- Sitta: Lazima tuisafishe CCM yetu
- Mkapa kuzindua kampeni Arumeru kwa kishindo
- Udhalilishaji walimu Karatu haukubaliki!
- Mifuko ya NHIF, CHF yakwamishwa
- Serikali yatangaza kuwapa wakulima miche ya karafuu
- CHADEMA wajitokeza kuwania Ubunge EAC
- Wachezaji Yanga tuhuma nzinto
TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Tuesday, March 13, 2012
Lipumba arejea kuinusuru CUF
Sunday, March 11, 2012
RC awashukia watendaji wenye majungu ofisini
Na Charles Mwakipesile, Mbarali
MKUU wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro, amewataka watumishi wenye tabia ya kuwasema wenzao ofisini 'majungu', kuacha mara moja ambapo watakaobainika kuwa na tabia hiyo, watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Bw. Kandoro aliyasema hayo juzi katika hafla ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Mbaarali, mkoani hapa Bw. George Kagomba.
Hafla hiyo ilifanuyika katika Makao Makuu ya halmashauri hiyo baada ya kustaafu utumishi wa umma na kuongeza kuwa, siri ya mafanikio kwa mtendaji yeyote wa Serikali ni kuchapa kazi kwa bidii, kuepuka majungu.
Alisema kitendo cha kuwagawa wafanyakazi kinakwamisha maendeleo ya wannchi na utekelezaji wa shughuli za Serikali.
“Kiongozi ambaye leo tunamuaga, amefanya kazi kwa bidii na kufanikiwa kuleta mabadiliko makubwa, kufyeka kichaka porini na kujenga Makao Makuu ya Halmashauri.
“Bw. Kagomba ni kielelezo cha watendaji bora wa serikali wasio na majungu ambaye amewaunganisha wafanyakazi kuwa kitu kimoja na kuharakisha maendeleo,” alisema.
Alisema watendaji wa Serikali ambao wanaendeleza majungu badala ya kufanya kazi, huambulia kufukuzwa na kutokumbukwa kwa lolote walilofanya wakati wa utumishi wao serikalini.
“Sipendi kusikia Mkoa wetu unakosa maendeleo kwa sababu watumishi hutumia muda mwingi kuzungumza habari za majungu badala ya kufanya kazi kwa bidii,” alisema.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Bw. Keneth Ndingo, alisema Bw. Kagomba atakumbukwa kwa mambo mengi pamoja na kujenga Makuu Makuu ya halmashauri hiyo ambayo ina majengo ya kisasa yaliyozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete.
Mbali ya kufanikisha ujenzi wa majengo hayo pia ameweza kukuza pato la halmashauri na ujenzi wa majengo ya sekondari za kata hivyo aliiomba Serikali iangalie uwezekano wa kumuongezea muda wa utumishi kwa mkataba maalumu.
Kwa upande wake, Bw. Kagomba alisema bila kupata ushirikiano kutoka kwa watumishi wengine, asingeweza kufanikisha majukumu aliyopewa ambayo yamezaa matunda.
MKUU wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro, amewataka watumishi wenye tabia ya kuwasema wenzao ofisini 'majungu', kuacha mara moja ambapo watakaobainika kuwa na tabia hiyo, watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Bw. Kandoro aliyasema hayo juzi katika hafla ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Mbaarali, mkoani hapa Bw. George Kagomba.
Hafla hiyo ilifanuyika katika Makao Makuu ya halmashauri hiyo baada ya kustaafu utumishi wa umma na kuongeza kuwa, siri ya mafanikio kwa mtendaji yeyote wa Serikali ni kuchapa kazi kwa bidii, kuepuka majungu.
Alisema kitendo cha kuwagawa wafanyakazi kinakwamisha maendeleo ya wannchi na utekelezaji wa shughuli za Serikali.
“Kiongozi ambaye leo tunamuaga, amefanya kazi kwa bidii na kufanikiwa kuleta mabadiliko makubwa, kufyeka kichaka porini na kujenga Makao Makuu ya Halmashauri.
“Bw. Kagomba ni kielelezo cha watendaji bora wa serikali wasio na majungu ambaye amewaunganisha wafanyakazi kuwa kitu kimoja na kuharakisha maendeleo,” alisema.
Alisema watendaji wa Serikali ambao wanaendeleza majungu badala ya kufanya kazi, huambulia kufukuzwa na kutokumbukwa kwa lolote walilofanya wakati wa utumishi wao serikalini.
“Sipendi kusikia Mkoa wetu unakosa maendeleo kwa sababu watumishi hutumia muda mwingi kuzungumza habari za majungu badala ya kufanya kazi kwa bidii,” alisema.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Bw. Keneth Ndingo, alisema Bw. Kagomba atakumbukwa kwa mambo mengi pamoja na kujenga Makuu Makuu ya halmashauri hiyo ambayo ina majengo ya kisasa yaliyozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete.
Mbali ya kufanikisha ujenzi wa majengo hayo pia ameweza kukuza pato la halmashauri na ujenzi wa majengo ya sekondari za kata hivyo aliiomba Serikali iangalie uwezekano wa kumuongezea muda wa utumishi kwa mkataba maalumu.
Kwa upande wake, Bw. Kagomba alisema bila kupata ushirikiano kutoka kwa watumishi wengine, asingeweza kufanikisha majukumu aliyopewa ambayo yamezaa matunda.
Posted: 08 Mar 2012 10:45 PM PST
Na Zahoro Mlanzi
SERIKALI
imesema mpaka kufikia mwishoni mwa Aprili mwaka huu Uwanja wa Uhuru,
Dar es Salaam utakuwa tayari umekamilika kwa asilimia 75 na utaanza
kutumika kwa shughuli mbalimbali rasmi Juni, mwaka huu.
Uwanja huo awali ulitakiwa kukamilika kabla ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru lakini mpaka kufikia Desemba 9, mwaka jana ulikuwa haujakamilika, hivyo sherehe hizo kulazimika kufanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Serikali ulisimamisha shughuli za uwanja huo, tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2010/2011.
Akijibu swali kuhusu uwanja huo utakamilika lini, baada ya kushindwa kukamilika kabla ya kuanza kwa sherehe za Uhuru wa miaka 50 Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini, Leonard Thadeo alisema ni kweli ulitakiwa kukamilika kabla ya sherehe za Uhuru, lakini kikubwa kilichokwamisha ni mkandarasi alichelewesha baadhi ya mambo muhimu.
“Hivi sasa ujenzi unaendelea kama kawaida na ninakuhakikishia mpaka kufikia mwishoni mwa Aprili, mwaka huu utakuwa umekamilika kwa asilimia 75, kwani kazi kubwa iliyobaki ni kuweka viti katika jukwaa mbalimbali zilizojengwa,” alisema Thadeo.
Alisema wakati maboresho hayo yakiendelea kwa kuhakikisha viti vinawekwa na mambo mengine, mpaka kufikia Juni mwaka huu ana imani kila kitu kitakuwa kimekamilika na shughuli mbalimbali zilizokuwa zikifanyika katika uwanja zitaendelea kama kawaida.
Thadeo alisema kukamilika kwa uwanja huo kutapunguza matumizi ya Uwanja wa Taifa, kwani mechi zitakazokuwa si za lazima kuchezewa kwenye uwanja huo, zitafanyika Uwanja wa Uhuru kama ilivyokuwa hapo awali.
Pia alitoa wito kwa mashabiki na wanamichezo kwa ujumla kuhakikisha kuutumia vizuri uwanja huo, pindi utakapokamilika ili kuepusha madhara yatakayoweza kujitokeza kama ilivyokuwa katika mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba na Kiyovu ya Rwanda.
Katika mechi hiyo ya Simba, viti 152 viliharibiwa na 11 vilivunjwa kutokana na mashabiki hao kuvunja na kurushiana wakati mechi hiyo ikiwa mapumziko.
