TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, August 20, 2013

PEPSI YATINGISHA JIJI LA MWANZA- MICHUANO YA MAYOR'S CUP GUMZO

 Mkurugenzi Mkuu wa Pepsi Mwanza, Nico Coetzer, akifuatilia kwa makini Fainal ya Michuano hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Pepsi Mwanza, Nico Coetzer, akifuatilia kwa makini Fainal ya Michuano hiyo huku akijipongeza na moja ya Kinywaji cha Kampuni
 Baadhi ya Wasanii Chipukizi wa jiji la Mwanza, wakitoa Burudani wakati wa Fainali hizo.
 Wakazi na Mashabiki wa JIJI la Mwanza, wakishangaa Jambo, wakati wa Fainali hizo
 Zawadi ya Mshindi wa Kwanza(BAJAJI) ikiwa mbele ya Viongozi(Wageni Rasmi) wakati wa Fainali hizo, Kulia ni Mkurugenzi wa May Way Entertainment, Waandaaji wa Michuano hiyo, Poul Mganga,
 Meneja Masoko wa Kampuni ya Vinywaji Baridi, PEPSI TANZANIA-MWANZA, Sameer Joqlekar, (kushoto) na Mkurugenzi wa May Way Entertainment, Poul Mganga, wakibadilishana jambo wakati Fainali hizo Zikiendelea Uwanja wa Nyamagana.
 Mkurugenzi wa May Way Entertainment, Poul Mganga, Muda mfupi baada ya kukabidhi Zawadi ya Mshindi wa Kwanza kwa Maafisa Utamaduni na wakuu wa Halmashauri ya Nyamagana, kama zawadi ya Fainali ya Michuano hiyo iliyofanyika  Uwanja wa Nyamagana.
 Baadhi ya Mameya wa Nyamagana, Kagera, Mbeya, Ilala, Arusha, Muda Mfupi kabla ya Kukabidhi Zawadi za Washindi
 Zawadi za Washindi wa Fainali ya Michuano hiyo zikiwa Mezani wakati Mchezo wa Fainali Ukiendelea.
 Mmoja wa Waratibu kutoka Halmashauri ya jiji, Joseph Mlinzi(kushoto) na Mkurugenzi wa May Way Entertainment, Poul Mganga, kulia ni  MC wa Fainali hizo.
 Mgeni Rasmi wa Fainali ya Michuano ya PEPSI Mayor's Cup, Stanlaus Mabula, akiinua juu kitita cha Fedha, ambazo ni Zawadi za Washindi wa Michuano hiyo.
 Mgeni Rasmi wa Fainali ya Michuano ya PEPSI Mayor's Cup, Stanlaus Mabula,akihesabu kwa Mafungu zawadi za wachezaji na washindi wa kwanza.
Mchezaji wa Timu ya Polisi(Captain), Ismail Juma, akionyesha juu Kikombe cha Washindi wa tatu baada ya Kutwa Ubingwa wa PEPSI Mayor's Cup katika Uwanja wa Nyamagana
Baadhi ya Wachezaji wa Timu ya Polisi, washindi wa Pili wa Michuano hiyo wakipita kupokea zawadi.
Wakazi wa jiji la Mwanza, wakishuhudia Fainal hizo
Mgeni Rasmi wa Fainali ya Michuano ya PEPSI Mayor's Cup, Stanlaus Mabula,akiwa na Fungu la zawadi za wachezaji na washindi .
Mayor wa Ilala, Jerry Slaa(kati) akielekeza jambo wakati wa kugawa zawadi kwa washindi
Wachezaji wa Timu ya Polisii, washindi wa pili wakivalishwa Medali na mmoja wa wageni waalikwa
Wachezaji wa Timu ya Polisi, washindi wa pili wakivalishwa Medali na mmoja wa wageni waalikwa
Mfungaji Bora wa michuano hiyo, akionyesha kitita cha shilingi laki moja alizokabidhiwa.
Washindi wa tatu timu ya Polisi wakipokea kati ya zawadi ya Furana kutoka kampuni ya DUME.
Mabingwa wa michuano ya PEPSI Mayor's Cup, Timu ya Mkoalani, wakipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa wadhamini wa Michuano hiyo, Pepsi, Vodacom na DUME
Timu capt wa Timu yaMkolani, akipokea zawadi mbalimbali ya Fedha Taslim, Kombe kama zawadi za washindi wa Kwanza wa Michuano hiyo



Mabingwa wa Michuano ya PEPSI Mayor's Cup, timu ya ISAMILO, wakipokea zawadi  na Vikombe
Nyota wa Muziki Kizazi kipya, Kala Jeremihar, akipagawisha mashabiki waliofurika katika Uwanja wa Nyamagana kushuhudia Fainali hzo.
Baadhi ya wachezaji wa Isamilo muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi, wakionyesha furaha yao.
Mayor wa Nyamagana, Stanlaus Mabula, akizungumza na Vyombo vya habari muda mfupi baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa Fainali hizo.
Askari Polisi wakiwa katika hekaheka za kutuliza purukushani kutoka kwa mashabiki waliofurika uwanjani hapo

