NAIBU Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mwiguru Nchemba, amesema
Serikali imevutiwa na utendaji kazi mzuri wa Taaisisi ya kifedha ya UTT
Microfinance kuwa na matawi 10 katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa muda mfupi.
Akizungumza wakati wa kukata utepe kuzindua rasmi Taasisi hiyo
Sukari House Dar es Salaam jana, Naibu Waziri amesema, Serikali imefurahishwa na
dhamira ya kweli ya kufikisha huduma za kifedha karibu na wananchi kila pembe
ya nchi kunakofanywa na UTT.
“Hii inaonyesha, mmeshaanza kutoa aina nane ya huduma kama
mikopo, uwakala wa Bima, Uwakala wa Benki, uwakala mkuu wa mitandao ya
simu (mobile money super agent) kwa mwaka mmoja tangu kuanzishwa”.
Bw. Nchemba amesema, kazi kubwa iliyoifanya ndani ya muda mfupi
na kuwa na matawi 10 katika maeneo mbalimbali ya nchi yameifurahisha na kuahidi
kuwa Serikali itatoa ushirikiano wa karibu kwa taasisi hiyo ili iweze kufikia
malengo iliyokusudia.
Naibu Waziri amebainisha kuwa uwa serikali iliamua kwa makusudi
kuanzisha taasisi hiyo ili kuwezesha wananchi kiuchumii hususan wenye miradi,
kama biashara ndogondogo na za kati ambao wamekuwa wakipata changamoto nyingi
katika kupata mikopo na huduma nyingine za kifedha toka taasisi kubwa za
kifedha na mabenki ya biashara ambayo mara nyingi muundo na mfumo wa
taasisi hizo huambatana na masharti magumu.
“Wengi walishindwa kupata mikopo stahiki kutokana na masharti,
hususani wenye vipato vya chini, sharti la dhamana ya mali isiyo hamishika kama
nyumba, kiwanja na mali, ambavyo hawana”, anasema Bw. Nchemba na kusisitiza
kuwa Serikali imeanzisha UTT Microfinance kuchochea ukuaji wa uchumi na
kuwainua watanzania walio wengi.
Awali kabla ya uzinduzi huo, UTT Microfinance imezindua rasmi
mtandao wa matawi sehemu mbalimbali nchini kwa lengo la kufikisha huduma za
kifedha karibu na wananchi hususan mikopo nafuu kwa wajasiriamaliri ambapo
matawi 10 yaliyopo katika miji ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Mbeya, Mwanza
na Zanzibar ulizinduliwa rasmi katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na
viongozi mbalimbali, wakurugenzi wa mashirika, Makampuni na Taasisi mbalimbali
pamoja na wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Mweneykiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya UTT MFI
Balozi Fadhili Mbaga, alisema watahakikisha kuwa UTT MFI inatekeleza azma yake
kwa ufanisi na pia itashirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali.
“Tunapenda kusisitiza dhamira yetu ya kuendelea kushirikaiana na
wadau mbalimbali hususan Tanzania Microfinance Association katika jitihada za
jumla za kuwa na mfumo mzuri wa huduma za kifedha na mitaji midogo na
kuhakikisha kuwa huduma hizi zinawafikia watanzania wengi zaidi na kuwa chachu
muhimu ya maendeleo ya jamii yetu”, anasema Balozi Mbaga.
Ameishukuru serikali kwa ushirikiano inayotoa kwa taasisi hiyo
na kuahidi kuzifanyia kazi changamoto zilizo mbele yao kuhakikisha wanavuka
malengo waliyojiwekea. ameiomba serekali isisite kuwaunganisha na wabia na
washirika mbalimbali ili kuwa na mtandao mpana zaidi wenye nguvu ya kuwafikia
wananchi wengi zaidi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa UTT MFI James Washima, alisema wanaamini
Serikali haikufanya makosa hata kidogo katika kuanzisha UTT MFI, akiahidi
kututumia uzoefu wao wa mwaka mmoja, ambao umebaini kuwa huduma za kifedha na
mikopo hususan kwa wajasiriamali na watanzania wa kada za kati na chini zilisubiriwa
kwa hamu kubwa sana.
Bw. Washima amesema kiu ya Watanzania kwa huduma za UTT hivyo
taasisi yao imejipanga kutoa huduma nzuri. Ameahidi kuwa ndani ya miezi sita wataongeza
idadi ya wafanyakazi kwani waliopo ni wachache ambapo mfanyakazi mmoja
anahudumia wateja zaini ya 1,000.
“Huu ni muitikio mzuri
kutoka kwa jamii na sisi tunajitahidi kukabiliana nao kwa ufanisi” anabainisha
Bw. Washima na kuongeza kuwa hivi sasa wana matawi 10, manne yakiwa Dare
s Salaam - Sukari House, Azikiwe, Kijitonyama na Chang’ombe.
Bw. Washima anayataja matawi mengine kuwa ni Arusha lililopo Ngarenaro,
Meru lililopo Jengo la Posta Meru, Dodoma lililopo Posta Dodoma, Mbeya barabara
ya KKKT, Mwanza katika jengo la Posta na Zanzibar, Jengo la Posta Kijangwani.
Akizungumzia m,afanikio ndani ya mwaka mmoja wa uwepo wao, Bw.
Washima anasema wameweza kukuza mtaji wa Taasisi toka Shilingi billion
5.4 mnamo Julai mwaka 2013 na kufikia bilioni 12 Juni, 2014. Pia taasisi imefanikiwa kutoa
mikopo yenye thamani ya Tsh 5.316 bilioni, kwa wakopaji
6,102 – huku 84% ya wakopaji wote wakiwa ni wanawake.
Anabainisha kuwa pia wameanzisha huduma za moja kwa moja kwa muhusika
(Tailor-made) kama vile mikopo kwa ajili ya Bima ya matibabu, Hati Malipo
(Contract Financing loans), mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali wadogo wadogo (Group
loans), Mikopo kwa ajili ya SACCOS, Mikopo maalumu kwa miradi inayolenga
kuongeza thamani ya bidhaa na ajira ikiwemo viwanda vidogo vidogo, mikopo kwa
wafanyakazi wa Serikali. Hata hivyo, pamoja na mafanikio makubwa
yaliyopatikana, Washima alieleza baadhi ya changamoto zinazowakabili ikiwa
kuibuka kwa taasisi na kampuni zisizo rasmi ambazo hutoa huduma za kifedha
hususan mikopo kwa watu wa kada za chini.
Mtendaji huyo amesema mengi ya makampuni haya mara huwa ya
kilaghai na yenye kuchukua riba kubwa bila utaratibu maalum suala ambalo badala
ya kuwasaidia watu, huwaumiza na kuwaua kabisa kiuchumi.
“Tunaiomba serikali iharakishe utungwaji wa sera ya kurasimisha
huduma hizi ili zifanywe kwa utaratibu maalum na pia ziratibiwe na kudhibitiwa
vizuri ili wananchi wasiendelee kutaabika na kufilisiwa na watu wasio na nia
njema ambao hutumia fursa ya udhaifu wa kisera kujinufaisha” alisema Washima.
UTT MFI ni Taasisi ya huduma za fedha na mikopo iliyoanzishwa
mnamo Juni 2013 kwa lengo la kutekeleza sera za serikali katika uwezeshaji
kiuchumi hususan kwa wajarisiamali, watumishi wa umma, wakulima, wenye viwanda
vidogo, watu wasio na ajira rasmi na wananchi wote kwa ujumla.
UTT MFI pia inalenga kuwapa fursa wamiliki wa
Vipande vya UTT AMIS kutumia vipande vyao kama dhamana wakati wa kuchukua
mikopo, kupanua wigo na kurahisisha uwekezaji wa vipande vya UTT na hivyo
kukuza utamaduni wa kuwekeza kwa wananchi.