa yakiathiriwa na milipuko ya wadudu sugu wanaoshambulia mazao kwa haraka.Alisema viwavi jeshi wamekuwa wakipoteza nguvu kazi za wakulima hivyo imeamua kutafuta mbinu za kuwatokomeza. Aliongeza kuwa, maofisa hao watafundishwa mambo mengi hususan jinsi ya kufahamu mlipuko unavyotokea na kuimarisha mawasiliano kati ya vijiji, kata, Wilaya hadi Taifa.“Lengo ni kujilinda na viwavi, katika kuhakikisha operesheni hii inakuwa endelevu, tutashirikiana na kampuni za simu ili wakulima waweze kufahamu utabiri wa hawa wadudu waharibifu,” alisema na kuongeza kuwa, mradi huo mbali ya Tanzania pia unaendeshwa katika nchi za Kenya na Ethiopia. |
Posted: 05 Feb 2013 10:29 PM PST
Na Rose Itono WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imekabidhiwa majukumu ya kuweka viwango vya ubora wa elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za elimu kuanzia awali mpaka sekondari.Sambamba na hilo wizara pia ina wajibu wa kuhakikisha kuwa elimu ya awali,msingi,sekondari na ile ya watu wazima inatolewa kwa kuzingatia viwango vinavyokubalika. Wizara pia ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa utoaji wa elimu kwa kufanya ufuatiliaji na tathmini pamoja na kufanya mapitio,kuandaa na kutoa mapendekezo ya marekebisho ya Sera, Mipango, Sheria na kanuni za elimu zilizopo,kulingana na mabadiliko ya dhima na dira ya Serikali huku ikiandaa mikakati ya utekelezaji wake. Aidha, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ndiye msimamizi mkuu wa masuala ya taaluma katika ngazi zote za elimu na mafunzo.Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatekeleza mipango mbalimbali ili kuinua ubora wa elimu Ili yote hayo yaweze kufanikiwa juhudi za wazazi na walezi kwa kushirikiana na wanafunzi zinahitajika kwa kiasi kikubwa katika kuleta matokeo mazuri.Nimeongea hivyo kwa makusudi kwani kumekuwa na baadhi ya wazazi,walezi ambao wamekuwa wakiwakatisha masomo wanafunzi hasa wa kike kwa kutaka kuwaoza kwa nguvu kwa nia ya kujipatia fedha ama mali. Nionavyo kwa kufanya hivyo kutalipunguza tatizo la wazazi ambao wana tamaa za kujipatia pesa kwa mahari kupitia watoto wao bila kuangalia madhara na vitu vya msingi ambavyo mtoto wa kike atavikosa kutokana na kuolewa bila kuwa na elimu. Hivi karibuni tumeshuhudia mtoto wa kike ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Tongani kata ya Mkaramo wilayani Pangani akitoroka kwao na kukimbilia kujificha porini akikwepa kuachishwa shule.Nionavyo hali hii ni hatari kiusalama kwa mtoto huyo ambaye angeweza kupata madhara ya kukutana na wanyama wakali na hata kupoteza maisha.Hali ya mtoto huyo kuamua kulala porini ilimuwezesha kufika kwa Mkuu wa Wilaya ya handeni kuomba msaada ambao utamuwezesha kuweza kuendelea na masomo. Nionavyo kulingana na hali hiyo ni wanafunzi wangapi wenye ujasiri kama aliouonyesha msichana huyo ambaye aliamua kujitoa muhanga na kuamua kulala porini ili kukimbia kuolewa.Kwa maelezo ya mtoto huyo anasema aliamua kukimbilia kwa Mkuu wa Wilaya baada ya kusikia kuwa kuna mradi wa 'Niache Nisome' ambao umeanzishwa kwa ajili ya kumkomboa mtoto wa kike dhidi ya mimba na ndoa za utotoni. Nionavyo kwa mfano wa mradi huu ni wazi serikali ikaona umuhimu wa mradi huo kusambaa nchi nzima ili kuwawezesha vijana wa kike kujikomboa na ndoa na mimba za utotoni. |
TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Thursday, February 7, 2013
UTUNZAJI CHADEMA kuwashtaki Makinda, Ndugai *Dkt. Slaa adai wameshindwa kuliongoza bunge Hukumu ya vigogo Shirika la VUKA kutolewa Machi 11 NYANYA Mgogoro Moravian wachukua sura mpya Mabaharia 6 wahofiwa kufa maji Serikali yajipanga kukomesha ujangili nchini MADAFU Mtendaji anusurika kifo akidaiwa kuiba mahindi Wakazi waishio mabondeni Tegeta waomba viwanja Jela miaka 2 kwa kuua akidai sh. 4,000 MKATABA Jela miaka 2 kwa kuua akidai sh. 4,000 Wapema mafunzo kupunguza viwavi jeshi Mradi wa 'Niache Nisome' usambazwe nchi nzima
Monday, February 4, 2013
Lowasa awakonga nyoyo Walimu na Wanafunzi katika Shule ya Benjamini Mkapa Sekondari
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya kuwaga wanafunzi wa kidato cha sita shule ya Benjamini Mkapa, Waziri Mkuu Mstaafu-na Mbunge jimbo la Monduli Edward Lowasa, akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya kuwaga wanafunzi wa kidato
cha sita shule ya Benjamini Mkapa, Waziri Mkuu Mstaafu-na Mbunge jimbo
la Monduli Edward Lowasa, akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo
Mhitimu wa Kkidato cha Sita katika shule ya Sekondari Benjamini Mkapa na Msanii wa Commedy,Daudi Festo, akionyesha moja ya vichekesho wakati wa hafla hiyo kwa mgeni Rasmi
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa, akipiga picha na Wanafunzi wa Shule hiyo
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa, akipiga picha na Viongozi wa Shule hiyo
washiriki wa Onyesho la Miss Demokrasia Tanzania-Benjamini Mkapa Sekondari katika miondoko ya kimiss
