Ajali
za Madereva wa Pikipiki(Bodaboda) Barabarani Zinaongezeka kila
kukicha kutokana na Madereva wengi wa pikipiki kuwa na mafunzo ya Muda Mrefu,
Kijana Jumanne juma, ambaye hayupo pichani muda mfupi baada ya kunusurika na
kuikimbia pikipiki katikati ya barabara kitendo ambacho pia ni chanzo cha
ajali.
Barabara
kuelekea Iringa
Hii
ndiyo Tanzania yetu unayosikia kila siku kuwa ina rutuba na rasilimali nyingi
kutokana na ardhi yetu, lakini kwa sasa unaweza kujiuliza imeisaidia vipi jamii
yake ya watanzania, lakini wakati ardhi kwa tanzania ikionekana kuwa siyo
tatizo, ongezeko la vijana kukimbilia mijini limezidi kuongezeka na hivyo
kujaza zaidi maeneo ya Mijini kuliko Vijijini, pamoja na kwamba wanaishi katika
mazingira ya kukabiliwa na tatizo la ajira kwa watu wake zaidi ikiwa Vijana.
Wakati
Tanzania inapata Uhuru, Mapambano makubwa kwa ardhi yake katika kutafuta
maendeleo ilikuwa ni kupata barabara zitakazounganisha katika ya mji, mkoa na
mkoa, watawala waliotangulia waliweza kuipigania zaidi na kwa kutumia umoja wao
katika kufanya vitu vya msingi ikiwa ni pamoja na kufanya barabara kati ya
mikoa ya iringa na morogoro inapitika kwa urahisi, lakini changamoto kubwa
waliyokutana nayo ilikuwa Milima Mikubwa. je Ingekuwa ni wakati huu ufanyike
ujenzi kama huu Tanzania ? Toa Maoni!!
Pamoja
na Kwamba kuna Taadhali kubwa zimewekwa Barabarani lakini bado Madereva Wetu
wanashindwa kuzingatia, je wanachukuliwa hatua zipi na Tanzania ama Wamiliki wa
Barabara(TANRODS) wamenufaika vipi na watu hao, ni kati ya matatizo ambayo
yameikumba Tanzania na hivyo kuzidi kutumia barabara zenye wembamba usiostahili
kupunguza ajali za barabarani.
Mkoa
wa Iringa ni kati ya Mikoa ambayo imevuma na kusikika muda mrefu, hivyo
ulitakiwa kuwa na maendeleo makubwa kwa kutumia ardhi na rasilimali walizonazo
za nguvu kazi, Mkoa wa Iringa ni kati ya Mikoa yenye Baridi muda Mwingi, lakini
je wakazi wa Mkoa huo wamenufaika vipi na Mkoa wao, ni vyanzo gani vya ajira
ambavyo Mkoa umejiwekea katika kuwawezesha vijana kutokimbilia miji ya Mbeya na
Dar es Salaam,
Miwa
ni kati ya Mazao ambayo miaka ya nyuma ilikuwa si adimu kama wakati wa sasa,
kutokana na kwamba wakazi wa zamani walikuwa wakithamini Mazao kama Kinga
Muhimu kwao kwa Chakula, Tofauti na sasa watu wengi kinga imekuwa ni hela mbayo
kama isipotafutwa uwezi kuwa na uhakika wa kuitunza familia kwa familia.
Mwendo
kasi ni hatari kwa maana ni chanzo cha ajali za barabarani, na hata pia
Matumizi Mazuri ya Barabara ni chanzo kizuri cha kuhepusha ajali, kuwa na tumia
uhangalifu barabarani.
Sehemu
nyingi za barabara chanzo kimojawapo cha ajali ni Kona, hivyo Madereva mnapaswa
kuwa waangalifu zaidi sehemu zenye kona kali.Kona hii ni katika Milima Kitonga.
Sehemu ambazo wakati wote Madereva wa Magari ya Abiria(BUS) upita wakiwa na
zaidi ya spidi 70, kitendo ambacho ni hatari na ni chanzo kimojawapo cha ajali.
Gari
la Mizigo likiwa limekatisha safari zake na kufunga nusu ya barabara, kitu
ambacho ni hatari kwa madereva wasiyokuwa waaangalifu barabarani.
Viwanja
Tatizo la Soka la Tanzania ama Soka na viwango kwa wachezaji ? ni kati ya
maswali ambayo watu wengi kwa Tanzania wameendelea kujiuliza, zaidi ikiwa ni
vijijini ambako sasa imekuwa kimya kusikiwa wakitokea wachezaji wenye
kutumainiwa na Taifa kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, lakini hata hivyo
ikionyesha kutokuwa na mwamko kwa kizazi cha sasa katika michezo kutokana na
wengi wa vijana kuwa na mawazo ya kutafuta pesa waweze kuishi, upungufu wa
kufika katika viwanja vya wazi limeendea kuikumba Tanzania na hivyo kuifanya
kuzidi kuwa na upungufu wa wachezaji wenye vipaji.
Moja
ya taswira ya maeneo ya Mikoa ya Tanzania. nchi ambayo inasadikika kuwa na
Demokrasia kubwa kuliko nchi ingine yeyote duniani, Ardhi ambayo mpaka sasa
Bado imeendelea kuyanufaisha Mataifa kutoka nje, kutokana na kukosa wataalamu
wa kutambua na kufanya uchunguzi wa Uwepo wa Baadhi ya Mazingira ambayo mara
nyingi yamekuwa yakiibuliwa na wageni , ambao mpaka sasa wameendelea kumiminika
katika kuomba kuwekeza.
Eneo
hili ni Moja ya Maeneo ambayo wakandarasi , eneo hili baada ya mradi kumalizika
kitakachofuata !!!
Tukumbuke
kukata miti kisha kupanda miti!!
Kitakachofuata
baada ya hapo unadhani ni nini,
(Picha Zote
kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania)