TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Saturday, February 18, 2012
Monday, February 13, 2012
JK AONANA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA URUSI LEO IKULU, DAR ES SALAAM
Rais
Jakaya Kikwete akiagana na mjumbe maalumu wa Rais wa Urusi Bw. Mikhail
V. Margelov Ikulu jijini Dar es salaam leo January 13 Februari
2012baada ya mazungumzo yao
PICHA NA IKULU
MC
Angel Catering and Decoration, Inakualika kwenye Usiku wa wapendanao
(Valentine Party) itakayofanyika siku ya Valentine Jumanne kwenye ukumbi
wa Makumbusho ndani MAKUTI HALL kuanzia saa 12:00 jioni, Chakula,
Vinywaji na Muziki kwa Wapendanao vitakuwepo pamoja na zawadi
mbalimbali.
Price: 50,000 Tshs. KWA DOUBLE
SIMU
0714-800225 Angel.
0715-686358 Monica Mariam
0754-265689 Doreen
0712-710621 Makala John.
MWENYEKITI
WA KAMATI YA SHEREHE AMBAYE NI MKURUGENZI WA UENDESHAJI WA NHIF BWN.
EUGEN MIKONGOTI HAKUWA NYUMA KATIKA KUWAKARIBISHA WAALIKWA KATIKA
SHEREHE HIYO.
MAMBO YA KWAITO HAYAKUWA NYUMA TIMU YA WANA NHIF IKIJIMWAGA KAMA KAWA, KWANI NI SEHEMU YA KUJENGA AFYA.
MAFANNIKIO
YOYOTE HAYAWEZI KWENDA BILA UWEPO WA MWANAMKE,MAMA MKURUGENZI AKIFANYA
MAMBO MENYU HUKU AKIAMBATANA NA MKURUGENZI MKUU KATIKA KUFANYA
MAJUMUISHO NA MAKARIBISHO YA MWAKA MPYA.
Na Faki Mjaka Maelezo Zanzibar 13/02/2012
Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko Zanzibar imetoa ufafanuzi juu ya hali ya ununuzi na uhifadhi wa Zao la Karafuu Kisiwani Pemba kutokana na taarifa zilizochapishwa na Gazeti la Daily News la Februari 4 mwaka huu ambapo inadaiwa kwamba wakulima wa Zao la Karafuu wamekataa kuliuzia Shirika la Taifa la Biashara la Zanzibar ZSTC
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Wizara hiyo imesema kuwa kauli hiyo siyo sahihi na wakulima bado wanaendelea kuliuzia Shirika hilo Karafuu zao kama ilivyopangwa ambapo hadi sasa jumla ya Tani 588.735 zenye thamani ya Tshs 8,824,850,750.00 zimeuzwa kwa Shirika hilo kwa Wilaya ya Micheweni tu.
Aidha kwa Wilaya ya Wete jumla ya tani 1,530.536 za Karafuu zenye thamani ya Tshs 22,923,724,500.00 zimeshauzwa kwa ZSTC jambo ambalo linaonesha utayari wa wakulima kuliuzia Shirika hilo.
Taarifa hiyo pia imefafanua kwamba Mkulima anaruhusiwa kuhifadhi karafuu zake kwa muda apendao iwapo tu Karafuu hizo zitahifadhiwa katika Maghala ya ZSTC na Mkulima hupewa Stakabadhi inayoonesha kiasi kinachohohifadhiwa ambapo kwa sasa kuna idadi kubwa ya wakulima wanaotumia utaratibu huo wa kuzihifadhi na kuziuza kwa siku za usoni.