wanafunzi wa shule hiyo katika picha
washiriki wa Onyesho la Miss Demokrasia Tanzania-Benjamini Mkapa Sekondari-wakijibu maswali
Wwashiriki wa Onyesho la Miss Demokrasia Tanzania-Benjamini Mkapa Sekondari katika pozi
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa, akipiga picha na Wwashiriki wa Onyesho la Miss Demokrasia Tanzania-Benjamini Mkapa Sekondari
Wanafunzi wa Kidato cha Sita wakifuatilia kwa makini
Wazazi wa wanafunzi wakifuatilia hafla hiyo
Wahitimu wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa, wakiimba Shairi(Picha kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzanzania)
Mbatia alitikisa Bunge Dodoma *Ni kuhusu hoja ya udhaifu sekta ya elimu *Wabunge wa CHADEMA, CCM wavutana Jahazi lazama Z'bar, 10 wahofiwa kufa *22 waokolewa, lilikuwa na abiria 32 Madiwani Kigamboni waponzwa na mwaliko wa Tibaijuka Pinda ataka amani itawale Mtwara Mvua yaua mwanafunzi, yajeruhi Mkakati wa kumtoa Ponda waandaliwa Sijaridhishwa na taarifa Waziri Pinda kuhusu gesi Hoja ya Mbatia imeona mbali ILALA YAANIKA MAFANIKIO YA RAIS KIKWETE Kaseba aapa kuonesha uwezo wake UZITO Ligi Kuu ya Grand Malt kuanza leo Azam yatamba kuendeleza vipigo Meru yazipa 'tafu' timu sita MICHEZO Kocha Stars aita wa kuivaa Cameroon *Amir Maftah, John Bocco watemwa TFF yatupa pingamizi zote zilizowekwa
Posted: 01 Feb 2013 02:01 AM PST
Rose Itono na Goodluck Hongo MBUNGE wa kuteuliwa kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia, jana aliwasilisha hoja binafsi iliyoainisha suala zima la udhaifu uliopo katika sekta ya elimu nchini. Alisema kukosekana kwa mitaala katika shule za msingi na sekondari kunachangia wanafunzi kufanya vibaya na utendaji mbovu wa kitengo cha kuandaa mitaala hiyo, kimeshindwa kufanya kazi zake ipasavyo na kusababisha usambazaji vitabu kunuka harufu ya rushwa. Hoja hiyo iliyoibua mvutano mkali wa wabunge, iliwasilishwa bungeni mjini Dodoma. Baadhi ya wabunge walishauri iundwe Kamati Teule ya Bunge kuchukuza udhaifu huo na wengine wakitaka hoja hiyo ifanyiwe kazi na Serikali. Kutokana na hali hiyo, Spika wa Bunge Bi. Anne Makinda alilazimika kusimama na kujibu hoja za wabunge lakini kambi ya upinzani ilikuwa na msimamo wa kutaka iundwe Kamati Teule ya Bunge kuchunguza udhaifu ulioainishwa na Bw. Mbatia.Wabunge wa CCM walipinga msimamo wa kambi ya upinzani na kutaka hoja hiyo ifanyiwe kazi na Serikali wakidai Bw. Mbatia ameainisha mambo mengi ambayo kaamati haiwezi kuyafuatilia kwa wakati mmoja yakiwemo ya kisera.Akichangia hoja hiyo, Mbunge wa Simanjiro, mkoani Manyara, Bw. Christopher Ole Sendeka (CCM), alishauri hoja hiyo iachewe Serikali na kusisitiza kuwa, kikanuni kazi ya kuunda Kamati Teule hasa kwa suala la elimu linahitaji ujuzi na utaalamu wa hali ya juu.“Japo kuwa wabunge ni wasomi, hakuna ambaye ni mtaalamu wa masuala hayo hivyo jambo hili liachiwe Serikali ifanyie kazi hoja ambazo zimewasilishwa na Bw. Mbatia,” alisema. Mbunge wa Arumeru Mashariki, mkoani Arusha Bw. Joshua Nassari (CHADEMA), alisema inaonekana wabunge wameanza kukimbia majukumu ya kibunge kwa kukataa tume hiyo isiundwe. Alisema kazi kubwa ya wabunge ni kuisimamia Serikali ambayo haiwezi kujisimamia yenyewe. “Katika Bunge hili, iliungwa Kamati Teule ikiongozwa na Dkt. Harrison Mwakyembe, kuchunguza sakata la Richmond...” alisema Bw. Nassari. Mbunge wa Peramiho, mkoani Ruvuma, Bi. Jenista Mhagama (CCM), alisema kwa mtazamo wake wabunge wote wanajenga nyumba moja hivyo jambo la msingi ni kuangalia namna ya kuiboresha hiyo iweze kufanya kazi zake vizuri. Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA), alisema elimu ni gharama hivyo lazima madudu yaliyomo ndani ya sekta hiyo yaondolewe na kupatiwa ufumbuzi wa kudumu. “Hoja aliyoitoa Bw. Mbatia ni ya msingi kwani elimu ni gharama kubwa hivyo lazima ijadiliwe kiundani na kukokotoa madudu yote, kazi ya bunge ni kuisimamia Serikali si vinginevyo,” alisema na kuongeza kuwa, kamwe Serikali haiwezi kujichunguza yenyewe. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, alisema Serikali imezingatia hoja zilizotolewa na Bw. Mbatia na kuahisi kuifanyia kazi ambapo hivi sasa wapo katika mapitio ya sera ambayo yamechukua muda mrefu. “Ieleweke kuwa, kuna mambo makubwa yanapaswa kuangaliwa ili ifikapo 2020, Taifa liweze kufikia hadhi ya kimataifa,” alisema. Katika hoja yake, Bw. Mbatia alidai pamoja na mambo mengine, kuna kasoro nyingi kwenye mitaala wakati mwingine mtuzi wa vitabu anageuka kuwa Mhariri jambo ambalo si sahihi. Jahazi lazama Z'bar, 10 wahofiwa kufa *22 waokolewa, lilikuwa na abiria 32 |
Posted: 01 Feb 2013 02:00 AM PST
