Kamati ya Sheria na Hadhi za
Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imempiga faini
ya sh. 600,000 au kifungo cha mwaka mmoja Katibu Mkuu wa Villa Squad,
Mbarouk Kassanda kwa kusika na uhamisho wa mchezaji Omari Ramadhan ambao
haukufuata kanuni za usajili.
Villa Squad iliingiza majina
tofauti ya mchezaji huyo wa African Lyon, ambapo badala ya Omari
Ramadhan ikaingiza Omari Issa Ibrahim’. Kamati imeona Villa Squad
ilifanya hivyo ili kudanganya, kuwezesha mfumo wa usajili wa
kielektroniki ukubali jina la mchezaji.
Malalamiko ya kutaka kupewa pointi
tatu na mabao matatu kwenye mechi dhidi ya Villa Squad kwa kumchezesha
mchezaji huyo, yametupwa na Kamati kwa sababu alikuwa ni mchezaji halali
aliyethibitishwa (eligible) na TFF.
Kamati ilimuita mchezaji huyo na
kumhoji kama alishiriki au alifahamu udanganyifu wa kubadili majina ili
aweze kuingizwa katika mfumo wa eletroniki wa usajili lilibaki kuwa
suala la mashaka. Inawezakana alishiriki au hakushiriki; Kamati
haikupata ushahidi thabiti. Hivyo, Kamati iliamua kumpa mchezaji faida
ya mashaka (benefit of doubts) na hivyo kutompa adhabu yoyote.
Kassanda ameadhibiwa kwa mujibu wa
kanuni ya 40(11) ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) wakati Omari Ramadhan
ni mchezaji wa African Lyon kwa vile ana mkataba na klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment