Mkurugenzi Mkuu wa Pepsi Mwanza, Nico Coetzer, akifuatilia kwa makini Fainal ya Michuano hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Pepsi Mwanza, Nico Coetzer, akifuatilia kwa makini Fainal ya Michuano hiyo huku akijipongeza na moja ya Kinywaji cha Kampuni
Baadhi ya Wasanii Chipukizi wa jiji la Mwanza, wakitoa Burudani wakati wa Fainali hizo.
Wakazi na Mashabiki wa JIJI la Mwanza, wakishangaa Jambo, wakati wa Fainali hizo
Zawadi
ya Mshindi wa Kwanza(BAJAJI) ikiwa mbele ya Viongozi(Wageni Rasmi)
wakati wa Fainali hizo, Kulia ni Mkurugenzi wa May Way Entertainment,
Waandaaji wa Michuano hiyo, Poul Mganga,
Meneja
Masoko wa Kampuni ya Vinywaji Baridi, PEPSI TANZANIA-MWANZA, Sameer
Joqlekar, (kushoto) na Mkurugenzi wa May Way Entertainment, Poul Mganga,
wakibadilishana jambo wakati Fainali hizo Zikiendelea Uwanja wa
Nyamagana.
Mkurugenzi
wa May Way Entertainment, Poul Mganga, Muda mfupi baada ya kukabidhi
Zawadi ya Mshindi wa Kwanza kwa Maafisa Utamaduni na wakuu wa
Halmashauri ya Nyamagana, kama zawadi ya Fainali ya Michuano hiyo
iliyofanyika Uwanja wa Nyamagana.
Baadhi ya Mameya wa Nyamagana, Kagera, Mbeya, Ilala, Arusha, Muda Mfupi kabla ya Kukabidhi Zawadi za Washindi
Zawadi za Washindi wa Fainali ya Michuano hiyo zikiwa Mezani wakati Mchezo wa Fainali Ukiendelea.
Mmoja
wa Waratibu kutoka Halmashauri ya jiji, Joseph Mlinzi(kushoto) na
Mkurugenzi wa May Way Entertainment, Poul Mganga, kulia ni MC wa
Fainali hizo.
Mgeni
Rasmi wa Fainali ya Michuano ya PEPSI Mayor's Cup, Stanlaus Mabula,
akiinua juu kitita cha Fedha, ambazo ni Zawadi za Washindi wa Michuano
hiyo.
Mgeni
Rasmi wa Fainali ya Michuano ya PEPSI Mayor's Cup, Stanlaus
Mabula,akihesabu kwa Mafungu zawadi za wachezaji na washindi wa kwanza.
Mchezaji
wa Timu ya Polisi(Captain), Ismail Juma, akionyesha juu Kikombe cha
Washindi wa tatu baada ya Kutwa Ubingwa wa PEPSI Mayor's Cup katika
Uwanja wa Nyamagana
Baadhi ya Wachezaji wa Timu ya Polisi, washindi wa Pili wa Michuano hiyo wakipita kupokea zawadi.
Wakazi wa jiji la Mwanza, wakishuhudia Fainal hizo
Mgeni Rasmi wa
Fainali ya Michuano ya PEPSI Mayor's Cup, Stanlaus Mabula,akiwa na Fungu la zawadi za wachezaji na washindi .
Mayor wa Ilala, Jerry Slaa(kati) akielekeza jambo wakati wa kugawa zawadi kwa washindi
Wachezaji wa Timu ya Polisii, washindi wa pili wakivalishwa Medali na mmoja wa wageni waalikwa
Wachezaji wa Timu ya Polisi, washindi wa pili wakivalishwa Medali na mmoja wa wageni waalikwa
Mfungaji Bora wa michuano hiyo, akionyesha kitita cha shilingi laki moja alizokabidhiwa.
Washindi wa tatu timu ya Polisi wakipokea kati ya zawadi ya Furana kutoka kampuni ya DUME.
Mabingwa
wa michuano ya PEPSI Mayor's Cup, Timu ya Mkoalani, wakipokea zawadi
mbalimbali kutoka kwa wadhamini wa Michuano hiyo, Pepsi, Vodacom na DUME
Timu
capt wa Timu yaMkolani, akipokea zawadi mbalimbali ya Fedha Taslim,
Kombe kama zawadi za washindi wa Kwanza wa Michuano hiyo
Mabingwa wa Michuano ya PEPSI Mayor's Cup, timu ya ISAMILO, wakipokea zawadi na Vikombe
Nyota
wa Muziki Kizazi kipya, Kala Jeremihar, akipagawisha mashabiki
waliofurika katika Uwanja wa Nyamagana kushuhudia Fainali hzo.
Baadhi ya wachezaji wa Isamilo muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi, wakionyesha furaha yao.
Mayor wa
Nyamagana, Stanlaus Mabula, akizungumza na Vyombo vya habari muda mfupi
baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa Fainali hizo.