Na Mwandishi Wetu WATU 11 wanahofiwa kufa maji baada ya jahazi la Sunrise, ambalo lilikuwa likitokea mkoani Tanga kwenda Zanzibar kuzama katika eneo la Nungwi. Habari zilizolifikia gazeti hili ambazo zimethibitishwa na baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Polisi Zanzibar, zilidai jahazi hilo lilibeba watu 32 ambapo hadi jana mchana, 21 walikuwa wameokolewa. Inadaiwa kuwa, jahazi hilo mbali ya kubeba abiria pia lilikuwa na mizigo ambapo jitihada za kuwatafuta abiria wengine zinaendelea na hakuna taarifa za mtu aliyepoteza maisha hadi sasa kutoka pangani kwenda kwenda zanzibar- abiria 27 na manahodha watano eneo la maziwe, jirani na Nungwi kati yao 21 wameokolewa wakiwa hai 11 hawjulikani walipopigwa lilikuwa la kusafirisha mizigo kwenda zanzibar Msemaji Mohamed Muhina msemaji wa Jeshi la Polisi wakati akihojiwa na idhaa ya kiswahili ya BBC alisema manahodha wameokolewa baadhi yao hawajapatikana "Ni Kweli taarifa za tukio hilo zipo lakini sina taarifa zaidi, labda unaweza kuwasiliana na Kamanda wa Polisi Kaskazini Unguja, aliyeko eneo la tukio anaweza kukupa taarifa zaidi," alisema mmoja wa maofisa wa polisi Zanzibar. Juhudi za kumpata kamanda hiyo aliyetwa kwa jina moja la Ahamada hazikuweza kuzaa matunda kutokana na simu yake kutopokelewa muda. Kuzama kwa jahazi hilo na mfululizo wa ajali za baharini ambazo zimekuwa zikitokea katika habari ya Hindi na kusababisha vifo vya watu wengi. Mwaka jana Meli moja inayomilikiwa na kampuni ya SEAGAL iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Zanzibar Tanzania ilizama katika bahari ya Hindi baada ya kukumbwa na dhoruba kali na hatimaye kupinduka. Kwa mujibu wa jeshi la polisi visiwani Zanzibar meli hiyo iliondoka Dar es Salaam mchana na imepatwa na ajali hiyo huku ndani yake kukiwa na abiria zaidi ya 200. Kabla ya meli hiyo kuzama, meli nyingine iliyokuwa ikitoka Zanzibar kwenda Pemba ya MV Spice, ilizama kwenye mkondo wa Nungwe na kusababisha vifi vya watu karibu 200. |
Posted: 01 Feb 2013 01:57 AM PST
Na Andrew Ignas
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Temeke, limemtaka Meya wa halmashuri hiyo, Bw. Maabadi Hoja, awachukulie hatua za kinidhamu madiwani wa Kigamboni waliokubali mwaliko wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka. Hali hiyo inatokana na madiwani hao kuridhia kuundwa kwa Kamati Maalumu ya kusimamia mradi wa Mji Mpya wa Kigamboni bila kumshikilisha Mwenyekiti wa halmashauri hiyo na madiwani wa Temeke ili kutetea haki na masilahi ya wananchi. Wakizungumza katika kikao cha baraza hilo kilichokuwa kikijadili ajenda mbalimbali za halmashauri, madiwani hao akiwemo Bw. Wilfred Kimati (Kata ya Kurasini) na Naibu Meya Bw. Noel Kipangule (Kata ya Chang'ombe), walisema umefika wakati wa Bw. Hoja kuonesha makucha yake kwa madiwani hao. Walisema madiwani hao wameonesha usaliti mkubwa kwa kukubali mwaliko huo na kuridhia uundwaji wa kamati hiyo. “Suala hili kama tutalifumbia macho, litaleta vita kwa sababu kama madiwani wa Temeke tumetelekezwa, itakuwa vigumu wananchi kupata taarifa za jambo hili ndio maana tunamuomba Meya atoe adhabu kwa madiwani hawa,” walisema. Waliongeza kuwa, licha ya kuundwa kamati hiyo bado Serikali ilitakiwa kuwashirikisha madiwani wa Temeke ili waweze kuzungumza na wananchi wao. Diwani wa Kata ya Makangalawe, Bw. Victor Mwakasindile, Prof. Tibaijuka anapaswa kuandaa semina maalumu itakayoshirikisha madiwani ili waweze kutoa elimu kwa umma juu ya mradi huo ili kuepukana vurugu kama zilizotokea mkoani Mtwara. “Kama mradi utahusisha maeneo ambayo wananchi wanyamiliki kihalali, madiwani wanapoulizwa watashindwa kutoa majibu hivyo ipo hatari ya kutokea vurugu,” alisema Bw. Mwakasindile. |
Posted: 01 Feb 2013 01:56 AM PST
Goodluck Hongo na Rose Itono WAZIRI Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, amesema Serikali haitawachukulia hatua viongozi wa Serikali na Jeshi la Polisi wanaotuhumiwa kusababisha vurugu zilizotokea mkoani Mtwara, kusababisha vifo na uhalibifu mkubwa wa mali bali jambo la msingini kuhakikisha amani inatawala mkoani humo. Vurugu hizo zilichangiwa na maandamano ya wananchi waliokuwa wakipinga ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Bw. Pinda aliyasema hayo katika kipindi cha maswali na majibu bungeni mjini Dodoma jana baada ya kuulizwa swali na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Bw. Freeman Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro. Katika swali lake, Bw. Mbowe alitaka kujua hatua ambazo Serikali itazichukua kwa viongozi wa Serikali na Jeshi la Polisi ambao kauli zao zimechangia vurugu hizo kwa namna moja au nyingine. Alisema kilichotokea mkoani humo ni matokeo ya mahusiano hafifu kati ya wananchi na Serikali ambapo hata kauli za viongozi wa CCM nazo zilichangia vurugu hizo je, kwanini wasichukuliwe hatua. Msingi wa swali hilo ulitokana na malalamiko ya wananchi ambao waliitaka Serikali iwaondoe baadhi ya viongozi mkoani humo kwa kupingana na madai yao ya kutokana gesi hiyo isisafirishwe. Akijibu swali hilo, Bw. Pinda alisema Serikali haiwezi kuwachukulia hatua ili kuepusha lawama hasa ukizingatia