TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Saturday, May 26, 2012
ICD yazindua mtandao wa taarifa kuhusu walemavu
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Habari Kuhusu Ulemavu nchini
Tanzania (ICD), Fredrick Mkatambo akizungumza na wageni waalikwa katika
hafla hiyo. Kushoto ni Kamishna kutoka Wizara ya Ustawi wa Jamii,
Danford Makala aliyekuwa mgeni.
Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa ICD wakiwa katika hafla hiyo
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa ICD mara baada ya uzinduzi.
KITUO cha Habari Kuhusu Ulemavu (ICD) nchini Tanzania kimezindua mtandao (Blogu) ambayo itakuwa ikikusanya taarifa mbalimbali kuhusiana na masuala ya walemavu na kuziweka katika mtandao huo ili wadau anuai waweze kujua taarifa hizo.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika hafla ya
uzinduzi wa mtandao huo ambao utakuwa ukisimamiwa na ICD, Mkurugenzi Mtendaji
wa kituo hicho, Fredrick Mkatambo amesema kwa muda mrefu imekuwa ni vigumu kupata
taarifa zote juu ya masuala ya walemavu jambo ambalo ni moja ya vikwazo.
Alisema kuanzishwa kwa mtandao huo utasaidia wadau wa
masuala ya walemavu ikiwemo Serikali kuingia na kupata taarifa mbalimbali
zikiwemo changamoto inayokumbana nayo jamii hiyo na ikiwezekana wahusika
kuwasaidia kundi hilo.
Aidha alisema “Najua kwa sasa kazi ni ngumu kupata taarifa
muhimu juu ya masuala mbalimbali ya ulemavu…lakini naamini kwa sasa itakuwa ni
rahisi maana tunasehemu ambayo unaweza kupata taarifa zote muhimu juu ya
walemavu,” alisema Mkurugenzi.
Akifafanua namna mtandao huo utakavyokuwa ukifanya kazi,
Mshauri wa Kiufundi kutoka kituo cha ICD, Natalia Lintner alisema katika blogu
hiyo walemavu wanaweza kupata taarifa mbalimbali zinazowagusa kama
ufadhili wa masomo, vyuo vikuu rafiki wa walemavu, matangazo muhimu
yanayowagusa walemavu na habari za kawaida kuhusu watu wenye ulemavu.
Alisema taarifa nyingine ambazo zitakuwa zikioneshwa katika
mtandao huo ni mashirika na taasisi mbalimbali zinazofanya kazi na watu wenye
ulemavu na shughuli zake, pamoja na wadau anuai kuwa na uwezo wa kuchangia/kusaidia
walemavu kupitia mtandao huo.
Naye Kamishna kutoka Wizara ya Ustawi wa Jamii, Danford
Makala akizindua mtandao huo pamoja na kitabu cha ‘Maisha Yangu’ ambacho
kimeandaliwa na ICD na wafadhili wengine, alisema mtandao na kitabu hicho
vitakuwa ni vyanzo vizuri vya taarifa kuhusu watu wenye ulemavu.
Alisema mtandao huo ambao ni sawa na jukaa la taarifa kuhusu
watu wenye ulemavu litaisaidia Serikali pia kupata taarifa anuai juu ya masuala
ya watu wenye ulemavu, ambazo zitakuwa chachu ya maboresho ya sera mbalimbali
kila uchao.
“Hii ni njia ambayo watu wenye ulemavu wanaweza kupaza sauti
yao kwa
pamoja…kwa kutumia mtandao huu, tujitokeze kuchangia basi ili kweli mtandao huu
uweze kufanya kazi ipasavya,” alisema Makala.
Kitabu cha maisha yangu ambacho kimezinduliwa pia katika
hafla hiyo kimekusanya mahojiano ya watu wenye ulemavu jijini Dar es Salaam nia
kuainisha changamoto mbalimbali katika maisha yao,
hivyo kuleta picha halisi ya walemavu Tanzania.
*Habari hii imeandaliwa na Mtandao wa Thehabari.com (www.thehabari.com)
VIKUNDI VYA KUWEKA NA KUKOPA VINAVYOSAIDIWA NA TAASISI YA WAMA VYAPEWA SEMINA YA UMUHIMU WA KUJIUNGA NA MFUKO WA BIMA WA AFYA (NHIF)
Tabu Likoko Mkurugenzi wa Idara ya
Uwezeshaji Wanawake katika Taasisi ya (WAMA) akifungua rasmi semina ya
wanawake kutoka vikundi mbalimbali vya kuweka na kukopa vinavyosimamiwa
na Taasisi ya (WAMA) kuhusu huduma za Mfuko wa Bima wa Afya NHIF
inayofanyika kwenye viwanja vya Taasisi ya WAMA asubuhi hii jijini Dar
es salaam kutoka kulia pichani ni Rehani Athumani Mkurugenzi mifuko ya
Afya ya Jamii (CHF), Michael Mhando Mkurugenzi wa Tathmini ya Uhai wa
Mfuko na Utafiti na Eugen Mikongoti Mkurugenzi wa Uendeshaji.