Askari Polisi wakiwa katika hekaheka za kutuliza purukushani kutoka kwa mashabiki waliofurika uwanjani hapo
Baadhi ya wadau wa Soka, akiwemo Mh. Mbunge jimbo la Lorya, Akairo Lameck(kulia), wengine ni Mameya wa majiji
Wageni mbalimbali wakijiandaa kugawa zawadi
Mashabiki wakifuatilia kila jambo uwanjani hapo
Mkurugenzi Mkuu wa PEPSI Nico Coetzer, akipunga mkono kwa Mashabiki muda mfupi kabla ya kukabidhi zawadi
Msemaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Joseph Mlinzi, akifafanua jambo
Mwakilishi wa Vodacom Mwanza, akifafanua jambo, Vodacom walikuwa ni kati ya wadhamini wa Michuano hiyo.
Mwakilishi wa DUME Condom, akifafanua jambo, Dume ilikuwa ni kati ya wadhamini
Hapa anampongeza kabla ya kumkabidhi zawadi
Meya wa Manspaa ya ILALA, Jerry Slaa, akikabidhi zawadi kwa Captain wa timu ya Polisi, washindi wa Tatu zawadi ya Kombe
Fainali
za Michuano ya PEPSI Mayor's Cup, imemalizika jijini Mwanza huku ikiwa
imeacha Gumzo kwa wakazi wa jiji hilo pia ikiwa ni Elimu tosha kwa
wapenda soka kutokana na Jinsi ilivyoweza kuandaliwa vizuri na Kampuni
ya May Way Entertainment ya jijini Dar es Salaam.
Katika michuano
ikiwa ni katika jitihada za kukuza michezo miongoni
mwa vijana na maendeleo ya Jiji la Mwanza kwa kujenga mahusiano mazuri kati ya Halmashauri
ya Jiji la Mwanza na wananchi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hapa nchini, Meya wa Jiji la Mwanza Mstahiki
Stanslaus Mabula, akiongea mara tu baada ya fainali hizo jijini Mwanza alisema kuwa , “waliamua kuanzisha michuano hiyo rasmi kama mashindano ya
2013 MWANZA PEPSI MAYOR CUP na timu zilizoshinda zimepatiwa zawadi bila ubabaishaji wa aina yoyote, zawadi nono
ambazo haijawahi kutolewa kwenye mashindano kama hayo hiyo ikiwa ni chachu kubwa
ya mashindano hayo ya kipekee”. “Hili ni tukio la kipekee la kila mwaka ili
kuwainua vijana”. Alisema Meya.
Mashindano ya mpira wa miguu na netball kombe la
Meya wa Jiji la Mwanza Mstahiki Stanlaus Mabula, yamelindima kuanzia
Jumamosi tarehe 15 Mwezi June katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
na kuendelea hadi Jumapili ya tarehe 16 June katika viwanja vya Nyamagana,
Nyegezi Kona na Mabatini Polisi kila mwisho wa wiki kwa mzunguko wa kwanza, robo fainali na fainali zilimalizika katika
uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
Akiongea jijini Mwanza pia Mratibu wa
mashindano hayo na Mkurugenzi wa MyWay Entertainment Paul Mganga, alisema,
“Tumeamua kuanzisha mashindano haya ya 2013 PEPSI MAYOR CUP kukishirikiana na Halmashauri ya Jiji la Mwanza ili kuwakutanisha pamoja vijana
mbalimbali Jijini hapa kupitia michezo na kuwawezesha kuwa na vikundi vya
ujasiliamali ili kuondokana na umaskini hali kadhalika vishawishi vya mienendo
mibaya kwa kuanzisha miradi nakujiunga na saccoss za taasisi mbalimbali.
Mganga alisema, “Mashindano hayo yalihusisha timu
18 kutoka kata 12 za wilaya ya Nyamagana na timu 6 kutoka Polisi Jamii, Mafundi
Gereji, Machinga, Jiji, wanahabari na waendesha Bodaboda zote za Jijini Mwanza.
Mashindano ya 2013 PEPSI MAYOR CUP yalijumuisha timu za mpira wa miguu na
netball za Jijini Mwanza”.
Vilevile ametoa wito wa dhati kwa Halmashauri ya
Jiji la Mwanza, mashirika na wadau mbalimbali wa michezo na wananchi wa Jiji la
Mwanza kwa ujumla kuzidi kujitokeza kwa wingi na kuonyesha ushirikiano wa karibu ili
katika kufanikisha mashindano hayo kuwa yenye tija na endelevu.
"Tumejipanga vizuri katika kufanikisha mashindano
haya makubwa ya 2013 MWANZA
PEPSI MAYOR CUP kila mwaka chini ya udhamini mnono wa kampuni ya soda ya PEPSI,
tukishirikiana kwa ukaribu na Halmashauri ya Jiji la Mwanza" alisema Mganga
MyWay
Entertainment ndio waandaaji wa mashindano
hayo kwa udhamini mnono wa PEPSI, Kilimanjaro Premium Beer, Vodacom,
Barmedas
TV, Dume Condoms na Mwanza City FM pamoja na Kampuni ya Miss Demokrasia
Tanzania ambao ni wadhamini kupitia Tovuti ya Mtandao wa
.www.missdemokrasia.blogspot.com, pamoja na Blogs ya .
www.shaabanmpalule.blogspot.com
-END-
No comments:
Post a Comment