Uwanja huo awali ulitakiwa kukamilika kabla ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru lakini mpaka kufikia Desemba 9, mwaka jana ulikuwa haujakamilika, hivyo sherehe hizo kulazimika kufanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Serikali ulisimamisha shughuli za uwanja huo, tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2010/2011.
Akijibu swali kuhusu uwanja huo utakamilika lini, baada ya kushindwa kukamilika kabla ya kuanza kwa sherehe za Uhuru wa miaka 50 Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini, Leonard Thadeo alisema ni kweli ulitakiwa kukamilika kabla ya sherehe za Uhuru, lakini kikubwa kilichokwamisha ni mkandarasi alichelewesha baadhi ya mambo muhimu.
“Hivi sasa ujenzi unaendelea kama kawaida na ninakuhakikishia mpaka kufikia mwishoni mwa Aprili, mwaka huu utakuwa umekamilika kwa asilimia 75, kwani kazi kubwa iliyobaki ni kuweka viti katika jukwaa mbalimbali zilizojengwa,” alisema Thadeo.
Alisema wakati maboresho hayo yakiendelea kwa kuhakikisha viti vinawekwa na mambo mengine, mpaka kufikia Juni mwaka huu ana imani kila kitu kitakuwa kimekamilika na shughuli mbalimbali zilizokuwa zikifanyika katika uwanja zitaendelea kama kawaida.
Thadeo alisema kukamilika kwa uwanja huo kutapunguza matumizi ya Uwanja wa Taifa, kwani mechi zitakazokuwa si za lazima kuchezewa kwenye uwanja huo, zitafanyika Uwanja wa Uhuru kama ilivyokuwa hapo awali.
Pia alitoa wito kwa mashabiki na wanamichezo kwa ujumla kuhakikisha kuutumia vizuri uwanja huo, pindi utakapokamilika ili kuepusha madhara yatakayoweza kujitokeza kama ilivyokuwa katika mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba na Kiyovu ya Rwanda.
Katika mechi hiyo ya Simba, viti 152 viliharibiwa na 11 vilivunjwa kutokana na mashabiki hao kuvunja na kurushiana wakati mechi hiyo ikiwa mapumziko.
MNYAMA SIMBA ASHINDWA KUUNGURUMA MWANZA,
Mchezaji
wa timu ya Simba Felix Sunzu akimtoka beki wa timu ya Toto Africa ya
Mwanza katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom unaofanyika kwenye uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam jioni hii, Mpira umekwisha na hakuna timu
iliyofanikiwa kupata goli katika dakika tisini matokeo yamekuwa 1-1.
Kocha Milovan ameipongeza timu ya Toto Africa kwa kucheza vizuri, wao
walitaka kushinda lakini hawakuweza kufanya vizuri.
Na Mwandishi Wetu
MALKIA wa muziki wa Injili nchini,
Rose Muhando, naye atakuwa miongoni mwa waimbaji watakaopamba tamasha
la nyimbo za Injili litakalofanyika Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Alex Msama, ambaye ni
Mwenyekiti wa Kamati inayoratibu tamasha hilo chini ya Kampuni ya Msama
Promotions ya Dar es Salaam, Muhando amethibitisha kushiriki tamasha
hilo.
"Katika tamasha la Pasaka mwaka huu
ndipo Rose Muhando atapata fursa ya kutambulisha albamu yake ya nne ya
Utamu wa Yesu ambayo haijawahi kuzinduliwa tangu aikamilishe," alisema
Msama.
Albamu ya Utamu wa Yesu inabeba nyimbo
saba ambazo ni Utamu wa Yesu uliobeba jina la albamu hiyo, Raha Tupu,
Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia.
Mbali na Utamu wa Yesu, Rose Muhando
pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya
Krismasi) na Jipange Sawa Sawa.
Msama alisema pia Muhando ataimba
pamoja na Anastazia Mukabwa wa Kenya aliyeshirikiana naye katika albamu
ya Vua Kiatu, na baada ya kutikisa Uwanja wa Taifa, mashambulizi
mengine yatahamia kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Aprili 9 mwaka huu.
"Mpaka sasa tunaendelea na mazungumzo
na waimbaji wengine mahiri wa muziki wa Injili, lakini Muhando
atakuwepo na Mukabwa atakuja na kundi la waimbaji wake," alisema Msama.
Albamu ya Vua Kiatu inabeba nyimbo
nane ambazo ni Vua Kiatu uliobeba jina la albamu hiyo, Ee Mungu, Usiwe
Manamba, Nzizilela, Nishike Mkono Bwana, Wanaokudharau na Mfalme.
Mbali na Mukabwa, wengine
waliothibitisha kushiriki tamasha hilo litakalofanyika Sikukuu ya
Pasaka ni Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Christina Shusho wa Dar es
Salaam, kundi la Glorious Celebration na Atosha Kissava kutoka Iringa.
Kwa mujibu wa Msama, tamasha hilo
baada ya kufanyika Dar es Salaam, pia litarindima kwenye Uwanja wa
Jamhuri mjini Dodoma Aprili 9 mwaka huu.
Tamasha la mwaka huu malengo yake
makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na
kuwasaidia mitaji wanawake wajane.
Kiingilio katika tamasha hilo
kimetengwa katika kategoria tatu na kitakuwa sh. 2,000 kwa watoto, sh.
5,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu sh. 10,000.
Tamasha la Pasaka la mwaka huu pia
litashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchi sita za Afrika
ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,
Afrika Kusini na Zambia. Pia kutakuwa na kwaya.
The Girl Empowerment Program” under the theme ” Build Your Future”,
aimed at empowering Secondary school girls
Saturday 10th March 2012, As part of our Corporate Social
Responsibility initiative, Airtel Tanzania has today launch ”The Girl
Empowerment Program” under the theme ” Build Your Future”, aimed at
empowering Secondary school girls aged 14 to 18 years, in achieving
their future career goals and build self confidence amongst young
women.
The Girl Empowerment Program is key to Airtel as it goes hand in hand
with Airtel’s mission of educating the girl child and creating brand
loyalty. Apart from the fact that they need clear rules, consistent
consequences for breaking rules and encouragement to do their best,
young girls need opportunities outside of school curriculum to learn
and develop new skills and interests with other youth and adults.
Speaking during the launch held at Canossa Girls Secondary School in
Tegeta, Dar es Salam Airtel customer Care Director Adrianna Lyamba
said ”Today we kick start the program this quarter with “Canossa
Girls Secondary School in Tegeta, The Girl Empowerment Program will be
an ongoing program which will be done quarterly to Girls Secondary
Schools around Tanzania and in this program we will be covering
different topics relating to career management, building self
confidence and making the right decisions in life.
We will be
requesting our own employees to volunteer to speak in schools and
share their career experiences and skills with the students. This will
enable the students understand what it takes to build a career and
select the right career path in life”.
“There is the say that saying, when you educate a women you have
educated the whole community, we therefore believe the knowledge
acquired will be a great significance to girl’s destiny and for the
upcoming generation. She added
We are highly committed towards supporting Tanzanian community, apart
from Girl empowerment program we have been supporting education sector
through Shule yetu program were we provide books to Secondary schools
in the country, our aim is to improve education level through
availability books to secondary schools students. Since we started our
books support programme, approximately seven years ago, we have
reached more than 800 secondary schools that are spread across the
country”
Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Azam lililochezwa Machi 10
mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 72,731,000.
Jumla
ya watazamaji 19,339 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa
kiingilio cha sh. 3,000 viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 viti vya
rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B wakati kwa VIP A ilikuwa sh.
15,000.
Baada
ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 11,303,932.20 kila timu ilipata
sh. 14,726,592.20, uwanja sh. 4,908,864.07.
Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,963,545.63, TFF
sh. 4,908,864.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,454,432.03, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 490,886.41 na
asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 4,908,864.07.
Gharama
za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000,
nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. waamuzi wa akiba sh.
30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna sh. 40,000, tiketi sh.
3,540,000, maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000,
usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing
Construction) sh. 2,000,000.
Gharama
nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu
ilipata tena sh. 1,353,730 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar
es Salaam (DRFA) kilipata tena sh. 1,160,340.
Saturday, March 10, 2012
Mwamuzi
Israel Mujuni pamoja na wasaidizi wake akitoka nje kwa kusindikizwa na
askali wa kikosi cha kutuliza Ghasia FFU mara baada ya kupuliza kipenga
cha mwisho kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliokutanisha timu ya
Yanga ya Jangwani na timu ya Azam FC kutoka Chamazi ambapo Yanga
imekandamizwa magoli 3-1 na wauza Sembe hao wa Chamazi kwenye uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam.
Mwanzo ulikuwa ni
mchezo mzuri uliokuwa wa vuta nikuvute kwa kila upande lakini mambo
yalibadilika mara baada ya Azam kuandika goli la kwanza, mchezaji Haruna
Niyonzima wa Yanga alionekana kumlalamikia refa mara kwa mara jambo
ambalo refa alimuonya mara kadhaa lakini, hata hivyo Niyonzima
aliendelea baada ya muda, alitolewa nje kwa kadi nyekundu, jambo
ambalo lilizua tafrani uwanjani huku makonde yakirushwa hovyo, baadae
naye mchezaji Nadir Haroub Canavaro alipewa kadi nyekundu kutokana na
vurugu hizo na kuzua tifu lingine uwanjani.
Hali ilikuwa kama hivi angalia matukioo ya picha hizi.
Mratibu
wa Kitaifa Mradi wa athari za Mabadiliko ya tabia Nchi Bw Faraja
Ngeregeza akitoa Mada kwa Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais juu ya
athari za mabadiliko ya tabianchi leo Ukumbi katika wa Karimjee jijini
Dar es Salaam[Picha na Ali meja]
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rasi wakimsikiliza Mkurugenzi
Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Bw Richard Muyungi[Pichani
hayupo]akitoa Mafunzo ya Utaratibu wa Utekelezaji wa Miradi ya
Kupunguza Gesi joto huko kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
Salaam.[Picha na Ali Meja]
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula akizungumza na Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Tathimini na Ufuatiliaji Bi Grace
Ngallu wakati wa Mafunzo ya Utaratibu wa Utekelezaji wa Mradi wa
Kupunguza Gesi Joto Mafunzo hayo yalioandaliwa Kwenye Ukumbi wa
Karimjee Mjini Dar es Salaam Katikati Naibu Katibu Mkuu Ofisiya Makamu
wa Rais Eng Ngosi Mwihava[Picha na Ali meja]
Baadhi
ya washiriki wa semina maalum ya mafunzo kwa waandishi wa habari
kutoka nchi 20 duniani iliyofanyika hivi karibuni nchini Misri wakiwa
katika picha ya pamoja nje ya ofisi za gazeti la Serikali la Al Haram
Jijini Cairo. Wa pili kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari
(Maelezo) Ismail Ngayonga na anayemfutia ni Afisa Habari wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Concilia Niyibitanga.
Afisa
Habari wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Concilia
Niyibitanga akiwa katika picha ya pamoja na watoto katika eneo la
Tahrir Square Jijini Cairo nchini Misri hivi karibuni wakati wa
kumbukumbu ya maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kutokea kwa vurugu katika sehemu hiyo ambazo zilimwondoa madarakani Rais wa zamani wa nchi hiyo, Hosni Mubarak.
Afisa Habari wa Idara ya Habari (Maelezo) Ismail Ngayonga akitazama sehemu ya mitambo inayochapisha
gazeti la Al Haram linalomilikiwa na Serikali ya Misri wakati wa ziara
ya mafunzo kwa waandishi kutoka nchi 20 duniani iliyofanyika hivi
karibuni nchini humo.
Afisa
Habari wa Idara ya Habari (Maelezo) Ismail Ngayonga akiwa katika eneo
la Tahrir Square Jijini Cairo nchini Misri hivi karibuni. Sehemu hiyo
ni chimbuko la vuguvugu la wananchi katika kupinga na hatimaye kuung’oa
madarakani utawala wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Hosni Mubarak.
