- CCM yakosoa ujenzi daraja Rau
- Serikali yatangaza mikakati kupunguza umaskini nchini
- PPF yajivunia mafanikio Dodoma
- Wauguzi walia kucheleweshewa mishahara
- Mwenge kumulika miradi ya zaidi ya bilioni 1/-
- Walimu wauponda mfumo wa elimu nchini
- Umeme waiangusha CCM Bumbuli
- Kukua kwa teknolojia duniani kunasababisha kuenea uhalifu
- Wanachama 331 MIMCO waanza kugawiwa viwanja
- Madiwani wawasimamisha kazi watumishi kwa ubadhirifu
- Madiwani wawasimamisha kazi watumishi kwa ubadhirifu
- Waandishi wa habari washauriwa kujilinda
- Denmark yashauri utoaji misamaha ya kodi
- Walimu wafananisha elimu nchini na maghorofa mabovu
- uchimbwaji dhahabu wasimamishwa kitundu
- CCM yaibana serikali uchomaji makanisa
- Mbunge aibana Serikali utekelezaji wa bajeti
- Wanafunzi 15 mbaroni kwa kuchoma moto bweni
- Ndugu wagombea maiti mochari
Posted: 16 May 2013 01:06 AM PDT
|
|
Posted: 16 May 2013 12:24 AM PDT
|
|
Posted: 15 May 2013 11:01 PM PDT
Na Florah Temba, Moshi
KAMATI
ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi na Sekretarieti ya
halmashauri kuu ya chama hicho Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro,
imesema haijaridhishwa na ujenzi wa daraja la Rau Mbokomu linalojengwa
na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, hivyo kuitaka manispaa hiyo kupitia
upya ujenzi huo na kuhakikisha magari makubwa hayapiti, hadi pale
litakapothibitishwa kuwa liko imara.
Daraja
hilo ambalo litagharimu sh. milioni 102 bado halijakamilika lakini
limeonekana kubomoka, hali ambayo imesababisha watu kuhofia kuwa
hata kama litakamilika na kukabidhiwa linaweza kuleta maafa kutokana na kujengwa chini ya kiwango.
Akizungumza
wakati wa ukaguzi wa miradi iliyotekelezwa na manispaa kwa kipindi cha
mwaka 2012/2013 Katibu wa CCM Manispaa ya Moshi, Aluu Segamba, alisema
wao hawajaridhishwa na ujenzi wa daraja hilo ambalo lina umuhimu mkubwa
kwa wananchi.
"Sisi
si wataalamu lakini naomba niseme kuwa hatujaaridhishwa na ujenzi wa
daraja hili,kwani haiwezekani daraja lijengwe halijakamilika lakini
libomoke, kunahitajika uangalizi mkubwa hapa ili kuhakikisha daraja hili
linakamilishwa kwa kiwango kinachostahili ili kuokoa maafa yatakayoweza
kutokea kutokana na kukamilisha chini ya kiwango," alisema Segamba.
Aidha
Segamba alisema kwa sasa wanaangalia uwezekano wa kutuma wataalamu ili
kwenda kukagua daraja hilo na kujiridhisha kabla halijaanza kutumika.
Katibu
huyo alishauri daraja hilo lisitumike kupitisha magari makubwa hata
baada ya kukabidhiwa hadi pale watakapokwenda wataalamu kukagua na
kujiridhisha hatua ambayo itasaidia kuepuka maafa.
Mjumbe
wa NecManispaa ya Moshi, Agrey Marialle alisema licha ya taarifa
kutolewa kuwa daraja hilo limeshakamilika kwa asilimia 80 bado kazi ni
kubwa na inahitaji umakini wa hali ya juu.
Kwa
upande wake mkadiriaji wa ujenzi manispaa hiyo, Charles Huka
akizungumza kwa niaba ya mkandarasi wa manispaa hiyo alisema wao
wanaridhishwa na ujenzi wa daraja hilo ambalo limekamilika kwa asilimia
80 na kwamba linatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka huu.
Kwa
upande wake Eveta Lyimo msaidizi wa mchumi wa manispaa hiyo alisema
mradi wa daraja hilo ambao uliibuliwa na wananchi kama mradi wa TASAF
ulianza kujengwa mwaka 2009/2010 na kwamba ulihitajika uwe umekamilika
lakini kutokana na mvua umeshindwa kukamilika kwa wakati uliopangwa.
|
|
Posted: 15 May 2013 11:03 PM PDT
Na David John
IMEELEZWA
kuwa katika kufikia Dira ya Maendeleo ya Taifa (VISION 2025) Tanzania
imejiwekea mikakati mbalimbali ikiwemo MKUKUTA yenye malengo ya
kuhakikisha kiwango cha ukosefu wa ajira kinapungua.
Akizungumza
katika mkutano uliwakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo nchini Dar
es Salaam jana Mkurugenzi Mkuu wa Ajira, Ally Msack alisema malengo hayo
yanalenga kupunguza ajira isiyotimilifu, utumikishwaji wa watoto
unapungua na uwepo wa hifadhi ya jamii kutokana na ajira.
Msack aliongeza kuwa kwa sasa imebakia miaka miwili kufikia malengo ya
maendeleo ya Millenia MDGS ambapo mwaka 2015, malengo ya Mkukuta11 2010/11 -2014/15 na malengo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano 2011/12-2015/16 ambapo nchi inapaswa kutoa taarifa ya viwango vya viashiria vya malengo hayo.
Alisema
kwa Tanzania zaidi ya asilimia 75.1 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi
wanajihusisha na shughuli zilizopo katika sekta zisizo rasmi kwa maana
hiyo utafiti unagusa sehemu kubwa ya nguvu kazi na utaiwezesha Serikali
kupata picha halisi ya hali ya ajira nchini.
"Unajua
utafiti huu unawezesha kutoa taarifa juu ya hali ya ajira nchini katika
sekta rasmi na isiyo rasmi, utumikishwaji wa watoto, hali ya hifadhi ya
jamii, hali kipato nchini, matumizi ya muda na ajira mpya
zilizozalishwa katika sekta zote kwa kipindi husika (2006-2013).
Alisema
viashiria hivi vya soko la ajira ndiyo kigezo kikubwa kinachotokea
picha halisi ya mafanikio ya kiuchumi na kuchochea maendeleo ya nchi.
Aliongeza
kuwa kwa mara ya mwisho utafiti huo ulifanyika mwaka 2006 na kuwezesha
nchi kupata viashiria vyote muhimu vya soko la ajira vikiwemo vya
MkukutaMalengo ya Maendeleo ya Millenia MDGS mipango ya maendeleo ya
Taifa na kazi yenye staha.
Hata
hivyo ili kupanga matumizi sahihi nguvu kazi kwa maendeleo ya kiuchumi
lazima nchi iwe na taarifa sahihi ya soko la ajira, hivyo mchakato huo
wa masuala ya ajira na kazi ni masuala mtambuka ambayo juhudi za pamoja
zinahitajika kati ya Serikali na taasisi za elimu na utafiti wawekezaji,
mashirika yasiyo ya kiserikali, wabia wa maendeleo waandishi wa habari
na wananchi kwa ujumla ili kufikia malengo waliyojiwekea.
|
|
Posted: 15 May 2013 11:09 PM PDT
Na Pendo Mtibuche,
Dodoma
MFUKO
wa Pensheni ya Mashirika ya Umma ( P P F ) umesema kuwa kwa muda wa
siku tatu za maonesho ya mifuko ya hifadhi ya jamii yanayofanyika mjini
Dodoma chini ya usimamizi wa Mamlaka ya mifuko hiyo (SSRA) umefanikiwa
kutembelewa na wananchi wapatao 572 na kupata elimu.
Akizungumza
na gazeti hili katika viwanja vya maonesho hayo vya Mwalimu Nyerere
Square, Meneja wa Kanda ya Mashariki na Kati, John Mwalisu alisema kuwa
maonesho hayo ya mifuko ya hifadhi ya jamii yamekuwa na manufaa makubwa
kwa jamii ya mkoa
huo.
Alisema
kuwa kwa muda wa siku tatu za maonesho hayo mfuko wao wa PPF
umefanikiwa kutembelewa na wananchi mbalimbali wapatao 572 lakini pia
wamefanikiwa kutoa taarifa zaidi ya 217 za michango ya wanachama wao.
Mbali
na hilo pia alisema kuwa walifanikiwa pia hata kuandikisha wanachama
wapya wakiwemo wabunge ambaowameonesha kuufurahia mfuko wao na kuahidi
kueneza ujumbe huo kwa wabunge wengine.
Akizungumzia
hali halisi ya mfuko huo alisema upo katika hali nzuri kwani unaweza
kulipa madeni yake na hata kubakiwa na ziada na kueleza kuwa thamani ya
mfuko huo kwa sasa ni sh. trilioni 1.09 lakini lengo lao hadi kufikia
2015 mfuko huo uwe na thamani ya sh.trilioni 2.
Akizungumzia
suala la wanachama wa mfuko huo kwa nchi nzima wanafika zaidi ya
218,000 ambapo kwa mwezi mfuko huo unatoa zaidi ya bilioni tatu kwa
ajili ya pensheni za wastaafu.
Kwa
upande wake naye Ofisa Mwandamizi wa uwekezaji katika mfuko huo, Anna
Shayo akizungumzia hali halisi ya uwekezaji katika mfuko huo alisema
kuwa mfuko huo umewekeza katika mali zinazohamishika na zisizohamishika.
Alisemakuwa
wamefanikiwa kuwekeza katika majengo ya kuishi, majengo ya biashara,
hisa za makampuni wamefanikiwa kuwekeza katik a vitegauchumi ambavyo
riba zake zinajulikana kabla.
Kwa
upande mwingine pia alisema kuwa wamefanikiwa kuwekeza katika mikopo
amb a p o kwa s e h emu wamefanikiwa kujenga baadhi ya majengo katika
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Ukumbi wa Bunge, majengo mengine Arusha na
hata kuwa na saccosza wanachama wa PPF 42 ambazo wameshazikopesha
bilioni 54 tangu mwaka 2004.
"Kwa
upande wa saccosmwezi huu yaani Mei tunakusudia kutoa bilioni moja
nyingine kwa ajili ya kufungua saccosnyingine mbili katika jiji la Dar
es Salaam na hivyo tutakuwa na saccos44, hayo ni mafanikio ya mfuko,"
alisema.
Kwa
upande wake Ofisa uhusiano wa Mfuko huo, Lulu Megele akizungumzia suala
zima la wao kushiriki maonesho hayo alisema kuwa mfuko wa pensheni wa
PPF umeshiriki maonesho hayo lengo likiwa ni kutoa elimu kwa umma juu ya
umuhimu wa kujiunga na mfuko huo.
Alisema
kuwa umuhimu wa wananchi kujiunga na mfuko huo ni kutokana na kuwa na
faida nyingi ambazo ni pamoja na kuwepo kwa fao la uzee, ugonjwa, kifo,
wategeneziu, elimu, kiinua mgongo na fao la kujitoa.
Akizungumzia
mafanikio ya mfuko huo alisema kuwa umewezesha kuwasomesha zaidi ya
watoto 1,333 katika shule za msingi na sekondari katika mikoa mbalimbali
hapa nchini.
Alisema
kuwa mfuko huo ulifikia uamuzi wa kuwasomesha watoto hao kutokana na
kuwepo kwa tatizo kwa wasimamizi wa mirathi pindi wazazi wa watoto hao
wanapopoteza maisha.
Alisema kuwa hadi kufikia Desemba mwaka jana jumla ya sh. milioni 682.9 zililipwa kama mahitaji mbalimbali kwa wanafunzi hao.
|
|
Posted: 15 May 2013 10:41 PM PDT
Na Steven William, Muheza
WAUGUZI
wa Afya katika Hospitali Teule wilayani Muheza wamedai kwamba wamekuwa
wakicheleweshewa mishahara yao katika hospitali hiyo hali ambayo
inasababisha wafanye kazi katika mazingira magumu.
Hayo
yalisemwa katika risala ya wauguzi katika siku ya wauguzi duniani
iliyoadhimishwa kiwilaya hivi karibuni katika Kijiji cha Magoda ambayo
ilisomwa na Furaha Kiswaka.
