BAO
pekee la kiungo mtata wa Wekundu wa Msimbazi, Simba sc, Amri Ramadhan
Kiemba limetosha kuibuka na pointi 3 muhimu za kwanza usiku jana katika
mechi yao ya kwanza kombe la Mapinduzi 2014 iliyoanza kutimua vumbi leo
hii viwanja viwili vya Amaan, Unguja na Gombani, Pemba.
Mgeni
rasmi katika mchezo huo alikuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Italia,
Cesare Prandelli ambaye alikagua timu zote na kwenda katikati ya dimba
la Amaan na kuudunda mpira ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa michuano ya
mwaka huu.
Mchezo
huo wa kundi B ulioanza majira ya saa 2:00 usiku ndio uliochaguliwa
kuwa wa ufunguzi katika michuano ya mwaka huu ambayo ni maalumu
kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
|
Amri Kiemba amewaliza AFC Leopard
|
Fundi
Kiemba aliyeanzia benchi leo hii na kuingia dakika ya 47 kuchukua
nafasi ya Kiungo mpya wa Simba aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar dirisha
dogo mwaka jana, Awadh Juma Issa, alifunga bao hilo baada ya kuuwahi
mpira uliookolewa na beki wa AFC Leopard kufuatia Amisi Tambwe kujaribu
kuunganisha krosi maridadi uliochongwa na Ramadhan Singano `Messi`
dakika ya 77 ya mchezo.
`Messi`
huyu mtoto ni nuksi tupu!, alifanya vitu vyake vya Nani Mtani Jembe
baada ya kumlamba chenga ya aibu beki mrefu zaidi na mkongwe, Joseph
Shikokoti na kupiga krosi iliyosababisha bao hilo muhimu.
Ushindi
wa leo kwa Simba sc umewapatia nguvu zaidi katika harakati zao za
kuusaka ubingwa ambao kwa mara ya mwisho kuutwaa ni mwaka 2011.
Kwasasa Azam fc ndio mabingwa watetezi mara mbili mfululizo, yaani walitwaa `ndoo` hiyo 2012 na 2013.
Hata
hivyo imekuwa neema kwa kocha msaidizi wa Simba, Suleiman Matola `Veron`
ambaye alisimama kwenye benchi la ufundi wakati akimsubiri bosi wake
Mcroatia, Zdravko Logarusic ambaye atawasili kesho Zanzibar.
Mechi
ya leo ilijigawa kwa timu zote kwani Leopard walicheza vizuri dakika 45
za kwanza, lakini Simba SC walichachamaa kipindi cha pili na kucheza
soka safi, lakini kukosa umakini kwa washambuliaji wa klabu hiyo
kumewanyima ushindi mnono.
Simba
sasa wanashika nafasi ya pili kundi B wakijikusanyia pointi tatu sawa
na KCC ya Uganda wenye pointi 3, lakini wao wanawastani mzuri wa mabao
ya kufunga.
Kikosi
cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Haruna Shamte, Issa Rid, Joseph
Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Ramadhani
Chombo/Uhuru Suleiman dk89, Amisi Tambwe/Betram Mombeki dk81, Ramadhan
Singano, Awadhi Juma/Amri Kiemba dk47.
AFC
Leopard; Martin Masalia, Etenesy Augustin, Abdallah Juma, Saleh Jackson,
Joseph Shikokoti, Imbalebala Martin, Okwemba Charles, Mussa Mude, Kelly
Jacb, Mang’ole Benard/Seda Edwin dk86 na Oscar Kadenge/Hassan Mohamed
dk86.
Awali
katika dimba hilo, mabingwa wa Zanzibar KMKM walilala kwa mabao 3-2
dhidi ya KCC kutoka nchini Uganda katika mchezo wa Kundi A.
Mabao
ya KCC yalifungwa na Herman Waswa dakika ya 10, Tony Odur katika dakika
ya 20 na William Waoro dakika ya 82, wakati ya KMKM yalifungwa na
Hamisi Ali dakika ya saba na Maulid Ibrahim dakika ya 79.
Huko uwanja wa Gombani, Pemba, vijana wa Juma Mwabusi, Mbeya City wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Clove Stars.
Bao la Mbeya City lilifungwa dakika ya 13 na Deus Kaseke, lakini dakika ya 24 kipindi hicho cha kwanza, Clove Stars.