TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, August 20, 2013

Matukio katika Picha na taswira yetu kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2015

 Halii ni hatari sana na ni chanzo cha ajali za barabarani, Baadhi ya wafanyabiashara wakitoka kufanya biashara za Mitumba katika Vijiji vya Mkoa wa Shinyanga
 Pamoja na Ahadi nyingi kutoka kwa viongozi wetu, ususani wakati wa kuomba kura wakati wa Uchaguzi, tatizo kubwa linazidi kuwa Maji  kwenye maeneo mengi ya Vijiji, Vijana wakichota maji kwa ajili ya matumizi ya kila siku katika vijiji vya mkoa wa Tabora.
 Ajali nyingi usababishwa na ukaidi ama uzembe wa Madereva, pichani baadhi ya wafanya biashara wa Vijiji vya Mkoa wa Shinyanga wakitoka katika biashara zao za Mitumba Gulioni(MNADA)
 Baada ya Kumalizika Ujenzi wa Barabara ya Mkoa Shinyanga kwenda Mwanza, Hali si shwari kwa Watumiaji wa Barabara hiyo ususani Madereva wa Magari Makubwa yakiwemo Mabasi ya Abiria, Tatizo la Uchakachuaji ni chanzo kinachosadikiwa kuifanya Barabara hiyo kutokuwa bora na ya Ufanisi.
 Wakati Mwingine Magari ya Abiria mabasi upata ajali kutokana na kwenda Safari zao kwa Mashindano, kama walivyoonekana Madereva wa Barabara itokayo Singida kwenda Tabora.
 Wakati Tanzania ikielekea Uchaguzi Mkuu wa Viongozi  2015, Vijana nwengi wameendelea kukumbwa na Tatizo la Ajira, pamoja na ahadi nyingi kutoka kwa Viongozi Maisha Bora kwa Kila Mtanzania.
 Tatizo la Vijana wengi kutoka Vijijini kukimbia mijini linazidi kuongezeka, hiyo ikitokana na uwepo wa Maisha magumu Vijijini, ambapo wameamua kwenda Mijini ili kufanya Biashara na kuwaacha sasa Watoto wadogo wakiendelea kujikongoja na aina mbali mbali za Biashara, kitendo kinachozidi kudidimiza Elimu ya Tanzania( kwa watoto kujiingiza katika soko la Biashara na kukimbia Masomo Darasani).
 Maisha ya Kina mama wakazi wa vijiji inazidi kuwa tete, ambapo sasa kina mama wamejitokeza kwa wingi kuingia katika soko la kujiajiri na hivyo kusahau hali ya kuendeleza kilimo bora, Maisha ambayo yamesababishwa na udanganyifu wa Viongozi wao wakati wa kuomba kura ili wachaguliwe.
  Maisha ya Kina mama wakazi wa vijiji inazidi kuwa tete, ambapo sasa kina mama wanazidi kuangaikia maji, Maisha ambayo yamesababishwa na udanganyifu wa Viongozi wao wakati wa kuomba kura ili wachaguliwe.
 Maslahi ya Wakulima wa Pamba katika Mkoa wa Shinyanga inazidi kulalamikiwa , ambapo serikali inatakiwa kuingilia kati na kuboresha hali hiyo.ambapo wanaofaidika ni wale wafanyabiashara kubwa ya Pamba kuliko wale wadogo.
Ajali nyingi zinazidi kutokea kutokana na Madereva wengi kutotimia ama kufuata masharti ya barabarani, huku tatizo la usafiri pia likizidi kuvikumba vijiji mbalimbali nchini Tanzania ususani kutoka katika Mikoa kwenda kwenye Vijiji. kama walivyokutwa wakazi hawa wa Mkoa wa Shinyanga.
(Picha Zote kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).

No comments:

Post a Comment