Alisema
kuwa wafanyakazi wa hospitali wamekuwa wakicheleweshewa mishahara hali
ambayo inawafanya washindwe kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Kiswaka alisema pia wauguzi hao wanakabiliwa na tatizo la
nyumba kwa wanaoishi vijijini ambapo wanaishi katika makazi duni.
Alisema
kuwa wauguzi wengine wanaishi mbali na vituo vya kufanyia kazi kitu
ambacho wanahatarisha maisha yao hasa wakati wa usiku wanapokuwa na zamu
huku wakishauri panapojengwa zahanati pajengwe na nyumba ya muuguzi.
Kiswaka
alisema kuwa wauguzi wanakabiliwa na upungufu wa vifaa tiba, vifaa vya
usafi na mahitaji muhimu kwa ajili ya usafi ambapo alisema mganga mkuu
wa wilaya amekuwa akijitahidi kupatikana vifaa hivyo isipokuwa hospitali
ya wilaya Teule bado kuna uhaba mkubwa wa dawa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Muheza, Ibrahim
Matovu ambae aliwakilishwa na Kaimu wake, Maurd Mbugi aliwataka wauguzi
kufanya kazi kwa moyo mmoja ili kuboresha afya za wananchi na hatimae
kuongeza uchumi wa nchi.
Alisema
kuwa matatizo yote waliyoyaeleza ameyasikia na atayafanyia kazi kwa
kuyapeleka kunakohusika ili yafanyiwe kazi na kuwataka wasife moyo.
Kwa
upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Zahanati ya Magoda, Leticia Ibrahim
alisema kuwa zahanati hiyo wanatibu zaidi ya wagonjwa 20 kwa siku pamoja
na kutoa huduma ya CHF.
Nae Muuguzi Mkuu, Victoria Wasapa aliongoza kuwaapisha wauguzi katika sherehe hiyo ili wawe na nidhamu katika kazi.
Mwenge kumulika miradi ya zaidi ya bilioni 1/- | |
Posted: 15 May 2013 10:38 PM PDT
Na Steven William, Muheza
ZAIDI
ya miradi sita ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.9
itapitiwa na Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Muheza mkoani Tanga
Miongoni mwa miradi hiyo itakaguliwa, kufunguliwa na kuweka mawe ya msingi pindi utakapowasili wilayani humo Mei 18, mwaka huu.
Mkuu
wa wilaya ya Muheza, Subira Mgalu ametoa taarifa hiyo wakati
akizungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na ujio wa Mwenge huo
wa Uhuru wilayani humo.
Alisema kuwa miradi ambayo itapitiwa na Mwenge huo ni
pamoja na kukagua mradi wa hifadhi ya bahari Kijiji cha Kigombe,
kufungua ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Kijiji cha Mtiti.
Miradi
mingine itakayotembelewa na Mwenge huo ni kukagua shamba la miti katika
Kijiji cha Kigombe na kuweka jiwe la msingi Zahanati ya Kijiji cha
Kilulu.
Mkuu
huyo wa wilaya alitaja miradi mingine itakayopitiwa na kuweka jiwe la
msingi kisima cha maji kilichopo Mang'enya Kata ya Genge na kukagua
mabweni ya wanafunzi shule ya Livingstone.
Alisema
kuwa baada ya Mwenge huo kukagua miradi hiyo utakagua mabanda ya
maonyesho katika uwanja wa Jitegemee ambako mwenge huo utakesha mpaka
asubuhi.
Kwa
upande wake Mratibu wa Mwenge Wilaya ya Muheza, Athumani Komolanya
aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuupokea mwenge huo katika
barabara ambapo utapokelewa Kijiji cha Mjesani ukitokea wilayani Mkinga
na asubuhi yake utakabidhiwa Kijiji cha Masaika ukielekea wilayani
Pangani.
|
|
Posted: 15 May 2013 10:36 PM PDT
Na Yusuph Mussa, Lushoto
BAADHI
ya walimu wilayani Lushoto wameifananisha elimu ya Tanzania kama
maghorofa mabovu yanayojengwa jijini Dar es Salaam, kwani inazidi
kushuka kutokana na mfumo mbovu wa mitaala na uingizaji holela wa vitabu
vya kufundishia na kujifunzia shuleni.
Wakizungumza
juzi kwenye mkutano wa wakuu wa shule za msingi na sekondari katika
Halmashauri ya Bumbuli, ulioandaliwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Bumbuli, January Makamba waliitaka
Serikali ishirikishe wadau kwenye
mitaala.
"Kama
mchakato wa Katiba Mpya unavyoshirikisha wadau, vivyo hivyo utungaji
ama uanzishwaji wa mitaala mipya iwashirikishe wadau ili kupata mitaala
itakayokubalika au sivyo elimu yetu itaendelea kuwa kama maghorofa ya
Dar es Salaam.
"Itazidi
kuporomoka kwa vile haina misingi mizuri. Hivi inakuwaje mtoto wa
darasa la kwanza anakwenda shuleni na madaftari tisa, turudishe
utaratibu wa K tatu yaani Kusoma, Kuandika na Kuhesabu" alisema Mratibu
wa Elimu Kata ya Soni, Luth Msagati.
Mratibu
wa Elimu Kata ya Milingano alisema mitaala iliyopo kwa sasa hata walimu
hawaijui, hivyo ni vigumu mwalimu kumfundisha mwanafunzi akaelewa, huku
akisema changamoto nyingine ni kuwaingiza sekondari wanafunzi waliopata
alama 70.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari Kwamongo, Anthony Kihiyo alisema kwa Serikali
kuruhusu wanafunzi wa shule za kata na zile za Mtakatifu kufanya mtihani
mmoja ni sawa na kumpambanisha Francis Cheka na mgonjwa aliyelazwa
Hospitali ya Muhimbili.
"Wanafunzi
wa shule za kata kufanya mtihani mmoja na wale wa shule binafsi ni
kuwaonea. Hata mabondia uzito wao unapimwa na unatakiwa ulingane ndipo
wapigane," alisema Kihiyo.
Makamba
alisema pamoja na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuunda tume ya kuchunguza
kisa cha matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka jana, bado walengwa
ambao ni walimu hawajapewa nafasi ya kutoa maoni yao juu ya suala hilo.
"Sauti
ya mwalimu haijasikika zaidi ya wanasiasa na makundi mengine, lakini
walimu hasa ndiyo wanajua kitu gani kimefanya wanafunzi wamefanya
vibaya, sababu ndiyo wanakaa na wanafunzi hawa kati ya saa nane hadi
tisa," alisema Makamba.
Makamba
aliungana na walimu kwa kusema mitaala isitegemee mapenzi ya waziri
aliyepo madarakani ama Serikali inayoongoza dola, bali iwe ni suala la
kitaifa ambapo kila Serikali ama waziri atakaekuja atafuata mitaala
hiyo.
|
|
Posted: 15 May 2013 10:35 PM PDT
Na Yusuph Mussa, Lushoto
UMEME
kupita juu ya Kijiji cha Wanga kilichopo Kata ya Mgwashi wilayani
Lushoto na wao kushindwa kuwekewa trasfoma ili wapate huduma hiyo
kumekigharimu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa wananchi kuamua kumchagua
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho kupitia CHADEMA.
Wakizungumza
juzi kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Bumbuli, January Makamba
wananchi walisema kupitisha nyaya za
umeme juu na kuwapelekea wanakijiji wenzao wa Mgwashi ni kuonesha Serikali ya CCM haiwajali.
"Umeme
kupita juu kwa juu kwenda Kijiji cha Mgwashi na kutuacha sisi, tumeona
Serikali haitujali. Lakini pia tunachangishwa michango mara mbili mbili,
kwani tulikamilisha boma (darasa) la Shule ya Sekondari Handeni.
"Awali
tulijenga likakamilika kwa kutoa kila mtu sh. 5,000, lakini kwa vile
lilijengwa chini ya kiwango ikabidi tuchangishwe tena sh. 3,000.
Wananchi wananyanyaswa kwa kuambulwa (kushikwa faini) kuku ili kujenga
tena boma hilo," alisema Athuman Amir.
Makamba
aliwataka wananchi wawe na subira kwani ipo mikakati ya kufikisha umeme
kwenye kata kadhaa kwenye Halmashauri ya Bumbuli ikiwemo eneo hilo.
Pia
alisema kwa kupata halmashauri wataweza kuipandisha barabara ya Mbelei-
Mgwashi- Milingano- Mashewa kuwa chini ya Wakala wa Barabara
(TANROADS).
|
|
Posted: 15 May 2013 10:26 PM PDT
Na Rehema Maigala
KATIBU
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbaraka Abdul Wakili amesema
kukua kwa teknolojia duniani kunasababisha kuenea kwa wingi uhalifu.
Hayo
alisema jana wakati akifunga mkutano wa 18 wa Maofisa wa Jeshi la
Polisi Katika Nchi za Kanda ya Kusini mwa Afrika (SARPCCO) ambao ulikuwa
na lengo la kujadili jinsi ya kukabiliana ya uhalifu.
Alisema wakuu hao kutoka nchi 14 wamekutana kwa ajili ya
kukaa pamoja na kuweka mikakati ya ushirikiano ili kupambana ugaidi ulioenea katika nchi za Afrika.
"Hivi
sasa uhalifu umevuka mipaka kwa sababu ya kukua kwa teknolojia hivyo
inatakiwa kukaa pamoja na kujadili suala hili ili liweze
kupungua,"alisema Wakili.
Aliongeza
kusema kuwa nchi moja ikikaa peke yake ili iweze kutatua tatizo la
ugaidi haiwezi kufanikiwa inatakiwa kukaa pamoja na nchi zingine ili
kupanga nini cha kufanya.
Alisema
kuwa kukaa kwa nchi zaidi ya tatu kutasaidia kuleta mafanikio makubwa
kwani nchi nyingine inakuwa na uwezo mdogo na nyingine inakuwa na uwezo
mkubwa wa kujua nini cha kufanya ili kumaliza tatizo la uhalifu.
Vilevile alisema hivi sasa wahalifu wengi hutumia teknolojia ya kisasa ili kufanikiwa na mambo yao wanayoyafanya.
Naye
Mwenyekiti wa SARPCCO, Saidi Mwema ambaye pia ni Mkuu wa Jeshi la
Polisi Tanzania mkutano huo umesaidia kujua njia mbalimbali za kuweza
kuwafichua wahalifu wanaozitesa nchi za Afrika.
Alisema
kuwa, sasa hivi wanataka kufichua vyanzo vinne ambavyo ndivyo vya
uhalifu ni wachocheaji, wawezeshaji na wanaojilipua wenyewe kwa ajili ya
uhalifu.
Mwema
alisema kuwa k a t i k a mk u t a n o h u o watapeana taarifa na
kubadilishana taarifa hasa katika makosa ya uharamia baharini na kuzagaa
kwa silaha katika nchi za Afrika.
|
|
Posted: 15 May 2013 10:24 PM PDT
Na Heri Shaaban
WANACHAMA
331 wa Umoja wa Wauza Mitumba wa soko la Mchikichini (MIMCO)wameanza
kupewa viwanja kwa kila mwanachama wa umoja huo ili wajenge nyumba za
kuishi.
Viwanja
hivyo walivyopewa wanachama wameuziwa na umoja wao wa MIMCO baada
kununua shamba zaidi ya heka 20 eneo la Pemba Mnazi Wilayani
Temeke,ambapo kila mwanachama hulipia sh.milioni 1.2 pamoja na kupatiwa
leseni ya kiwanja kilichopimwa na Serikali.
Akisoma taarifa ya Bodi ya MIMCO Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bw.
Ajali Mohamed alisema kila mwanachama hai wa umoja huo ambaye hadaiwi ada atapatiwa eneo la kujenga.
Alisema
kila mwanachama atagawiwa eneo la kujenga baada kukamilisha taratibu na
fedha atalipa kwa awamu tofauti kwa kuanzia sh. 400,000.
"Madhumuni
ya wanachama wangu kuwagawia kila mmoja kiwanja ni ili wajenge nyumba
za kuishi watoke katika nyumba za kupanga halafu waweze kupata mikopo
kwa urahisi kutokana dhamana ya leseni zao," alisema Bw. Mohamed.
Bw.Mohamed
alisema umoja huo ulianzishwa mwaka 2005 mwezi Mei kikiwa na wanachama
331 kati yao wanawake 24 wanaume 307 na wajumbe wanane wa bodi hiyo.
Aliwataka wanachama wa umoja huo kulipa ada kila mwaka ili umoja huo uweze kukua sambamba na kukuza hisa zao.
Pia
bodi hiyo imependekeza viwanja hivyo wauziwe wanachama walio hai ambao
hawadaiwi hisa wala ada na mtu atakayepewa kiwanja alipe pesa ndani ya
miezi mitatu ili waweze kupata fedha kwa maendeleo ya MIMCO na wanachama
wake.
Kwa
upande wake Mwenyekiti Mstaafu wa soko la Mchikichini Bw. Deo Mkali,
aliwataka wanachama wa MIMCO wachague viongozi bora na si bora viongozi
ili chama hicho kisipoteze mwelekeo katika uongozi wake.
Bw.Mkali
alisema chama hicho kinapofanya chaguzi zake kichague viongozi bora na
wenye upeo katika utendaji ambao watasaidia chama kupiga hatua zaidi
katika elimu ya ujasiriamali.
Pia
alikitaka chama hicho kiwape kipaumbele wanawake kuwa sehemu ya uongozi
wa bodi na viwanja vigawiwe pasipo dhana ya ubaguzi.
"Nimestaafu
kwa hiari yangu ila natoa wosia kwa chama tujiepushe na wanachama
wanaojitokeza kuleta vurugu na uchochezi sokoni kwa ujumla pamoja na
kujiepusha na masuala ya udini, siasa ukabila na ubaguzi vinavyoashiria
kujitokeza sokoni kwa sasa,"alisema Bw.Mkali.
|
|
Posted: 15 May 2013 10:15 PM PDT
Na Queen lema, Arusha
BARAZA
la Madiwani Halmashauri ya ArushaVijijini,WilayayaArumeru limewa
simamisha kazi watu mish iwatano wa halmashauri hiyo kwatuhuma za
ubadhirifu.
Watumishi
haowanakabiliwanatuhuma ya ubadhirifuwash.milio ni 56 6,654,173zilizoto
lewa kwaajili yakujenga v yumbavyam ada rasaka tikabaadhi ya shule za
sekondari zahalm ashaurih iyo.
Mwenyekiti
wa HalmashauriyaArusha,Bw.SaimonSaning'oakitangaza uamuzi huo jana, a
lisemamhusikamkuu katikakatikashauri hilo ni wasaid izi wake watatu .
Alisemawatumishi
hao wamesimamishwa kupishauchunguzi.Aliongezakuwa wamebainikabaada
yaMku rugenzi Mtendaji aliyehamishiwa katika Halmashauri hiyo kumuagiza
Mkaguzi
wandanikatikahalmashauri hiyo, Bw. Jackson Laizer, kufanya ukaguzi.
Mwenyekiti
huyo alisema wamebaini wizi wa fedha hizo Februari, mwaka huu na kuwa
mchezo ulianza kufanyika Desemba mwaka uliopita.
Alisema kuwa, fedha hizo hazikupelekwa shuleni kama ilivyoelekezwa.
Mkaguzi
huyo anadaiwa kubaini kuwa hati za malipo ziliandaliwa nje bila mfumo
funganishi wa EPICOR na malipo kufanyika bila hidhini ya Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri hiyo, malipo kufanyika bila vifungu vya bajeti
na hati za malipo zilizoandikwa kwa mkono.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha kwa sasa, Fedelist Lumato
akizungumzia tukio la kusimamishwa kwa watumishi hao, alisema kuwa
watumishi hao watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
|
|
Posted: 15 May 2013 10:18 PM PDT
Na Queen lema, Arusha
BARAZA
la Madiwani Halmashauriya ArushaVijijini,WilayayaArumeru
limewasimamishakazi watumish iwatano wahalmashauri hiyokwatuhuma
zaubadhirifu.
Watumishi
hao wanakabiliwanatuhuma yaubadhirifuwash.milio ni 56 6,654,173zilizoto
lewa kwaajili yakujenga vyumbavyamada rasaka tikabaadhi ya shule za
sekondari zahalmashaurih iyo.
M wenye kitiwaHal mashauriyaArusha,Bw.Sai monSaning'o, akitangaza uamuzi huo
jana,a lisemamhusikamkuu katikakatikashauri hilo ni wasaidizi wake watatu .
Alisemawatumi
shih a o wamesimam ishwaku pishauchunguzi.Alionge zakuwa wamebain
ikabaada yaMku rugenzi Mtendajiali yehamish iwakatikaHalmashauri hiyo
kumuagiza Mkaguzi wandanikatikahalmashauri hiyo, Bw. Jackson Laizer,
kufanya ukaguzi.
Mwenyekiti
huyo alisema wamebaini wizi wa fedha hizo Februari, mwaka huu na kuwa
mchezo ulianza kufanyika Desemba mwaka uliopita.
Alisema kuwa, fedha hizo hazikupelekwa shuleni kama ilivyoelekezwa.
Mkaguzi
huyo anadaiwa kubaini kuwa hati za malipo ziliandaliwa nje bila mfumo
funganishi wa EPICOR na malipo kufanyika bila hidhini ya Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri hiyo, malipo kufanyika bila vifungu vya bajeti
na hati za malipo zilizoandikwa kwa mkono.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha kwa sasa, Fedelist Lumato
akizungumzia tukio la kusimamishwa kwa watumishi hao, alisema kuwa
watumishi hao watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
|
|
Posted: 15 May 2013 10:19 PM PDT
WAANDISHI
wahabarinchini wametakiwa kuhakikisha wanajilinda dhidiya
maaduiwabayakwaki lekilichoda iwakuwahivisasausalama waonimdogo, anaripoti AnnethKagenda.
Wito
huo umetolewaDaresSalaamjananaMwe nyekitiwaMakampuni ya IPPkwenyeMk
utanowakenavyom bovya habari ulio lenga kuang alia nikwajinsi ganiusalam
awawaand ishi utaboreshwa.
“Lakini
ninachoweza kusema nikwamba maran yingiwapowa andishiambao wame kuwa
wakihata risham aishay awaa ndishiwenzaokwa kutoa s irinje... jamani
naombat abiahiitu iacheili
tusitoemwanya kwa ha owaba yakuhatarisham aisha yetu,” alisema.
