Mtendaji
Mkuu wa PDB Bw. Omari Issa akielezeaumuhimu wa sekta ya Afya kuingia
BRN kuungana na sekta nyingine zilizotangulia zinazoendelea kuzaa
matunda
Dr
Linda Ezekiel ambae ni Mkurugenzi wa sekta za jamii (Afya, Elimu na
Maji) PDB akiwasilisha mada kuhusu malengo ya kipaumbele sekta ya afya
kwa miaka
Bw. Omari Issa akimkabidhi mwakilishi wa wahisani wa maendeleo mkakati wa sekta ya Afya chini ya BRN
Mmoja wa wahisani akisisitiza umuhimu wa wizara ya afya kuwajibika ki BRN katika maeneo mengine yasiyo ya kipaumbele katika BRN
Dr
Oberline Kisanga wa kitengo cha mageuzi katika wizara ya afya akifafanua
ushiriki wa TAMISEMI katika mkakati huu wa afya chini ya BRN
Mwakilishi wa jumuiya ya wahisani akipongeza uamuzi wa serikari kuiweka sekta ya afya katika BRN
…………………………………………………………………………………………
Annastazia Rugaba, PDB habari, 05 Februari 2015
Mtendaji mkuu wa Ofisi ya Rais,
usimamizi wa utekelezaji wa miradi (PDB) Bwana Omari Issa, leo
amekabidhi rasmi taarifa ya mkakati wa kuboresha sekta ya afya chini ya
BRN kwa jumuia ya wahisani wa maendeleo. Makabidhiano hayo yamefanyika
katika ofisi za PDB ambapo jumuiya ya wahisani ilipata fursa ya
kusikiliza kwa kina namna BRN inavyofanya kazi ya kuleta matumaini mapya
kwa watanzania kupitia sekta za kipaumbele.
Sekta ya afya imekuwa ikijaribu
kuboresha utendaji wake lakini kuingia katika BRN kutaleta tija Zaidi.
BRN inaamini katika misingi mikuu ambayo ni kuweka vipaumbele, kuwa na
adabu ya utekelezaji, uwajibikaji na uaminifu, ufuatiliaji wa kina na wa
mara kwa mara na Mawasiliano thabiti kati ya watoa huduma na wapokea
huduma. Hizi ni nguzo muhimu zitakazotufikisha katika dira ya maendeleo
ya taifa ya Mwaka 2025.
Awamu ya kwanza ya BRN
iliziangazia sekta sita ambazo ni Kilimo, Elimu, Maji, Uchukuzi, Nishati
na ukusanyaji wa mapato ambapo sekta za Afya na Uboreshaji wa mazingira
ya Biashara zimeanza rasmi Mwaka huu. Sekta sita za mwanzo
zimedhihirisha mafanikio anuwai ambayo yaliwavutia jopo la wataalamu wa
maendeleo wakiongozwa na Rais Mstaafu wa Botswana Bw Mogae. Ripoti
kamili ya utekelezaji wa BRN kwa Mwaka wa kwanza itazinduliwa rasmi
mapema mwezi Machi Mwaka huu.
Sekta ya afya inakusudia
kutekeleza vipaumbele vine ambavyo ni mosi; ugawanyaji sawia wa wahudumu
wa afya wenye ujuzi takikana kuanzia ngazi ya chini ya afya ya msingi,
pili; utoaji huduma wenye ubora wa nyota tatu katika ngazi zote, tatu;
upatikanaji wa dawa na bidhaa muhimu za afya katika ngazi zote, nne;
kuimarisha afya ya uzazi na usalama wa mama na mtoto ili kupunguza vifo
vya kundi hili muhimu kwa angalau asilimia 60 ifikapo Mwaka 2018.
Jumuiya ya wahisani wamepongeza
uamuzi wa kuiingiza sekta ya afya katika BRN na wakithibisha utayari wao
wa kufanikisha mkakati huu, wametoa wito kwa wizara ya afya, PDB, Sekta
binafsi na jamii ya kitanzania kwa ujumla kuhakikisha kuwa mkakati huu
utafanikiwa.
Malengo haya yote yanahitaji
juhudi kubwa na ya pamoja kutoka kwa jamii, wizara na taasisi zake zote
hadi ngazi ya kijiji, wahisani wa maendeleo na sekta binafsi. “tusingoje
nani aanze, sote tuwajibike, kila mmoja ajitazame kama anawajibika
ipasavyo. Dira ya maendeleo ya Taifa tunayotaka itupeleke kuwa nchi
yenye uchumi wa kati haiwezi kufikiwa tusipofanya kazi kwa pamoja bila
kunyoosheana vidole. BRN ni treni iliyoanza safari tayari, kila mmoja
anawajibika kuingia kwa wakati na kwa nia Chanya, ukichelewa ukakuta
imeondoka bado una fursa ya kuikimbilia kituo kinachofuata ili twende
pamoja” Bw Omari Issa ametoa wito huo kwa wahisani wa maendeleo na jamii kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment