Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la
Katiba, Mhe. Samia Suluhu akiwaeleza jambo Wawakilishi wa Umoja wa Machifu
Tanzania (UMT) kuhusu mapendekezo yao waliyoyawasilisha kwake kwaajili ya
Katiba Mpya.
Chifu John Nyanza (aliyekaa katikati)
wa kutoka Magu akimueleza jambo Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,
Mhe. Samia Suluhu (kulia) juu ya uwasilishaji wa mapendekezo yao kwa ajili ya
Katiba Mpya alipokutana naye leo kwenye Ofisi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge
Maalum.
Chifu Agnes Ndaturu (kushoto) wa
kutoka Ntuzu, Bariadi akimueleza jambo Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la
Katiba, Mhe. Samia Suluhu (kulia) juu ya uwasilishaji wa mapendekezo yao kwa
ajili ya Katiba Mpya alipokutana naye leo kwenye Ofisi ya Makamu Mwenyekiti wa
Bunge Maalum.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la
Katiba, Mhe. Samia Suluhu (kulia) akipokea mapendekezo ya maoni toka kwa Chifu
John Nyanza alieuwakilisha Umoja wa Machifu wa Tanzania (UMT) leo kwenye Ofisi
ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari walikifuatilia uwasilishwaji wa mapendekezo toka kwa
Machifu waliouwakilisha Umoja wa Machifu wa Tanzania (UMT) leo kwenye Ofisi ya
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
Na Benedict Liwenga,
Maelezo-Dodoma.
26/08/2014.
UMOJA wa Machifu wa Tanzania (UMT) kupitia wawakilishi wake,
leo umewasilisha nyongeza ya mapendekezo yake kuhusu Katiba Mpya kwa Makamu
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Akiuwakilisha Umoja wa Machifu Tanzani (UMT), Chifu kutoka
Magu John Nyanza amemueleza Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba kuwa
wanaishauri Serikali kutayarisha mkakati wa Kitaifa wa Utamaduni kwa
kuwashirikisha wadau wakuu wa masuala ya Utamaduni ili mpango mkakati huo uwe
na Dira ya Utamaduni itakayobainisha cha kufanya ili kujenga, kuhamasisha na
kuendeleza Utamduni katika maeneo yote nchini.
“Chifu kutoka Magu, John Nyanza amesema kuwa lengo la
kuwasilisha mapendekezo hayo kwaajili ya kusisitiza masuala mazuri ya Utamduni
kuendelea ili kuweza kudumisha madili kwa nia nzuri ya kudumisha amni na
ushirikiano”. Alisema Chifu Nyanza.
Naye Chifu kutoka Ntuzu, Bariadi Chifu Agnes Ndaturu ameeleza
kuwa mapendekezo yao yatasaidia kuweza kuwatambua waganga wa Jadi ambapo hapo
zamani , mganga wa Jadi alikuwa anatambulika na kufanya kazi katika eneo husika
analotoka, lakini hivi sasa waganga wengi wa jadi wamekuwa na tabia ya kufanya
kazi zao bila mipaka.
”Mapendekezo haya
yatasaidia viongozi wa waganga wa jadi nchini kuwatambua wale waganga
wanaokiuka maadili ya shughuli zao mfano mauaji ya Albino, kwakuwa kila
kiongozi atakuwa anawatambua waganga wa eneo lake husika”. Alisema Chifu
Ndaturu.
Aidha, Machifu hao wameongeza kuwa, Wajumbe wenzao
waliowatuma kuwawakilisha wanasisitiza juu ya umuhimu wa Utamaduni kupewa
nafasi rasmi katika Katiba mpya na Serikali ili pawepo na kipaumbele katika
utekelezaji wake nchini.
Wakizungumza kwa kauli moja Umoja wa Machifu wa Tanzania
wamesema kuwa suala la Utamaduni katika Rasimu ya Pili ya Katiba lifanyiwe
marekebisho kwa kuzingatia mapendekezo yaliyoibainishwa huku msisitizo wao
ukiwa katika Katiba kueleza wazi kuwa sera na Sheria mpya zitakazotungwa zihakikishe kuwa Tume ya Taifa ya Utamaduni
inaanzishwa kisheria ili kusimamia masuala ya Utamaduni.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia
Suluhu Hassan amewatotoa wasiwasi wawakilishi wa Umoja wa Machifu hao wa
Tanzania aliokutana nao kwa kuwaeleza kuwa atayawasilisha katika Uongozi wa
Kamati ya Bunge ambapo Kamati Ndogo ya Uongozi inatarajiwa kukutana leo jioni
ili kuweza kuyajadili.
“Nimeyapokea mapendekezo yenu, kwakuwa Kamati zinaendelea na
kazi ambapo wiki hii kamati zitakuwa zimemaliza kazi zake na hakutakuwa na
nafasi tena ya kuyapokea mapendekezo na maoni mengine”. Alisema Samia.
Hivi karibuni, makundi mbalimbali yaliwasilisha mapendekezo
yao ambapo baadhi ya makundi hayo yakiwemo Wafugaji, Wasanii na Wanahabari
yaliwasilisha.