Alisema
wengine ambaowamekuwa wakisababisha waandishikupigwa,kuteswana
kuuawaniviongoz iwasiokuwa waadilifua mbaowamekuwa wakishiriki
ananawaandishi wasiokuwa waadilifu kufanyavitendo viovu.
Bw.
Mengi alisema kwa muda mrefu sasa Tanzania imekuwa ikitajwa kuwa ni
nchi ya amani, amani lakini kwa wakati huu mambo yanayojitokeza yamekuwa
yakitisha wananchi.
Hata
hivyo, alisema usalama unaotakiwa kwa waandishi ni kuanzia kwa mmiliki
pamoja na mwandishi mwenyewe. Mratibu wa Kitaifa katika mtandao wa
utetezi haki za Binadamu, Bw. Onesmo Olengurumwa, alisema usalama wa
waandishi ni muhimu kwa taifa lolote linalotaka kusonga mbele.
Alisema ni jambo la kusikitisha kuona kila siku waandishi 30 duniani wanauawa kuteswa na kupigwa.
“Taifa
lolote linalotaka maendeleo haliwezi kukwepa waandishi wa habari,
lakini pia usalama wa waandishi unatakiwa kwani bila wao hatuwezi kujua
ni fedha shilingi ngapi zimeidhinishwa kwa ajili ya maendeleo."
|
|
Posted: 15 May 2013 09:38 PM PDT
Grace Ndossa na Mariam Mziwanda
NAIBU
Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kitaifa wa Serikali ya Denmark,
Bw. Charlotte Slett, ameshauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
ihakikishe malengo ya misamaha ya kodi yanapunguza umaskini na kuleta
usawa katika jamii. Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Naibu
waziri huyo, alipotembelea Mamlaka hiyo kujua mipango ya miaka mitano
iliyowekwa kuhakikisha inapunguza umaskini Tanzania. Alisema Serikali ya
Denmark inahakikisha misamaha ya kodi ni
asilimia hamsini kwa hamsini, ambayo haiwaumizi wananchi wake. Hata
hivyo alisema Serikali ya Denmark inasaidia Tanzania kila mwaka kwa dola
milioni 80 na kwamba watakutana na waziri wa fedha kuangalia ni namna
gani wanaweza kusaidia bajeti ya wizara yake. Naye Kamishna Mkuu TRA,
Bw. Harry Kitillya, alisema misamaha ya kodi inatolewa kama mtu akikosa
sababu za msingi zinazofanya asamehewe au kupunguziwa kodi. Wakati huo huo TRA
imezindua awamu ya pili utekelezaji wa mradi wa Mashine za
kielektroniki ambayo imelenga kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani.
Hayo yalibainishwa jana na Naibu Kamishna MKuu wa Mamlaka hiyo Bw.
Rished Bade, alipokuwa anazindua mashine hiyo na kueleza kuwa awamu hiyo
imelenga kuanza na kundi la wafanyabiashara 200,000. Alisema matumizi
ya mfumo huo kwa miaka miwili ya utekelezaji yameonesha mafanikio katika
ukuaji wa makusanyo yatokanayo kodi. |
|
Posted: 15 May 2013 09:32 PM PDT
N a Yu s u p h Mu s s a , Lushoto
BAADHI
ya walimu wilayani Lushoto wamefananisha elimu nchini na maghorofa
mabovu yanayojengwa jijini Dar es Salaam, kwani inazidi kushuka kutokana
na mfumo mbovu wa mitaala na uingizaji holela wa vitabu vya kufundishia
na kujifunzia shuleni. Wakizungumza juzi kwenye mkutano wa wakuu wa
shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya Bumbuli, uliondaliwa
na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa
Bumbuli,Bw. January Makamba, walisema Serikali ishirikishe wadau kwenye
utungaji wa mitaala. "Kama mchakato wa Katiba Mpya unavyoshirikisha
wadau, vivyo hivyo utungaji au uanzishwaji wa mitaala m i p y a i w a s h
i r i k i s h e wadau ili kupata mitaala itakayokubalika vinginevyo
elimu itaendelea kushuka. "Itazidi kuporomoka kwa vile haina misingi
mizuri. Hivi inakuwaje mtoto wa darasa la kwanza anakwenda shuleni na
madaftari tisa, turudishe utaratibu wa 'K' tatu yaani masomo ya Kusoma,
Kuandika na Kuhesabu" alisema Mratibu wa Elimu Kata ya Soni, Bi. Luth
Msagati. Mratibu wa Elimu Kata ya Milingano alisema mitaala iliyopo kwa
sasa hata walimu hawaijui, hivyo ni vigumu mwalimu kumfundisha
mwanafunzi akaelewa, huku akisema changamoto nyingine ni kuwaingiza
sekondari wanafunzi waliopata alama 70.Mkuu wa Shule ya Sekondari Kwa
Mongo,Bw. Anthony Kihiyo, alisema kwa Serikali kuruhusu wanafunzi
wa shule za kata na zile za Mtakatifu kufanya mtihani mmoja ni sawa na
kumpambanisha Francis Cheka na mgonjwa aliyelazwa Hospitali ya
Muhimbili. "Wanafunzi wa shule za kata kufanya mtihani mmoja na wale wa
shule binafsi ni kuwaonea. Hata mabondia uzito wao unapimwa na unatakiwa
ulingane ndipo wapigane," alisema,Bw. Kihiyo. Kwa upande wake Bw.
Makamba alisema pamoja na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuunda tume ya
kuchunguza kiini cha matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka jana, bado
walengwa ambao ni walimu hawajapewa nafasi ya kutoa maoni yao juu ya
suala hilo . |
|
Posted: 15 May 2013 09:27 PM PDT
Na Allan Ntana, Tabora
SERIKALI
mkoani Tabora, kupitia kwa Ofisa madini mkazi wa mkoa huo, BW. Elias
Mutelani, imeagiza kufungwa kwa machimbo ya dhahabu yaliyopo katika
kijiji cha Kapumpa, kata ya Kitunda, wilayani Sikonge, mkoani humo na
wachimbaji wote wameamriwa kuondoka mara moja katika eneo hilo ili
kuweka utaratibu na usimamizi mpya wa uchimbaji madini hayo. Ak i t o a t
a a r i f a y a kufungwa kwa machimbo hayo, Bw. Mutelani alisema kuwa
Serikali ya mkoa imeagiza kufungwa mara moja kwa shughuli zote za
uchimbaji
katika eneo hilo ili kuweka utaratibu mpya utakaowezesha shughuli za
uchimbaji zifanyike kwa utaratibu unaoeleweka vizuri zaidi. Akizungumzia
agizo la kufungwa machimbo hayo afisa mtendaji wa kata ya Kitunda, Bw.
