Mkurugenzi wa Stopper Entertainment, Mukhsin Mambo, akifafanua jambo kuhusiana na Mashindano ya Shule za Sekondari(Interschools Debate Compatations) |
Mwalimu wa Shule ya Bwiru Boys, George George, akichangia jambo wakati wa Semina ya Walimu wa Shule za Sekondari..
Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kitangiri ya jijini Mwanza, Luciana Ududa, akichangia jambo wakati wa Mafunzo hayo
Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Nyabulogoya ya jijini Mwanza, Witness Mbogora, akichangia jambo wakati wa Mafunzo hayo
Baadhi ya Walimu wa Shule za Sekondari waliofanikiwa kuhudhuria Seminja hiyo katika Ukumbi wa Kimataifa wa JB. Bellemonte Hoteli jijini Mwanza leo.
(Picha Zote kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).
===================================================
Mashindano
ya Mijadala kwa shule za sekondari mkoani Mwanza (Interschools Debate
Competition), yanatarajiwa kuanza septemba 02 mwaka huu.
Akizungumza
katika semina elekezi, iliyowakutanisha baadhi ya walimu wa mijadala
kutoka katika shule mbalimbali za sekondari mkoani Mwanza, mkurugenzi
wa Stoppers Entertainment ambao ndio waandaji wa shindano hilo, Bwana
Mukhsin Mambo, amesema jumla ya shule 32 kutoka mkoani Mwanza,
zitashiriki katika shindano hilo ambalo ni la kwanza kufanyika mkoani
humo na Tanzania kwa ujumla.
Mambo,
amesema shindano hilo pia litaonyeshwa kwenye moja ya runinga hapa
nchini kuwapa fursa watazamaji kushuhudia vipaji vya wanafunzi katika
kujieleza mbele ya jamii.
Amesema
nia na madhumuni ya shjindano hilo, mbali na kuondoka na kitita cha
zawadi kwa washindi lakini pia ni njia mojawapo ya kuinua kiwango cha
elimu hapa nchini kwa wanafunzi kupata nafasi ya kujieleza mbele za
watu, kufanya utafiti kutokana na mada itakayowekwa mezani, kuweka
mahusiano mema dhidi ya wanafunzi na kujenga kizazi kipya katika nyanja
ya elimu kupitia mfumo wa mijadala.
Miongoni mwa shule zitakazoshiriki shindano
hilo ni pamojana Nsumba sekondari, Nganza Sekondari, Butimba sekondari,
St. Joseph Girls Sekondari, Buswelu Sekondari, New Hellen Sekondari,
Hill crest Sekondari, Bismark Sekondari.
No comments:
Post a Comment