TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 13, 2012

JK AONANA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA URUSI LEO IKULU, DAR ES SALAAM

Rais Jakaya Kikwete akiagana na mjumbe maalumu wa Rais wa Urusi Bw. Mikhail V. Margelov Ikulu jijini Dar es salaam leo January 13 Februari 2012baada ya mazungumzo yao
PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Kikwete akimsindikiza mjumbe maalumu wa Rais wa Urusi Bw. Mikhail V. Margelov mara baada ya kuzungumza naye.

MC Angel Catering and Decoration, Inakualika kwenye Usiku wa wapendanao (Valentine Party) itakayofanyika siku ya Valentine Jumanne kwenye ukumbi wa Makumbusho ndani MAKUTI HALL kuanzia saa 12:00 jioni, Chakula, Vinywaji na Muziki kwa Wapendanao vitakuwepo pamoja na zawadi mbalimbali.
Price: 50,000 Tshs. KWA DOUBLE
SIMU
0714-800225 Angel.
0715-686358 Monica Mariam
0754-265689 Doreen
0712-710621 Makala John.

MWENYEKITI WA KAMATI YA SHEREHE AMBAYE NI MKURUGENZI WA UENDESHAJI WA NHIF BWN. EUGEN MIKONGOTI HAKUWA NYUMA KATIKA KUWAKARIBISHA WAALIKWA KATIKA SHEREHE HIYO.
MAMBO YA KWAITO HAYAKUWA NYUMA TIMU YA WANA NHIF IKIJIMWAGA KAMA KAWA, KWANI NI SEHEMU YA KUJENGA AFYA.
MAFANNIKIO YOYOTE HAYAWEZI KWENDA BILA UWEPO WA MWANAMKE,MAMA MKURUGENZI AKIFANYA MAMBO MENYU HUKU AKIAMBATANA NA MKURUGENZI MKUU KATIKA KUFANYA MAJUMUISHO NA MAKARIBISHO YA MWAKA MPYA.
MKURUGENZI WA UHAI WA MFUKO,TAKWIMU NA UTAFITI BWN. MICHAEL MHANDO ALIPATA TUZO YA UTAMBUZI KWA KUTUMIKIA MFUKO KWA MIAKA 10.
WANASHOW LOVE KWENYE REDCARPET NI BAADA YA KUTUMIKIA UMMA KWA MWAKA MZIMA 2011.

Na Faki Mjaka Maelezo Zanzibar 13/02/2012


Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko Zanzibar imetoa ufafanuzi juu ya hali ya ununuzi na uhifadhi wa Zao la Karafuu Kisiwani Pemba kutokana na taarifa zilizochapishwa na Gazeti la Daily News la Februari 4 mwaka huu ambapo inadaiwa kwamba wakulima wa Zao la Karafuu wamekataa kuliuzia Shirika la Taifa la Biashara la Zanzibar ZSTC



Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Wizara hiyo imesema kuwa kauli hiyo siyo sahihi na wakulima bado wanaendelea kuliuzia Shirika hilo Karafuu zao kama ilivyopangwa ambapo hadi sasa jumla ya Tani 588.735 zenye thamani ya Tshs 8,824,850,750.00 zimeuzwa kwa Shirika hilo kwa Wilaya ya Micheweni tu.


Aidha kwa Wilaya ya Wete jumla ya tani 1,530.536 za Karafuu zenye thamani ya Tshs 22,923,724,500.00 zimeshauzwa kwa ZSTC jambo ambalo linaonesha utayari wa wakulima kuliuzia Shirika hilo.


Taarifa hiyo pia imefafanua kwamba Mkulima anaruhusiwa kuhifadhi karafuu zake kwa muda apendao iwapo tu Karafuu hizo zitahifadhiwa katika Maghala ya ZSTC na Mkulima hupewa Stakabadhi inayoonesha kiasi kinachohohifadhiwa ambapo kwa sasa kuna idadi kubwa ya wakulima wanaotumia utaratibu huo wa kuzihifadhi na kuziuza kwa siku za usoni.


