TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, January 25, 2012
MRADI WA KUDHIBITI MAAMBUKIZI YA VVU/UKIMWI ULIOFADHILIWA NA SERIKALI YA JAPAN KWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA AFYA WAFUNGWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM.
Mwakilishi
mkuu wa Shirika la Kimataifa la ushirikiano wa kimaendeleo la Japan
(JICA) Bw. Yukihinde Katsuta akitoa maelezo juu ya ukamilishwaji wa
mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini Tanzania uliofadhiliwa na serikali ya Japan kwa lengo la kupunguza maambukizi ya VVU sanjari na usambazaji
wa vifaa vya kupimia maambukizi hayo na kuahidi kuendeleza ushirikiano
na serikali ya Tanzania katika utoaji wa vifaa vya kutolea huduma za
afya.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akimkabidhi Zawadi iliyoandaliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii mwakilishi mkuu wa JICA wakati wa hafla fupi ya ukamilishaji wa
mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini uliofadhiliwa na serikali ya Japan jijini Dar es salaam.
Baadhi ya watendaji wa wizara ya afya na wawakili kutoka Shirika la
kimataifa la maendeleo la Japan (JICA) wakifuatilia taarifa mbalimbali
zilizokuwa zinatolewa wakati wa hafla fupi ya ukamilishaji wa mradi wa
kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini uliofadhiliwa na serikali ya Japan jijini Dar es salaam.
Katibu
mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni
akizungumza watendaji wa Wizara hiyo na wawakilishi wa Shirika la
Kimataifa la ushirikiano wa kimaendeleo la Japan (JICA) wakati wa hafla
fupi ya ukamilishaji wa mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya
Ukimwi nchini ulioanza mwaka 2009 chini ya ufaufadhili wa serikali ya Japan, jijini Dar es salaam.
Airtel yatoa vitabu Kilimanjaro
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Siha,Bw.Rashid
Kitambulo akizungumza na kuishukuru kampuni ya Airtel kwa msaada mkubwa wa vitabu ilioutoa kwa shule nne za sekondari zailizopo wilayani hapo, mwisho kushoto ni Mwalimu mkuu wa sekondari ya Oshara
Elieta Kaaya akifatiwa na wawakilishi wa Airtel Pascal Bikomagu na
Jane matinde (kulia) ni Afisa Elimu Taaluma wa sekondari Wilaya ya
Siha,Bw. Mussa Shaban Ally.hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika
shule ya sekondari Oshara jana.
Airtel yatoa msaada wa vitabu shule 4 za secondari wilaya ya SIHA - Kilimanjaro
Chini ya mpango wake wa Airtel Shule Yetu kampuni ya simu za mkononi
ya Airtel imetoa vitabu vya ziada na kiada kwa shule 4 za sekondari
zilizoko wilaya ya Siha ili kusaidia maendeleo ya elimu wilayani hapo.
Hafla hiyo fupi imefanyika katika shule ya sekondari Oshara ambapo
shule zilizonufaika na msaada huo ni za sekondari ya
Oshara,Kilingi,Magadini na Namwai zote za wilayani humo ambapo
wawakilishi wa shule hizo walikabidhiwa msaada huo na Mkurugenzi wa
Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Siha bw, Rashid Kitambulo ambaye
alikabidhiwa vitabu hivyo na Afisa Uhusiano wa kampuni ya airtel bi,
Jane Matinde. kila shule imepewa msaada wa vitabu vyenye thamani ya
shilling milio moja.
Akiongea katika hafla ya makabithiano iliyofanyika katika shule ya
sekondari Oshara Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde
alisema" Airtel kwa kupitia programme ya shule yetu imeweza kuwafikia
wanafunzi wengi na shule nyingi nchini Tanzania na leo tunafurahi kuwa
sehemu ya maendeleo ya shule hizi 4 za sekondari wilayani Siha na
kuweza kuchangia vitabu zitakavyotumika katika kufundishia na kuwa
nyenzo muhimu kwa walimu na wanafunzi wa shule hizi”
“Tutaendelea kushirikiana na Serikali chini ya Wizara ya Elimu katika
kuinuia na kuboresha kiwango cha elimu nchini kwani tunatambua elimu
ndio ufunguo wa maisha na vijana ndio nguvukazi ya kesho” Aliongeza
Matinde.
