Baadhi
ya washiriki wa warsha ya siku moja iliyoendeshwa na kampuni ya NFT
Consult kwa maofisa rasilimali watu na watoa mafunzo kutoka makampuni
mbalimbali nchini wakifanya usajili kabla ya kuanza kwa warsha hiyo.
Na Mwandishi wetu
MOJA
ya makampuni makubwa yanayoshughulika na ushauri wa jinsi ya kuongeza
ufanisi katika maeneo ya kazi, NFT Consult wameendesha kongamano kubwa
la kutambua haja ya mahitaji ya wadau mbalimbali wa maendeleo hapa
nchini.
Kampuni
hiyo ya kimataifa ambayo imeingia nchini mwaka 2010 ikiwa na matawi
Uganda, Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini imesema
kongamano hilo limelenga kuonesha uwezo wao katika kubadili mifumo ya
utendaji kazi.
Ofisa
Mtendaji wa kampuni hiyo, Badru Ntege amesema kwamba wamekuwa
wakiendesha mafunzo mbalimbali yenye kueleza thamani ya mfanyakazi na
mdau wowote ambapo uthamini wa wadau ndio unaotoa mwanya wa mabadiliko
chanya yanayotakiwa
“Mafanikio
ya eneo lolote lile linatokana na wadau kusikiliza wenzao na kisha
kufanyia kazi kauli za upande wa pili.” Alisema Ntege.
Timu
ya NFT Consult ikijitambulisha kwa washiriki kabla ya kuanza warsha
hiyo. Kutoka kushoto ni Inside Business Partner wa NFT Consult, Aisu
Mori, Client Partner wa NFT Consult, Immaculate Mwaluko, Ofisa Mtendaji
mkuu wa kampuni ya NFT Consult, Badru Ntege, Meneja biashara mkazi wa
NFT Consult/Franklin Covey Tanzania, Joan Ajilong na Client Partner wa
NFT Consult, Sophia Shuma.
Alisema
katika mafunzo ya kuthamini ,kanuni kubwa inayotumika ni kujipanga
katika nafasi husika na kutumia changamoto kama fursa za kubadili
mazingira ya kazi na kazi yenyewe ili kupata matokeo yanayotakiwa.