WAZIRI wa
Uchukuzi, Samuel Sitta ameelezea kufurahishwa na waandaaji wa Tamasha la
Pasaka na kusema kuwa katika miaka 15 ya tamasha hilo wana mengi ya
kujivunia.
Taarifa kwa
vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na kusainiwa na
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza
kuwa kamati yake imepokea salamu kutoka kwa Waziri Sitta akizungumzia
maandalizi ya miaka 15 ya tamasha hilo.
“Ni tamasha
lenye tija kwa Watanzania, mimi mwenyewe nimekuwa shahidi wa namna
mnavyosaidia yatima, wajane na makundi mbalimbali ya kijamii.
“Nimesikia
mwaka huu mna tamasha kubwa la miaka 15 tangu muanze kufanya Tamasha la
Pasaka, niwatakie kila la heri katika maandalizi na naamini litakuwa
tamasha la aina yake,” alisema Msama katika taarifa yake akimnukuu
Sitta.
Alisema
wamekuwa wakipokea salamu kutoka kwa wadau mbalimbali wakizungumzia
kuhusiana na maandalizi ya Miaka 15 ya Tamasha la Pasaka na wakielezea
pia mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kwa kipindi hicho.
Baadhi ya
walioguswa na maandalizi ya tamasha hilo ni waimbaji mahiri wa muziki wa
Injili kutoka Afrika Kusini Solly Mahlangu ‘Obrigado’ na Rebecca
Malope.
Wasanii
hao wamewahi kwa nyakati tofauti kuja nchini katika Tamasha la Pasaka,
ambapo mwaka huu waandaji wamepanga kufanya sherehe ya Miaka 15 ya
Tamasha la Pasaka.
No comments:
Post a Comment