wanamuziki Mafumu Bilali, Anania Ngoliga na Hamza kalala,
John Kitime leo walikaribishwa na uongozi wa Mashujaa Band katika ukumbi wao wa nyumbani
kule Vinginguti ili kusikiliza nyimbo mpya za Mashujaa Band. kwa lengo la kupata ushauri toka kwa wapenzi na waalikwa kuhusu nyimbo zao mbili
mpya. Ushauri ulitoka mwingi toka kwa viongozi mbalimbali wa bendi na
wapenzi waliokuwa wameruhusiwa kuingia na kusikiliza nyimbo hizo.
Baada ya utambulisho wa shughuli toka kwa Chalz Baba, Mashujaa Band ilileta show yao mpya
Baada ya show nyimbo ya kwanza ambayo ni utunzi wa Chalz Baba iliyoenda kwa jina la Kidole Risasi
ilipigwa. Maoni baada ya wimbo yalihusu urefu wa wimbo, ambao
ulionekana kutokana na uwingi wa waimbaji katika bendi na wote kuwa na
vipande vya kutuma katika wimbo, hivyo kuufanya wimbo uwe mrefu sana.
Jingine lilikuwa ni kugundua kuwa wapiga magita walikuwa wakipiga bila
ya kutyuni magitaa. Kulikuweko na mawazo kuhusu uchezaji wa show, ambapo
wengi walikubaliana kuwa show ilikuwa safi katika onyesho hilo tofauti
na kawaida katika madansi mengine. Pia ulitolewa ushauri kuwa mafundi
mitambo walikuwa hawajiipatia kazi yao ya kurekibisha vyombo sawasawa.
Mpiga tumba na wale mabingwa wa kurap waliambiwa waongeze ubunifu.
Wacheza Shoo wa Bendi hiyo, Rose Masaki (kushoto) na Sweety Baby wakiongoza wenzao kuteka mashabiki waliofulika usiku wa jumanne kwenda jumatano.
Wakurugenzi wa Bendi hiyo, Mama Sakina wa Pili kushoto, na Mumewe Hosea Hopaje(Maisha) kati ,Mkurugenzi wa Blogu hii na ambaye aliwahi kuwa Meneja Mstaafu wa Bendi hiyo, Shaaban Mpalule(kushoto) na Mdau wa Mziki kutoka Uingereza mzee wa Ulaya(kulia) wakifuatilia kwa makini onyesho hilo
Rais wa Bendi hiyo Kajo Litunguru
Mwanamuziki Mkongwe Mafumo Bombenga na Mkewe wakifuatilia kwa makini
Rais Mstaafu wa Bendi hiyo, Mwimbaji Nguli , Jembe, Mbishi wa Maisha asiyeogopa Vita(Jado Fid) kulia na Pasia Budansi Kengere
Makamu wa Rais wa Bendi hiyo Charlz Baba,
Mwimbaji wa Bendi hiyo, Raja Radha mbele na Masooud
Rapa wa Bendi hiyo 33 akiwa wenzake
Mpiga Gitaa Bes(Profa)
Kutoka kulia, Jado Fid, Pasia Budansi, Charz Baba, na Masoud
Mpiga Kinanda wa Bendi hiyo Fredy Manzaka
Mpiga Gitaa la Solo Amosi Mkono wa Nabii
Mpiga Ngoma(Dram) Sele Kadanser
Mwimbaji wa Bendi hiyo Masoud
Wacheza Shoo wa Kike na wa Kiume wakichuana vikali