kuwa, tayari kilio cha wananchi kimesikilizwa. “Nilikwenda Mtwara nikakutana na viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini, Serikali na wananchi ambapo walitoa maoni yao bila kificho na kuitak Serikali iwaondoe baadhi ya viongozi ambao walikuwa kikwazo kutokana na kauli zao,” alisema Bw. Pinda ambaye majibu yake yalionekana 'kuwakuna' wabunge wa CCM. “Niwaombe Watanzania wenzangu, viongozi na wanasiasa, jambo hili limekwisha hivi sasa tuongee lugha moja ya amani...kwani Tanzania ni moja,” alisema Bw. Pinda. Alisema kutokana na vurugu hizo, baadhi ya kampuni ambazo zimewekeza mkoani humo zimeingiwa na hofu na nyingine kuomba kukaa miezi mitatu bila kufanya shughuli zao hadi watakaporidhika na hali ya utulivu. Bw. Pinda alitomia fursa hiyo kutoa pole kwa watu waliofikwa na matatizo ambapo Serikali itaangalia uwezekano wa kuwasaidia. |
Posted: 01 Feb 2013 01:55 AM PST
Na Yusuph Mussa, Korogwe
MVUA kubwa iliyoambatana na upepo mkali imeleta maafa katika Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, baada ya kuua mwanafunzi mmoja wa sekondari, kujeruhi, kuezua paa za nyumba, mabweni na madarasa ya Shule ya Sekondari Mkalamo iliyopo Kata ya Magamba-Kwalukonge, Tarafa ya Mombo. Akizungumza na Majira kwa njia ya simu jana, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Constantine Masawe, alisema tukio hilo limetokea juzi saa 11.45 jioni ambapo wanafunzi waliojeruhiwa wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya, Magunga. Majeruhi hao ni Salma Bakari (15), ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Mkalamo aliyevunjika mguu wa kulia, Omar Haji (13) na Catherine Albert wa Shule ya Msingi Magamba- Kwalukonge na Asha Bakari wa Sekondari ya Mkalamo. Albert aliumia kichwani, Haji (mgongo na mbavu) wakati Bakari aliumia mguu wa kushoto baada ya kukimbilia katika nyumba ya Bw. Mustapha Abdallah ndipo walipopigwa na miti, mabati, kuangukiwa na ukuta. Alisema bweni moja la wasichana katika Shule ya Msingi Magamba- Kwalukonge, limeanguka kabisa na jingine likitoa nyufa ambapo madarasa mawili ya Sekondari ya Mkalamo yameezuliwa paa zake. “Inaaminika bado kuna nyumba nyingine zimeanguka au kuezuliwa paa zake na upepo lakini tutatoa taarifa kadiri muda unavyokwenda,” alisema Kamanda Masawe na kuongeza kuwa, inaaminika nyumba nyingine za wenyeji zimekwenda na upepo kwenye Kijiji cha Magamba Kwalukonge. Wakati huo huo, mvua hiyo imesababisha kifo cha mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Semkiwa, iliyopo Mtaa wa Mtonga, mjini Korogwe, mkoani Tanga, Patrick Paul (14). Mwanafunzi huyo amefariki dunia jana katika Hospitali ya Wilaya, Magunga wakati akiendelea kupatiwa matibabu baada ya upepo mkali ulioambana na mvua kumuangusha akiwa juu ya mti. Mvua hiyo pia imeezua paa katika nyumba tisa zilizopo mitaa ya Mtonga na Kwamkole. Taarifa iliyotolewa na Ofisa Mtendaji Kata ya Mtonga ambayo Majira inayo nakala yake, Bw. Maurice Kinyashi, ilisema tukio hilo limetokea juzi saa 12 jioni. Alisema pamoja na mvua hiyo kusababisha kifo cha mtu mmoja, mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Semkiwa, Rahim Ramadhani amejeruhiwa baada ya kuangukiwa na paa wakati mtoto wa miaka mitatu, Halifa Shabaan, alifunikwa na paa lakini hakuumia. “Ukuta wa Kanisa la TAG nao ulianguka, hivi sasa waathirika wote wapo katika wakati mgumu wakiishi katika nyumba ambazo hazina paa,” alisema Bw. Kinyashi. |
Posted: 01 Feb 2013 01:53 AM PST
Na Rehema Mohamed
WAKATI Katibu wa Taasisi za Jumuiya za Kiislamu nchini, Shekhe Ponda Issa Ponda na Shekhe Swaleh Mkadam, wakiendelea kusota rumande baada ya kunyimwa dhamana na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), wafuasi wao wamepanga kufanya kongamano maalumu la kujadili namna ya kuwatoa washtakiwa hao. Shekhe Ponda na wenzake wanakabiliwa na kesi ya uchochezi pamoja na wizi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam ambapo dhamana zao zimefungwa kwa sababu za kiusalama. Jana kesi hiyo ililetwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusikilizwa na baada ya kuahirishwa, wafuasi hao walionekana wakigawana vikatarasi vilivyokuwa na ujumbe wa kufanya kongamano hilo. Vikaratasi hivyo vilikuwa na ujumbe uliowataka Waislamu wote nchini kukutana Februari 3 mwaka huu, saa 8 mchana eneo la Temeke kwenye kiwanja cha Nurul Yaqiin (Uwanja wa Pumba) karibu na Uwanja wa Mwembeyanga. Ujumbe huo uliongeza kuwa, kitendo cha washtakiwa hao kuendelea kunyimea dhamana ambayo ni haki yao, kinawafanya waendelee kuteseka kwa sababu ya kutetea mali za Waislamu ambazo zinaendelea kuuzwa na kupolwa. Pia ujumbe huo uliwataka Waislam wajumuike pamoja, kuonesha mshikamano wao na kutoa maamuzi ya pamoja juu ya nini cha kufanya ili haki itendeke kwani Muislamu wa kweli hawezi kukubali dhuruma yoyote dhidi yake. Wakati huo huo, akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo, shahidi