Na Kiza Sungura-MAELEZO
Wakazi
wa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wanakusudia kuanzisha Kituo cha Redio
ya kijamii kwa ajili ya kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii na
shughuli nyingine za maendeleo katika eneo hilo ili kuongeza kipato kwa
wananchi wake na taifa kwa ujumla.
Kauli
hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya
Mandalizi ya Harambee ya uanzishaji wa Redio Rungwe FM Bw. Christopher
Andendekisye wakati akizungumza waandishi wa habari .
Alisema
kuwa Mkoa wa Mbeya na husasani Wilaya ya Rungwe inavyo vivutio vingi
ambavyo kwa sababu ya kukosa chombo cha mawasiliano kama vile Redio
vimekuwa havifahamiki kwa wananchi wengi wan je ya Wilaya hiyo na hivyo
kuikosesha Serikali mapato ambayo yangetokana na sekta ya utalii.
Bw.
Andendekisye alisema kuwa kutokana na changamoto mbalimbali
zinazoikabili Wilaya Rungwe, Uongozi wa Christian na Gospel Ministry
umeamua kuanzisha mchakato wa usajili Redio inayoitwa Rungwe FM, ikiwa
ni Redio ya kijamii kwa ajili ya kuhamasisha shughuli mbalimbali za
kiuchumi, kijamii na kisiasa ndani ya Wilaya ya Rungwe.
Alisema
Redio hii tayari ipo katika orodha ya redio zilizoomba usajili wa
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [TCRA], imesajiliwa mwezi septemba mwaka
2013.
Kufuatia
hali hiyo Bw. Andendekisye aliwaomba wananchi na wakazi wa Wilaya ya
Rungwe kusaidia upatikanaji wa shilingi milioni 170 zinahitaji
kukamilisha ununuzi wa vifaa vitakavyosaidia uanzishwaji wa redio hiyo
mapema.
Aliongeza
kuwa hadi hivi sasa wameshapata ahadi ya shilingi milioni 92 na
kuongeza kuwa ili kumalisha kiwango chote wanatarajia kufanya harambee
mwezi Machi 2014 katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Bw.
Andendekisye alisema kuwa kwa mwananchi atakayehitaji kuwachangia
anaweza kutuma fedha zake kupitia akaunti 038201043087 Tukuyu Christian
Fellowship –NBC Bank
No comments:
Post a Comment