Jovago imetangaza leo kwamba
imeingia katika ushirikiano na Tigo Tanzania, kampuni ya simu
inayoongoza nchini. Katika ushirikiano huu, wateja wa Tigo Pesa sasa
wataweza kulipia malazi yao kupitia akaunti zao za Tigo Pesa. Hii
inakuja wakati muafaka ambapo muingiliano wa malipo ya pesa kupitia simu
za mkononi katika tovuti za intanet umeonekana kama kiungo muhimu
katika ukuaji wa sekta ya utalii katika mitandao.
Huu ni ushirikiano wa pili kwa
utoaji huduma ya malipo ya mtandao wa sim katika sekta hii ya kufanya
booking. Ushirikiano huu unaruhusu watumiaji uhakika na urahisi zaidi
wa kupata malazi kwa njia ya mtandao.
Mtandao unaoongoza barani Afrika kwa kufanya booking za hoteli na malazi www.Jovago.com
umetangaza ushirikiano na Tigo Pesa, moja ya huduma za kutuma na
kupokea fedha zinazoongoza katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na
Kati. Ushirikiano huu unawapatia fursa nyingine wateja kupata huduma
yenye ufanisi zaidi tofauti na ulipaji uliozoeleka wa kulipa kwa kadi na
kulipa kwa fedha taslimu papo kwa papo.
“Hakika bara la Afrika sasa
linaelekea katika ulimwengu wa kidijitali, ni kwa sababu hiyo tunataka
kujumuisha mahitaji ya soko na mienendo yake, na hivyo kutengeneza
mikakati yetu kutokana na mahitaji hayo,” alisema Mkurugenzi Mkuu,
Estell Verdier.
Tigo Pesa ni huduma ya kwanza
Afrika Mashariki iliyoanzisha App yake mahususi na iliyowezesha utumiaji
na upokeaji wa fedha kutoka nchi moja na nyingine yenye uwezo wa
kubadilisha ankara ya fedha moja kwa moja kwenye akaunti ya mteja na
kuepusha haja ya kwenda kubadili fedha kwenye masoko ya ubadilishaji
fedha. Ni dhahiri kwamba maendeleo mengi makubwa yanatokea katika
teknolojia ya simu za mkononi.
Mkuu wa Idara ya kutuma na
kupokea fedha kutoka Tigo, Ruan Swanepoel alisema, “Tunayo furaha
kushirikiana na Jovago kuwapatia wateja wetu urahisi wa kulipia kwa
usalama malazi yao ya hoteli kupitia simu zao za mkononi. Kulipia kwa
Tigo Pesa ni namna rahisi ya kusafiri.
Verdier pia alisema kwamba
ukiondoa urahisi watakaopata wateja kupitia njia hiyo ya malipo, Jovago
kwa sasa pia wanatoa orodha kubwa zaidi ya hoteli barani Afrika ambapo
mteja anaweza kuchagua na vilevile wanazungumza na hoteli hizo kwa
niaba ya wateja kuhusu punguzo za bei, ili wateja waweze kupata sehemu
ya malazi mazuri na kwa bei nzuri zaidi.
Ni muhimu pia kutambua kwamba
katika robo ya mwisho ya mwaka wa 2014, ukuaji wa huduma za simu
Tanzania umeongezeka kwa kiasi cha asilimia 2.8 kutoka asilimia 2.0 ya
awali. Tanzania kwa sasa ina jumla ya watumiaji wa simu za mkononi
milioni 28, ambayo ni takribani asilimia 63 ya watu wote.
Kutokana na ripoti ya World
Tourism, Afrika Mashariki ni kanda yenye mafanikio na maarufu kwa
matumizi ya malipo kwa njia ya simu za mkononi, Kenya ikiongoza kwa
asilimia 80 katika kundi la watu wazima wanaofanya hiyo miamala.
Kwa kumalizia, Verdier pia alisema kwamba kwa sasa zaidi ya asilimia 30 ya wanaotembelea www.jovago.com wanatumia simu zao za mkononi. Katika muktadha huu malipo ya simu za mkononi ni kiungo muhimu sana katika ukuaji wa sekta hii.
Hii si mara ya kwanza kwa kampuni hizi mbili kushirikiana,
Jovago.com na Tigo Pesa hapo awali wameshashirikiana katika mradi wa
UNICEF Passport to Life yenye malengo ya kumpatia kila mtoto wa kiafrika
cheti cha kuzaliwa. Wakati wa kufanya booking Jovago, wateja wanapewa
nafasi ya kutoa mchango kwa mradi huu wa usajili wa uzazi (dola 5 kwa
booking ambaye inaenda kwa UNICEF) bila malipo yoyote ya ziada.
No comments:
Post a Comment