Baadhi ya wadau wa Soka, akiwemo Mh. Mbunge jimbo la Lorya, Akairo Lameck(kulia), wengine ni Mameya wa majiji
Wageni mbalimbali wakijiandaa kugawa zawadi
Mashabiki wakifuatilia kila jambo uwanjani hapo


Mkurugenzi Mkuu wa PEPSI Nico Coetzer, akipunga mkono kwa  Mashabiki muda mfupi kabla ya kukabidhi zawadi
Msemaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Joseph Mlinzi, akifafanua jambo
Mwakilishi wa Vodacom Mwanza, akifafanua jambo, Vodacom walikuwa ni kati ya wadhamini wa Michuano hiyo.
Mwakilishi wa DUME Condom, akifafanua jambo, Dume ilikuwa ni kati ya wadhamini

Hapa anampongeza kabla ya kumkabidhi zawadi
Meya wa Manspaa ya ILALA, Jerry Slaa, akikabidhi zawadi kwa Captain wa timu ya Polisi, washindi wa Tatu zawadi ya Kombe
Fainali za Michuano ya PEPSI Mayor's Cup, imemalizika jijini Mwanza huku ikiwa imeacha Gumzo kwa wakazi wa jiji hilo pia ikiwa ni Elimu tosha kwa wapenda soka kutokana na Jinsi ilivyoweza kuandaliwa vizuri  na Kampuni ya May Way Entertainment ya jijini Dar es Salaam.
Katika michuano 

ikiwa ni katika jitihada za  kukuza michezo miongoni mwa vijana na maendeleo ya Jiji la Mwanza kwa kujenga mahusiano mazuri kati ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza na wananchi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hapa nchini, Meya wa Jiji la Mwanza Mstahiki Stanslaus Mabula, akiongea mara tu baada ya fainali hizo jijini Mwanza  alisema kuwa , “waliamua kuanzisha michuano hiyo rasmi kama mashindano ya 2013 MWANZA PEPSI MAYOR CUP na timu zilizoshinda zimepatiwa zawadi bila ubabaishaji wa aina yoyote,  zawadi nono ambazo haijawahi kutolewa kwenye mashindano kama hayo hiyo ikiwa ni chachu kubwa ya mashindano hayo ya kipekee”. “Hili ni tukio la kipekee la kila mwaka ili kuwainua vijana”. Alisema Meya.


Mashindano ya mpira wa miguu na netball kombe la Meya wa Jiji la Mwanza Mstahiki Stanlaus Mabula, yamelindima kuanzia Jumamosi tarehe 15 Mwezi June katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. na kuendelea hadi Jumapili ya tarehe 16 June katika viwanja vya Nyamagana, Nyegezi Kona na Mabatini Polisi kila mwisho wa wiki kwa mzunguko wa kwanza,  robo fainali na fainali zilimalizika katika uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.


Akiongea jijini Mwanza pia Mratibu wa mashindano hayo na Mkurugenzi wa MyWay Entertainment Paul Mganga, alisema, “Tumeamua kuanzisha mashindano haya ya 2013 PEPSI MAYOR CUP kukishirikiana na Halmashauri ya Jiji la Mwanza ili kuwakutanisha pamoja vijana mbalimbali Jijini hapa kupitia michezo na kuwawezesha kuwa na vikundi vya ujasiliamali ili kuondokana na umaskini hali kadhalika vishawishi vya mienendo mibaya kwa kuanzisha miradi nakujiunga na saccoss za taasisi mbalimbali.


Mganga alisema, “Mashindano hayo yalihusisha timu 18 kutoka kata 12 za wilaya ya Nyamagana na timu 6 kutoka Polisi Jamii, Mafundi Gereji, Machinga, Jiji, wanahabari na waendesha Bodaboda zote za Jijini Mwanza. Mashindano ya 2013 PEPSI MAYOR CUP yalijumuisha timu za mpira wa miguu na netball za Jijini Mwanza”.


Vilevile ametoa wito wa dhati kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, mashirika na wadau mbalimbali wa michezo na wananchi wa Jiji la Mwanza kwa ujumla kuzidi kujitokeza kwa wingi na kuonyesha ushirikiano wa karibu ili katika kufanikisha mashindano hayo kuwa yenye tija na endelevu.


"Tumejipanga vizuri katika kufanikisha mashindano haya makubwa ya 2013 MWANZA PEPSI MAYOR CUP kila mwaka chini ya udhamini mnono wa kampuni ya soda ya PEPSI, tukishirikiana kwa ukaribu na Halmashauri ya Jiji la Mwanza" alisema Mganga


MyWay Entertainment ndio waandaaji wa mashindano hayo kwa udhamini mnono wa PEPSI, Kilimanjaro Premium Beer, Vodacom, Barmedas TV, Dume Condoms na Mwanza City FM pamoja na Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania ambao ni wadhamini kupitia Tovuti ya Mtandao wa .www.missdemokrasia.blogspot.com, pamoja na Blogs ya . www.shaabanmpalule.blogspot.com

-END-