Matumizi
ya wanyama kazi kama farasi na punda Farasi na Punda ni makubwa sana
katika nchi ya Misri. Pichani ni Farasi wakiwa wamebeba miti na kuwekwa
pembeni mwa barabara katika mtaa wa Zamalek Jijini Cairo kama
walivyokutwa na kamera yetu hivi karibuni nchini humo.
Waandishi
wa habari na wapigapicha kutoka nchi 20 duniani wakiwa katika picha ya
pamoja hivi karibuni mara baada ya kuwasili katika piramidi za Misri
zilizopo katika mji wa Giza nje kidogo ya Jiji la Cairo nchini Misri,
aliyechumaa mstari wa mbele wa pili kushoto ni Afisa
Habari wa Idara ya Habari (Maelezo) Ismail Ngayonga. Piramidi za Misri
ni miongoni mwa vivutio vya utalii ambavyo vipo katika orodha ya maajabu
saba ya dunia.
(PICHA KWA HISANI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akikagua ujenzi wa Kituo cha kimataifa cha
Mikutano cha Kimataifa cha Julius Kambarage Nyerere kwenye Mtaa wa
Shaaban Robert jijini Dar es salaam March 10,2012. Kushoto kwake ni
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na
Kulia kwake ni Balozi wa China nchini, LV Youqing. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mzengo Pinda akijadili jambo na Waziri wa mamboya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kulia) , Balozi wa China
Nchini, LV Youqing baada ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere , Mtaa wa Shaban Robert jijini Dar
es salaam March 10,2012. Wengine pichani na wahadisi kutoka China
wanaosimmia ujezi huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amezitaka kampuni na taasisi zinazohusika na kutoa huduma muhimu katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwl. Julius Kambarage Nyerere ziharakishe kufanya hivyo ili ujenzi wake ukamilike mapema.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumamosi, Machi 10, 2012)
mara bada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa kituo hicho na kukagua ujenzi
wake katika mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam.
Kampuni
zinazotakiwa kufanya hivyo ni TANESCO kwa ajili ya umeme wa jengo hilo,
Kampuni ya Simu (TTCL) kwa ajili ya mkonga wa mawasiliano na Idara ya
Kodi ya Mapato (TRA).
Waziri Mkuu amesema ujenzi
wa kituo hicho cha mikutano ni ishara ya urafiki wa muda mrefu
ulikuwepo baina ya Tanzania na China na kwamba kukamilika kwake
kutaboresha mandhari ya Jiji la Dar es Salaam.
Mapema,
akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa jengo ambalo litagharimu yen milioni
183.5 sawa na dola za Marekani milioni 30, Balozi wa China nchini
Tanzania, Bw. Lv Youqing alisema ujenzi wa jengo hilo ulianza mara baada
ya sherehe za uzinduzi Januari 15, 2010.
Awali,
ujenzi wa jengo hilo ulitarajiwa kukamilika Aprili, 2012 lakini
kutokana na uchelewashaji wa miundombinu hiyo muhimu hivi sasa
linatarajiwa kukamilika Agosti, mwaka huu.
Litakapokamilika
jengo hilo litakuwa na uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 1,000; litakuwa
na kumbi ndogo ndogo nne zenye uwezo wa watu zaidi ya 20, ukumbi wa
chakula wa watu zaidi ya 700 na ofisi za watumishi wa ukumbi huo.
Vilevile, kutakuwa na ukumbi mmoja ambao unaweza kugawanywa
(partitioned) na kutengeneza ofisi za muda kwa watu wanaoendesha mkutano
mkubwa katika ukumbi huo.
Naye
Mkurugenzi wa mradi wa ujenzi wa kituo hicho, Bw. Huang Meiluan alisema
ujenzi wa ghorofa ya chini umekamilika kwa asilimia 40 kwa sababu bado
wanasubiri huduma muhimu zikamilike ili waanze kuweka sakafu.
“Tunasubiri kuunganishwa na mkonga wa mawasiliano wa Taifa, bado
hatujaweka njia kuu za umeme za kuingia katika jengo... kasi ya ujenzi
imeathirika kutokana na kutokamilika kwa huduma hizi muhimu,” alisema.