Serikali ilichukua hatua hiyo ya uhifadhi kwenye maghala salama ya ZSTC kwa lengo la kuziepusha Karafuu Kusinyaa,kupungua kwa daraja la ubora na kuziepusha kushika moto,mambo ambayo yanaweza kupelekea maafa na kumkosesha mkulima faida iwapo zitahifadhiwa nyumbani
Kuhusu madai ya bei ya Karafuu taarifa hiyo imesema ukweli ni kuwa katika bei ya soko la dunia kilo moja inauzwa kwa Dola za Marekani 11-13 ambapo wastani wake ni sawa na Tshs 17,270 hadi 20.410 jambo ambalo linaifanya tofauti kati ya soko la ndani na nje iwe ni kati ya Tshs. 2,270 hadi 5,410
Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko Zanzibar imetoa ufafanuzi juu ya hali ya ununuzi na uhifadhi wa Zao la Karafuu Kisiwani Pemba kutokana na taarifa zilizochapishwa na Gazeti la Daily News la Februari 4 mwaka huu ambapo inadaiwa kwamba wakulima wa Zao la Karafuu wamekataa kuliuzia Shirika la Taifa la Biashara la Zanzibar ZSTC
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Wizara hiyo imesema kuwa kauli hiyo siyo sahihi na wakulima bado wanaendelea kuliuzia Shirika hilo Karafuu zao kama ilivyopangwa ambapo hadi sasa jumla ya Tani 588.735 zenye thamani ya Tshs 8,824,850,750.00 zimeuzwa kwa Shirika hilo kwa Wilaya ya Micheweni tu.
Aidha kwa Wilaya ya Wete jumla ya tani 1,530.536 za Karafuu zenye thamani ya Tshs 22,923,724,500.00 zimeshauzwa kwa ZSTC jambo ambalo linaonesha utayari wa wakulima kuliuzia Shirika hilo.
Taarifa hiyo pia imefafanua kwamba Mkulima anaruhusiwa kuhifadhi karafuu zake kwa muda apendao iwapo tu Karafuu hizo zitahifadhiwa katika Maghala ya ZSTC na Mkulima hupewa Stakabadhi inayoonesha kiasi kinachohohifadhiwa ambapo kwa sasa kuna idadi kubwa ya wakulima wanaotumia utaratibu huo wa kuzihifadhi na kuziuza kwa siku za usoni.
Serikali ilichukua hatua hiyo ya uhifadhi kwenye maghala salama ya ZSTC kwa lengo la kuziepusha Karafuu Kusinyaa,kupungua kwa daraja la ubora na kuziepusha kushika moto,mambo ambayo yanaweza kupelekea maafa na kumkosesha mkulima faida iwapo zitahifadhiwa nyumbani
Kuhusu madai ya bei ya Karafuu taarifa hiyo imesema ukweli ni kuwa katika bei ya soko la dunia kilo moja inauzwa kwa Dola za Marekani 11-13 ambapo wastani wake ni sawa na Tshs 17,270 hadi 20.410 jambo ambalo linaifanya tofauti kati ya soko la ndani na nje iwe ni kati ya Tshs. 2,270 hadi 5,410
Mwenyekiti
wa CCM, Rais Kikwete akiwasili ukumbini kuendesha kikao cha
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM jana kwenye ukumbi wa Sekretarieti,
Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto Mwenyekiti wa CCM Mstaafu Ali
Hassa Mwinyi, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Sheni na Makamu
Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Amani Abeid Karume. Kulia ni makamu
Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na Katibu Mkuu wa CCM Wilson
Mukama.
Wajumbe wa NEC kutoka Tanzania Bara wakiunga mkono marekebisho ya Katiba ya CCM yaliyopitishwa na NEC
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za
kifo cha aliyewahi kuwa mjumbe wake wa Kamati ya Utendaji, Kassim
Kashulwe kilichotokea Februari 9 mwaka huu nyumbani kwake Kigurunyembe
mkoani Morogoro.
Licha
ya kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF (wakati huo Chama cha
Mpira wa Miguu Tanzania- FAT), pia Kashulwe aliwahi kuwa kiongozi wa
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) na baadaye kamishna wa
mechi za Ligi Kuu.
Kwa
mujibu wa taarifa tulizopata leo (Februari 13 mwaka huu) kutoka MRFA,
Kashulwe alifia nyumbani kwake na kuzikwa juzi (Februari 11 mwaka huu)
kwenye makaburi ya Kora yaliyoko nje kidogo ya mji wa Morogoro.
Mbali
ya Kashulwe, wengine waliochaguliwa katika uchaguzi wa FAT uliofanyika
mwaka 1993 mjini Kibaha ni Muhidin Ndolanga (Mwenyekiti), Alhaji Omari
Juma (Makamu Mwenyekiti) na Kanali Ali Hassan Mwanakatwe (Katibu Mkuu)
na wajumbe Abdul Msimbazi, Amin Bakhresa, Job Asunga, Joel Bendera,
Masalu Ngofilo na Wilson Mwanja.
Msiba
huo ni pigo kwa familia ya Kashulwe, TFF na familia ya mpira wa miguu
nchini kwa kuwa mchango wake ulikuwa bado unahitajika.
TFF
inatoa pole kwa familia ya marehemu Kashulwe, na MRFA na kuwataka kuwa
na uvumilivu kipindi hiki cha msiba huo mzito. Pia TFF itatoa ubani wa
sh. 200,000 kwa familia ya marehemu kama rambirambi zake.
Mungu aiweke roho ya marehemu Kashulwe mahali pema peponi. Amina
KITUO
cha maraha cha Dar Live kilichoko Mbagala jijini Dar kilirindima kwa
vifijo vya burudani ya muziki kutoka vikundi mbalimbali vya wasanii.
Ilikuwa
ni ‘kufuru tupu’ wakati wasanii AY akishirikiana na Mwana FA
walipotoana jasho na wenzao kina Chegge na Temba kutoka katika kundi
la Wanaume Family yote hayo yakisindikizwa na burudani kutoka kundi la
taarab la East Africa Melody, Wakali Dancers, Dogo Aslay, Shilole na
bendi ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga Pepeta..
AY (kushoto) na Mwana FA wakikamua.
We
are delighted to announce that CFAO MOTORS TANZANIA, on behalf of CFAO
SOLIDARITY in France, is donating TZS 22m to help CCBRT Hospital.
CFAO
has been involved in business in Africa for over 125 years. The group
employs around 9,200 staff in 31 African countries and 7 French
overseas territories. Since its future is inextricably linked with that
of Africa, it is only right that CFAO should assist in its development.
Via
its various lines of business, CFAO makes its contributions to
sustainable development issues in Africa and is forging ahead with a
far-reaching strategy in terms of Corporate Social Responsibility.
At
CFAO MOTORS TANZANIA we have studied with great admiration the truly
amazing work that CCBRT does. We have persuaded our head office to
provide financial support so that CCBRT can continue to do wonders in
our society.
We
all know how difficult it is sometimes for sick or disabled people in
our country to get quality medical care, even for the most basic
ailments. CCBRT has been fantastic in ensuring medical care is available
to the community and at the most affordable prices.
We
have also noted that monies donated to CCBRT are always used in a
responsible manner for the maximum benefits of its patients. This makes
us very comfortable supporting the project as we know that our money
will definitely benefit the needy.
On
behalf of CFAO SOLIDARITY in France and CFAO MOTORS TANZANIA, I would
like to present this cheque which I am sure will be put into good use in
the community.
Watoto
wanaolelewa katika kituo cha yatima cha Taifa cha Kurasini kilichopo
jijini Dar es Salaam,wakishindana kuvuta kamba wakati wa hafla ya
kukabidhiwa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula na ngua vyenye
jumla ya shilingi milioni 10.Vilivyotolewa na Blogs ya U-turn kwa
kushirikiana na wasomaji wake wakuu.
.Ofisa
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiwa
amebeba mmoja wa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha kulea
watoto yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam.Wakati wa blog ya
U-turn kwa kushirikiana na wasomaji wake wakuu walipokwenda kutoa msaada
wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na nguo vyenye jumla ya shilingi
Milioni 10.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano akifurahia pamoja na watoto yatima
walipofika katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira
magumu cha Kurasini jijini Dar es Salaam,msaada wa vyakula na vitu
mbalimbali uliokuwa na thamani ya shilingi Milioni 10 ulitolewa na
U-turn blog kwa ushirikiano wapamoja na wasomaji wakuu wa Blog hiyo.
Watoto
wanaolelewa katika kituo cha yatima cha Taifa cha Kurasini kilichopo
jijini Dar es Salaam,wakishindana kuvuta kamba wakati wa hafla ya
kukabidhiwa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula na ngua vyenye
jumla ya shilingi milioni 10.Vilivyotolewa na Blogs ya U-turn kwa
kushirikiana na wasomaji wake wakuu.
Mmoja
wa wasanii wanaochipukia Dogo Aslay akiwapagawaisha watoto wa
naolelewa katika kituo cha Yatima cha Kurasini cha jijini Dar es
Salaam,kwa wimbo wa naenda kusema kwa mama, wakati wa hafla ya Blogs ya
U-turn kwa kushirikiana na wasomaji wake wakuu walipokwenda katika
kituo hicho kutoa misaada mbalimbali ikiwemo vyakula na nguo vyote
vyenye thamani ya shilingi milioni 10.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk,Mwinyihaji Makame akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na
malengo, mafanikio ya Wizara yake kwa kipindi cha miezi sita kuanzia
Julay hadi Disemba.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk,Mwinyihaji Makame akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana
namalengo na mafanikio ya Wizara yake kwa kipindi cha miezi sita kuanzia
Julai hadi Disemba
Kuliani kwake ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Salum Maulid.na kushoto kwake ni Naibu katibu Mkuu idara Maalum Capt,Abdalla Juma.
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa katika kikao chake cha siku moja chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa Taifa Dr. Jakaya M. Kikwete, pamoja na mambo mengine imetoa ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea wa CCM kwa uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki. Katika kikao chake hicho kilichofanyika tarehe 12/02/2012 mjini Dodoma, NEC pia imetoa ratiba ya mchakato wa kuwapata wagombea udiwani kwa tiketi ya CCM kwenye kata nane zilizotangazwa kufanya chaguzi Ndogo na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
1. UBUNGE: Katika nafasi ya Ubunge kwa Arumeru Mashariki, utaratibu utakaotumika ni ule wa kupiga kura za maoni kwenye Mkutano Mkuu wa Jimbo. (i) Tarehe 13 – 18/02/2012 Kuchukua na kurejesha fomu. (ii) Tarehe 20/02/2012 Mkutano Mkuu wa Jimbo kupiga Kura za maoni. (iii) Tarehe 21/02/2012 Kamati ya Siasa ya Wilaya kujadili Wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati ya Siasa ya Mkoa. (iv) Tarehe 24/02/2012 Kamati ya Siasa ya Mkoa kujadili Kutoa mapendekezo yake kwa Kamati kuu. (v) Tarehe 27/02/2012 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kufanya uteuzi wa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi.
2. UDIWANI Nafasi ya Udiwani katika kata 8 za Tanzania Bara Katika nafasi hii kura za maoni zitapigwa kwenye Mikutano Mikuu ya Matawi. (i) Tarehe 13 – 16/02/2012Kuchukua na kurejesha fomu. (ii) Tarehe 17 – 21/02/2012 Kampeni za Uchaguzi kwenye Matawi. (iii) Tarehe 22/02/2012Mikutano Mikuu ya Matawi kupiga kura za maoni. (iv) Tarehe 25/02/2012 Kamati za Siasa za Wilaya kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati za Siasa za Mikoa. (v) Tarehe 27/02/2012 Kamati za Siasa za Mikoa kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu za Mikoa. (vi) Tarehe 29/02/2012 Halmashauri Kuu za Mikoa kufanya uteuzi wa wagombea.
Katika hatua nyingine Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imepokea maelezo juu ya mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya na maelezo juu ya mgomo wa madaktari nchini.
Kwa ujumla NEC imepokea maelezo hayo kutoka serikalini na kuiagiza serikali kukamilisha mchakato wa kumaliza kabisa mgogoro wa madaktari nchini na kuhakikisha migogoro ya namna hiyo inashughulikiwa mapema ili isiwe na madhara makubwa kwa wananchi.
NEC imeridhishwa na jinsi mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya unavyoendelea na kuipongeza serikali kwa jinsi inavyolisimamia swala hilo. Imewataka wana CCM na wananchi wote kushiriki mchakato huo, huku wakizingatia kutunza amani na utulivu uliopo nchini.
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imewapongeza viongozi, wanachama na wananchi wa Mkoa wa Mwanza kwa jinsi walivyofanikisha sherehe za miaka 35 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi ambapo kitaifa mwaka huu zilifanyika mkoani humo.