wa sita Bw. Hamis Mkangama (30), aliieleza mahakama hiyo kuwa Shekhe Ponda aliwakataza wasiendelee na ujenzi wa uzio katika kiwanja kinachodaiwa kuvamiwa. Bw. Mkangama ambaye ni fundi mwashi, alisema yeye na wenzie 20 walikuwa wakichimba msingi wa uzio kwenye kiwanja cha Markaz ambapo Shekhe Ponda na wenzake, walikwenda eneo hilo na kuwahoji aliyewapa idhini ya kujenga eneo hilo. “Tulimjibu kuwa bosi wetu Selemani ndiye aliyeturuhusu kujenga na kututaka tusitishe ujenzi akidai kiwanja husika kina mgogoro,” alidai shahidi huyo. Aliongeza kuwa, pamoja na kuambiwa wasimamishe ujenzi wao waliendelea ndipo Shekhe Ponda, aliamua kupiga picha eneo hilo. Alidai kuwa, walimweleza bosi wao juu ya suala la Shekhe Ponda ambaye aliwataka wasitishe ujenzi huo na kudai kuna matatizo yameanza kujitokeza. Wakati Shekhe Ponda akiondoka katika viwanja vya mahakama hiyo akiwa ndani ya gari la Magereza, wafuasi wake walimuaga kwa kunyoosha mikono wakisema 'Takbirr -alahu akbar', wengine wakilikimbiza gari hilo hadi barabarani. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 14 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na Februari 18 kwa ajili ya kusikilizwa. |
Posted: 01 Feb 2013 01:52 AM PST
Na John Mnyika SIJARIDHISHA na taarifa ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na uamuzi wa Spika Anna Makinda bungeni jana kuhusu mgogoro wa gesi Mtwara, hatua ambazo zinadhihirisha kwamba nchi imefika hali hiyo kutokana na udhaifu wa Serikali na ombwe la kiuongozi na kiusimamizi ikiwemo wa kibunge.
Taarifa
aliyoyatoa Waziri Mkuu jana imejibu baadhi tu ya madai ya wananchi,
lakini pia imefafanua sehemu ndogo ya masuala ambayo niliyahoji bungeni
Julai 27, 2012 lakini Serikali ikakwepa kutoa ufafanuzi.
Taarifa hiyo itawezesha kutuliza mgogoro kwa muda, lakini haijengi msingi wa ufumbuzi endelevu. Sikubaliani na uamuzi wa Spika wa kubadili uamuzi wake wa awali alioutangaza wa kuunda kamati kufuatia maelezo ya Waziri Mkuu yasiyokuwa na vielelezo vyovyote kwa kuwa kufanya hivyo ni kulinyima bunge fursa ya kuisimamia Serikali ambayo ndio chanzo cha migogoro kuhusu gesi asili. Spika alipaswa ikiwa amebadili uamuzi wa kuunda kamati ya kwenda Mtwara aunde Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ili ipitie vielelezo kubaini usahihi wa maelezo hayo ya Waziri Mkuu bungeni katika hali ya sasa ambayo nchi ina ombwe la kutokuwa na usimamizi wa kibunge kwenye sekta hizo nyeti kufuatia hatua yake ya kuvunja kamati iliyokuwepo bila kuunda kamati mbadala mpaka sasa. Ikiwa hana nia ya kuunda kamati ya nishati na madini mpaka mwisho wa mkutano huu wa Bunge, basi anapaswa kurejea barua zangu nilizomwandikia na kutumia madaraka na mamlaka yake kuelekeza kamati nyingine ya Bunge kati ya kamati zilizopo hivi sasa iweze kukutana kwa haraka kuchukua hatua zinazostahili na kuwasilisha taarifa bungeni. Kwa upande wangu, nafuatilia kumbukumbu rasmi za Bunge (Hansard) kupata nakala kamili ya ufafanuzi huo na nitaeleza hatua za ziada ambazo nitazichukua kama mbunge na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini. Kwa ujumla, maelezo hayo hayana tofauti kubwa na yaliyotolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, Januari 2013, hivyo sikubaliani na Waziri Mkuu kueleza kuwa suala hilo limekwisha kwa maelezo matupu yasiyokuwa na vielelezo. Maelezo hayo ya Waziri Mkuu yamedhihirisha kwamba iwapo Wizara ya Nishati na Madini ingetoa majibu bungeni kama nilivyohoji Julai 27, 2012, maandamano na migogoro iliyosababisha vifo na uharibifu wa mali Desemba 2012 na Januari 2013 yasingetokea hivyo ni muhimu waliosababisha hali hiyo wawajibishwe. Maelezo hayo hayajaeleza hali halisi kuhusu kasoro katika ujenzi wa miundombinu ya gesi katika mradi unaoendelea hivi sasa kuhusu mitambo ya kusafisha gesi Madimba, ujenzi wa bomba kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam na mpango wa uzalishaji wa umeme mkoani Mtwara, na hivyo hatua zisipochukuliwa hivi sasa kurekebisha hali hiyo mgogoro utazimwa kwa muda mfupi lakini utaibuka mgogoro mkubwa zaidi baadaye. Aidha, Waziri Mkuu hajatoa maelezo kamili kuhusu mipango ya matumizi ya gesi asili katika eneo la viwanda Bagamoyo na pia ujenzi wa Bandari ya Mbegani Bagamoyo, na mahusiano ya mipango hiyo na ile ya Mtwara na Dar es Salaam kuhusu matumizi ya gesi asili na bandari. Ni muhimu maelezo ya ukweli, uwazi na ukamilifu yakatolewa. Katika muktadha huo, Bunge kwa niaba ya wananchi linapaswa kutokuridhika tu na maelezo ya Waziri Mkuu kwamba suala hili limemalizika, bali lipewe nafasi ya kutimiza wajibu wake wa kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 63 wa kuisimamia Serikali. Spika wa Bunge atumie mamlaka yake kuelekeza Kamati mojawapo ya kudumu ya Bunge kushughulikia suala la gesi asili kama nilivyoomba katika barua zangu kwake za Oktoba 2012 na Januari 2013 ambazo mpaka sasa hazijapatiwa majibu. Kamati hiyo ipitie maelezo hayo ya Waziri Mkuu na kuitaka Serikali kuwasilisha vielelezo ikiwemo mikataba ili kurekebisha kasoro zilizopo katika mipango na mfumo wa utekelezaji wa miradi ya utafutaji, uvunaji, usafirishaji, uendelezaji na utumiaji wa gesi asili. Mwandishi ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) |
Posted: 01 Feb 2013 01:46 AM PST
JANA Mbunge wa kuteuliwa kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia, aliwasilisha hoja binafsi bungeni mjini Dodoma iliyoainisha suala zima la udhaifu uliopo katika sekta ya elimu nchini. Katika hoja hiyo, Bw. Mbatia alisema kukosekana kwa mitaala katika shule za msingi na sekondari, kunachangia wanafunzi kufanya vibaya. Alisema hali hiyo inachangiwa na utendaji mbovu wa kitengo cha kuandaa mitaala hiyo ambacho kimeshindwa kufanya kazi zake ipasavyo na kusababisha usambazaji vitabu kunuka rushwa. Hoja hiyo iliibua mvutano mkali kwa wabunge ambao baadhi yao walishauri iundwe Kamati Teule ya Bunge kuchukuza udhaifu huo na wengine wakitaka hoja hiyo ifanyiwe kazi na Serikali. Ulimwengu mzima unatambua kuwa, hakuna nchi iliyowahi kuendelea bila wananchi wake kuwa na elimu bora. Kwa maana hiyo, maendeleo yote yametokana na elimu sahihi iliyojaa maarifa, ubunifu, uwezo mkubwa wa kufikiri na kuvumbua dhana mpya. Elimu inayojenga ujuzi na ufundi wa aina mbalimbali, kudadisi, kujiamini na kutumia fursa zilizopo kutafuta masuluhisho ya matatizo ndiyo inayoleta maendeleo kwenye jamii. Ni ukweli usiopingika kuwa, wafadhili wametoa pesa nyingi kusaidia nchi masikini ikiwemo Tanzania lakini umaskini bado unaendelea kuitafuna nchi yetu. Suala la kuwekeza katika elimu sahihi kwa kuwa na mitaala bora haliepukiki. Hivi sasa, nchi mbalimbali zilizoendelea zinatafuta maarifa mapya ya kuibadili dunia wapendavyo kwa kurahisisha kila kitu wakitumia teknolojia na uvumbuzi mpya. Hii ndio nguvu ya elimu! Na hii inazaa changamoto nyingi katika sekta ya elimu, kama vile- Sisi tunasema kwamba, mitaala tunayoitumia katika shule zetu haiwezi kumjenga mwanafunzi kupata maarifa, ujuzi na stadi za aina mbalimabali zitakazowasaidia wanafunzi kuishi pindi wamalizapo shule. Mitaala tuliyonayo haiwafundishi wanafunzi wetu na kuwapa uwezo wa kutatua matatizo yao au kupambana na changamoto zinazoikabili kwenye jamii. Mitaala yetu imetungwa na wataalamu wachache bila kuzingatia mahitaji wa jamii. Hali hiyo inachangia wanafunzi wetu kukata tamaa na kuwa tegemezi wamalizapo shule na kibaya zaidi, ziara za mafunzo na kazi za nje zinazokazia maarifa hazifuatiliwi kabisa. Mbinu za ufundishaji, haziwaelekezi wanafunzi kuwa na ari ya kujifunza, bali zinakaririsha tu. Walimu wengi wanatumia mfumo wa kuandika ubaoni na wanafunzi wananakili maelezo. Mfumo huu unajulikana kama “ubao-chaki” ambao unawafanya wanafunzi kuwa vikapu vya kupokea maelezo ya mwalimu. Katika karne hii ya maarifa na changamoto nyingi, mfumo huu haufai. Mbinu shirikishi zinazowapa muda na fursa wanafunzi kujadili wenyewe na kutoa mawazo yao kwa uwazi ndio sahihi. Mbinu hizo zinaamsha ari ya wanafunzi kujifunza, kudadisi, ubunifu na fikra yakinifu za kukuza uhodari wa kutafuta maarifa hata kama hawapo shule. Umefika wakti wa Serikali kuweka mikakati ya kifikra ya kuzifanya shule kuwa mahali salama pa kujifunza na kuibua vipaji vya watoto ambapo pengo hili bado halijafanyiwa juhudi za dhati ili kuzibwa. Hivi sasa mtoto wa masikini anayelilia elimu imkomboe, anahitaji mfumo mzuri ambao utampa dira na dhamira ya kweli ili kuifanya elimu kuwa ni haki ya msingi kwa kila mtoto badala ya watoto wa viongozi pekee. |
Posted: 01 Feb 2013 01:45 AM PST
Na Heri Shaaban
WILAYA Ilala imetoa taarifa ya Serikali ya awamu ya nne ya vitu walivyotekeleza kwa kipindi cha miaka saba,ikiwemo miradi waliosimamia.Baadhi ya mafanikio hayo kuongeza vituo vya afya,ujenzi wa daraja la Vingugunti,kujenga shule za sekondari 91 kwa kipindi cha miaka saba kuanzia mwaka 2005 hadi 2013. Hayo yalisemwa na Dar es Salaam jana, Mkuu wa Wilaya hiyo Raimond Mushi wakati wa kutoa taarifa ya Serikali ya awamu ya nne kwa kipindi cha miaka hiyo.Mushi alisema kuwa kati ya shule hizo 91 za sekondari zilizojengwa ambazo zinamilikiwa na serikali 49 shule zisizo za seriklai 42 kufanya jumla 91."Shule za sekondari awali zilikuwa 11 zikaongezwa 80,shule kongwe Pugu, Azania,Tambaza juhudi zilifanyiwa ukarabati ya majengo ya mahabara na vyoo na kuzirudisha katika hadhi yake ya awali."alisema Mushi. Pia alisema kuwa katika kipindi hicho wamefanikiwa kujenga nyumba za walimu 18 kutoka 52 na kufikia 70 mwaka 2012,Na madawati 9,330 yameongezeka kutoka 14,812 mwaka 2015 na kufikia 24,142 mwaka 2012. Alisema kuwa katika kipindi hicho pia katika sekta ya afya wamefanikiwa kujenga vituo saba kutoka 15 vya awali na kufikia 22 mwaka 2012 kati ya vituo hivyo vilivyojengwa ni Guluka Kwalala,Bonyokwa,Segerea,Zingiziwa ,Kivule,Gongo lamboto,na Kiwalani. Aidha alisema kuwa idadi ya zahanati zimeongezeka kutoka 13 mwaka 2005 na kufikia 20 na na kituo cha afya Mnazi Mmoja kimekarabatiwa,na kupata hadhi ya hospitali ambapo inatoa huduma za mama na mtoto (MHC)na upasuaji pia. Kwa upande wa hospitali ya wilaya Amana imeongezewa wodi ya wazazi na kuwezesha kulaza wazazi kutoka 30 mwaka 2005 hadi 120 mwaka 2012,ujenzi wa jengo la mapokezi (OPD) ujenzi wa mahabara ya wilaya na jengo la mazoezi kwa wagojwa na mifupa. |
