TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, February 14, 2015

Lyimo atangaza kupeperusha bendera ya TLP katika kuwania Urais wa Tanzaia

max 
Mwanachama wa chama cha siasa cha TLP Bwn Macmillan Lyimo (kushoto) akirejesha fomu ya kuomba kugombea uraisi kwa tiketi ya chama hicho kwa katibu mkuu wa chama hicho Meja Jesse Makundi huku katibu msaidizi wa TLP Bwn Hamad Tao akishuhudia.Picha ilipigwa mwaka 2010 kwa hisani ya http://changamotoyetu.blogspot.com                           
………………………………………………………………………….
Na Happy Shirima-MAELEZO-
Dar es salaam Mwanachama wa chama cha Tanzania Labour Party [TLP] Macmillan Lyimo ametangaza nia ya kugombea nafasi ya uraisi kupitia chama hicho. Lyimo ametangaza azma hiyo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu nia yake ya kuamua kugombea urais kupitia Chama hicho na sababu zilizo mfanya agombee Amesema kuwa sababu zilizomfanya agombee nafasi hiyo kupitia chama hicho ni kuendeleza juhudi za Mwenyekiti wa chama hicho Mhe. Augustino Mrema za kutunza historia nzuri alioiweka kwenye chama hicho wakati wa uchaguzi wa mwaka 1995. ”Mhe.Mrema ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa chama na Mbunge wa Jimbo la Vunjo itakuwa ni aibu na fedheha kwa mtu yeyote kutotambua mchango wa kiongozi huyo wakati akiwa kiongozi serikalini na hatimaye wakati akiwa upinzani toka 1995 ”alisema Lyimo. Aidha amesema kuwa sera kuu ya chama hicho ni amani , kuandaa kizazi kipya na taifa jipya Tanzani litakalo jengwa na misingi mkuu ukiwa ni Mungu kupewa nafasi ya kwanza lengo kuu ikiwa ni kuifanya Tanzania kuwa taifa kubwa la dunia katika kipindi kifupi. Ametoa wito kwa viongozi wa kada zote na wananchi wote kushiriki kwa amani na upendo katika matukio makuu muhimu kwa Taifa hilo ambayo ni kupigia kura Katiba inayopendekezwa ,uchaguzi mkuu na kujenga umoja ili kuepuka ufa uliojitokeza katika masuala ya dini kwa ajili ya mustakabali mzuri wa Tanzania .

WAREMBO WA MISS VALENTANE DAY 2015-GREEN TREES KIGAMBONI HAWA HAPA.

Friday, February 13, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA UONGOZI WA KAMPUNI YA NARI YA CHINA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya NARI ya China, Bw. Bao Tianhua, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 13, 2015 kwa mazungumzo. Katikati ni Katikati ni Mkurugenzi wa Bosandra Professionals Co Ltd, Bora Joachim. 

Mhe. Dkt. Bilal, leo amekutana na Uongozi wa Kampuni hiyo ya NARI kutoka Nchini China ambayo pia inajishughulisha na Uwekezaji wa Miundombinu ya Umeme  Nchini Tanzania kwa kushirikiana na Wakala wa Umeme Vijijini.
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Meneja Mkuu wa Kampuni ya NARI ya China, Bw. Bao Tianhua, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 13, 2015 kwa mazungumzo.  

TWANGA PEPETA KUFANYA ONYESHO MAALUM LA VALENTINE DAY.

 
BENDI ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ usiku wa kesho itafanya onyesho maalum ya kusherekea siku ya wapendanao ‘Valentine Day’, kwenye ukumbi wao wa nyunmbi Mango Garden, Kinondoni.

Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka amesema kuwa pia onyesho hilo watatambulisha nyimbo zao mpya zilizoko kwenye chati. Pia mkurugenzi huyo alisema kuwa bendi hiyo itapiga nyimbo zao zote za zamani zilizovuma wakati huo. Aliwataka mashabiki wa bendi hiyo kujitokeza kwa wingi kuhudhuria onyesho la aina yake ambalo  litabubikwa na zawadi kibao za Valentine.

“Tumejianda vizuri kwa onyesho la Valentine. Onyesho hili limeboreshwa zaidi ya lile la kumpongeza mwanamuziki wao kongwe Lwiza Mbutu lililofanyika wiki iliyopita ambalo iliudhuriwa na umati wa mashabiki,” alisema Asha.

Serikali na Wadau binafsi washauriwa kuwasaidia Wajasiriamali wa Kitanzania

 Balozi wa Tanzania nchini Oman Ali Ahmed Saleh kushoto Aliyekaa kwenye kiti akipata burudani ya Msewe iliyoandaliwa kwa ajili yake na Kikundi cha Sanaa cha Zanzibar mara baada ya Balozi huyo kumaliza ziara yake ya kuwatembelea Watanzania na kushauriana nao mambo mbalimbali ya kukuza soko katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mjini Mascut nchini humo. Picha na Faki Mjaka.
 Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Zanzibar wakicheza Ngoma aina ya Uringe kwa Balozi wa Tanzania nchini Oman (hayupo pichani) mara baada ya Balozi huyo kuwatembelea Watanzania na kushauriana nao mambo mbalimbali ya kukuza soko katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mjini Mascut nchini humo.

Tamasha la Pasaka kamili kusaidia jamii



WAANDAAJI wa Tamasha la Pasaka wamesema wataendelea kusaidia jamii katika kila tamasha lao litakapofanyika.
 
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam  leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya miaka 15 ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama ilieleza kuwa kwa miaka yote hiyo wamekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii.
"Tumedhamiria kwa dhati kusaidia jamii kwa namna mbalimbali, hii haitakuwa mara ya kwanza kwetu kufanya hivyo, tulisaidia matamasha yaliyopita, tutaendelea na juhudi hizo kila tutakapopata nafasi, “ alisema Msama katika taarifa hiyo.

Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, NHC mafunzoni Afrika Kusini

Ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Mazingira ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Abdulkarim Esmail Hassan Shah (Mafia), Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki na kuambatana na uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Tumaini Thika jana. Kamati hiyo iko katika ziara ya mafunzo nchini humo.
Ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Mazingira uliofuatana na uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa ukiwa katika picha ya pamoja nje ya Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, jana. Kamati hiyo iko katika ziara ya mafunzo nchini humo.

Umeisikia kampeni ya EATV, East Africa Radio iitwayo “Zamu Yako 2015″?

Thursday, February 12, 2015

DKT. REGINALD MENGI KUMZAWADIA MILIONI 10 MSHINDI WA WAZO LA BIASHARA LA 3N

mengi2
Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi.
Na Mwanadishi Wetu
Mshindi wa Januari 2015 wa shindano la wazo la biashara 3N alitarajiwa kutangazwa siku ya leo Alhamisi ya Februari 12 kuanzia saa tano asubuhi jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Dk. Reginald Mengi kupitia kurasa wake wa twitter, alitangazia umma kuwa Shindano hilo jipya lijulikanalo kwa kifupi -3N, ikiwa ni kifupisho cha ‘Nitabuni wazo la biashara, Nitatekeleza, na Nitafanikiwa’, ambapo mshindi wa kwanza wa mwezi Januari alitarajiwa kutangazwa siku ya leo ya alhamisi Februari 12.

Dk. Mengi aliweka ujumbe huo twittter : “Kutokana na sababu zisizozuilika mshindi wa Januari wa shindano la 3N atatangazwa Februari 12 saa 5 asubuhi. Samahani kwa usumbufu wowote”.
Kwa mujibu wa Dk. Mengi awali mshind I alitakiwa kutangazwa Jumatano ya jana ya Februari 11, kabla ya kusogeza mbele hiyo Februari 12.