Serikali ilichukua hatua hiyo ya uhifadhi kwenye maghala salama ya ZSTC kwa lengo la kuziepusha Karafuu Kusinyaa,kupungua kwa daraja la ubora na kuziepusha kushika moto,mambo ambayo yanaweza kupelekea maafa na kumkosesha mkulima faida iwapo zitahifadhiwa nyumbani



Kuhusu madai ya bei ya Karafuu taarifa hiyo imesema ukweli ni kuwa katika bei ya soko la dunia kilo moja inauzwa kwa Dola za Marekani 11-13 ambapo wastani wake ni sawa na Tshs 17,270 hadi 20.410 jambo ambalo linaifanya tofauti kati ya soko la ndani na nje iwe ni kati ya Tshs. 2,270 hadi 5,410

Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akiwasili ukumbini kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM jana kwenye ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto Mwenyekiti wa CCM Mstaafu Ali Hassa Mwinyi, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Sheni na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Amani Abeid Karume. Kulia ni makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama.
Wajumbe wa NEC kutoka Tanzania Bara wakiunga mkono marekebisho ya Katiba ya CCM yaliyopitishwa na NEC
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akisisitiza jambo kwenye kikao hicho. Kushoto ni Rais wa Zanzibar Dk. Sheni na Makamu Mkt (Zanzibar) Amani Karume
Rais Kikwete, Mukama na Msekwa wakiunga mkono marekebisho ya Katiba ya CCM
Kikwete, Mukama na Msekwa wakifurahia jambo kikaoni
Wajumbe wa Zanzibar wakiunga mkono marekebisho ya Katiba mpya ya CCM

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha aliyewahi kuwa mjumbe wake wa Kamati ya Utendaji, Kassim Kashulwe kilichotokea Februari 9 mwaka huu nyumbani kwake Kigurunyembe mkoani Morogoro.
Licha ya kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF (wakati huo Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania- FAT), pia Kashulwe aliwahi kuwa kiongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) na baadaye kamishna wa mechi za Ligi Kuu.
Kwa mujibu wa taarifa tulizopata leo (Februari 13 mwaka huu) kutoka MRFA, Kashulwe alifia nyumbani kwake na kuzikwa juzi (Februari 11 mwaka huu) kwenye makaburi ya Kora yaliyoko nje kidogo ya mji wa Morogoro.
Mbali ya Kashulwe, wengine waliochaguliwa katika uchaguzi wa FAT uliofanyika mwaka 1993 mjini Kibaha ni Muhidin Ndolanga (Mwenyekiti), Alhaji Omari Juma (Makamu Mwenyekiti) na Kanali Ali Hassan Mwanakatwe (Katibu Mkuu) na wajumbe Abdul Msimbazi, Amin Bakhresa, Job Asunga, Joel Bendera, Masalu Ngofilo na Wilson Mwanja.
Msiba huo ni pigo kwa familia ya Kashulwe, TFF na familia ya mpira wa miguu nchini kwa kuwa mchango wake ulikuwa bado unahitajika.
TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Kashulwe, na MRFA na kuwataka kuwa na uvumilivu kipindi hiki cha msiba huo mzito. Pia TFF itatoa ubani wa sh. 200,000 kwa familia ya marehemu kama rambirambi zake.
Mungu aiweke roho ya marehemu Kashulwe mahali pema peponi. Amina

KITUO cha maraha cha Dar Live kilichoko Mbagala jijini Dar kilirindima kwa vifijo vya burudani ya muziki kutoka vikundi mbalimbali vya wasanii.
Ilikuwa ni ‘kufuru tupu’ wakati wasanii AY akishirikiana na Mwana FA walipotoana jasho na wenzao kina Chegge na Temba kutoka katika kundi la Wanaume Family yote hayo yakisindikizwa na burudani kutoka kundi la taarab la East Africa Melody, Wakali Dancers, Dogo Aslay, Shilole na bendi ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga Pepeta.. AY (kushoto) na Mwana FA wakikamua.
Temba akichana mistari.
Mwanamuziki wa 'Twanga Pepeta', Luiza Mbutu, akiimba na kucheza.
Wanenguaji wa Twanga Pepeta wakionyesha ‘matindo
Kina ‘Rihanna’ wakiwa katika picha ya pamoja.

We are delighted to announce that CFAO MOTORS TANZANIA, on behalf of CFAO SOLIDARITY in France, is donating TZS 22m to help CCBRT Hospital.
CFAO has been involved in business in Africa for over 125 years. The group employs around 9,200 staff in 31 African countries and 7 French overseas territories. Since its future is inextricably linked with that of Africa, it is only right that CFAO should assist in its development.
Via its various lines of business, CFAO makes its contributions to sustainable development issues in Africa and is forging ahead with a far-reaching strategy in terms of Corporate Social Responsibility.
At CFAO MOTORS TANZANIA we have studied with great admiration the truly amazing work that CCBRT does. We have persuaded our head office to provide financial support so that CCBRT can continue to do wonders in our society.
We all know how difficult it is sometimes for sick or disabled people in our country to get quality medical care, even for the most basic ailments. CCBRT has been fantastic in ensuring medical care is available to the community and at the most affordable prices.
We have also noted that monies donated to CCBRT are always used in a responsible manner for the maximum benefits of its patients. This makes us very comfortable supporting the project as we know that our money will definitely benefit the needy.
On behalf of CFAO SOLIDARITY in France and CFAO MOTORS TANZANIA, I would like to present this cheque which I am sure will be put into good use in the community.

Watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha Taifa cha Kurasini kilichopo jijini Dar es Salaam,wakishindana kuvuta kamba wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula na ngua vyenye jumla ya shilingi milioni 10.Vilivyotolewa na Blogs ya U-turn kwa kushirikiana na wasomaji wake wakuu.
.Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiwa amebeba mmoja wa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha kulea watoto yatima cha Kurasini jijini Dar es Salaam.Wakati wa blog ya U-turn kwa kushirikiana na wasomaji wake wakuu walipokwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na nguo vyenye jumla ya shilingi Milioni 10.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano akifurahia pamoja na watoto yatima walipofika katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Kurasini jijini Dar es Salaam,msaada wa vyakula na vitu mbalimbali uliokuwa na thamani ya shilingi Milioni 10 ulitolewa na U-turn blog kwa ushirikiano wapamoja na wasomaji wakuu wa Blog hiyo.
Vyakula mbalimbali vilivyotolewa kama msaada kwa watoto hao.
Watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha Taifa cha Kurasini kilichopo jijini Dar es Salaam,wakishindana kuvuta kamba wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula na ngua vyenye jumla ya shilingi milioni 10.Vilivyotolewa na Blogs ya U-turn kwa kushirikiana na wasomaji wake wakuu.
Mmoja wa wasanii wanaochipukia Dogo Aslay akiwapagawaisha watoto wa naolelewa katika kituo cha Yatima cha Kurasini cha jijini Dar es Salaam,kwa wimbo wa naenda kusema kwa mama, wakati wa hafla ya Blogs ya U-turn kwa kushirikiana na wasomaji wake wakuu walipokwenda katika kituo hicho kutoa misaada mbalimbali ikiwemo vyakula na nguo vyote vyenye thamani ya shilingi milioni 10.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Mwinyihaji Makame akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na malengo, mafanikio ya Wizara yake kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Julay hadi Disemba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Mwinyihaji Makame akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana namalengo na mafanikio ya Wizara yake kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Julai hadi Disemba
Kuliani kwake ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Salum Maulid.na kushoto kwake ni Naibu katibu Mkuu idara Maalum Capt,Abdalla Juma.

Halmashauri Kuu ya CCM Taifa katika kikao chake cha siku moja chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa Taifa Dr. Jakaya M. Kikwete, pamoja na mambo mengine imetoa ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea wa CCM kwa uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki. Katika kikao chake hicho kilichofanyika tarehe 12/02/2012 mjini Dodoma, NEC pia imetoa ratiba ya mchakato wa kuwapata wagombea udiwani kwa tiketi ya CCM kwenye kata nane zilizotangazwa kufanya chaguzi Ndogo na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. 1. UBUNGE: Katika nafasi ya Ubunge kwa Arumeru Mashariki, utaratibu utakaotumika ni ule wa kupiga kura za maoni kwenye Mkutano Mkuu wa Jimbo. (i) Tarehe 13 – 18/02/2012 Kuchukua na kurejesha fomu. (ii) Tarehe 20/02/2012 Mkutano Mkuu wa Jimbo kupiga Kura za maoni. (iii) Tarehe 21/02/2012 Kamati ya Siasa ya Wilaya kujadili Wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati ya Siasa ya Mkoa. (iv) Tarehe 24/02/2012 Kamati ya Siasa ya Mkoa kujadili Kutoa mapendekezo yake kwa Kamati kuu. (v) Tarehe 27/02/2012 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kufanya uteuzi wa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi. 2. UDIWANI Nafasi ya Udiwani katika kata 8 za Tanzania Bara Katika nafasi hii kura za maoni zitapigwa kwenye Mikutano Mikuu ya Matawi. (i) Tarehe 13 – 16/02/2012Kuchukua na kurejesha fomu. (ii) Tarehe 17 – 21/02/2012 Kampeni za Uchaguzi kwenye Matawi. (iii) Tarehe 22/02/2012Mikutano Mikuu ya Matawi kupiga kura za maoni. (iv) Tarehe 25/02/2012 Kamati za Siasa za Wilaya kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati za Siasa za Mikoa. (v) Tarehe 27/02/2012 Kamati za Siasa za Mikoa kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu za Mikoa. (vi) Tarehe 29/02/2012 Halmashauri Kuu za Mikoa kufanya uteuzi wa wagombea. Katika hatua nyingine Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imepokea maelezo juu ya mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya na maelezo juu ya mgomo wa madaktari nchini. Kwa ujumla NEC imepokea maelezo hayo kutoka serikalini na kuiagiza serikali kukamilisha mchakato wa kumaliza kabisa mgogoro wa madaktari nchini na kuhakikisha migogoro ya namna hiyo inashughulikiwa mapema ili isiwe na madhara makubwa kwa wananchi. NEC imeridhishwa na jinsi mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya unavyoendelea na kuipongeza serikali kwa jinsi inavyolisimamia swala hilo. Imewataka wana CCM na wananchi wote kushiriki mchakato huo, huku wakizingatia kutunza amani na utulivu uliopo nchini. Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imewapongeza viongozi, wanachama na wananchi wa Mkoa wa Mwanza kwa jinsi walivyofanikisha sherehe za miaka 35 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi ambapo kitaifa mwaka huu zilifanyika mkoani humo. Sherehe hizo ziliandaliwa na kufanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu kabisa, hivyo NEC inawapongeza kwa kufanikisha sherehe hizo. Pamoja na Mkoa wa Mwanza NEC inawapongeza wanachama, viongozi na wananchi kwa ujumla nchi nzima kwa jinsi walivyofanikisha sherehe hizo za miaka 35 ya kuzaliwa kwa CCM kwenye maeneo yao. Imetolewa na; Nape Moses Nnauye Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya akihamasisha usafi wa mazingira kwa wafanyabiashara wadogowadogo wanaoendesha shughuli zao katika soko dogo la majengo wilaya ya Sumbawanga Mkoani humo. Hatua hiyo ni sehemu ya kampeni ya kudumu ya Usafi wa mazingira katika Mji wa Sumbawanga ambayo inashirikisha taasisi na wananchi wote katika kuhakikisha Mji wa Sumbawanga unakuwa safi. Kampeni hiyo ilianzishwa na uongozi wa Mkoa wa Rukwa ukiongozwa na Mkuu huyo wa Mkoa tarehe 12 Januari 2012 iliyokuwa siku ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kampeni hiyo itazinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Billal ambaye atakuwa Mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi ya siku 7 kuanzia tarehe 18-24 Februari 2012.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alihamasika kuona mkusanyiko mkubwa wa watoto ambao walitoka kwenye mafundisho ya komunio ya kwanza katika kanisa la Kristo Mfalme na kuamua kuongea nao. Alitumia fursa hiyo kuwahamasisha kuchukia uchafu na hivyo kuwa mstari wa mbele katika kupenda usafi kwa kufanya usafi majumbani mwao, mashuleni na hata nje ya maeneo hayo. Wanafunzi hao walifurahi kuongea na Mkuu wa huyo wa Mkoa na kuahidi kushiriki katika usafi wa mazingira.
Mkuu wa Mkoa aliendelea na uhamasishaji kwa wafanyabiashara wanaochoma mahindi katika maeneo ya kata ya Majengo katika Manispaa hiyo. Aliwaasa wafanyabiashara hao kuheshimu sheria kwa kuhakikisha maeneo ya biashara yao yanakuwa safi kuepuka magonjwa ya mlipuko kama Kipindupindu. Aliwaomba wafanyabiashara wote wamuunge mkono katika kampeni hiyo ili Mji wa Sumbawanga uweze kufanya mapinduzi katika usafi wa mazingira
HAMZA TEMBA-AFISA HABARI-MKUU WA MKOA RUKWA

Watazamaji 14,150 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Ruvu Shooting lililochezwa jana (Februari 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 47,554,000.
Hata hivyo ni watazamaji saba tu waliokata tiketi za VIP A zilizokuwa zikiuzwa sh. 15,000. Viingilio vingine vilikuwa sh. 10,000 kwa VIP B na C, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa na kiiingilio cha sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani kilichovutia watazamaji 12,853.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mechi hiyo namba 119 na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 7,254,000 kila timu ilipata sh. 8,583,000 wakati mgawo wa uwanja ulikuwa sh. 2,861,000.
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,144,400, TFF sh. 2,861,000, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,430,500, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 286,100 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 2,861,000.
Gharama za awali za mechi ni nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna sh. 10,000, posho ya kujikimu kamishna sh. 40,000, posho ya kujikimu waamuzi sh. 120,000 na mwamuzi wa akiba sh. 30,000. Gharama za tiketi sh. 4,000,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.
Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 990,500 wakati DRFA ilipata sh. 849,000.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Idd kabla ya kupokea hundi ya Shilingi milioni hamsini (50,000,000/=) ukiwa ni mchango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea Dar es salaam hivi karibuni.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea hundi ya 50,000,000/= kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd ukiwa ni mchango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea Dar es salaam hivi karibuni. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)

NA SAMIA MUSSA
ZAIDI ya watu milioni moja wenye matatizo wanatarajia kufaidika na Tamasha la Pasaka litakapotimiza miaka 20, tangu kuanzishwa kwake na kufanyika katika mikoa mbalimbali nchini.
Akizungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama, alisema tamasha hilo limelenga kiwasaidia watanzania, hivyo limekusudia kuwasaidia watanzania milioni moja kwa kuwapatia misaada mbalimbali.
Walengwa katika misaada hiyo ni wasiojiweza, walemavu, wajane na watoto yatima ambao wanasaidiwa fedha za ada na matumizi mbalimbali ya shule.
Msama alisema lengo lake kubwa la tamsha hilo litakapotimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake, watanzania wasiopungua milioni moja wawe wamenufaika nalo, ambapo mwaka huu ni la kimataifa.
“Tusiitegemee Serikali kwa kila kitu, haiwezi kumsaidia kila mtu, vitu vingine tunatakiwa tufanye wenyewe kwa ajili ya kusaidia wenzetu kupitia vyanzo mbalimbali kama hili tamasha,” alisema.
Msama alisema kuwa, maandalizi ya tamasha la mwaka huu yanaendelea vizuri, ambapo tayari wamepatiwa kibali na litafanyika sehemu ya wazi ili liweze kushuhudiwa na wadau wengi wa muziki huo.
Licha ya maandalizi kuanza mapema, Msama alisema tamasha hilo la kimataifa litawahusisha waimbaji wa muziki huyo wa kimataifa ambao watatangazwa hapo baadaye.
Msama aliwataka waimbaji wazawa kuhakikisha mwaka huu, wanatumia vyombo vya muziki moja kwa moja, kwani suala la CD linaweza lisitumiwe.
“Wasanii mwaka huu watakuwa wengi zaidi ya mwaka jana, nawaomba waimbaji wa nyumbani wasitumie CD, kama ilivyokuwa mwaka jana nusu nzima ya wasanii walitumia,” alisema
Mbali ya mandalizi hayo kuendelea, wamekuwa na wakati mgumu kuamua tamasha hilo lifanyike mkoa gani kwasababu mikoa kama Mbeya, Kilimanjaro, Mwanza na Morogoro imeomba baada ya kufamnyika Jijini Dar es Salaam Aprili nane lihamie huko.
“Hatujajua litaelekea wapi baada ya Dar es Salaam, ila tuko katika mazungumzo kuona lifanyike mkoa gani kati ya mikoa hii iliyoomba baada ya siku chache tutatoa taarifa rasmi litaendelea wapi,” alisema