Eugen Mikongoti Mkurugenzi wa Uendeshaji
(NHIF) akizungumza katika semina hiyo jinsi mfuko huo unavyosaidia
jamii kupata matibabu, kulia ni Rehani Athumani Mkurugenzi mifuko ya
Afya ya Jamii (CHF) na katikati ni Michael Mhando Mkurugenzi wa Tathmini
ya Uhai wa Mfuko na Utafiti na
Afisa wa Masoko na Elimu kwa Umma NHIF
Grace Michael akifuatilia mada katika semina hiyo, kushoto ni Philomena
Marijani Afisa Uraghibishi na Mawasiliano Taasisi ya (WAMA).
Rehani Athumani Mkurugenzi mifuko ya
Afya ya Jamii (CHF) akitoa mada mbalimbali juu ya huduma za mfuko wa
bima ya Afya, huku washiriki wa semina hiyo wakimsikiliza kwa makini,
katikati ni Michael Mhando Mkurugenzi wa Tathmini ya Uhai wa Mfuko na
Utafiti na kulia Eugen Mikongoti Mkurugenzi wa Uendeshaji.
Washiriki wa semina hiyo wakiandika
mambo muhimu yaliyojadiliwa katika semina hiyo inayofanyika katika
viwanja vya Taasisi ya (WAMA).
Washiriki wa semina hiyo wakiandika mambo muhimu yaliyojadiliwa katika
semina hiyo inayofanyika katika viwanja vya Taasisi ya (WAMA).
Washiriki wa semina hiyo wakiandika mambo muhimu yaliyojadiliwa katika
semina hiyo inayofanyika katika viwanja vya Taasisi ya (WAMA).
Tabu Likoko Mkurugenzi wa Idara ya
Uwezeshaji Wanawake katika Taasisi ya (WAMA) kulia na Philomena Marijani
Afisa Uraghibishi na Mawasiliano Taasisi ya (WAMA) ambao ndiyo wenyeji
wa wanasemina wakiwa katika semina hiyo.
ZIARA YA NAPE BUKOBA MKOANI KAGERA
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) CCM, Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye akimsalimia Mwenyekiti wa Chama Cha Walemavu wilaya
ya Misenyi mkoani Kagera, Simon Andrea, baada ya kufungua Baraza la
Vijana wa CCM wilaya hiyo, jana, May 25, kwenye Uwanja wa Mashujaa,
wilayani humo. Waliosimama ni baadhi ya viongozi wa CCM na UVCCM
walioshiriki ufunguzi huo.
Nape akiwa ka Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Avelyne Mushi
baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Bukoba, kuanza ziara a kikazi ya
siku moja mkoani Kagera.
Nape akizungumza na viongozi katika Ofisi ya CCM mkoa wa Kagera.
Nape akitoa salam za Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya
Kikwete kwenye msiba wa mtumishi wa siku nyingi waserikali, Balozi, Dk.
Vedasto Kyaruzi, mjini Bukoba, baada ya kwenda kwenye msiba huo wakati
wa kuaga mwili wa marehemu tayari kwa mazishi yaliyofanyika jana mjini
Bukoba.
Nape akikata utepe kuingia kwenye kambi ya Baraza la
Umoja wa Vijana wa CCM, wilaya ya Missenyi mkoani Kagera, kwa ajili ya
kufungua baraza hilo la mwaka.
Vijana wa CCM waliopiga kambi hiyo ya Baraza la Vijana, Missenyi, wakimsikiliza Nape alipowahutubia.
Nape akimkabidhi cheti Kamanda wa Vijana wa CCM mkoa wa
Kagera, Dioniz Malinzi kwa kuwa mmoja wa waliowezesha kambi hiyo ya
Baraza la Vijana kufanyika.
Baadhi ya viongozi kwenye kambi hiyo wakimpungia mkono Nape wakati akiondoka
Mama Asha Bilal akizungumza na Watanzania wanaoishi Botswana
Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal, akiwa katika picha ya pamoja
na Watanzania wanaoishi nchini Botswana baada ya kuzungumza na
Watanzania hao jana jioni mjini Gaborone Botswana.
na Watanzania wanaoishi nchini Botswana baada ya kuzungumza na
Watanzania hao jana jioni mjini Gaborone Botswana.
PICHA NA
VPO.
Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal akizungumza na Watanzania
wanaishi Nchini Botswana jana.
wanaishi Nchini Botswana jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza na Makamu wa Rais wa For Conervation Policy kulia
na Waziri wa Fedha wa Kenya Mhe. Robinson Njeru baada ya kumalizika
kwa mkutano wa siku mbili kwa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu maendeleo
endelevu kwa nchi za bara la Afrika uliomalizika mjini Gaborone
Botswana jana jioni.
Bilal, akizungumza na Makamu wa Rais wa For Conervation Policy kulia
na Waziri wa Fedha wa Kenya Mhe. Robinson Njeru baada ya kumalizika
kwa mkutano wa siku mbili kwa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu maendeleo
endelevu kwa nchi za bara la Afrika uliomalizika mjini Gaborone
Botswana jana jioni.
MBALI NA SHUGHULI ZA CHAMA PIA NAPE AKACHEZA GOFU KWENYE VIWANJA VYA DIONIZ MALINZI
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwasili na ujumbe wake
kwenye Uwanja wa ndege wa Bukoba, kwa ajili ya ziara ya siku moja ya
kikazi mkoani Kagera ambako pamoja na shughuli nyingine alifungua Baraza
la Vijana wa CCM, Wilaya ya Missenyi mkoani humo.
Nape alipata fursa pia kucheza gofu kwenye viwanja vya mchezo huo vya Dioniz Malizni (kulia) nje kidogo ya mji wa Bukoba
RAIS KIKWETE KUFUNGUA MKUTANO WA AFDB AMBAO UTAGARIMU BILIONI 12
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa (AFDB) Bw. Ngosha
Magonya katikati akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini
Arusha.
Baadhi ya wanakamati wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa AFDBwakiwa katika viwanja vya AICC jijini Arusha leo.
NA GLADNESS MUSHI-ARUSHA
Benki ya maendeleo ya
Afrika (AFDB)inatarajia kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 12 katika mkutano
wake unaoanza Jumatatu jijini Arusha na kufunguliwa na Raisi Jakaya Kikwete huku kiasi cha fedha hizo zikitumika kukarabati
Kumbi mbalimbali za jengo la Kimaitaifa la ukumbi wa AICC kwa kuwa baadhi ya
kumbi za jengo hilo zinaonekana kupitwa na wakati kutokana na utandawazi uliopo
kwa sasa ndani ya nchi zilizoendelea
Akizungumza jijini hapa na waandishi wa habari mwenyekiti wa
kamati ya kitaifa ya mkutano wa benki ya AFDB kwa mwaka 2012 Bw Ngosha Magonya ambapo alisema kuwa mkutano huo utakuwa na
faida kubwa sana
Alifafanua kuwa kupitia mkutano huo ambao utaanza Jumatatu ijayo
utakuwa na faida kubwa sana kwa jiji la Arusha kwa kuwa hata kiwango cha uchumi
kitaaimarika sana kwa kuwa wageni mbalimbali kutoka katika maeneo ya nchi
mbalimbali duniani watabadilishana hata uzoefu
“kwa kipindi hiki ambacho kuna mikutano ndani ya jiji la
Arusha tunatarajia kuwepo na utoafuti wa khali ya juu sana hasa katika mchakato
wa uchumi na kwa hali hii pia tunatarajia hata kufanya maendeleo
mbalimbali ikiwemo kufanya marekebisho
kwa jengo la kimataifa la AICC”alisema bw Magonya
Katika hatua nyingine alifafanua kuwa mbali na kuweza kuimarisha
uchumi wa mkoa wa Arusha pia wanatarajia kutumia fursa mbalimbali za
kuhakikisha kuwa wanakutanisha wafanyabiashara mbalimbali huku malengo yakiwa
ni kuendeleza uchumi kwa walengwa.
Pia alifafanua kuwa mbali na kuweza kuwasaidia
wafanyabiashara hao katika michakato ya kukuza uchumi pia benki hiyo ina
mikakati mbalimbali ya kuendeleza barabara ambazo zitaweza kutumika kama njia
ya mawasiliano hapa Tanzania hali ambayo nayo itachangia kwa kiwango kikubwa
sana hata kuimarisha uchumi wa nchi ya Tanzania
Aliongeza kuwa hapo awali benki hiyo ilikuwa imeshajenga
barabara ya Arusha –Namanga kwa sasa ana mpango wa kujenga barabara ya Arusha –
Holile ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro hali ambayo itachangia sana maendeleo hasa
ya mawasiliano
Alimalizia kwa kusema kuwa wafanyabiashara hasa wa mkoa wa
Arusha wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatumia vema fursa za mkutano huo ili
kuweza kuimarisha biashara zao za kila siku.