Shindano hilo litakuwa linafanyika kila mwezi kwa muda wa miezi sita kuanzia Januari Mosi 2015, hadi Juni 30, 2015, na mshindi wa kila mwezi atajishindia ruzuku ya shilingi milioni 10 atakazozitumia kutekeleza kwa vitendo wazo lake la biashara.

Shindano hilo, linawashirikisha Watanzania pekee, litaendeshwa kwa njia ya mtandao wa kompyuta ambapo mshiriki atatuma wazo lake la biashara kwa anuani ya twita @regmengi Shindano la Wazo la Biashara. Katika mchujo wa kwanza jopo la wataalamu litateua mawazo 10 bora Zaidi na waliotoa mawazo hayo watafanyiwa usaili kwa njia ya simu ili jopo hilo lijiridhishe kama mawazo waliyoyotuma ni yao binafsi, na kama wamejipanga vizuri kutekeleza kibiashara.
Kutokana na mawazo hayo 10 teule, jopo litachagua wazo moja kuwa mshindi. Hii ni mara ya tatu kwa Dkt. Mengi kuendesha shindano kwa kutumia mtandao wa kompyuta wa twitter kwa kuamini kwake kuwa mitandao ya kijamii ina nguvu kubwa katika kuchochea ujasiriamali hasa kwa kizazi cha sasa.
Shindano la kwanza na la pili lililoendeshwa mwaka jana lilikusudiwa kushawishi mawazo ya kuondoa umaskini katika taifa lenye utajiri mkubwa, lakini watu wake wengi wakiwa bado wametopea katika lindi la umaskini.
Awali akizungumza katika uzinduzi wa shindano hilo, Dkt. Mengi alisema shindano hilo limelenga kuhimiza watu kuwa na upeo mkubwa wa kuona fursa za kibiashara na kuzitumia kujikwamua kiuchumi. Pia alisema shindano hilo ni mchango wake binafsi wa kuunga mkono jitihada za serikali na sekta binafsi za kuwakomboa wananchi kiuchumi kwa njia za ujasirimali, kwani amesema Sera zote mbili za kitaifa za Elimu ya juu na maendeleo ya viwanda vya kati na vidogo zina vipengele vya kuchochea na kuendeleza utamaduni wa ujasirimali wa mtu mmoja mmoja.
“Kwa muda mrefu nimekuwa nikishawishi uwepo wa moyo wa ujasirimali miongoni mwa wa Watanzania na hasa kwa vijana. Ni ndoto yangu kuona uchumi wetu unakua kwa kasi kiasi cha kuzalisha zaidi ya mamilionea 100 kila mwaka wanaoendesha biashara halali,” alisema.
Alisema kuwa na wazo sahihi la biashara, katika muda muafaka na eneo sahihi ni muhimu zaidi kuliko ruzuku ya fedha.
“Nataka vijana watambue kwamba wanaweza kuanza na kitu kidogo na kukua kufikia kampuni kubwa kabisa ya kimataifa unayoweza kufikiria,” alisema na kusisitiza kwamba anaamini siku moja mazingira ya ujasirimali nchini Tanzania yakuwa miongoni mwa mazingira bora kabisa barani Afrika.
Amesisitiza kuwa Shindano hilo liko wazi kwa watanzania wote na wanachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wanapeleka wazo lao la biashara kwa Dk Mengi kupitia mtandao wa kompyuta wa twita, kwa kumtag Dk Mengi kwenye @regmengi.
Aidha amesema ni wale tu watakaomtag ndio watafikiriwa na jopo la wataalamu, na kusisitiza kuwa maamuzi ya jopo la Wataalamu yatakuwa ni ya mwisho.
Washindi wa kila mwezi wataarifiwa kwa kutumiwa ujumbe mfupi kwa kupitia akaunti zao za twita (DM) na kupewa ruzuku yao katika sherehe fupi itakayohudhuriwa na waandishi wa habari.