Ndugu zangu,
Ukitaka kuukata na kuuangusha mbuyu usianze kufikiria unene wake. Jana usiku jirani zetu Zambia wameafanya maajabu ya soka. Vijana wa Chipolopolo wamatwaa ubingwa wa Afrika kwa kuwafunga Ivory Coast.
Ndio, Zambia jana wametufanya tujisikie, kuwa; “ We are all Zambians”. Kwamba sote ni Wazambia.
Siri ya ushindi wa Zambia?
Ni Uzambia. Ni utaifa. Ni uzalendo. Tuliwaona vijana wa Chipolopolo wanaojituma uwanjani. Vijana waliokuwa tayari kufia uwanjani, Vijana kama akina Kampamba, Mulenga, Sunzu, Nkausu, Chansa na wengineo. Na katika maisha, ili mwanadamu afanikiwe unahitaji kuwa na ‘ K’ tatu; Kujitambua, Kujiamini na Kuthubutu.
Vijana wa Chipolopolo wamejitambua. Wameijua historia yao. Wamejua walikotoka. Wamejua, kuwa kuna baba zao, mwaka 1993 walikuwa njiani kwenda Senegal kucheza mechi muhimu kufuzu kutafuta tiketi ya kucheza Kombe La Dunia. Usafiri ulikuwa mgumu. Walipanda ndege ya jeshi. Ndege ilianguka pwani ya Gabon, wachezaji wote 18 walipoteza maisha. Walikufa kwa ajili ya nchi yao.
Ndio maana jana, kwa kuitambua historia hiyo. Wazambia wale waliingia uwanjani wakiwa tayari kufia uwanjani kwa ajili ya nchi yao. Tulimwona beki Joseph Mussonda akiumia vibaya. Alijikaza kuendelea. Ikaonekana haiwezekani kabisa. Akatolewa nje. Alitokwa na machozi kwa muda mwingi. Si kwa maumivu ya mguu tu, ni kwa kuona uchungu wa kukosa kuwa uwanjani kuipigania nchi yake. Huo ni moyo mkubwa wa uzalendo. Wazambia wale hawakuwa wakifikiria posho zao, bali taifa lao. Na hakuna ahadi yoyote ya fedha waliyopewa kabla ya mechi ya jana.
Ndio, Wazambia wale walionyesha kujiamini sana. Walicheza mpira wao. Walikuwa focused muda wote.Hawakujali majina makubwa kama ya akina Drogba, Kolo Toure, Yahya Toure, Koite, Gervinjo, Gosso Gosso na mengineyo. Hawakujali kama walicheza na nyota wanaovichezea vilabu vikubwa huko Ulaya. Chipolopolo walicheza mchezo wao. Mwanzo hadi mwisho. Hata pale Ivory Coast walipokuwa wakijaribu kubadilisha mbinu na hata kubadilisha nafasi za wachezaji uwanjani, bado Zambia waliendelea kucheza mpira wao.
Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa jirani zetu wa Zambia. Nitaendelea na uchambuzi wangu…

Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya utalii, Omani Adventures ya nchini Oman imeahidi kuungana na Bodi ya Utalii ya Tanzania (TTB) kwa lengo la kuuza utalii wa Tanzania nchini Omani.
Ujumbe wa watalii sita ulioingia nchini mwishoni mwa wiki ulisema jukumu lao kubwa litakuwa ni kuisaidia serikali ya Tanzania kuongeza idadi ya watalii kutoka Omani kutembelea vivutio vya utalii nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari, kiongozi wa watalii hao, Majid Abdullah Al Anboon alisema wamevutiwa sana na vivutio vya utalii nchini na wako tayari kusaidia kuutangaza vivutio hivyo nchini kwao.
Alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi yenye vivutio vya kuvutia vya utalii ambapo aliahidi kuungana na serikali ya Tanzania katika kukuza uelewa wa vivutio hivyo nchi za nje.
“Haya yamekuwa matembezi ya historia kwetu, tumetembelea Bonde la Ngorongoro, Hifadhi ya Taifa Serengeti, Ziwa Victoria, Ziwa Nyasa, Tanganyika na Mlima Kilimanjaro. Maeneo yote yana mvuto wa kipekee,” alisema.
“Tutakuwa mabalozi wazuri nchini Omani, tutajitahidi kusambaza taarifa tulizokusanya katika matembezi yetu ambazo ni pamoja na picha, video na vipeperushi tulivyopokea kutoka bodi ya utalii Tanzania kwenye vyombo vya habari nchini na kuhamasisha watu wa Omani watembelee Tanzania ili kujionea mali za asili nzuri zilizopo nchini,” aliongeza.
ujio wa watalii nchini pamoja na ushirikiano walioahidi itakuwa chachu ya ongezeko la watalii kutoka Oman na kwingineko duniani.
Watalii kutoka Omani watasaidia katika kutangaza utalii wa Tanzania kimataifa. Mpango uliopo ni kuona watalii wengi zaidi wanakuja Tanzania.
Pamoja na msaada wa Balozi wa Tanzania nchini Omani, bodi ya utalii itaongeza jitihada za kuhakikisha mahusiano mazuri na imara yanakua kati ya nchi hizo mbili ambayo yatawezesha kukua kwa sekta ya utalii ya nchi zote mbili.
Meneja Masoko wa TTB, Geofrey Meena aliwaasa watalii wa Omani hao kujenga tabia endelevu ya kila mwaka kutembelea Tanzania katika kudumisha mahusiano baina ya pande mbili husika.

No comments:

Post a Comment