Mwakilishi
mkuu wa Shirika la Kimataifa la ushirikiano wa kimaendeleo la Japan
(JICA) Bw. Yukihinde Katsuta akitoa maelezo juu ya ukamilishwaji wa
mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini Tanzania uliofadhiliwa na serikali ya Japan kwa lengo la kupunguza maambukizi ya VVU sanjari na usambazaji
wa vifaa vya kupimia maambukizi hayo na kuahidi kuendeleza ushirikiano
na serikali ya Tanzania katika utoaji wa vifaa vya kutolea huduma za
afya.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akimkabidhi Zawadi iliyoandaliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii mwakilishi mkuu wa JICA wakati wa hafla fupi ya ukamilishaji wa
mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini uliofadhiliwa na serikali ya Japan jijini Dar es salaam.
Baadhi ya watendaji wa wizara ya afya na wawakili kutoka Shirika la
kimataifa la maendeleo la Japan (JICA) wakifuatilia taarifa mbalimbali
zilizokuwa zinatolewa wakati wa hafla fupi ya ukamilishaji wa mradi wa
kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini uliofadhiliwa na serikali ya Japan jijini Dar es salaam.
Katibu
mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni
akizungumza watendaji wa Wizara hiyo na wawakilishi wa Shirika la
Kimataifa la ushirikiano wa kimaendeleo la Japan (JICA) wakati wa hafla
fupi ya ukamilishaji wa mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya
Ukimwi nchini ulioanza mwaka 2009 chini ya ufaufadhili wa serikali ya Japan, jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment