Aliyekuwa
MNEC wa wilaya ya Ludewa Elizabeth Haule wa pili kushoto enzi za
uhai wake akiwa na viongozi wa wilaya hiyo wakati wa mkutano mkuu
wa wilaya ya Ludewa mwaka jana ,kulia ni mbunge wa jimbo la Ludewa
Deo Filikunjombe ,aliyesimama ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa
Stanley Kolimba na wa kwanza kushoto katibu wa CCM wilaya ya Ludewa
Eliud Semauye .
…………………………………………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu.
CHAMA cha
mapinduzi (CCM) wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kimepata pigo
kubwa kufuatia kifo cha aliyekuwa mjumbe wa Halmashauri kuu ya
wilaya hiyo (NEC) Bi Elizabeth Haule.
Mbali ya kuwa MNEC wa wilaya hiyo Haule pia alikuwa ni mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Ludewa kabla ya kujiuzulu kwake mwezi February mwaka jana baada ya kuchaguliwa nafasi hiyo ya NEC na nafasi hiyo kuwa wazi hadi sasa.
katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Ludewa Felix Haule alisema kuwa kifo cha kionozi huyo kimetokea usiku wa kuamkia leo akiwa katika Hospitali ya wilaya ya Ludewa ambako alilazwa jana mchana kwa tatizo la moyo.
Bw Haule alisema kuwa siku ya jumatatu wiki iliyopita marehemu alipata kuongoza kikao chake cha mwisho cha baraza la vijana la wilaya ya Ludewa na baada ya hapo hali yake ya afya ilianza kuzidi kuwa mbaya zaidi kabla ya kuamua jana kwenda Hospitali ambako walimlaza
Alisema kuwa mazishi ya mjumbe huyo wa NEC wilaya ya Ludewa yanataraji kufanyika kesho kutwa jumamosi kijijini kwake Mholo kata ya Luana wilayani Ludewa .

Kwa
upande wake mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akielezea
kifo cha MNEC huyo alisema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa
taarifa ya kifo hicho na kuwa kwa sasa anafanya maandalizi ya
kuelekea jimboni Ludewa ili kuungana na wana CCM na wananchi wa
wilaya hiyo katika mazishi ya kiongozi huyo.
Marehemu Elizabeth Haule enzi za uhai wake |
Mbunge
Filikunjombe alisema kuwa CCM wilaya ya Ludewa imempoteza kiongozi
mchapa kazi na aliyekuwa na uwezo mkubwa katika kukitumikia chama
ngazi ya wilaya na Taifa na kuwa kati ya vijana ambao wamekuwa
mbele kujenga chama katika wilaya hiyo ni pamoja na marehemu huyo
kwani siku zote za uhai wake alikuwa ni mhumini mzuri wa kunadi
sera za CCM na hakuwa kiongozi mwenye majivuno wala makundi.
Hivyo
alisema kuwa kifo cha MNEC huyo kimekuja huku wilaya ya Ludewa
ikiwa katika maandalizi ya kuanzimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM
sherehe iliyopangwa kufanyika siku ya jumapili ya February 8 mwaka
huu kwa mara ya kwanza katika kata ya Kilondo mwambao mwa ziwa nyasa
lakini kutokana na msiba huo mkubwa sherehe hizo zitasogezwa
mbele hadi Februari 15 mwaka huu.” Mimi pia nilikuwa nikijiandaa kwa ajili ya kuanza safari ya kuelekea wilayani Ludewa katika sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM kama mgeni rasmi ila sitaweza kufanya hivyo na chama kimeamua kusogeza sherehe hizo hadi jumapili ya ijayo ili kupisha maombolezo kwa wana CCM kwa kifo cha kiongozi huyo
No comments:
Post a Comment