Mgeni rasmi katika halfa hiyo Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya
Siha bwana Kitambulio Rashidi alisema tunayo fuhara kuona Airtel
inajitoa katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu nchini, moja kati
mikakati ya elimu halmashauri yetu iliyojiwekea ni kuhakikisha kwamba
kila nyumba moja ya mkazi wa siha anatoka graduate na ili kufikia
malengo yake kuna mahitaji ya vitabu vya kufindishia, tunashukuru sana
Airtel kwa kutusaidia katika kutimiza malengo tuliojiwekea
Bw Rashidi pia alichukua fulsa hiyou kuwaasa wanafunzi kuvitumia
vizuri vitabu hivyo ili vilete matokeo vizuri kwa wanafunzi na kufikia
lengo halmshauri hiyo iliyojiwekea
Kwa upande wake Afisa Elimu Taaluma wa sekondari wilaya ya Siha Mussa
Shaabani Ally wameishukuru Airtel kwa kuwawezesha vitendea kazi na
kuongeza kuwa wilaya hiyo mpya bado inakabiliwa na changamoto nyingi
katika elimu hivyo kuiomba kampuni hiyo kuendelea kuisaidia katika
mambo mengine.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali
kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, wiki iliyopita Airtel ilitoa
msaada wa kutoa computer 4 kwa shule ya sekondari mlangarini iliyoko
wilaya ya Arumeru mkoani na pia kuchangia katika sekta ya afya ambapo
Airtel iligawa baskeli kumi kwa vituo vya afya wilayani misungwi
Mkoani Mwanza. Hii ikiwa nikatika kurudisha faida inayoipata na
kuchangia katika huduma kwa jamii.
NSSF YAFANIKIWA KUKUSANYA ZAIDI YA BILIONI 16
Na Gladness Mushi -Arusha
MFUKO wa hifadhi ya jamii( NSSF)mkoani Arusha umefanikiwa kukusanya
shilingi bilioni 16.745 kwa kipindi cha Jully hadi desemba 2011 ambapo
fedha hizo ni sawa na asilimia 92 ya lengo walilokusudia
Hayo yalisemwa na meneja kiongozi wa mfuko huo mkoani hapa Bw Jackton
Ochieng' alipokuwa akiongea na gazeti hili kuhusiana na hali ya mfuko
huo .ilivyo kwa sasa.
Aidha alisema kuwa mfuko huo umeweza kuandikisha wanachama 3582
ambapo ni sawa na asilimia 49.8 ambapo hilo ndilo lengo hailsi
Vile vile aliongeza kuwa kwa kipindi hicho pia wameweza kuandikisha
waajiri 72 ambapo ni sawa na asilimia 79 ya lengo
Hata hivyo bw Ochieng' alieleza kuwa mfuko huo umeweza kulipa mafao
kwa wanachama wake 2416 ambapo kifedha wamelipwa shilingi bilioni
4033.65.
Alieleza changamoto zinazoukabili mfuko huo kuwa ni pamoja na watu
kutojua dhana ya elimu ya mfuko wa jamii na hivyo kuwafanya kuwa waoga
kujiunga na mfuko huo ambapo alisema kuwa hadi sasa wamejitahidi kutoa
elimu hiyo kwa waajiri 53 .
Aliitaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na baadhi ya wafanyakazi
kurubuniwa na waajiri hali ambayo inaleta matatizo katika mfuko huo.
Aliwataka wanachama na wasio wanachama kutokubali kurubuniwa na
waajiri kwa kuwa ni haki ya mfuko kuhudumia wanachama wake kuanzia
sasa na hata uzeeni
WACHOMA MAHINDI WAPEWA MAJIKO KUJIKWAMUA KIUCHUMI JIJINI ARUSHA
NA GLADNESS MUSHI- ARUSHA
Kikundi
cha akinamama wapatao 50 kinaojishughulisha na biashara ya kuchoma
mahindi katika jiji la Arusha kinatarajia kuongeza kipato kupitia
biashara hiyo baada ya wanachama wake kupatiwa majiko yaliyosanifiwa kwa
tenknolojia ya kisasa.
Upatikanaji
wa majiko hayo yaliyotengenezwa kwa teknolojia ya aina yake unaelezwa
kuiongezea dhamani biashara hiyo ya uchomaji mahindi ambayo akinamama
wengi na vijana wamekuwa wakiifanya.
Kwa
msaada mkubwa wa mtandao wa vijana nchini,kikundi kinachofahamika kama
Wamama Wachoma Mahindi Arusha kimeweza kufadhiliwa na kupata majiko sita
yenye dhamani ya shilingi milioni mbili ambapo mwenyekiti wa kikundi
hicho Bi Sophia Juma anasema yatasaidia kuongeza ufanisi katika biashara
hiyo.
