Mabadiliko
madogo katika Baraza la Mawaziri na Uteuzi wa Naibu Waziri.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein
amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri na pia kumteuwa Naibu
Waziri kama ifuatavyo-
(a) Mhe. Dkt.
Sira Ubwa Mamboya ameteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili akijaza nafasi
ilioachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Suleiman Othman Nyanga.
(b) Mhe. Juma
Duni Haji ameteuliwa kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano akichukuwa
nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Rashid Seif
Suleiman ambaye sasa anakuwa Waziri wa Afya.
(c) Mhe. Rashid Seif Suleiman ameteuliwa kuwa
Waziri wa Afya akijaza nafasi ya Mhe. Juma Duni Haji ambaye sasa anakuwa Waziri
wa Miundombinu na Mawasiliano.
(d) Mhe. Mahamoud
Thabit Kombo ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Afya akijaza nafasi ilioachwa wazi
na Mhe. Dkt. Sira Ubwa Mamboya ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo na
Maliasili.
Na pia
amefanya mabadiliko ya baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya.
Aidha, Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein
amefanya mabadiliko ya baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya kama ifuatavyo:-
(1). Major Mstaafu
Juma Kassim Tindwa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja akijaza nafasi
ilioachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Bwana Pembe Juma Khamis.
(2). Bibi
Mwajuma Majid Abdulla ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kusini, Pemba akijaza nafasi
ilioachwa wazi na Major Mstaafu Juma Kassim Tindwa ambaye amehamishiwa Mkoa
Kaskazini, Unguja.
(3). Bwana
Omar Khamis Othman ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, Pemba akijaza
nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Bwa. Dadi Faki Dadi.
(4). Bwana
Ayoub Mohamed Mahmoud ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi akijaza
nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bwa. Hassan Mussa
Takrima.
(5). Bibi
Hanuna Masoud Ibrahim ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake akijaza
nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bibi Mwanajuma Majid Abdulla ambaye
ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kusini, Pemba. Utezi huo umeanza leo tarehe 24
Agosti 2014.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment