Watu wapatao 140,000 wameokolewa kufuatia mafuriko makubwa katika mataifa manne ya Amerika ya Kusini. Paraguay ndiyo nchi iliyoathirika vibaya na mafuriko hayo, ambapo hali ya hatari imetangazwa. Maafisa wanasema wengi wa watu waliopoteza makaazi yao ni familia masikini zinazoishi kandoni mwa Mto Paraguay, karibu na mji mkuu, Asuncion. Maelfu ya watu nchini Uruguay, Brazil na Argentina pia wamekimbia makaazi yao. Watabiri wa hali ya hewa wanasema kumekuwa na mvua kali za El Nino na zisizo za kawaida katika msimu huu wa kaskazi. Kwengineko, barani Ulaya mvua kubwa imesababisha mafuriko kaskazini mwa kisiwa cha England. Mito mikubwa katika miji ya Manchester na Leeds imefurika na wakaazi kwenye kaunti za Lancashire na West Yorkshire wamehamishwa. Jeshi la Uingereza limeitwa kusaidia uokozi.
Liverpool wamepunguza kasi ya Leicester kileleni mwa Ligi ya Uingereza baada ya kuwalaza 1-0 uwanjani Anfield.
Leicester walikuwa wameenda mechi tisa bila kushindwa ligini na leo imekuwa mara yao ya kwanza kumaliza bila kufunga bao ligini msimu huu.
Uwanjani Britannia, masaibu ya meneja Louis Van Gaal yamezidi baada ya Red Devils kucharazwa 2-0 na Stoke City. Meneja huyo amekabiliwa na shinikizo baada ya klabu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo mabaya.