Mwenyekiti
wa mtandao wa vijana nchini YDN,Bw.Elipokea Urio amesema upatikanaji wa
majiko hayo ni sehemu ya mikopo midogomidogo ambayo imekuwa ikitolewa
na halmashauri ya jiji la Arusha katika kuinua vipato cha vya
wafanyabiashara wadogo na wakati.
Naye
Fundi aliyesanifu majiko hayo Bw.John Werema amesema kitaalamu aina
hiyo ya majiko ni rafiki wa mazingira kutokana na muundo wake
Biashara
ya uchomaji wa mahindi licha ya kutengeneza ajira kwa baadhi ya
kinamama na vijana imekuwa ikielezwa kuchangia uchafuzi wa mazingira
katika baadhi ya maeneo nchini lakini sasa aina hii ya majiko inaelezwa kuwa tiba sahihi katika kukabiliana na hali hiyo.
SIMBA YAPATA MTEREMKO TANGA- YAIFUNGA COASTAL UNION 2-1
Mchezaji
wa timu ya Simba akikokota mpira baada ya kumtoka beki wa timu ya
Coastal Union ya Tanga Felix Stanley katika mchezo wa Ligi kuu ya
Vodacom mzunguko wa pili unaoendelea kwenye uwanja wa Taifa jioni
hii,Mpira umekwisha Simba imeshinda goli 2-1goli la kwanza limefungwa
na mchezaji Haruna Moshi "Boban" katika
kipindi cha kwanza na goli la pili likafungwa na mchezaji Gelvas Kago
akipokea pasi nzuri ya Haruna Moshi.
Timu ya Coastal Union ilifanikiwa kupata goli katika kipindi cha pili
kwa njia ya penati lililofungwa na mchezaji Hamis Shengo, mpaka mpira
unakwisha simba 2 na Coastal Union 1.
Baadhi
ya Maafisa Kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga na wakulima
wakikagua shamba katika kijiji cha Kaoze.
NA :Ramadhani Juma, Afisa habari wilaya ya Sumbawanga
VIKUNDI vya wakulima katika Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa vimeanza kufaidika na miradi ya
kilimo kupitia Mashamba Darasa inayodaiwa kuwaongezea mbinu za kisasa
za kilimo bora hali inayotarajiwa kuwaongezea mavuno na kipato ikiwa ni
juhudi za kujikwamua kutoka katika lindi la umasikini.
Baadhi
ya wanachama wa kikundi cha CHEMKA kilichopo katika kijiji cha Kaoze
kilichopo bonde la ziwa Rukwa walisema wamenufaika sana na elimu ya
mradi wa shamba darasa uliotekelezwa katika kijiji hicho na kwamba wamekuwa wakipoteza mazao mengi kwa kulima kilimo cha kiasili.
Walisema
kuwa, kwa kipindi kirefu wamekuwa wakivuna magunia matatu mpaka matano
kwa hekari moja walipokuwa wakilima kilimo cha asili lakini kwa kilimo
bora cha kisasa wanategemea kupata magunia 25 mpaka 30 kwa hekari moja
hivyo wanategemea kujiongezea kipato na kujikwamua katika umasikini.
Kwa mujibu wa
Afisa Kilimo wa wilaya hiyo Shaaban Bahari, Halmashauri hiyo ina jumla
ya mashamba Darasa 151 katika vijiji mbalimbali wilayani humo na
kwamba hali hiyo inatarajiwa kuwafaidisha wakulima.
“Tunategemea
miradu hii itawasaidia wakulima wetu kujiongezea mbinu mbalimbali za
kilimo cha kisasa ikiwemo matumizi ya mbolea, kupanda kwa kuzingatia
nafasi, pamoja na kutumia mbegu bora” alisema Juma.
Miradi
hiyo ya mashamba darasa inatekelezwa na wilaya hiyo katika vijiji na
Kata mbalimbali kwa lengo la kuwaongezea ujuzi wakulima wilayani humo,
ikiwa ni pamoja na matumizi ya mbolea pamoja na mbinu nyingine za kilimo
cha kisasa.
President
Jakaya Kikwete is received by the Minister for Agriculture, Food
Security and Cooperatives Professor Jumanne Maghembe as he arrives at
the Davos Sheraton ahead of the four day World Economic Forum held
annually in the mountainous health resort. The forum, that goes under
the theme: " The Great Transformation: Shaping New Models",
Ais being attended by mong others President Kikwete is also scheduled
to hold a number of private meetings and bilateral talks with
prominent world leaders and entrepreneurs, besides attending
interactive sessions on different issues.