Julius Ndege, alisema ni kweli machimbo yamefungwa rasmi, lengo likiwa
ni kuweka utaratibu mzuri wa namna gani uchimbaji wa madini hayo uweze
kufanyika na kubainisha kuwa agizo hilo limetolewa na uongozi wa
Serikali ya mkoa. Kufungwa kwa machimbo hayo kumeleta kizaazaa na hali
ya sintofahamu kwa wachimbaji zaidi ya 4,000 waliokuwepo katika eneo
hilo, baada ya Mei 3, mwaka huu kukuta mabango la kuwataka waondoke. Wa k
i z u n g u m z a n a waandishi wa habari mkoani hapa, Mwenyekiti wa
wachimbaji hao, George Mtasha, alisema baada ya kupewa amri ya kuondoka,
baadhi yao walipotea njia na wengine zaidi ya 2,000 walilazimika
kutembea kwa miguu hadi Sikonge mjini umbali wa zaidi ya kilomita
kutokana na kukosa nauli. Bw. Mtasha alibainisha kuwa askari walipofika
katika machimbo hayo, walianza kuwafukuza huku wakichoma mahema ambayo
walikuwa wakitumia kulala. Katibu wa kamati ya wachimbaji hao, Bw.
Ibrahim Tundu, alisema kuwa katika eneo hilo dhahabu ipo ya kutosha sana
na hadi sasa kuna askari polisi ambao wamebakisha wachimbaji wachache. | |
Posted: 15 May 2013 09:06 PM PDT
Na Salim Nyomolelo
MBUNGE
wa Fuoni kwa tiketi ya CCM, Bw.Said Mussa Zuberi, ameshangazwa na
wabunge kupitisha bajeti za wizara mbalimbali, lakini fedha hizo
hazipelekwi kama zinavyoidhinishwa.
Alitoa
kauli hiyo mjini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya
Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2013/2014. Alisema inashangaza
wabunge kupitisha bajeti, lakini
fedha zinazotolewa ni kidogo na vilevile hazipelekwi zote kwenye wizara husika.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya CCM,jijini Dar es
Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM
(NEC), Bw. Nape Nnauye, alisema mkutano wa Kamati Kuu ya CCM uliofanyika
hivi karibuni, umeitaka Serikali kuhakikisha mizizi inang’olewa ili
kukomesha matukio ya aina hiyo.
Nape
alisema kuwa CCM i m e r i d h i s h w a n a h a t u a zilizochukuliwa
na Jeshi la Polisi wakati wa tukio hilo. Alisema Kamati Kuu, ililaani
matukio hayo kutokana na kuwa yanavuruga amani, upendo na umoja wa
Watanzania.
“Kamati
Kuu imeishauri Serikali kuongeza kasi kuwasaka na kung’oa mzizi huo ili
kukomesha vitendo vya namna hiyo,” alisema, Bw. Nape
Hata
hivyo, Bw. Nape alisema Mei 18 na 19 mwaka huu Mwenyekiti wa CCM, Rais
Jakaya Kikwete, atakutana na wabunge wa chama chake pamoja na
sekretarieti ya chama ili kupata maoni ya wabunge pamoja na kushauriana
katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Akijibu
maswali ya waandishi wa habari, Bw. Nape alisema kuwa miongoni mwa
ajenda zitakazozungumzwa ni pamoja na utekelezaji wa ilani ya chama na
mwenendo wa maendeleo pamoja na kuweka mikakati thabiti ya maendeleo.
“Kikao
kitakuwa kati ya mwe n y e k i t i , wa b u n g e n a sekretarieti
ambayo ndiyo wamiliki wa ilani inayotekelezwa,” alisema.
Alisema
kuwa baada ya kikao hicho na wabunge hao, Kamati Kuu ya CCM itakutana
tena Mei 20 na 21 ili kujadili mambo yatakayoongelewa katika kikao cha
wabunge.
|
|
Posted: 15 May 2013 09:06 PM PDT
Na Goodluck Hongo
MBUNGE
wa Fuoni kwa tiketi ya CCM, Bw.Said Mussa Zuberi, ameshangazwa na
wabunge kupitisha bajeti za wizara mbalimbali, lakini fedha hizo
hazipelekwi kama zinavyoidhinishwa.
Alitoa
kauli hiyo mjini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya
Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2013/2014. Alisema inashangaza
wabunge kupitisha bajeti, lakini fedha zinazotolewa ni kidogo na
vilevile hazipelekwi zote kwenye wizara husika.
Alitolea mfano mradi wa Kurasini jijini Dar es Salaam, ambapo zilitakiwa zitolewe zaidi ya sh. bilioni
120 kwa ajili ya mradi huo, lakini ni kiasi cha sh.bilioni 10 ndizo zilizotolewa na Serikali.
“Kama
kwe l i t u n a t a k a kutengeneza ajira kwa kusaidia vijana zaidi ya
100,000, kwa nini bunge likipitisha bajeti ya Wizara fedha hazipelekwi
zote?”Alihoji Bw. Zuberi.
Alibainisha
kuwa mradi huo wa Kurasini ambapo Wachina wangewekeza zaidi ya
sh.bilioni 60 unashindikana hadi leo kutokana na Wizara kutopewa fedha
zote kama ilivyoomba katika bajeti iliyopita, ambapo watu wengi
wangepata ajira.
Alishangazwa
na kitendo cha bunge hilo kutenga muda kidogo kuchangia bajeti ya
wizara hiyo wakati hiyo ndiyo wizara muhimu kwani ndiyo inatoa ajira
kupitia viwanda.