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA SHULE YA MSINGI MPILIPILI KWENYE KITENGO CHA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM NA PIA MATAWI YA CCM LINDI MJINI

1
Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mwalimu Mkuu Ndugu Fadhili Mtitima wa Shule ya Msingi Mpilipili iliyoko Manispaa ya Lindi tarehe 11.2.2015. Mama Salma alikwenda shuleni hapo kuwatembelea wanafunzi wenye mahitaji maaalum.
2
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete akimsikiliza mtoto mwenye mahitaji maalum Mohammed Hashim aliyeweza kuimba vizuri wimbo wa Taifa.

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA KITUO CHA AFYA CHA LINDI MJINI NA KUZURU MATAWI YA CCM

1
Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiongea na viongozi wa CCM wa Tawi la Ufukoni katika Kata ya Rahaleo huko Lindi Mjini tarehe 9.2.2015.  Mama Salma Kikwete yupo wilayani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku 5.
3
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Lindi Mjini Dkt. Zulfa Msami wakati Mama alipotembelea kituo hicho tarehe 10.2.2015.

“HATUTAFAIDIKA NA MIRADI YA MAJI TUNAYOITEKELEZA, KAMA HATUTATUNZA VYANZO VYA MAJI TULIVYONAVYO”-MAKALLA

mak2Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla mara akiwa amesimama pembeni ya mradi wa Kijiji cha Managhat, Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara,pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Omari Chambo na Mkurugenzi wa Mji wa Babati, Omari Mkombole mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye mradi huo.

WAZIRI CHIKAWE AWAPA SOMO MAKATIBU KATA CCM NACHINGWEA, MKOANI LINDI

chik1Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) akizungumza na Makatibu Kata wa CCM, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi leo. Katika mazungumzo hayo yaliyojumuisha Makatibu Kata zaidi ya 30, Waziri Chikawe aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanazunguka katika kata zao kuhakikisha wanawahamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwa ajili ya maandalizi ya kuipigia kura Katiba inayopendekezwa pamoja na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwaka huu nchini. Katikati Meza Kuu ni Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Mussa Liliyo akifuatiwa na Mwenyekiti wa Makatibu Kata hao, Ally Napepa.

JAMII YATAKIWA KUWASAIDIA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM – MAMA SALMA KIKWETE

3
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpongeza mtoto Mohammed Hashim mara baada ya kuimba wimbo wa Taifa.
……………………………………………………………………………………..
Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete ameitaka jamii kutumia sauti zao  kuwasemea watoto wenye mahitaji maalum kwani watoto hao wanakabiliwa na changamoto  mbalimbali na hawana mtu wa kumwambia matatizo yao.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

index
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MHAMIAJI HARAMU MMOJA RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MEKESA ABADA (27) KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI. AIDHA MHAMIAJI HUYO ALIKUWA PAMOJA NA MWENYEJI WAKE AITWAYE ADIKO MICHAEL (32) MKAZI WA MWANJELWA AMBAYE NAE AMEKAMATWA.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 11.02.2015 MAJIRA YA SAA 22:30 USIKU HUKO KATIKA ENEO LA BARABARA YA SITA, SOKOMATOLA, KATA NA TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA. KATIKA MSAKO WA PILI:
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MAKONGOLOSI WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JUMA JUMA (18) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI MSOKOTO MMOJA SAWA NA UZITO WA GRAM 05.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 11.02.2015 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA BAADA YA KUFANYIKA MSAKO KATIKA MAENEO HAYO. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA VITENDO VYA KUSHIRIKI KUWAINGIA RAIA WA KIGENI NCHINI BILA KUFUATA TARATIBU KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWAO. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII/VIJANA KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. Imesainiwa na: [AHMED Z. MSANGI – SACP] KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