Posted: 01 Feb 2013 01:44 AM PST
Na Mwali Ibrahim
BONDIA Japhet Kaseba, ameapa kuwaonesha Watanzania kilichomfanya bondia, Francis Cheka kumkimbia ulingoni katika pambano lake na Ramadhani Maneno.Pambano hilo linatarajia kufanyika Machi 2, mwaka huu kuwania ubingwa wa Taifa katika Ukumbi wa DDC Kondoa huku likishuhudiwa na Mbunge wa Kinondoni Idd Azan. Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Japhet Kaseba alisema ameanza kujifua kwa ajili ya pambano hilo, ambapo anataka kuwaonesha Watanzania uwezo wake unaowatisha mabondia wengine na kumfanya wamkimbie, akimtolea mfano Cheka. "Najua watu wanatamani kuona mpambano huu, ambapo kwa muda mrefu sijapanda ulingoni kutokana na kukosa mabondia wakupigana nao, kwani wamekuwa wakikwepa kupigana na mimi sasa basi pambano hili litadhihirisha hayo," alisema.Aliongeza kuwa anajifua katika gym yake iliyopo Mwananyamala, ambapo ana imani kwa kuanaza maandalizi mapema kutamsaidia kujiweka vizuri zaidi kwa mpambano huo. Alisema zaidi anamtaka mpinzani wake ajiandae, ili ushindi huo kwani ana imani atauchukua. |
Posted: 01 Feb 2013 01:43 AM PST
Bondia Selemani Kidunda wa Klabu ya Ngome, ambaye aliowakilisha Tanzania katika mashindano ya Olimpic yaliyofanyika London nchini Uingereza mwaka jana akipima uzito, Dar es salaam kwa ajili ya mashindano ya Klabu bingwa yaliyoanza juzi katika Uwanja wa ndani wa Taifa, Dar es Salaam. Picha na Rajabu Mhamila Bondia Selemani Kidunda wa Klabu ya Ngome, ambaye aliowakilisha Tanzania katika mashindano ya Olimpic yaliyofanyika London nchini Uingereza mwaka jana akipima uzito, Dar es salaam kwa ajili ya mashindano ya Klabu bingwa yaliyoanza juzi katika Uwanja wa ndani wa Taifa, Dar es Salaam. Picha na Rajabu Mhamila |
Posted: 01 Feb 2013 01:38 AM PST
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu ya Zanzibar maarufu zaidi kwa jina la Grand Malt Premier League, unatarajiwa kuanza leo kwa michezo miwili kati ya Mafunzo na KMKM zitakazokwaana Uwanja wa Amaan, huku Chipukizi na Falcon wakioneshana kazi Uwanja wa Gombani, Pemba KMKM wanaingia uwanjani wakitaka kuendeleza ubabe wao, kwani mpaka sasa ndiyo wanaoongoza ligi hiyo wakiwa wamejikusanyia pointi 23, wakati Mafunzo ikiwa nafasi ya pili ikiwa na pointi 22. Ugumu wa mchezo huo ni kuwa kila timu itataka kujiimarisha zaidi kwani kuteleza ni kujiweka katika mazingira magumu ya kutwaa taji na iwapo KMKM, itakubali kichapo, itaichia Mafunzo kushika usukani wa ligi hiyo yenye timu 12. Chipukizi wao watataka kuutumia vyema uwanja wa nyumbani, kwani ikiwa nafasi ya tano kwa pointi 17 ilizonazo itataka kuhakikisha inashinda, ili kuzidi kupaa katika msimamo wa ligi hiyo ambayo kwa sasa imeongezeka mvuto kutokana na udhamini wa Grand Malt. Hata hivyo wasitegemee mteremko kutokana na Falcon, nayo kutaka kujinasua kutoka nafasi za chini. Kwa sasa timu hiyo inashikilia nafasi ya tisa ikiwa na pointi 13. Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena kesho, kwa michezo miwili wakati Bandari na Malindi zitakapokwaana Uwanja wa Mao, huku Jamhuri na Duma zikioneshana ubabe Uwanja wa Gombani, Pemba na Jumapili kutakuwa na mchezo mmoja kati ya Zimamoto na Mtende zitakazocheza Uwanja wa Mao. Timu inayoshika mkia mpaka sasa ni Mundu ikifuatiwa na Malindi. Timu zote hizi zina pointi saba kila moja. |
Posted: 01 Feb 2013 01:37 AM PST
Na Shufaa Lyimo KLABU ya Azam FC, umesema utaendeleza kipigo katika mchezo wa Ligi Kuu, dhidi ya Mtibwa Sugar. Azam juzi iliinyuka Toto Africa ya Mwanza mabao 3-1 katika mechi ya Ligi Kuu mzunguko wa pili, iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Ofisa Habari wa klabu hiyo, Jafari Iddi alisema kinachoifanya timu yake ifanye vizuri ni mshikamano uliopo, kati ya wachezaji na viongozi. "Timu yetu itaendelea kufanya vizuri michezo yote na tunaahidi kuipa kipigo Mtibwa tutakapokutana," alisema. Hata hivyo alisema ligi ya mwaka huu, ina ushindani mkubwa kwa kuwa kila timu imejipanga kupata ubingwa. "Ligi hii kwa kweli ni ngumu kwani timu zote zimejiandaa kwa muda mrefu na kila moja, inataka ushindi," alisema. Aliwataka mashabiki wao kuendelea kuwapa sapoti kila wanapocheza, ili waweze kufanya vyema na kupata matokeo mazuri. Katika msimamo wa ligi, timu hiyo inakamata nafasi ya pili nyuma ya Yanga, inayoongoza. |
Posted: 01 Feb 2013 01:37 AM PST