President
Jakaya Kikwete holding a preparatory meeting with his delegations soon
after arrival at the Davos Sheraton ahead of the start of the four day
World Economic Forum held annually in the mountainous health resort.
The forum, that goes under the theme: " The Great Transformation: Shaping New Models",
Ais being attended by mong others President Kikwete is also scheduled
to hold a number of private meetings and bilateral talks with
prominent world leaders and entrepreneurs, besides attending
interactive sessions on different issues. (PHOTOS BY STATE HOUSE)
Tuesday, January 24, 2012
MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AANZA ZIARA YA MKOA WA TANGA LEO, AKAGUA UKUTA WA KUZUIA MAJI YA BAHARI PANGANI
Makamu
Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akikata utepe kuzindua rasmi Jengo la Ofisi ya Idara ya Maji, lililopo
Wilaya ya Pangani, wakati alipoanza ziara yake ya Mkoa wa Tanga leo,
Januari 24, 2012. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa (kushoto)
ni Mkurugenzi wa Maji wa wilaya hiyo, Mohamed Hamis.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu ukuta huo unaozuia maji ya Bahari
unaobomoka kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi na kutishia amani ya
wakazi wa maeneo hayo. Pangani Kivukoni.Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongozana na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Pangani wakati akitoka
kukagua ukuta wa kuzuia maji ya Bahari unaobomoka Pangani Kivukoni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiangalia ukuta unaozuia maji ya Bahari eneo la Pangani
Kivukoni, unaozidi kubomoka kutokana na kujengwa miaka 100 iliyopita na
kutishia amani kwa wakazi wa maeneo hayo. Makamu wa Rais ameanza ziara yake ya Mkoa wa Tanga leo Januari 24, 2012.
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Mashirika
ya Umma(PAC), imeagiza kwamba sheria inayoruhusu Mamlaka ya Nishati na
Madini(EWURA) kulipa mishahara ya watumishi wa Baraza Ushauri na Watumaji la Nishati na Madini (EWURA CCC) ibadilishwe ili baraza hilo liweze kufanya kazi ipasavyo.
Hayo
yalisemwa leo na Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe wakati
akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ofisi ndogo za Bunge
jijini Dares Salaam kuhusu shughuli zilizofanywa na kamati yake ,
ambapo alisema baraza hilo hesabu zake zinakwenda vizuri.
“Baraza hili hesabu zake ni nzuri , lakini halifanyi kazi ipasavyo kwa
kuwa halimtendei kazi ipasavyo liko pamoja na EWURA tumeagiza sheria
ibadilishwe ili liweze kufanya kazi kwa kuzingatia pande zote,” alisema Filikunjombe.
Makamu
Mwenyekiti huyo alishauri kuwa ni vyema mishahara hiyo ilipwe na wizara
husika ili baraza hilo lifanye kazi bila kuegemea upande mmoja.
Akizungumzia kuhusu upandaji wa umeme kwa asilimia 40 alihojia upanda kwa sababu zipi je mlaji wa chini wamemsikiliza wanasemaje, hivyo alisema haitakuwa sahihi ikiwa hakusikilizwa.
Aliongeza kuwa baraza hilo pia linatakiwa kuacha kulipa malipo
ya kila baada ya miaka mitano mtumishi anapostaafu badala yake yawe
katika mfumo ya mifuko ya hifadhi ya jamii, ikiwemo kuwaingiza watumishi
wake katika Mfuko wa Bima ya Afya ili kuepuka utumiaji wa risiti za
malipo ya matibabu.
Alitaka baraza hilo kutumia fedha kulingana na bajeti yake.
Wakati huohuo Filikunjombe alisema kamati
hiyo imemfukuza mwakilishi wa Shirika Hodhi la Mali za Umma (CHC)
kwa kuwa ni mtendaji wa chini hawawezi kuzungumza naye hivyo wanamtaka
Ofisa Mtendaji Mkuu.
Alisema mwakilishi aliyetumwa ni Ofisa Uhusiano ambayo ameitumwa na Kaimu Mkurugenzi.
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Kuanzishwa kwa mkakati wa kitaifa wa mabadiliko ya Tabia nchi kutaiwezesha na kuiongezea uwezo nchi
ya Tanzania kushirikiana na mataifa mbalimbali katika kukabiliana na
changamoto za mabadiliko ya tabia nchini yanayoendelea kuikumba dunia.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi msaidizi wa
Idara ya Mazingira, Ofisi ya makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi wakati
akifungua mkutano wa wadau wa mazingira kujadili mkakati wa kitaifa wa mabadiliko ya Tabia nchi.
Amesema
hivi sasa mabadiliko ya tabia nchi yameleta athari kubwa duniani
ikiwemo ongezeko la gesi joto angani jambo ambalo linahitaji juhudi za
mtu mmoja mmoja, vikundi, Taasisi na Jumuiya za kimataifa kushirikiana
kwa pamoja kuinusuru dunia kutokana na athari za mabadiliko hayo.
“ Tanzania na watanzania wote kwa ujumla watapata fursa ya kushiriki
katika fursa za miradi ya kupunguza gesi joto kupitia sekta binasfi
hasa fursa za miradi ya kupunguza gesi joto inayoanzishwa nchini na kuwawezesha watanzania kupata fedha huku wakiendelea kufanya shughuli zao za kila siku”
Amefafanua
kuwa mkakati huo wa kitaifa wa mabadiliko ya Tabia nchi utaisaidia
nchi ya Tanzania kushiriki katika masuala mbalimbali ya kimataifa na
kuiwezesha kuwa na msimamo kama nchi kupinga vitendo vyote vinavyofanywa
na mataifa mbalimbali yaliyoendelea kiviwanda ambayo yanachangia kwa
kiwango kikubwa ongezeko la gesi joto duniani.
Pia
amefafanua kuwa licha ya mkakakati huo kuanzishwa kwa mara ya kwanza
kwanza nchini utaiwezesha Tanzania kuwa ushirikiano na nchi nyingine za
Afrika, jumuiya mbalimbali za kimatifa ndani na nje ya bara la Afrika
na kuongeza kuwa ukamilishwaji wa mkakati huo utaiwezesha nchi kupanga
na kuamua masuala mbalimbali yahusuyo mabadiliko ya Tabia nchi.
Aidha amefafanua kuwa sanjari na kuwepo mkakati huo ambao ni mkubwa masuala ya mazingira yataendelea kuongozwa
na mkakati wa kitaifa wa mwaka 2006 na ule wa 2007 unaotoa mwongozo
kuhusu masuala mbalimbali ya mazingira yakiwemo uzuiaji wa uchafuzi na uharibifu wa vyanzo vya maji katika mito na uharibifu wa misitu na mazingira.
Kwa
upande wake mshiriki wa mkutano huo kutoka chuo kikuu cha Dar es
salaam Prof. Richard Kangalawe amefafanua kuwa mabadiliko ya tabia nchi
yanendelea kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wan chi yetu na hata
kutishia maisha ya kila siku.
Amezitaja baadhi ya changamoto ambazo Tanzania kwa sasa inakabiliana
nazo kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi kuwa ni pamoja na ukame
katika baadhi ya maeneo, mafuriko yanayojitokeza katika maeneo
mbalimbali nchini kutokana na mvua zinazonyesha kwa muda mfupi na
ongezeko la magonjwa mbalimbali.
“Kama
tunavyoona kuna dalili mbalimbali ambazo zinaonyesha kuwa hali ya
mabadiliko ya tabia nchi imekuwa kubwa sana tofauti na miaka 30
iliyopita na inaliathiri taifa hasa baadhi ya matukio mbalimbali
yaliyotokea hivi karibuni ikiwemo mvua kubwa zilizonyesha na kusababisha
mafuriko katika maeneo mbalimbali nchini na kusababisha madhara
makubwa katika jiji la Dar es salaam.
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) akiwekeana saini
na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Motherland Industries Limited
kutoka India Bw, V. K. Sood (Kulia) uwekaji saini wa mikataba mitatu
ya utafiti wa mafuta nchini, umefanyika leo jijini Dar es Salaam,
(Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)
Kamishna Msaidizi wa Nishati kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw,
Prosper Victus (alisimama mbele na Kabrasha) akitoa maelezo ya awali
wakati wa uwekaji wa saini mikataba mitatu ya utafii wa mafuta kutoka
kampuni za nje leo wakati wa hafla hiyo kwenye jengo la Wizara ya hiyo
jijiji Dar es Salaam. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Waziri
wa Nishati na Madini William Ngeleja (kulia) akifafanua jambo wakati
wa uwekaji saini wa mikataba mitatu ya uatafiti wa mafuta kutoka
kampuni za nje jijini leo DSM (Kulia) ni Kamishna Msaidizi wa Nishati
(Petroleum na Gas ) Bw, Prosper Victus, (Picha na Mwanakombo Jumaa-
MAELEZO).
Waziri wa Nishati na Madini Wiliam Ngeleja (kushoto) akibadilisha hati
za makubaliano ya utafiti wa mafuta nchini na Mkurugenzi Mtendaji wa
kampun i ya Petrobras kutoka Brazil Bw, Samuel Bastos de Miranda
(kulia) , hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Slaam wakati wa
hafla ya uwekaji saini wa mikataba mitatu ya utafiti wa mafuta wa
kampuni kutoka nje, (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (katikati) akiweka saini
mkataba wa utafiti wa mafuta nchini kwa kampuni tatu kutoka nje,
(kushoto) ni Mkurugenzi mtendaji wa TPDC Bw, Yona Killagane na
(kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Matherland industries LTD
kutoka India, Bw. V.K. Sood .(kulia). Mkataba huo umewekwa saini leo
kwenye jingo la Wizara ya Nishati na Madini, (Picha na Mwanakombo
Jumaa- MAELEZO).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk
Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na watendaji wa Wizara ya
Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati, Ikulu Mjini Zanzibar,katika mpangilio
wake wakuzungumza na kila Wizara ya Serikali ya Zanzibar,katika ukumbi
wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Picha na Ramadhan Othman IKULU.
Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kupitia kitengo chake cha
utatuzi wa migogoro (Dispute Resolution Chamber- DRC) limeagiza klabu
ya Yanga kumlipa mchezaji John Njoroge sh. 17,159,800 ikiwa ni fidia
kwa kuvunja mkataba wake kinyume cha taratibu.
Uamuzi
huo wa DRC chini ya Jaji Theo van Seggelen ambaye ni raia wa Uholanzi
ulifanywa Desemba 7 mwaka jana jijini Zurich, Uswisi na kutumwa TFF kwa
njia ya DHL, Januari 17 mwaka huu.
Njoroge
ambaye ni raia wa Kenya aliwasilisha kesi yake FIFA kupinga Yanga
kuvunja mkataba alioingia wa kuichezea timu yao kinyume na makubaliano.
Mchezaji huyo hivi sasa anachezea timu ya Tusker ambayo ni mabingwa wa
Kenya.
Yanga
ina siku nne za kukata rufani kupinga uamuzi huo kuanzia tarehe
iliyoupokea kama inataka kufanya hivyo. Klabu hiyo inatakiwa iwe
imeshamlipa Njoroge ndani ya siku 30 tangu ilipopokea uamuzi huo.
Ikishindwa kulipa ndani ya muda huo, itatozwa riba ya asilimia 5 kwa
mwaka ya fedha hizo.
Ikiwa
Yanga itashindwa kulipa ndani ya muda huo vilevile suala hilo
litafikishwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ya FIFA kwa hatua zaidi.
Kiingilio
cha chini kwa mechi ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC)
kati ya Twiga Stars na Namibia itakayochezwa Jumapili (Januari 29
mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 2,000.
Kiwango
hicho ni kwa washabiki kwa viti vya bluu na kijani. Viti hivyo kwa
pamoja vinachukua jumla ya watazamaji 36,693 kwenye uwanja huo wenye
uwezo wa kuchukua washabiki 60,000.
Pia
kutakuwa na kiingilio cha watoto wenye umri wa chini ya miaka 10
ambacho ni sh. 1,000. Watoto watakaotumia tiketi hizo wanatakiwa kuingia
uwanjani wakiwa na wazazi au walezi wao.
Viingilio vingine kwa mechi hiyo ni sh. 3,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 5,000 kwa VIP B na C n ash. 10,000 kwa VIP A.
Namibia inatarajia kuwasili nchini Ijumaa (Januari 27 mwaka huu) saa 12.45 jioni kwa ndege ya South Africa Airways.
Kamati
ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya
marekebisho madogo kwenye ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom kutokana na
Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kutumika kwa sherehe za kitaifa za
kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mechi
namba 111 kati ya Toto Africans na African Lyon ambayo kwa mujibu wa
ratiba ilikuwa ichezwe Februari 5 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza sasa itachezwa Aprili 18 mwaka huu.
Mabadiliko
hayo yamefanyika baada ya wamiliki wa Uwanja wa CCM Kirumba, Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kueleza kuwa watautumia kwa sherehe za kuzaliwa chama
chao, hivyo hautakuwa na nafasi kwa Februari 4, 5 na 6 mwaka huu.
Uamuzi
huo umesababisha pia mabadiliko kwa mechi nyingine mbili. Mechi namba
168 kati ya Villa Squad na African Lyon iliyokuwa ichezwe Aprili 18
mwaka huu Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam, sasa itachezwa Aprili
22 mwaka huu.
Pia
mechi namba 170 kati ya Azam na Toto Africans iliyokuwa ichezwe Aprili
29 mwaka huu jijini Dar es Salaam sasa imerudishwa nyuma hadi Aprili
26 mwaka huu ambayo ni Sikukuu ya Muungano.
Mkurugenzi
msaidizi wa Idara ya Mazingira,Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard
Muyungi akizungumza na wadau wa mazingira kutoka Taasisi
mbalimbali,wizara na wadau kutoka nchi wahisani wakati wa ufunguzi wa
mkutano wa wadau hao unaojadili mabadiliko ya Tabia nchi na mkakati wa
kitaifa kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi leo jijini Dar es salaam.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Mshauri wa masuala ya mabadiliko ya Tabia nchi kutoka
Idara ya Kimataifa ya Maendeleo (DFID) nchini Tanzania Bi. Magdalena
Banasiak (kushoto) akizungumzia athari za mabadiliko ya Tabia nchi
duniani na mchango wa wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi katika kuhakikisha kuwa athari za mabadiliko ya tabia nchi zilizoanza kujitokeza zinadhibitiwa.
Mkurugenzi
msaidizi wa Idara ya Mazingira,Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard
Muyungi akiwasilisha mada kuhusiana na mabadiliko ya Tabia nchi na
ripoti ya tafiti ya athari za kimazingira iliyofanyika katika baadhi ya
maeneo yakiwemo Zanzbar, Mbeya, Tanga, Manyara, Shinyanga na Mwanza leo
jijini Dar es salaam.
Ayoub
Mzee at the Africa Union Summit to attend the 18th ordinary
session of the assembly of heads of state and government s
The
advent of the African Union (AU) can be described as an event of
great magnitude in the institutional evolution of the continent. On
9.9.1999, the Heads of State and Government of the Organisation of
African Unity issued a Declaration (the Sirte Declaration) calling
for the establishment of an African Union, with a view, inter alia,
to accelerating the process of integration in the continent to
enable it play its rightful role in the global economy while addressing
multifaceted social, economic and political problems compounded as
they are by certain negative aspects of globalisation.
The
main objectives of the OAU were, inter alia, to rid the continent of
the remaining vestiges of colonization and apartheid; to promote unity
and solidarity among African States; to coordinate and intensify
cooperation for development; to safeguard the sovereignty and
territorial integrity of Member States and to promote international
cooperation within the framework of the United Nations.
Indeed,
as a continental organization the OAU provided an effective forum
that enabled all Member States to adopt coordinated positions on
matters of common concern to the continent in international fora and
defend the interests of Africa effectively.
Through
the OAU Coordinating Committee for the Liberation of Africa, the
Continent worked and spoke as one with undivided determination in
forging an international consensus in support of the liberation
struggle and the fight against apartheid.
HII
siyo bahati nasibu wala Bingo bali ni msaada wa kumuwezesha Mchungaji
Deogratius Mosha wa Kanisa la Elishadai Gospel Ministry katika
kumuwezesha kujikwamua kiuchumi kwenye Kanisa lake, hii ni sehemu ya
mkakati wa Kanisa la Amri kuu za Mungu (Akuzamu) lililoko Jijiji Dar es
salaam katika jengo la IPS,linalofundisha watu masuala ya uchumi na
kuwawezesha kwa mahitaji mbalimbali ambapo tukio hili lilifanyika
katika semina ya uchumi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nadd's uliko
Salender Bridge juzi (picha na Salesi Malula)
Na salesi Malula
Mchungaji
Edward Amri wa huduma ya Amri Kuu za Mungu (AKUZAMU) amewapiga
marufuku waumini wake kuacha kuilaumu Serikali kwani haisaidii chochote
katika maisha yao na kufanya hivyo ni kinyume na Neno la Mungu.
Ameyasema
hayo alipokua akifundisha Neno la Mungu katika ibada ya Jumapili,
ambapo aliwaasa wakristo kufuata Kanuni ya Neno la Mungu, ili waweze
kufanikiwa katika kila eneo na kuepuka kuilaumu serikali kila mara,
jambo ambalo haliwezi kuleta majibu katika maisha yao ya Kila siku.
Alisema
ifikie mahali Watanzania wajiulize nini wataifanyia nchi yao kwani
sisi kama Kanisa lazima tuwe Baraka kwa Taifa na siyo kugeuka
wapinzania kwa kuilaumu serikali; kinachotakiwa kila Kanisa liwe na
utaratibu wa kuwasaidia waumini wake kwa kuwapa mafundisho ya namna ya
kujikwamua kiuchumi, likiwepo suala la kuwahamasisha waweze kujiajiri
ili waweze kuisaidia serikali katika kutoa ajira na kulipa kodi kwa
usashihi.