MASHEHA WILAYA YA MICHEWENI PEMBA WATAKIWA KUTOUZA ARDHI BILA KUIARIFU SERIKALI

index Na Masanja Mabula -Pemba .
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Jabu Khamis Mbwana amewataka masheha kutoingia mikataba ya uuzaji au utoaji wa ardhi katika maeneo yao  bila ya kuiarifu Serikali ya Wilaya lengo ni kuzuia migogoro ya ardhi .
Akizungumza na masheha wa Wilaya hiyo huko Ofisini kwake Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa iwapo masheha watajiepusha na mikataba hiyo migogoro ya ardhi ambayo inaikabili jamii inaweza kupungua .
Amefahamisha kwamba ni kosa kwa Sheha kujichujkulia uwamuzi wa kuingia mkataba wa kuuza ardhi na kufahamisha kuwa Serikali ya Wilaya haitokuwa tayari kumvulia Sheha ambaye atasababisha mgogoro kwa kuingia mtakaba ya aina hiyo .

TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA YAENDESHA MAFUNZO YA SIKU MBILI KWA KAMATI ZA MAADILI ZA MIKOA YA RUKWA KATAVI

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Jaji Kakusulo Sambo akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo mapema leo tarehe 12 Februari 2015. Mafunzo hayo ya siku mbili yanayoshirikisha Mikoa ya Rukwa na Katavi yanafanyika Mkoani Rukwa. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Ibrahim Msengi. 
Jaji wa Mhakama Kuu ambae pia ni Mkuu wa Chuo cha Mahakama Lushoto Jaji Ferdinand Wambali akiendesha mafunzo hayo ambayo yameanza leo tarehe 12 Februari na yatamalizika kesho tarehe 13 Februari 2015 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa (RDC).

MKUU WA MKOA WA RUKWA AONANA NA VIONGOZI NA WAJUMBE WA MFUKO WA CHANGAMOTO ZA MILLENIA (MCAT), AWAPONGEZA KWA KAZI NZURI YA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA NCHINI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na viongozi na wajumbe wa Mfuko wa Changamoto za Millenia Tanzania (MCA-T) wakiongozwa na mwenyekiti wake ambae pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi  Dr. Servaciaus Likwelile (kulia)  ofisini kwake leo tarehe 12 Februari 2015. Katika salam zake ameishukuru Serikali na mfuko huo kwa kazi nzuri inayofanyika Mkoani Rukwa na taifa kwa ujumla hususani katika ujenzi wa miundombinu ya barabara za lami, Pamoja na hayo ameiomba Serikali na wafadhili wa MCC kusaidia pia katika ujenzi wa barabara muhim za Wampembe iliyopo Wilaya ya Nkasi, barabara ya bondeni kwa ajili ya kuunganisha ukanda wa bonde la Ziwa Rukwa unaoongoza kwa uzalishaji wa mpunga na Mikoa ya Katavi na Mbeya, barabara ya Kasesha kwa ajili ya kuunganisha Mkoa wa Rukwa na Zambia na barabara ya kuelekea Kalambo Falls yalipo maporomoko ya Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (kulia) akiendesha kikao ofisini kwake mapema leo tarehe 12 Februari 2015 kati yake na viongozi na wajumbe wa Mfuko wa Changamoto za Millenia Tanzania (MCA-T) .

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKUTANA NA VIONGOZI WA SIASA JIJINI DAR LEO.

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Damian Lubuva akizungumza wakati wa mkutano na Viongozi wa Vyama vya Siasa uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Julius Malaba na kulia ni Kamishina wa Tume yaTaifa ya Uchaguzi,Prof. Amon Challigha
Sehemu ya Viongozi wa Vyama vya Siasa waliohudhulia Mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Damian Lubuva (hayupo pichani) leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.

