1. Masafa ni rasilimali muhimu
katika shughuli za Mawasiliano (simu, wavuti, redio, na utangazaji).
Masafa ya Mawasiliano (Spectrum) hugawanywa na Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) (ikitambuliwa hapa kama Mamlaka) kwa kutoa leseni kwa
watoa huduma za mawasiliano nchini kwa mujibu wa sheria na masharti ya
leseni. Moja ya kazi za Mamlaka ni pamoja na kupokea na kusuluhisha
matatizo ya muingiliano wa masafa kati ya watoa huduma mbalimbali wa
mawasiliano kwa kutumia ujuzi na wataalamu na teknolojia ya mitambo
maalumu na mahususi ya kisayansi kufanya kazi hiyo. Kazi hizi
zimeainishwa katika Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano ya 2003 (TCRA Act
of 2003) na Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Electronic
and Postal Communications Act (EPOCA) ya mwaka 2010.
2. Mnamo tarehe 29 Januari 2015, Mamlaka ilipokea malalamiko
kuhusu ubora wa matangazo ya vituo vya ITV na EATV yanayorushwa na
Kampuni ya Star Media (T) Limited ambaye ni msambaza matangazo ya
dijitali. ITV na EATV wana leseni ya Maudhui (Content Service Lisence)
na Star Media wana leseni ya Miundombinu ya Utangazaji (Network Facility
License as a signal distributor) kutoka TCRA. Leseni zote za Mamlaka
zina masharti ya kuzingatia.
3. Huduma za Mawasiliano hutumia bendi ya masafa tofauti
(Spectrum bands). Huduma za mawasiliano ya setilaiti (satellite) hutumia
bendi 3.4 mpaka 4.2 GHz, inayofahamika kama C-Band. Ifahamike kuwa
masafa ya setilaiti ya kupokea matangazo (satellite downlink frequency)
ya 3.644 GHz yanatumika kupokea matangazo kutoka satelaiti ya Intelsat
906 (TP 10) kwa matangazo ya vituo vya utangazaji nchini kupitia mfumo
wa dijitali ambao mitambo yake iko katika kilima cha Makongo Juu area.
Hata hivyo, sehemu nyingi duniani, ikiwemo Tanzania, hutumia teknolojia
ya WiMAX katika bendi 3.5 GHz. Masafa haya yanafahamika duniani kote kwa
uwezo wake wa kutumika kiteknolojia kati ya mfumo wa “Fixed Satellite
Services (FSS)” na IMT kama vile mwendo kazi wa intaneti bila waya
(Broadband Wireless Access (BWA) transmission) ikiwemopia teknolojia ya
WiMAX.
4. Kufuatia malalamiko yaliyopokelewa na Mamlaka, TCRA iliteua
timu ya wataalamu Wahandisi wa Masafa kufanya uchunguzi ili kubaini
tatizo la muingiliano wa masafa yaliyosababisha ITV na EATV
kutokuonekana vizuri katika king’amuzi cha Star Media, kwa kutumia
utaratibu na jinsi sheria zinavyoelekeza. Timu hiyo ya wataalamu wa
masafa iliwasiliana na Star Media na kutembelea eneo la Makongo Juu
kwenye mitambo yao ili kubaini aina ya muingiliano, muda wa muingiliano
na maeneo husika. Timu hiyo ilifanya uchunguzi kwa kutumia vifaa maalumu
kwenye eneo lenye mitambo ya kurusha matangazo ili kubaini muingiliano
wa masafa kupitia watoa huduma wa intarneti za mwendo kasi kupitia
teknolojia ya WiMAX katika bendi 3.4 – 3.6 GHz. Aidha timu ilifanya
tathmini ya vipimo vya matumizi ya masafa na watoa huduma katika bendi
nzima ya C- ya kupokelea matangazo (downlink frequency) kutoka 3.4 GHz
hadi 4.2 GHz.
No comments:
Post a Comment