Katibu
Tawala Mkoa wa Mbeya Bibi Mariam A. Mtunguja (katikati) akizungumza na maafisa
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa ziara ya
kutembelea vijana wa Mkoa wa Mbeya na kutoa elimu ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi
za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Mwezeshaji
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa (kushoto)
akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Bw. Gullamhussein S. Kifu (katikati)
wakati wa ziara ya kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa vijana wa Wilaya hiyo.
Kulia ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele na
anayefuata ni Kaimu Afisa Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Bw. Athuman
Mustafa Kinza.
Mkuu wa Kituo cha
Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele akiwaelekeza vijana wa Mbarali namna ya
kuandika andiko la mradi wakati wa semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za
Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyotolewa kwa vijana wa Mbarali hivi
karibuni.
Maafisa
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na vijana wa
Kikundi cha Umati Sanaa Group wakiburudika na muziki uliokua ukitumbuizwa na
vijana wa kikundi hicho wakati wa ziara ya kutembelea vikundi vya vijana wa
Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya.
Mwezeshaji
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa (waliokaa
kushoto) akizungumza na vijana wa Umati Sanaa Group wanaofanya kazi za sanaa
walipofika kuangali kazi zinazofanywa na kikundi hicho wakati wa ziara ya
uhamasishaji kwa vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya
(Picha zote na: Genofeva Matemu – Mbarali, Mbeya)
No comments:
Post a Comment