Sherehe hizo ziliandaliwa na kufanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu kabisa, hivyo NEC inawapongeza kwa kufanikisha sherehe hizo. Pamoja na Mkoa wa Mwanza NEC inawapongeza wanachama, viongozi na wananchi kwa ujumla nchi nzima kwa jinsi walivyofanikisha sherehe hizo za miaka 35 ya kuzaliwa kwa CCM kwenye maeneo yao.
Imetolewa na; Nape Moses Nnauye Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya akihamasisha usafi wa
mazingira kwa wafanyabiashara wadogowadogo wanaoendesha shughuli zao
katika soko dogo la majengo wilaya ya Sumbawanga Mkoani humo. Hatua
hiyo ni sehemu ya kampeni ya kudumu ya Usafi wa mazingira katika Mji wa
Sumbawanga ambayo inashirikisha taasisi na wananchi wote katika
kuhakikisha Mji wa Sumbawanga unakuwa safi. Kampeni hiyo ilianzishwa
na uongozi wa Mkoa wa Rukwa ukiongozwa na Mkuu huyo wa Mkoa tarehe 12
Januari 2012 iliyokuwa siku ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kampeni hiyo
itazinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Billal ambaye atakuwa Mkoani Rukwa
kwa ziara ya kikazi ya siku 7 kuanzia tarehe 18-24 Februari 2012.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa alihamasika kuona mkusanyiko mkubwa wa watoto ambao
walitoka kwenye mafundisho ya komunio ya kwanza katika kanisa la Kristo
Mfalme na kuamua kuongea nao. Alitumia fursa hiyo kuwahamasisha
kuchukia uchafu na hivyo kuwa mstari wa mbele katika kupenda usafi kwa
kufanya usafi majumbani mwao, mashuleni na hata nje ya maeneo hayo.
Wanafunzi hao walifurahi kuongea na Mkuu wa huyo wa Mkoa na kuahidi
kushiriki katika usafi wa mazingira.
Mkuu
wa Mkoa aliendelea na uhamasishaji kwa wafanyabiashara wanaochoma
mahindi katika maeneo ya kata ya Majengo katika Manispaa hiyo. Aliwaasa
wafanyabiashara hao kuheshimu sheria kwa kuhakikisha maeneo ya
biashara yao yanakuwa safi kuepuka magonjwa ya mlipuko kama
Kipindupindu. Aliwaomba wafanyabiashara wote wamuunge mkono katika
kampeni hiyo ili Mji wa Sumbawanga uweze kufanya mapinduzi katika usafi
wa mazingira
HAMZA TEMBA-AFISA HABARI-MKUU WA MKOA RUKWA
Watazamaji
14,150 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia pambano la Ligi Kuu ya
Vodacom kati ya Yanga na Ruvu Shooting lililochezwa jana (Februari 12
mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 47,554,000.
Hata
hivyo ni watazamaji saba tu waliokata tiketi za VIP A zilizokuwa
zikiuzwa sh. 15,000. Viingilio vingine vilikuwa sh. 10,000 kwa VIP B na
C, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa na kiiingilio cha sh. 3,000 kwa
viti vya bluu na kijani kilichovutia watazamaji 12,853.
Baada
ya kuondoa gharama za awali za mechi hiyo namba 119 na asilimia 18 ya
Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 7,254,000 kila timu
ilipata sh. 8,583,000 wakati mgawo wa uwanja ulikuwa sh. 2,861,000.
Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,144,400, TFF sh.
2,861,000, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,430,500,
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 286,100 na asilimia 10 ya gharama
za mechi ni sh. 2,861,000.
Gharama
za awali za mechi ni nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya
ndani kwa kamishna sh. 10,000, posho ya kujikimu kamishna sh. 40,000,
posho ya kujikimu waamuzi sh. 120,000 na mwamuzi wa akiba sh. 30,000.
Gharama za tiketi sh. 4,000,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa
uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.
Gharama
nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu
ilipata sh. 990,500 wakati DRFA ilipata sh. 849,000.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar,Balozi Seif Idd kabla ya kupokea hundi ya Shilingi milioni
hamsini (50,000,000/=) ukiwa ni mchango wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea Dar es salaam hivi
karibuni.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NA SAMIA MUSSA
ZAIDI
ya watu milioni moja wenye matatizo wanatarajia kufaidika na Tamasha
la Pasaka litakapotimiza miaka 20, tangu kuanzishwa kwake na kufanyika
katika mikoa mbalimbali nchini.
Akizungumza
hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex
Msama, alisema tamasha hilo limelenga kiwasaidia watanzania, hivyo
limekusudia kuwasaidia watanzania milioni moja kwa kuwapatia misaada
mbalimbali.
Walengwa
katika misaada hiyo ni wasiojiweza, walemavu, wajane na watoto yatima
ambao wanasaidiwa fedha za ada na matumizi mbalimbali ya shule.
Msama
alisema lengo lake kubwa la tamsha hilo litakapotimiza miaka 20 tangu
kuanzishwa kwake, watanzania wasiopungua milioni moja wawe wamenufaika
nalo, ambapo mwaka huu ni la kimataifa.
“Tusiitegemee
Serikali kwa kila kitu, haiwezi kumsaidia kila mtu, vitu vingine
tunatakiwa tufanye wenyewe kwa ajili ya kusaidia wenzetu kupitia vyanzo
mbalimbali kama hili tamasha,” alisema.
Msama
alisema kuwa, maandalizi ya tamasha la mwaka huu yanaendelea vizuri,
ambapo tayari wamepatiwa kibali na litafanyika sehemu ya wazi ili
liweze kushuhudiwa na wadau wengi wa muziki huo.
Licha
ya maandalizi kuanza mapema, Msama alisema tamasha hilo la kimataifa
litawahusisha waimbaji wa muziki huyo wa kimataifa ambao watatangazwa
hapo baadaye.
Msama
aliwataka waimbaji wazawa kuhakikisha mwaka huu, wanatumia vyombo vya
muziki moja kwa moja, kwani suala la CD linaweza lisitumiwe.
“Wasanii
mwaka huu watakuwa wengi zaidi ya mwaka jana, nawaomba waimbaji wa
nyumbani wasitumie CD, kama ilivyokuwa mwaka jana nusu nzima ya wasanii
walitumia,” alisema
Mbali
ya mandalizi hayo kuendelea, wamekuwa na wakati mgumu kuamua tamasha
hilo lifanyike mkoa gani kwasababu mikoa kama Mbeya, Kilimanjaro,
Mwanza na Morogoro imeomba baada ya kufamnyika Jijini Dar es Salaam
Aprili nane lihamie huko.
“Hatujajua
litaelekea wapi baada ya Dar es Salaam, ila tuko katika mazungumzo
kuona lifanyike mkoa gani kati ya mikoa hii iliyoomba baada ya siku
chache tutatoa taarifa rasmi litaendelea wapi,” alisema
Ndugu zangu,
Ukitaka kuukata na kuuangusha mbuyu usianze kufikiria unene wake. Jana usiku jirani zetu Zambia wameafanya maajabu ya soka. Vijana wa Chipolopolo wamatwaa ubingwa wa Afrika kwa kuwafunga Ivory Coast.
Ndio, Zambia jana wametufanya tujisikie, kuwa; “ We are all Zambians”. Kwamba sote ni Wazambia.
Siri ya ushindi wa Zambia?
Ni Uzambia. Ni utaifa. Ni uzalendo. Tuliwaona
vijana wa Chipolopolo wanaojituma uwanjani. Vijana waliokuwa tayari
kufia uwanjani, Vijana kama akina Kampamba, Mulenga, Sunzu, Nkausu,
Chansa na wengineo.
Na katika maisha, ili mwanadamu afanikiwe unahitaji kuwa na ‘ K’ tatu;
Kujitambua, Kujiamini na Kuthubutu.
Vijana wa Chipolopolo wamejitambua. Wameijua historia yao. Wamejua walikotoka. Wamejua, kuwa kuna baba zao, mwaka 1993 walikuwa njiani kwenda Senegal kucheza mechi muhimu kufuzu kutafuta tiketi ya kucheza Kombe La Dunia. Usafiri ulikuwa mgumu. Walipanda ndege ya jeshi. Ndege ilianguka pwani ya Gabon, wachezaji wote 18 walipoteza maisha. Walikufa kwa ajili ya nchi yao.
Ndio maana jana, kwa kuitambua historia hiyo. Wazambia wale waliingia
uwanjani wakiwa tayari kufia uwanjani kwa ajili ya nchi yao. Tulimwona beki Joseph
Mussonda akiumia vibaya. Alijikaza kuendelea. Ikaonekana haiwezekani
kabisa. Akatolewa nje. Alitokwa na machozi kwa muda mwingi. Si kwa
maumivu ya mguu tu, ni kwa kuona uchungu wa kukosa kuwa uwanjani
kuipigania nchi yake. Huo ni moyo mkubwa wa uzalendo. Wazambia
wale hawakuwa wakifikiria posho zao, bali taifa lao. Na hakuna ahadi
yoyote ya fedha waliyopewa kabla ya mechi ya jana.
Ndio, Wazambia wale walionyesha kujiamini sana. Walicheza mpira wao.
Walikuwa focused muda wote.Hawakujali majina makubwa kama ya akina
Drogba, Kolo Toure, Yahya Toure, Koite, Gervinjo, Gosso
Gosso na mengineyo. Hawakujali kama walicheza na nyota wanaovichezea
vilabu vikubwa huko Ulaya. Chipolopolo walicheza mchezo wao. Mwanzo hadi
mwisho. Hata pale Ivory Coast walipokuwa wakijaribu kubadilisha mbinu na hata kubadilisha nafasi za wachezaji uwanjani, bado Zambia waliendelea kucheza mpira wao.
Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa jirani zetu wa Zambia. Nitaendelea na uchambuzi wangu…
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya utalii, Omani Adventures ya nchini Oman imeahidi kuungana na Bodi ya
Utalii ya Tanzania (TTB) kwa lengo la kuuza utalii wa Tanzania nchini
Omani.
Ujumbe
wa watalii sita ulioingia nchini mwishoni mwa wiki ulisema jukumu lao
kubwa litakuwa ni kuisaidia serikali ya Tanzania kuongeza idadi ya
watalii kutoka Omani kutembelea vivutio vya utalii nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari, kiongozi wa watalii hao, Majid Abdullah Al
Anboon alisema wamevutiwa sana na vivutio vya utalii nchini na wako
tayari kusaidia kuutangaza vivutio hivyo nchini kwao.
Alisema
kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi yenye vivutio vya kuvutia vya utalii
ambapo aliahidi kuungana na serikali ya Tanzania katika kukuza uelewa
wa vivutio hivyo nchi za nje.
“Haya
yamekuwa matembezi ya historia kwetu, tumetembelea Bonde la Ngorongoro,
Hifadhi ya Taifa Serengeti, Ziwa Victoria, Ziwa Nyasa, Tanganyika na
Mlima Kilimanjaro. Maeneo yote yana mvuto wa kipekee,” alisema.
“Tutakuwa mabalozi wazuri nchini Omani, tutajitahidi kusambaza taarifa tulizokusanya katika matembezi yetu ambazo ni pamoja na picha,
video na vipeperushi tulivyopokea kutoka bodi ya utalii Tanzania kwenye
vyombo vya habari nchini na kuhamasisha watu wa Omani watembelee
Tanzania ili kujionea mali za asili nzuri zilizopo nchini,” aliongeza.
ujio wa watalii nchini pamoja na ushirikiano walioahidi itakuwa chachu
ya ongezeko la watalii kutoka Oman na kwingineko duniani.
Watalii
kutoka Omani watasaidia katika kutangaza utalii wa Tanzania
kimataifa. Mpango uliopo ni kuona watalii wengi zaidi wanakuja Tanzania.
Pamoja na msaada wa Balozi wa Tanzania nchini Omani, bodi ya utalii itaongeza jitihada za kuhakikisha mahusiano mazuri na imara yanakua kati ya nchi hizo mbili ambayo yatawezesha kukua kwa sekta ya utalii ya nchi zote mbili.
Meneja
Masoko wa TTB, Geofrey Meena aliwaasa watalii wa Omani hao kujenga
tabia endelevu ya kila mwaka kutembelea Tanzania katika kudumisha
mahusiano baina ya pande mbili husika.
Subscribe to:
Posts (Atom)