Na Queen Lema, Meru WILAYA ya Meru, imetoa sh. milioni 8 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu sita za wilaya hiyo, lengo likiwa kuendeleza vipaji vya michezo ndani ya wilaya hiyo. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi wilayani hapa jana Mkuu wa wilaya hiyo, Munasa Nyirembe alisema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona kuwa kuna umuhimu wa wilaya yake kuhakikisha inaendeleza vipaji. Munasa alisema fedha hizo zilitolewa na wilaya hiyo kwa kuwa imegundulika wachezaji wengi, hasa wa soka ambao wana vipaji lakini tatizo linaonekana ukosekanaji wa vifaa vya michezo. Alisema fedha hizo zitaweza kunufaisha timu sita za wilaya hiyo, ambapo timu zao zitaweza kushiriki mashindano ya Kombe la CCM Wilaya ya Meru, ambayo yameanza na yanatarajiwa kumalizika Februari 5, mwaka huu. “Tunaona Meru ni moja ya wilaya ambazo zina vipaji vingi, lakini kitu kimoja ni kuwa bado wachezaji wetu wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa, tumeona kuna umuhimu mkubwa wa kuhakikisha tunawapa watu hawa fursa ya kuendelea kufanya vizuri zaidi," alisema Munasa. Pia alisema mbali na kuwapa vifaa vya hivyo timu sita za wilaya hiyo, lakini pia wilaya hiyo imejipanga kuhakikisha wanapanga, ili kuandaa mechi za kirafiki ambazo zitasaidia kuibua vipaji zaidi. Naye Ofisa Utamaduni wilaya hiyo, Senyaeli Palangyo alisema wamejipanga kuendelea zaidi katika michezo mbalimbali kwa kuwa vipaji vingi, vinaweza kuendelezwa ingawa awali hapakuwa na hamasa za kutosha. |
Posted: 01 Feb 2013 01:36 AM PST
|
Posted: 01 Feb 2013 01:29 AM PST
Na Elizabeth Mayemba
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars) inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini kesho kutwa kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimatifa, dhidi ya Cameroon 'Indomitable Lions'. Akizungumza Dar es Salaam jana, Kim alisema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu ni sehemu ya maandalizi, kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco, itakayofanyika Machi mwaka huu. "Itakuwa mechi ngumu na kipimo kizuri kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi, kabla ya mechi na Morocco. Ni mechi nzuri kwa sababu wachezaji wameonesha wako tayari. "Tumetoka kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza fainali za AFCON 2015 kwa hiyo, mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya mipango yetu kuhakikisha tunafika huko," alisema Kim. Kocha huyo amerejea nchini juzi akitokea Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory Coast, zilizo kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia. Taifa Stars itacheza na Morocco Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi ya pili katika kundi lake nyuma ya Ivory Coast, inayoongoza. Timu nyingine katika kundi hilo ni Gambia. Wachezaji aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam), mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Said 'Cholo' (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar). Wengine ni viungo ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakari (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC). |
Posted: 01 Feb 2013 01:28 AM PST
Na Mwandishi Wetu KAMATI ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ambayo ilikutana Januari 30 mwaka huu imetupa pingamizi zote, zilizowekwa kwa wagombea wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi katika chama hicho. Kamati hiyo ilijadili pingamizi zilizowekwa, dhidi ya waombaji uongozi wa TFF na Bodi ya Ligi Kuu Bara (TPL Board). Wagombea waliowekewa pingamizi hizo ni Jamal Malinzi na Athuman Nyamlani wanaowania nafasi ya Rais, Michael Wambura (Makamu wa Rais), Yusuf Manji (Mwenyekiti TPL) na Said Mohamed (Makamu Mwenyekiti TPL). Wengine waliowekewa pingamizi hizo, ambao wanawania nafasi za Ujumbe wa TFF ni Hamad Juma, Ephra Swai, Vedasus Lufano, Eliud Mvela na Athuman Kambi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura kwa niaba ya Katibu Mkuu wa chama hicho Angetile Osiah, ilieleza kwamba pingamizi za Malinzi na Nyamlani zimetupwa kwa kuwa walioweka pingamizi hizo, hawakutokea kutoa utetezi wao. "Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za TFF, Ibara ya 11(4) katika kikao chake kilichofanyika tarehe 30 Januari 2013, ilijadili pingamizi zilizowekwa dhidi ya waombaji uongozi wa TFF na TPL Board na kutoa maamuzi," ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo. Taarifa hiyo ilieleza kwamba Malinzi aliwekewa pingamizi na Agape Fue, huku Nyamlani akipingwa na Mintanga Chacha. Ilieleza kwamba pingamizi la Wambura, limetupwa kwa kuwa mpingaji mmoja Josea Msengi, hakutokea kutetea pingamizi lake wakati pingamizi alilowekewa na Said Rubeya, halikukidhi matakwa ya kanuni za uchaguzi. Taarifa hiyo ilieleza kuwa pingamizi aliyowekewa, Manji na Daniel Kamna na Juma Magoma yametupwa kwa kuwa nayo hayakukidhi matakwa ya uchaguzi. |
Subscribe to:
Posts (Atom)