NI SAFARI YA MIAKA 15 TAMASHA LA PASAKA

DSC_0333
 
“NILIAMUA kuanzisha Msama Promotions baada ya kuona muziki wa Injili umesahaulika na unashuka thamani yake.“Hivyo kwa kushirikiana na wenzangu nikaona ni busara kuuinua ili tuwe kama wenzetu Afrika Kusini ambao wana waimbaji wa nyimbo za Injili wanaotamba kama Rebecca Malope, Itani Madima, Steve Kekane, Vuyo Mokoena na wengine wengi,” hiyo ni kauli ya Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE MGENI RASMI MAADHIMISHO YA TAIFA LA IRAN

 Balozi wa Iran nchini Tanzania,Mh.Mehdi Aghajafari akimpokea Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb) alipowasili katika hafla ya kusherehekea siku ya Taifa la Iran iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi huyo Jijini Dar es Salaam jana usiku.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb) akizungumza mbele ya wageni mbalimbali walioalikwa katika hafla ya siku ya Taifa la Iran iliyofanyika kwenye makazi ya balozi wa Iran Jijini Dar es Salaam.

Rais kikwete awaapisha Balozi Mpya wa Tanzania nchini Kenya na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya na Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha. Katika hafla hiyo iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete amemwapisha Bwana John Haule kuwa balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya na Dkt.Hamisi Mwinyimvua ameapishwa kuwa naibu katibu mkuu wa Wizara ya Fedha.
Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya Bwana John Haule akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya Bwana John Haule akipeana mkono na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mara baara ya kula kiapo Ikulu jijini Dar es salaam leo.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA BALOZI WA SAUDI ARABIA ANAYEMALIZA MUDA WAKE NCHINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Saudi Arabia, Hani Abdullah Mominah, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2015 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Saudi Arabia, Hani Abdullah Mominah, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2015 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.

BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA LASAINI WARAKA WA BRIGHTON DECLARATION KUHUSIANA NA USAWA WA KIJINSIA KATIKA MICHEZO

Rais Jakaya Kikwete AWAFAGILIA NSSF KWA KUNG'ARISHA MJI WA MOSHI.

TPB Yasaini Ushirikiano na Benki ya Kijerumani

Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Kijerumani ya Kreissparkasse Tubingen, Christoph Gogler, (wapili kushoto0, akimkabidhi mfano wa hundi ya euro 2,000, mkurugenzi mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya TPB, jijini Dar es Salaam, Jumatanoi Feb 12, 2015. Benki hiyo YA kIJERUMANI NA tpb, pia wamesaini makubaliano ya ushirikiano baina yao. Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Kijerumani ya Kreissparkasse Tubingen, Christoph Gogler, (wapili kushoto0, akimkabidhi mfano wa hundi ya euro 2,000, mkurugenzi mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya TPB, jijini Dar es Salaam, Jumatanoi Feb 12, 2015. Benki hiyo YA kIJERUMANI NA tpb, pia wamesaini makubaliano ya ushirikiano baina yao.Mkurugenzi Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, (Kulia), na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Kijerumani ya Kreissparkasse Tubingen, Christoph Gogler wakitia saini makubaliano ya ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili za kifedha malao makuu ya TPB, jijini Dar es Salaam, Jumatano Feb. 11, 2015. Ujerumani itakuwa ikitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa TPB ili kuwajengea uwezo katika fani mablimbali hsusan huduma kwa wateja. Pia taasisi hiyo imeipatia TPB eURO 2,000 kwa madhumuni hayo hayo. Mkurugenzi Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, (Kulia), na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Kijerumani ya Kreissparkasse Tubingen, Christoph Gogler wakitia saini makubaliano ya ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili za kifedha malao makuu ya TPB, jijini Dar es Salaam, Jumatano Feb. 11, 2015. Ujerumani itakuwa ikitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa TPB ili kuwajengea uwezo katika fani mablimbali hususan kitengo cha huduma kwa wateja. Pia taasisi hiyo imeipatia TPB EURO 2,000 kwa madhumuni hayo hayo.

MAGUFULI AMSHUKURU BALOZI WA JAPAN NCHINI KUCHANGIA MIRADI YA MAENDELEO

DSC_8983
Balozi wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hussein Kidanto wakitiliana saini mkataba wa fedha za ruzuku shilingi milioni 70/ zilizotolewa na serikali ya Japan kwa ajili ya kununua magari mawili ya wagonjwa (Ambulance). Tukio hilo lilishuhudiwa na viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na Mkurugenzi wa Hospitali hiyo aliyemaliza muda wake Dkt. Marina Njelekela.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na modewjiblog team.

Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli ameishukuru Japan kupitia Balozi wake alioko nchini kwa kusaidia miradi inayochangia maendeleo ya moja kwa moja hususani afya, elimu na maji. Dk. Magufuli alisema hayo jana katika makazi ya Balozi wa Japan Nchini, Masaki Okada yaliyopo Masaki Jijini Dar es Salaam wakati wa kutiliana na saini za mkataba wa fedha za ruzuku zitakazoenda kusaidia maendeleo kwa jamii ikiwemo Jimbo la Chato na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Katika hafla hiyo, Dk. Magufuli aliambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Wilaya ya Chato, pamoja na Wakurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiwemo Mkurugenzi wa zamani wa hospitali hiyo Dk. Marina Njelekela pamoja na wa sasa Dk. Hussein Kidanto.
DSC_8984
Balozi Okada na Mkurugenzi Dkt. Kidanto wakibadilishana hati za mikataba hiyo. Dk. Magufuli alishuhudia utiaji wa saini wa mikataba hiyo ambapo Balozi Okada alitoa kiasi cha sh milioni 70, kwa ajili ya ununuzi wa magari ya kisasa ya kubebea wagonjwa (Ambulance) kwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo mpaka sasa inadaiwa wana Ambulance moja pekee.

SERIKALI YAANZA KUSAMBAZA KATIBA INAYOPENDEKEZWA

Serikali imeanza kusambaza nakala milioni mbili za Katiba Inayopendekezwa nchini kote ili kuwawezesha wananchi kuisoma na kushiriki katika Kura ya Maoni iliyopangwa kufanyika tarehe 30 Aprili mwaka huu.

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro amesema leo (Jumatano, Februari 11, 2015) jijini Dar es Salaam kuwa kati ya nakala hizo zilizochapwa jijini Dar es Salaam, nakala 1,800,000 zinasambazwa Tanzania bara na nakala 200,000 zinasambazwa Tanzania Zanzibar.

Kwa mujibu wa Waziri Migiro, hadi kufikia jana (Jumanne, Februari 10, 2015), jumla ya nakala 707,140 zilikuwa zimesambazwa katika mikoa 12 ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ambayo imepata nakala 200,000 na kuwa kazi hiyo inaendelea vizuri na inatarajiwa kukamilika katika muda mfupi ujao.

NINI UFANYE KISHERIA UNAPOHISI MWENZAKO KATIKA NDOA ANATAKA KUUZA NYUMBA/KIWANJA BILA RIDHAA YAKO.

Image result for kuweka zuio
NA  BASHIR  YAKUB-
Upo wakati kwenye  ndoa ambapo mmoja  wanandoa  anaweza akawa anataka  kuuza au kubadili jina la nyumba/kiwanja  bila ridhaa ya mwenzake ilihali  nyumba  hiyo  ni ya  familia. Lakini  pia  nje ya  hilo kuna  mazingira  ambayo  mtu anaweza  kuwa  si  mwanandoa lakini ana maslahi  katika  nyumba au  kiwanja cha mtu fulani  na anataka  kuzuia  nyumba/ kiwanja  hicho  kisibadilishwe  jina au kisiuzwe.  Kisheria jambo hilo linaruhusiwa  na huitwa zuio( Caveat).

Rais Kikwete alipozindua Jengo la Kitega Uchumi la NSSF mjini Moshi