Naye
Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Bw. Nimrod Mkono, alisema hawezi
kuunga mkono hoja ya bajeti ya wizara hiyo hadi pale atakapopata majibu
kutoka kwa Waziri, Dkt.Abdalaah Kigoda, kuhusiana na matatizo ya wizara
hiyo.
Alisema
ofisi ya Brela imeoza na haifai kuendelea kutoa huduma hizo, kwani hata
ofisini haina viti wala meza, majalada yamejaa na yametunzwa holela
hadi karibu na chooni.
Alisema
mtu anachukua miaka kati ya miwili hadi mitatu ndipo apate usajili.
“Ofisi ya Brela imeoza nakuomba waziri fumua hii na kuisuka upya kwa
mazingira hayo hataweza kufanya biashara kwa hali hii, kwani wizara hii
ina matatizo makubwa lakini hawa Brela wanafanya nini kwa kweli siungi
mkono hoja hadi nipate majibu ndiyo nitaunga mkono hoja,” alisema Bw.
Mkono
Naye
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa,
alisema wamachinga nchini wamekuwa wakipigwa mabomu badala ya wahusika
kukaa chini na kutafuta njia ya kutatua matatizo yao.
Akiwasilisha
bajeti ya Wizara yake kwa mwaka 2013/2014 Waziri wa Viwanda na
Biashara, Dkt. Kigoda aliliomba bunge kupitisha kiasi cha zaidi ya
sh.bilioni 108 kwa mwaka wa fedha ujao ili Wizara iweze kutekeleza
majukumu yake.
Alisema
sh. bilioni 29 zitatumika katika matumizi ya kawaida, sh. bilioni 22
kulipa mishahara na sh. bilioni 78 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
|
|
Posted: 15 May 2013 08:56 PM PDT
Na Esther Macha, Mbeya
WANAFUNZI
15 wa Shule ya Sekondari ya Wazazi ya Lupata wilayani Rungwe, mkoani
Mbeya wanashikiliwa na polisi kwa kosa la kuchoma moto bweni wakipinga
hatua ya wanafunzi wenzao kusimamishwa masomo kwa utovu wa nidhamu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Diwani
Athuman, alisema tukio hilo lilitokea Mei 14, mwaka huu saa 2.00 usiku.
Kamanda Athuman alisema kuwa wanafunzi hao baada ya
kuona wenzao watatu wamesimamishwa masomo walianza kufanya vurugu usiku
na kuanza kuchoma moto bweni moja la wanafunzi wa kiume. Kamanda
Athuman aliwataja wanafunzi waliosimamishwa masomo kwa utovu wa nidhamu
shuleni hapo kuwa ni, Joseph Robert (18), Mwita Chacha na Daniel David
(18).
“Hawa
wanafunzi watatu waliosimamishwa masomo walihamasisha wenzao kuunga
mkono kupinga adhabu hiyo kwa kufanya vurugu na kuchoma bweni
hilo,”alisema Kamanda Athuman.
Alisema
bweni lililochomwa moto walikuwa wanaishi wanafunzi ambao hawakuwa
tayari kuunga mkono uvunjifu huo wa amani shuleni hapo. Aidha Kamanda
Athuman alisema wanafunzi 15 wanashikiliwa na polisi wakiwemo vinara wa
fujo hizo.
Kuhusu
mali zilizoharibiwa, Kamanda huyo alisema thamani halisi ya uharibifu
uliotokea bado haijajulikana. Kamanda Athuman ametoa wito kwa jamii hasa
wanafunzi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume
cha sheria na badala yake watatue matatizo kwa njia ya mazungumzo kwa
kufuata mamlaka husika.
|
|
Posted: 15 May 2013 08:53 PM PDT
Na Sophia Fundi, Karatu
HOS
P ITALI Te u l e y a Karatu wilayani hapa nusura igeuke uwanja wa
masumbwi baada ya kutokea mgogoro mkubwa baina ya pande mbili zilizokuwa
zikigombea maiti kuhusu eneo atakalozikwa marehemu.
Tafrani
hiyo ilidumu kwa saa kadhaa mjini hapa jirani na chumba cha kuhifadhia
maiti. Hali hiyo ilitokea baada ya mume wa marehemu, Bw. Sauli Zakaria,
kutaka kwenda kumzika mke wake, Eliza Mathayo, nyumbani kwao mkoani
Mtwara.
Hata hivyo ndugu wa marehemu waligoma wakihoji iweje
azikwe
mbali na nyumba yake waliyokuwa wakiishi. Wakizungumza na gazeti hili,
ndugu wa marehemu walisema hawakubaliani na ndugu yao kuzikwa mbali
(mkoani Mtwara) kwani ndugu zake wengine hawataweza kwenda kushiriki
mazishi.
Akizungumza
kwa njia ya simu baada ya ndugu hao kuzuia maiti hiyo, iliyokuwa
isafirishwe jana saa nane mchana kwenda Mtwara, mume wa marehemu, Bw.
Zakaria alisema yeye kama mume wa marehemu ndiye ana mamlaka ya kupanga
ni wapi azikwe mke wake.
Alisema
anashangazwa na ndugu hao kukataa asimzike mke wake ambaye walimpa
akiwa hai na kufunga naye ndoa halali. “Leo hii wananikatalia nisimzike
ninakotaka... mimi naamua kuwaachia maiti yao na mimi nitaondoka na
watoto wangu,”alisema Bw. Zakaria na kuongeza;
“Nimeamua
kuwaachia maiti yao hivyo naishia zangu na watoto wangu, wamzike mtu
wao.” Baada ya malumbano hayo yaliyochukua muda mrefu, Bw. Zakaria
aliwashukuru majirani waliokuwa wamekusanyika nyumbani kwake na kuwataka
kutawanyika kwani msiba hautakuwepo katika eneo hilo.
Baada
ya kutoa kauli hiyo alifunga mlango wa nyumba yake na kwenda
kusikojulikana huku akiacha maiti ya mke wake hospitali kwenye chumba
cha kuhifadhia maiti.
Alipoulizwa
kuhusiana na hali hiyo Katibu wa Hospitali hiyo, Bi. Joyce Kajivo,
alisema kuwa wao kama viongozi wa hospitali wanasubiri maamuzi ya mume
wa marehemu kwani yeye ndiye mwenye maamuzi ya wapi amzike mke wake na
taratibu zote za hospitali zimekamilika.
|