SERIKALI YATAKIWA KUJENGA VYUO ZAIDI KWA AJILI YA KUTOA WALIMU WA WATOTO WENYE ULEMAVU
MWANDISHI WETU
SERIKALI imetakiwa kujenga Vyuo
vitakavyozalisha walimu wakutosha kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa
‘Viziwiwasiona’.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam leo , na Mwalimu wa
Kitengo cha walemavu katika shule ya Uhuru Mchanganyiko, Anjelica Mtwale wakati
alipokutana Mwakilishi Mkazi wa Shirika la ‘Sense International’ lenye makao
yake makuu nchini Uingereza.
Alisema pungufu huo wa walimu maalum
umetokana na kukosekana kwa vyuo vya kutosha, ambavyo vingesaidia kutoa taaluma
hiyo na kupatikana walimu wengi ambapo wangetumika kutoa elimu kuanzia elimu ya
awali hadi elimu ya juu.
Aidha, Anjelica alisema kutokana na baadhi ya
wazazi kupata mwamko wa kuwapeleka watoto hao shule kwa ajili ya kupata elimu, bado
kitengo chake kinashindwa kumudu kutoa mafunzo kwa kiwango kinachohitaji kutokana na upungufu huo.
“Unajua katika kuwaelimisha watoto hawa yani
Viziwiwasiona kunahitajika walimu wa kutosha kwa kuwa uelimishaji wao ni kwamba
kila mtoto mmoja mwalimu mmoja”alisema Mwalimu Anjelica.
Anjelica alisema katika shule hiyo, kuna
wanafunzi 13 huku walimu wakiwa 8 na walezi wa kujitolea wanne ambapo kwa
utaratibu mzima wa kuwatuza watoto hao hawatoshi.
Akitaja mafanikio tangu kuanzishwa kitengo hicho
mwaka 1994, Anjelika alisema wapo watoto waliofanikiwa kupata elimu ya
sekondari hadi kidato cha pili, kuishia kidato hicho kumetokana na kukosekana
walimu wenye elimu hiyo ya watu maalumu katika shule mbalimbali.
Aidha, Anjelica alitoa shukran kwa shirika la
Sense International kwa kushiriki
katika kutoa misaada mbalimbali ya kielimu na afya kwa watoto hao.
Alisema Shirika hilo limekuwa la kwanza
nchini katika kujishughulisha katika utoaji wa mafunzo kwa walimu wa watu wa
aina hiyo pia limehusika katika kuwapeleka walimu katika mafunzo ndani na nje
ya nchi.
Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika hilo,
Christopher Andendekisye alisema Shirika hilo limekuwa likifanya shughuli zake
kwa kushirikiana na serikali.
Alitoa wito kwa Watanzania kuwafikiria watu
hao kwa huruma kwani ni watu wenye ulemavu wakusikitisha, alisema “Hebu fikiria
mtu huyo haoni hasikii na hawezi kusema hivyo ni wakati kwa baadhi ya taratibu
za upatikanaji wa elimu ya walimu kuekebishwa ili iwe rahisi katika kupatikana
walimu wingi”
Hatimaye Redd's Miss IFM huyu hapa
Redds Miss IFM -Fina Revocatus
katikati akiwa na mshindi wa pili Jane Augustino na mshindi wa tatu
Theresia Issaya wakiwa katika Picha ya Pamoja baada ya kuibuka washindi
katika fainali za Redds Miss Tanzania ngazi ya Vitongoji iliyofanyika
usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar Es
Salaam.Ambapo watashiriki fainali ya ngazi ya kanda ya Dar Es Salaam.
USHINDI WA CHADEMA UBUNGO
MAJIRA - GAZETI HURU LA KILA SIKU:
|
|
- USHINDI WA CHADEMA UBUNGO
- KATUNI
- Kesi ya kupinga matokea zisifunguliwe kwa jazba
- MALALE
- Elimu kwa vijana mwarobaini kupunguza umashini nchini
- MDAU
- Watu wenye ulemavu wasema ya moyoni
- MAISHA
- Shule zilizozofanya vizuri Dar 'tiba' ya kuacha kusomesha nje
- Waziri awakabidhi bendera Twiga Stars
- Kibaha wahitaji fedha kupanua sekta ya afya
- MAOMBII
- Watumishi wa umma kugoma Julai-TUGHE
- Simba kuziba pengo la Mafisango *Wapo Santo, Kasule, Kije, Tegete naye yumo
Subscribe to:
Posts (Atom)