Alisema
ujenzi wa ghorofa ya kwanza na ya pili umekamilika kwa asilimia 90 na
imebakia kazi ya kumalizia kuweka nakshi za ndani tu (interior
decoration). “Kwa nje, kazi ya ujenzi imekamilika na tumeanza kuweka
nakshi, kazi hii imekamilika kwa asilimia 75,” alisema.
Alisema
wanakabiliwa na changamoto ya wizi wa vifaa vya ujenzi unaofanywa na
vibaka kila mara na kwamba inawapa mtihani kwani itawalazimu kuagiza
upya vifaa hivyo kutoka China. Aliomba polisi wawasaidie kuimarisha
ulinzi katika eneo la ujenzi.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe
alimweleza Waziri Mkuu kwamba wizara yake imeanza kushughulikia
upatikanaji wa kifaa muhimu cha umeme ambacho kilishindwa kupatikana
hapa nchini.
Alisema
vyuma vilivyotumika katika hatua za awali za ujenzi wa kituo hicho ni
tani nyingi, na kwamba yanahitajika malori ya kuvisomba na kibali kutoka
TRA ili yaweze kupelekwa katika eneo jingine kwa kuhifadhiwa.
Alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba wizara yake inafuatilia suala hilo
pia.
Kuhusu
uwekwaji wa nyaya za mkonga wa mawasiliano ambao unapaswa kufanya na
TTCL, waziri Membe aliomba apewe wiki moja zaidi kwani amekuwa
akisumbuana nao kwa zaidi ya mwezi mmoja bila mafanikio yoyote. Suala la
ulinzi pia alisema ameshaanza kulishughulikia.
Mbunge
wa Arusha Godbless Lema akiwa amebebwa juu juu mara baada ya kuwasili
hapo Meru Wilayani Arumeru ambapo mkutano mkubwa wa uzinduzi wa kampeni
wa chama cha Deomkrasia na maendeleo CHADEMA unafanyika kuanzia muda huu
katika viwanja vya Shule ya Msingi Leganza, Mwandishi Wetu
ambaye yuko katika eneo la tukio, anasema "Tayari helkopta
zilizowachukua viongozi kadhaa wa chama hicho zimeanza kutua katika
viwanja hivyo tayari kwa uzinduzi na mkutano huo utarushwa moja kwa moja
na televisheni kadhaa za hapa nyumbani.
Umati wa watu ukiwa unaelekea eneo la mkutano katika viwanja vya shule ya Msingi Leganza.
Meneja
Mkuu wa Multchoice Tanzania Bw. Peter Fuel akifurahia jambo na Meneja
wa Uendeshaji Ronald Shelukindo wakati wa hafla ya wateja iliyoandaliwa
na kampuni hiyo kwa ajili ya wateja wake, katika siku hii ya leo
ving'amuzi vya DSTV vinauzwa kwa silingi 120.000 pamoja na
kukuunganishia nyumbani kwako na ofaa hii ni ya leo tu.
Hafla hiyo inafanyika katika ofisi za Multichoice zilizopo Saint Peter Oysterbay jijini Dar es salaam.
Mwanafunzi
Diana Kimaro wa Chuo Kikuu cha Nilai Malasia akisomea masuala ya
biashara ambaye yuko katika benki ya NMB kwa mazoezi akimpatia huduma
mmoja wa wateja wa benki ya NMB aliyefika katika hafla hiyo, Benki ya
NMB pia imeshiriki katika hafla hiyo kwa ajili ya kuwaelezea wateja wao
huduma mbalimbali wanazozitoa.
Meneja uendeshaji wa Multchoice Ronald Shelukindo akizungumza na wateja wa kampuni hiyo katika hafla hiyo.
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara Jana (Machi 10 mwaka huu) amechangia sh. milioni moja kwenye uzinduzi wa
akaunti ya Twiga Stars kupitia Tigo Pesa kuichangia timu hiyo ambayo
inashiriki michuano ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC).
Akizungumza
kwenye hafla hiyo iliyofanyika Dar es Salaam, Dk. Mukangara alisema ni
jukumu la kila Mtanzania kuichangia Twiga badala ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuachiwa pekee mzigo huo wa kuendesha
timu hiyo.
Wachangiaji
wa Twiga Stars wanatakiwa kutuma mchango wao kwenda namba 13389 ambapo
kiwango cha juu kinachoweza kutumwa kwa muhamala (transaction) mmoja
ni sh. 500,000. Kwa Waziri Dk. Mukangara kuchangia sh. milioni moja
alifanya mihamala miwili.
Naye
Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani alisema Twiga Stars
kwa sasa haina mdhamini na Shirikisho limekuwa likibeba mzigo wa
kuhakikisha inashiriki katika mechi za kirafiki na mashindano mbalimbali
kwa vile imekuwa ikifanya vizuri.
Twiga
Stars inayofundishwa na kocha Charles Boniface Mkwasa iko kwenye
raundi ya pili ya mashindano ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC)
ambapo Mei 26 mwaka huu itacheza na Ethiopia jijini Addis Ababa.
Katika
raundi ya kwanza, Twiga Stars iliitoa Namibia kwa jumla ya mabao 7-2.
Ilishinda ugenini 2-0 na kuibuka na ushindi mnono nyumbani wa mabao
5-2. Fainali za AWC zitafanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial
Guinea.
o
Mkurugenzi
Mkuu Mwandamizi wa shirika la Millenium Challenge Account Tanzania
Dar es Salaam(MCA-T Dsm) Bw. Bernard Mchomvu akimkabidhi zawadi ya
Khanga yenye nembo ya shirika hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia
Stella Manyanya walipoonana ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said
Thabit Mwambungu (kulia) jana kujadili miradi ya barabara
inayodhaminiwa na shirika la Millenium Challenge Cooperation (MCC)
kupitia Tanzania Millenium Challenge Account (MCA-T Dsm). (Pichana
Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
Shirika hilo linafadhili ujenzi wa
barabara kuu za lami zinazojengwa Mkoani Rukwa zenye jumla ya Km. 224
kwa miradi ya Tunduma-Ikana, Ikana-Laela, na Laela-Sumbawanga. Kwa
mujibu wa Bwana Mchomvu miradi hiyo yote pamoja na changamoto zote
kuzingatiwa itakuwa imekamilika ifikapo mwezi June 2013 na barabara
zote zitakuwa zimekabidhiwa kabla ya mwezi wa nane 2013.
Kwa upande wa Ruvuma shirika hilo
linafadhili ujenzi wa barabara itokayo mjini Songea kuelekea Wilaya ya
Mbinga ambapo ujenzi huo unaendelea na unategemewa kukamilika mwakani.
Hata hivo Mkurugenzi huyo
aliushukuru uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano wanaoutoa
kuwaeleimisha wananchi wao juu ya umuhimu wa miradi hiyo na ulinzi wa
vifaa vya ujenzi kwani umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza wizi wa
vifaa vya ujenzi vilivyokuwa vinafanywa na baadhi ya wananchi na
wafanyakazi wasiokuwa waaminifu.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Injinia Stella Manyanya allishukuru shirika hilo kwa jitihada zao
za kuchangia maendeleo nchini. Aliwashukuru pia kwa hatua za hivi
karibuni walizochukua kujenga daraja la Laela ambalo ni kiunganishi
muhimu kwa wananchi wa eneo hilo katika shughuli zao za kila siku
hususani kuwaunganisha na kituo cha afya cha Laela.
Picha
ya pamoja kati Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu, Injinia
Stella Manyanya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa
Ruvuma Tarimo na wawakilishi wa Jumuiya ya Millenium Challenge
Cooperation (MCC) Bw. Carl Fickenscher Mkurugenzi Mkazi nchini
(kushoto) na Bw. Bernard Mchomvu Mkurugenzi Mkuu Mwandamizi wa shirika
la Millenium Challenge Account Tanzania Dar es Salaam(MCA-T Dsm).
Subscribe to:
Posts (Atom)