“Kazi
ya Kanisa ni kuisaidia serikali na siyo kuipinga na kuwatengeneza watu
wake yaani waumini kuwa raia wema wenye kuipenda nchi yao likiwepo
suala la kuwakwamua watu kiuchumi kwa kuwafundisha mafundisho sahihi ya
uchumi katika ufalme wa Mungu, kama ambavyo kanisa letu linafanya
ambapo muda si mrefu sisi tutakuwa Baraka katika Taifa kwani waumini
wetu wengi wataajiri na watakuwa na walipakodi wazuri katika nchi
yetu”.
Akiongea
kwa kujiamini alisema kwa sasa uchumi wa dunia nzima umekwama na
sababu yake ni kwamba ni vigumu sana uchumi wa mfumo huu kufaulu kwa
sababu hauna mbadala, yaani ziada kwani masomo hayo ya uchumi
yanayofundishwa shuleni miaka 20 iliyopita ndio hayo hayo yanafundishwa
hivyo wachumi wetu hawawezi kuwa na la ziada zaidi ya kujifunza masomo
ambayo wenzao waliyagundua zamani na ndio maana hadi hivi sasa
hawawezi kutoa majibu ya kuboresha maisha ya wananchi.
Akitoa
mfano alisema kwa sasa nchini kwetu hatuna vitu ambavyo tumegundua.
Kwa mfumo wa uchumi wa kwenye makaratasi hauwezi kutoa majibu kwani
hata hao wachumi endapo masomo yangekuwa na hatimiliki nadhani sisi
tusingekuwa na kitu kwani masomo hayo tunakopi kutoka kwa wenzetu ambapo
hatuwezi kuwa na mbadala na ndio maana unaweza kukuta tunao wasomi
wengi wa uchumi wasipoajiriwa hawawezi kuishi wanachanganyikiwa maana
hawana mbadala
Akieleza
mikakati ya Kanisa lake amesema wao wameamua kuisaidia serikali badala
ya kuilaumu kwa kuwaelimisha waumini wao masuala ya uchumi katika
ufalme wa Mungu kwa kutumia Neno la Mungu, pamoja na kuwahamasisha juu
ya umuhimu wa kujiajiri ili waweze kuwaajiri wengine.
Akijitolea
mfano yeye alisema kabla hajaanza kumtumikia Mungu alijiajiri kwa
kufungua biashara ambapo miaka hivi sasa anao wafanyakazi wasiopungua
mia moja wanaofanyakazi katika biashara zake hivyo amekua msaada kwa
serikali kwa kuipunguzia kero ya ajira kwani ameajiri na analipa kodi
serikalini hivyo amekua Baraka kwa nchi.
Mbali
na hilo amekuwa na mkakati wa kuwahamasisha wale aliowaajiri
kutojisahahu badala yake nao wafungue biashara zao nao waweze kuajiri
watu wengine kwani ifikie hatua tuipunguzie mzigo serikali badala ya
kuilaumu.
Amekemea
tabia ya baadhi ya watumishi pamoja na waumini kuilaumu serikali kwa
kusema eti inasababisha hali ngumu jambo ambalo amesema si kweli kwani
mazingira ya sasa karibu nchi zote zimekwama ni wakati wa Kanisa
kuisaidia serikali kwa kuwafundisha waumini Neno la Mungu kwa usahihi
pamoja na kuwasaidia kujiajiri badala ya kutumia muda mwingi kuilaumu
serikali jambo ambalo si sahihi.
Tangu
mwaka 2012 Kanisa la Akuzamu chini ya kiongozi wake Mchungaji Edward
Amri limeanzisha kampeni kabambe kuisaidia serikali kwa kuiombea pamoja
na kuwahamasisha waumini wake kujiajiri na kuwaajiri wale ambao bado
hawana ajira ambapo pia limekuwa likitoa mafundisho ya uchumi kila siku
katika ukumbi wa IPS Jijini Dar es salaam na kila mwezi, ambapo mwezi
ujao linatarajia kuendesha semina kubwa itakayofanyika katika ukumbi
wa Nadd’s ulioko salender bridge jijini Dar es salaam tarehe ishirini
na tano mwezi ujao ambapo wengi wamekuwa wakihudhuria na mara baada ya
mafundisho wengi wamebadilika katika ufahamu wao na wameanza kuchukua
hatua ya kujiajiri.
Subscribe to:
Posts (Atom)